Showing posts with label misiba. Show all posts
Showing posts with label misiba. Show all posts

Friday, August 15, 2014

WAKATI MAZISHI YA MAMA TUNDA YAKIENDELE AFANDE SELE AZIMIA AKIMZIKA MKEWE!

Mfalme wa Rhymes Bongo, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ ameshindwa kustahimili msiba wa mkewe, Asha Msindi (34) na kujikuta akizimia msibani wakati wa maziko, Risasi Jumamosi lina stori ya kusikitisha.
Mwili wa marehemu Asha Mohamed Shiengo 'Mama Tunda' ukiombewa kabla ya mazishi.
Tukio hilo ambalo liliibua simanzi nzito mkoani hapa na kuweka historia lilijiri juzi, Alhamisi katika Mtaa wa Amani, Mji Mkuu, alipokuwa akiishi Asha na mama yake.
Aliyekuwa mke wa Afande Sele, Asha Msindienzi za uhai wake.
RAFIKI AFUNGUKA
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Afande, gwiji huyo wa muziki ambaye alitengana na mkewe mapema mwaka huu, alipopewa taarifa hizo za msiba, hakuamini hadi alipofika nyumbani kwa marehemu na kukuta watu wamejaa msibani.
Mfalme wa Rhymes Bongo, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ akiwa amezimia msibani.
“Alipigiwa simu na baadhi ya ndugu wa mke kumueleza habari za msiba, hakushtuka sana maana hakuwa ameamini moja kwa moja hivyo akasema ataamini atakapofika msibani na kukuta msiba,” alisema mtu huyo wa karibu ambaye aliomba hifadhi ya jina gazeti.
Afande Sele akiweka udongo kwenye kaburi la mke wake Mama Tunda.
AZIMIA
Mtu huyo wa karibu alizidi kueleza kuwa, mara baada ya kufika nyumbani hapo na kukuta ndugu, jamaa na marafiki wamekusanyika ndipo Afande alipoanguka na kuzimia kwa takriban saa nne kisha akaziduka.
“Alipofika pale nyumbani kwa mkewe na kukuta umati ukiwa msibani, alijitahidi akaingia ndani na alipomuona mama mkwe wake, hapohapo alianguka na  kuzimia,” alisema mtu huyo.
Mama wa marehemu Asha Msindi (34), Hamida Rajab Sulu.
APEPEWA
Rafiki huyo wa Afande alizidi kueleza kwamba, baada ya kuzimia, ndugu wa mke walimlaza kwenye kochi kisha baadaye rafiki zake walimchukua na kumpeleka nyumbani kwake maeneo ya Msufini ambapo walimpepea kisha wakammwagia maji ya baridi, akazinduka.
Alipozinduka, aliwaomba marafiki zake wampeleke tena msibani ambapo alipofika aliomba kuletewa mwanaye mdogo, Asantesanaa, akambeba na kukaa naye msibani hapo.
Majirani waliofika msibani wakiwa pamoja na mama wa marehemu(Asha Msindi), Hamida Rajab Sulu(wa kwanza kulia).
CHANZO CHA KIFO
Akizungumza na mwandishi wetu, mama mzazi wa marehemu, Hamida Rajab Sulu, alisema kuwa mwanaye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria kali kwa takriban siku tatu, ndipo Jumatano iliyopita asubuhi walipompeleka katika Hospitali ya St. Mary mjini hapa.
Alisema kuwa alipofikishwa hospitalini hapa alilazwa na kuanzishiwa dozi ya malaria lakini baadaye hali ilizidi kuwa mbaya wakalazimika kumuhamishia kwenye Hospitali ya Manispaa ya Morogoro.
“Walimlaza pale kwa saa kadhaa, walipoona hali inazidi kuwa mbaya, walitushauri tumuhamishie kwenye Hospitali ya Manispaa Morogoro.“Tulipofika pale walimuanzishia dripu ya kutibu malaria, kabla hata haijaisha, mgonjwa alianza kutikisa miguu, hapohapo akafariki dunia. Ilikuwa muda wa saa 5:00 usiku,” alisema mama huyo.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania 'TAFF', Simon Mwakifwamba akimpa pole Afande Sele.
WASANII WATINGA MSIBANI
Msiba huo umeacha historia ya aina yake kwani kesho yake asubuhi (Alhamisi), wasanii wengi walifika msibani hapo kwa ajili ya kuomboleza hali ambayo iliwafanya baadhi ya watu kushangaa wasanii badala ya kuomboleza.
Picha ya familia: Kutoka kulia ni Asha Mohammed Shiengo ‘Mama Tunda’ enzi za uhai wake, Selemani Msindi ‘Afande Sele’, Asantesana Selemani na Tunda Selemani.
Miongoni mwa wasanii ambao walifika mapema msibani hapo ni pamoja na Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini, Simon Mwakifwamba na Joseph Haule ‘Profesa Jay’.
AFANDE ANENA
Akizungumza kwa uchungu makaburini hapo, Afande Sele alisema kifo cha mkewe ni pigo kubwa maishani mwake kwani ndiye aliyekuwa faraja ya pekee kwa wanaye, Tunda na Asantesanaa.
“Hili ni pigo kubwa maishani mwangu, mama Tunda alikuwa ndiye kila kitu kwa wanangu, inaniuma sana,” alisema Afande akitokwa machozi.
Mwanamuziki Profesa Jay (kulia) akimfariji Afande Sele.
AZIKWA
Baada ya umati kujikusanya msibani hapo, taratibu za mazishi zilifanyika siku hiyohiyo na wakaelekea kuzika kwenye Makaburi ya Kola mjini hapa.
TUJIKUMBUSHE
Kabla Afande Sele na mama Tunda hawajatengana mapema mwaka huu, waliishi kama mume na mke kwa zaidi ya miaka kumi na kufanikiwa kupata watoto wawili, Tunda na Asantesanaa
CREDIT:GPL

Saturday, July 5, 2014

yule Mfungwa askari wa jkt aliyemuua mtoto wa Fundikira afariki dunia





                                               Mfungwa Sajini Rhoda Robert

Mfungwa Sajini Rhoda Robert aliyekuwa anasubiri adhabu ya kunyongwa kwa kosa la kumuua mtoto wa kigogo Swetu Fundikira, amefariki dunia wakati akitibiwa katika hospitali ya mkoa ya Dodoma, kufuatia hali yake kubadilika kutokana na kuishiwa damu mwilini.

Rhoda aliyekuwa askari wa kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mbweni na wenzake Koplo Ally Ngumbe na Mohamed Rashid, walihukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam, baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtoto wa Chifu Abdallah Fundikira.
Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Zainabu Muruke Novemba 20, 2012.

Hadi mauti yanamkuta, Jaji Muruke aliyesikiliza na kutoa hukumu ya kesi hiyo alikuwa hajasaini hukumu hiyo na kuwafanya wafungwa hao kushindwa kukata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga hukumu hiyo.

Mapema mwaka huu wakili wa wafungwa hao, Kaloli Muruge, aliiambia NIPASHE kuwa aliwasilisha kusudio la kukata rufaa lakini kikwazo ilikuwa ni nakala ya hukumu ambayo jaji alikuwa hajaisaini.

Habari za kuaminika kutoka Gereza la Isanga mkoani Dodoma ambapo mfungwa huyo alikuwa akisubiri kunyongwa, zilisema kuwa Sajenti Rhoda alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo akisumbuliwa na maradhi.

Alisema hali ya mfungwa huyo ilibadilika na kufariki dunia akiwa hospitalini hapo.





“Alizikwa gerezani kwa sababu alikuwa ni mfungwa ambaye kisheria hairuhusiwi kuzikwa uraiani lakini mwishoni mwa wiki ndugu zake waliarifiwa kuhusu kifo chake kabla ya mazishi na walifika na kuonyeshwa kaburi lilipo,” kilieleza chanzo chetu cha habari.

NIPASHE ilizungumza na  Mkuu wa Gereza la Isanga, Makoti Mwaibale, ambaye alithibitisha kufariki kwa mfungwa huyo. Alisema mfungwa huyo alifariki dunia Juni 20, mwaka huu katika hospitali hiyo akiwa anapatiwa matibabu.

Alisema Rhoda aliumwa na kupelekwa hospitalini  Juni 15,  mwaka huu ambapo alilazwa huku akiendelea na matibabu kwani ugonjwa uliokuwa unamkabili ulimsababishia kupungua kwa damu.

"Ugonjwa wa mtu ni siri hivyo alikuwa akiongezewa damu na ilipofika Juni 20 majira ya saa 1 asubuhi alifariki dunia," alisema. Mwaibale alisema mfungwa huyo alizikwa siku hiyo katika makaburi ya wafungwa yaliyopo Dodoma.

Alisema mume wa marehemu pamoja na mjomba wake walitaka kuuchukua mwili huo kwa ajili ya mazishi lakini haikuwezekana kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, alisema kwa mfungwa ambaye amehukumiwa kunyongwa hadi kufa akifariki anazikwa na magereza lakini angekuwa ni mahabusu wa kawaida mwili huo ungekabidhiwa kwa ndugu zake.

Alisema ndugu wa marehemu hawakushirikishwa katika mazishi kwa kuwa kuna sheria zinazowaongoza katika jambo hilo.Mwaibale alisema ndugu zake akiwamo mume wake walifika Juni 22, na kuonyeshwa kaburi la mfungwa huyo lilipo.

Hukumu ya askari hao ilisomwa na Jaji Muruke alisema ingawa hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa washtakiwa hao ndiyo waliomuua Fundikira, ushahidi uliotolewa na  upande wa mashtaka (Jamhuri) ulikuwa ni ushahidi wa mazingira, kwamba Jamhuri imeweza kuthibitisha mashtaka hayo.

Alisema kuwa anakubaliana na mtiririko wa ushahidi wa upande wa mashtaka kama ulivyoelezwa na mashahidi wake sita akiwemo daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu pamoja na  askari polisi wawili ambao washtakiwa katika utetezi wao walishindwa kuuvunja.

“Sheria iko wazi ukiondoka na mtu au ukionekana naye kwa mara ya mwisho na baadaye mtu huyo akapatikana na madhara, wewe ndiyo unawajibika kutoa maelezo ya kina kuhusu yaliyompata mtu huyo,” alisema Jaji Muruke na kuongeza;

“Kisheria ukitoa maelezo ambayo hayajakidhi haja na yana utata ni faida kwa upande wa mashtaka ambao hutegemea ushahidi wa mazingira. Maelezo ya kina hayajatolewa na washtakiwa wote.”

Aliendelea,  “Ushahidi wa Jamhuri japokuwa ni wa mazingira, umejengwa thabiti na upande wa utetezi haukuweza kujenga matundu, ama kuuvunja mnyororo huo,  kidole kinawaelekea wao.”

Jaji Muruke alisisitiza kuwa katika kesi hiyo licha ya kuwa kuna ushahidi wa kimazingira, upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka.







                                             marehemu fundikira

Sajini Roda na Koplo Mohamed Rashid wote wa JKT Mbweni na Koplo Ally Ngumbe (37) wa Kikosi cha JWTZ Kunduchi, walimpiga Fundikira, Januari 23 mwaka huu  saa 7:30 usiku wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam na baadaye kufariki dunia usiku huohuo wa kuamkia Januari 24, mwaka 2010, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

 
CHANZO: NIPASHE

Monday, April 14, 2014

RATIBA YA MAZISHI YA MAALIM GURUMO

Mzee Muhidin Maalim Gurumo enzi za uhai wake.
-LEO saa 10 jioni kutakuwa na kisomo nyumbani kwa marehemu Tabata-Kisukulu jijini Dar es Salaam.
-Kesho saa 3 asubuhi mwili wa marehemu utawasili nyumbani kwake kwa ajili ya sala.
-Saa 4 asubuhi safari ya kuelekea kijiji cha Masaki wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani kwa maziko

Sunday, December 15, 2013

UPDATES:MAZIKO YA NELSON MANDELA KIJIJINI QUNU

 
Jeneza lenye mwili wa Mandela likiwa makaburini.
 
Jeneza lenye mwili wa Hayati Nelson Mandela likipelekwa makaburini tayari kwa maziko.
 
Hapa ndipo Hayati Nelson Mandela atakapozikwa.
 
Oprah Winfrey naye ni miongoni mwa waombolezaji. Hapa akielekea eneo la makaburi.
 
Askofu Desmond Mpilo Tutu ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa marehemu Mandela naye akielekea eneo la makaburi.
 
Jeneza baada ya kuwasili eneo la makaburi. Hapa likifunguliwa kutoka kwenye gari maalum.

Thursday, December 5, 2013

TWEET ZA WANAMUZIKI WAKUBWA DUNIANI BAADA YA KIFO CHA NELSON MANDELA


Mwanamuziki Robert Sylvester Kelly "R. Kelly" akiwa na Nelson Mandela enzi za uhai wake.

Wednesday, December 4, 2013

HUYU NDIO DENTI WA KIDATO CHA NNE ALIYEUAWA NA MPENZI WAKE KIMARA KW AKUCHOMWA VISU

KIFO cha kikatili cha mwanafunzi aliyeuawa siku chache baada ya kuhitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Luguruni na mkazi wa Kimara Golani, Dar, Sharifa Rajab (18) bado ni simanzi nzito katika familia yake.
Marehemu Sharifa Rajab enzi za uhai wake.
Sharifa aliuawa kikatili Novemba 22, mwaka huu, Kimara Golani jijini Dar na mtu anayedaiwa ni mpenzi wake ajulikanaye kwa jina la Abdul (22) ambaye ni dereva wa bodaboda.
SIMULIZI YENYE MAJONZI
Akizungumza kwa masikitiko makubwa, baba wa marehemu, Rajab Abdallah alisema siku ya tukio asubuhi, yeye na mke wake wakiwa kazini, Sharifa aliondoka nyumbani hapo  bila taarifa na kuwaacha wadogo zake tu.
“Tuliporudi jioni, mimi na mama yake tulianza kuhangaika kumtafuta bila mafanikio. Mwisho tuliamua kurudi kulala japokuwa usingizi ulikataa. Unajua tena mtoto ni mtoto. Huwezi kupata usingizi wakati mwanao hujui aliko.
“Tulipanga siku iliyofuata kwenda kutoa taarifa polisi, lakini ilipofika saa kumi na moja alfajiri, tuliletewa ujumbe kwamba kuna mwili wa mwanamke umekutwa kwenye chumba cha jirani.
“Ilikuwa vigumu kusema kwamba mwili huo ni wa mtoto wetu Sharifa, tuliamini kifo kipo, lakini watakufa wengine si mtoto wetu Sharifa.
“Hata hivyo, tulifunga safari kwenda kuuangalia mwili huo. Sikuamini hata kidogo nilipogundua kwamba ni mwanangu ndiye alilala kitandani, amekufa kwa kuchomwa kisu kooni na kwenye mbavu zote, kitanda chote kilijaa damu. Sharifa alikuwa si Sharifa tena bali marehemu Sharifa,” machozi yanamlengalenga.
Anaendelea: “Inaniuma sana! Mbaya zaidi nilijua  chumba hicho ni cha  kijana ambaye ni dereva wa bodaboda, anaitwa Abdul. Nikajiuliza ina maana alikuwa ni mpenzi wake? Sikupata jibu.”
TABIA YA MAREHEMU
Baba wa marehemu aliongeza kuwa, kwa kipindi chote cha uhai, Sharifa hakuwahi kuonesha dalili kwamba alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi, alikuwa ni msiri sana.
MTUHUMIWA WA MAUAJI AACHA UJUMBE
Habari zaidi zilidai kuwa, baada ya mtuhumiwa huyo kutekeleza mauaji ya binti huyo aliacha ujumbe wa maandishi akisema kuwa watu wasihangaike kumtafuta kwani na yeye anakwenda kujiua.
Hata hivyo, mtuhumiwa hakwenda kujiua, badala yake alifika Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mikoani (UBT) kutafuta usafiri wa kurudi kwao Tanga lakini alipokosa aliamua kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Ubungo na kukiri kuua.
Mmoja wa viongozi wa serikali ya mtaa (hakutaka kutaja jina lake) alisema mtuhumiwa huyo alipohojiwa polisi alisema hajui kilichotokea, akaomba apewe nafasi akamzike mpenzi wake huyo.
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambapo alisema kwa mujibu wa mtuhumiwa alifanya kitendo hicho kutokana na wazazi wa msichana huyo kukataa yeye asimuoe na tayari alikuwa na mchumba mwingine.
Marehemu Sharifa alizikwa Novemba 24, mwaka huu katika Makaburi ya Golani Nzasa, Dar. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.


GPL

MOROGORO: KONDAKTA AGONGWA NA LORI NA KUFA AKIWAVUSHA BARABARA WANAFUNZI WA CHEKECHEA.



Marehemu William Francis,28, enzi za uhai wake


Baadhi ya viongozi wa chama cha waendesha daladala wakiendelea kukusanja michango ya rambi rambi leo mchana




Baadhi ya madereva na makondakta wa daladala wakiwa na nyuso za hudhuni baada ya kupokea taarifa za tukio hilo.
NA DUSTAN SHEKIDELE, MOROGORO.
KATIKA hali ya kuhuzunisha kondakta wa Hiace inayofanya safari zake Kihonda - Mjini William Francis,28, jana mchana amegongwa na Lori na kufa papo hapo eneo la Kihonda barabra kuu ya Morogoro-Dodoma, alipokuwa akiwavusha abiria wake ambao ni wanafunzi wa chekechea uapande wa pili wa barabara hiyo isiyokuwa na vituo vya kushusha na kupakia abiria.

Akihojiwa na mwandishi wa habari hizi msemaji wa chama cha madereva na makondakta wa daladala mkoani Morogoro Bw Kigola Pazi alisema marehemu aligongwa na gari hilo alipokuwa akiwavusha abiri wake ambao ni madenti wa shule ya awali 'chekechea'

"Kwa nyinyi waandishi wa habari mtusaidia kufikisha kilio chetu kwa mamlaka husika mwenzetu amekufa akitetea roho za abiri wake kufutia barabara ya Kihonda kukosa vituo vya kushusha na kupakia abiri, Wille aligongwa na gari wakati akirudi upande wa pili wa barabra baada ya kuwavusha watoto wawili wa shule ya chekechea akisema kwa uchungu msemaji huyo wa chama hicho.

Mwandishi wa habari hizi alifika kwenye kituo kikuu cha daladala kilichopo katikatika ya mji kasoro bahari 'Morogoro' na kushuhudia baadhi ya madereva na makondakta wakiwa na nyuso za huzuni baada ya kupokea taariza hizo za kifo cha ghafla cha mwenzao.

'Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake libarikiwe Amen

Thursday, November 28, 2013

Mume Amuaa Mkewe Mjamzito wa miezi 9 kwa kumpiga mawe...Alikuwa amebakiza Siku 2 tu Ajifungue

JESHI la Polisi Mkoa wa dar es salaam Kinondoni, linamshikilia Philemon Ng’ambi, mkazi wa Madale Kata ya Wazo, jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kumuua mkewe, Enea Kagine kwa kumshambulia kwa mawe na matofali hadi kumuua.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Enea Kagine likibebwa na waombolezaji.


Philemon anadaiwa kufanya unyama huo kwa marehemu mkewe aliyekuwa amebakiza siku mbili kabla ya kujivungua usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita  nyumbani kwake Wazo-Hill.
Akisimulia mkasa huo kwa mapaparazi wetu, jirani wa wanandoa hao aliyejitambulisha kwa jina la Fikiri Rashid alisema:
“Mimi nyumba yangu na yao zinatazamana hivyo siku ya tukio majira ya saa tisa usiku, nilianza kumsikia marehemu akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema mumewe anamuua.

Marehemu Enea Kagine enzi za uhai wake.


“Nilitoka nje kwa lengo la kutaka kutoa msaada lakini nilihofia maisha yangu hivyo ilinibidi niwaite vijana wa ulinzi shirikishi ambao baada ya muda walifika eneo la tukio na kumkuta mtuhumiwa akivunja vyombo vya ndani kama mtu aliyechanganyikiwa, wakati huo tayari alikuwa ameshamuua mkewe.
 “Baada ya kuwaona ulinzi shirikishi, alikimbilia chumbani na kwenda kujificha uvunguni kwenye kitanda huku watoto wao watatu wakiwa wamelala.

Mtuhumiwa wa mauaji hayo, Philemon Ng’ambi.


“Bila kuchelewa, askari wa ulinzi shirikishi walimkamata na kuwasiliana na Askari wa Kituo cha Polisi cha Wazo ambao walifika eneo la tukio na kumtia mbaroni mtuhumiwa pamoja na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya taratibu za kipolisi,” alisema Fikiri.
Mama mzazi wa marehemu Enea akiwa na simanzi nzito.


Kufuatia tukio hilo la kusikitisha wanahabari wetu walifika katika Hospitali ya Mwananyamala ulipohifadhiwa mwili wa mwanamke huyo na mtoto wake waliyemtoa akiwa amefia tumboni.
Miili hiyo ilizikwa Jumatatu iliyopita (Novemba 25) mwaka huu katika kaburi moja kwenye Makaburi ya Madale, Dar es Salaam.

CREDIT: GPL

Thursday, November 21, 2013

Majeruhi Francis Shumira aliyepigwa risasi juzi na Gabriel Munis ili kulipiza kisasi kwa penzi la Christina afariki dunia



MAJERUHI Francis Shumira aliyejeruhiwa katika tukio la kushambuliwa kwa risasi Ilala Dar es salaam juzi  amefariki dunia jana asubuhi Hospitali ya Muhimbili alikolazwa MOI kwa matibabu. 
 
Kufariki kwa Francis kunafanya idadi ya watu  watatu waliofariki katika tukio hilo hadi hivi sasa huku ikiacha majeruhi wawili ambao  ni Christina Alfred Newa Mwanafunzi wa masuala ya Mawasiliano visiwa vya Syprus na mama mzazi wa Christina, Hellen Elieza Newa.

Familia imekiri kuwa Christina na Marehemu Munisi walikuwa na mahusiano lakini ni zamani na walitengana kutokana na vurugu alizowahi mfanyia siku za nyuma. 
Taarifa za Polisi zinapasha kuwa, Watu walio poteza maisha katika tukio hilo ni Gabriel  Munisi  ambaye aliwapiga  risasi  wenzake  na  kisha  kujiua  mwenyewe ,  Alfa Alfred ambaye  ni  mdogo wake Christina , na  Francis Khiranga Shumira ambaye  amefariki  jana  akiwa Muhimbili

Tuesday, November 12, 2013

BREAKING NEWZZ:Dk Mvungi afariki dunia


Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi amefariki dunia leo alasiri nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Dk Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.

SOURCE:MWANANCHI

Monday, November 11, 2013

INASIKITISHA:MWANAFUNZI WA KIDATO CHA 4 AFIRIKI DUNIA AKIWA KATIKA MTIHANI WA HISABATI MBAGALA DAR....


Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Mbande iliyopo Mbagala, Dar, Doricy Tryphone (18) amefariki dunia ghafla akiwa katika mtihani wake wa Hisabati wa kumaliza kidato cha nne, mwaka huu.
Tukio hilo la kuhuzunisha lilitokea Novemba 5, mwaka huu, Mbagala jijini Dar, wakati Doricy akifanya mtihani na wanafunzi wenzake.
Ilisemekana kuwa akiwa katikati ya mtihani huku ‘akisovu’ namba, ghafla binti huyo mzuri na mwenye mvuto  alizidiwa na kuishiwa nguvu, jambo lililowalazimu walimu na wasimamizi wamkimbize katika zahanati iliyopo jirani na shule hiyo.
Habari zilieleza kuwa baadaye hali ilizidi kuwa mbaya, ikabidi ahamishiwe kwenye Hospitali ya Temeke ili kuokoa uhai wake.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa huku akitokwa machozi, dada wa marehemu Doricy, Esther Tryphone alisema kuwa alipofikishwa hospitalini hapo, mdogo wake alikuwa ameshafariki dunia, huku vipimo vikionesha kuwa alikufa kwa kuzidiwa na sukari mwilini.
Dada huyo alieleza kuwa, Doricy alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu tangu akiwa darasa la sita, lakini baadaye alipata nafuu kabla ya ugonjwa huo kurejea ghafla siku hiyo na kuuchukua uhai wake.
Baada ya kutokea kwa msiba huo, mwili wa marehemu Doricy ulizikwa Novemba 7, mwaka huu, katika Makaburi ya Chang’ombe jijini Dar huku wanafunzi wenzake wakijitokeza kwa wingi kumsindikiza mwenzao katika safari yake ya mwisho

Wednesday, November 6, 2013

HUYU NDO MFANYAKAZI WA TBC ALIYE UWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA WATU WANAO SADIKIKA KUWA NI MAJAMBAZI USIKU WA KUAMKIA LEO

Mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji Nchini TBC, pichani,RAMADHAN GIZE ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosaidiwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo katika eneo la UBUNGO Maziwa Jijini DSM.* * * *Tukio hilo limetokea baada ya watu hao kuvamia duka moja katika eneo hilo la UBUNGO MAZIWA kwa lengo la kupora, ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la MWARAMI RAJABU amejeruhiwa kwa kupigwa risasi na watu hao wanaosaidiwa kuwa majambaz

Monday, October 28, 2013

WEMA AZIMIA MARA TATU KATIKA MSIBA WA BABA AKE....

MISS Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu, wikiendi iliyopita aliingia katika kipindi kigumu zaidi katika maisha yake, kwa vile lilikuwa tukio zito kulibeba baada ya kuzimia mara tatu ndani ya saa 7.
Wema Isaac Sepetu akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na baba yake mzazi.
Wema ambaye ni nyota wa filamu Tanzania, alizingirwa na maumivu makali, yaliyotokana na kumpoteza mtu anayempenda sana, baba yake mzazi, marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu.
Balozi Sepetu, alifikwa na mauti Jumapili iliyopita saa 12 asubuhi, ikiwa ni baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya kisukari na shinikizo la damu ambavyo vilimsababishia kupata ugonjwa wa kupooza viungo (kiharusi).
Mzee huyo aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, alifikwa na mauti akiwa katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa.
Awali, Balozi Sepetu alitolewa Zanzibar alikokuwa anaishi baada ya kuzidiwa kisha akapelekwa TMJ, alipopata nafuu aliruhusiwa kurejea nyumbani.
Hata hivyo, aliporuhusiwa hakurejeshwa Zanzibar, badala yake alipelekwa kwenye nyumba yake iliyopo Sinza Mori, jijini Dar es Salaam ambako alihudumiwa kwa muda kabla ya afya yake kubadilika na kukimbizwa TMJ ambako mauti yalimfika.
Wema akiwa na majonzi wakati wa msiba wa baba yake nyumbani kwao Sinza Mori jijini Dar.
WEMA KUZIMIA
Chanzo chetu kilisema: “Wema bado mdogo, katika maisha yake hakuwahi kupatwa na msiba mkubwa kama huu, kumpoteza baba yake kipenzi, ni jambo zito ndiyo maana mpaka sasa tunaongea ameshazimia mara tatu, yaani anazimia na kurejewa na fahamu.”
Jumapili saa 7 mchana baada ya kurejewa na fahamu, alisema: “Nimeumia sana kwani huu ni msiba mkubwa kwangu, Baba yangu alikuwa nguzo imara katika maisha yangu, sikuwahi kufikiria kama ningepata msiba mkubwa kama huu.
“Taarifa hizi wakati nazipokea nilijua kama utani lakini yote ni mipango ya Mungu, inaniuma sana,” alisema Wema.
WASIFU MFUPI WA MAREHEMU MZEE SEPETU

Balozi Sepetu aliwahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo visiwani Zanzibar, vilevile akawa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, miaka ya 1970 wakati wa utawala wa Awamu ya Kwanza chini ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwaka 1982, alteuliwa na Mwalimu Nyerere kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi, wadhifa ambao aliendelea kuushikilia mpaka kipindi cha Awamu ya Pili chini ya Rais Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Kati ya mwaka 2001 na 2006, Balozi Sepetu alichaguliwa kuwa mbunge katika Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM, Zanzibar.
Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi visiwani humo (Zipa).
Machi 27, mwaka huu, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alimteua Balozi Sepetu kuendelea na wadhifa huo wa Zipa kabla ya mauti kumchukua.
SOURCE:GPL

Sunday, October 27, 2013

UPDATES:HIKI NDICHO KINACHOENDELEA KWENYE MSIBA YA BABA MZAZI WA WEMA SEPETU HUKO SINZA JIJINI DAR...!

Saturday, October 26, 2013

WEMA SEPETU AFIWA NA BABA YAKE MZAZI

 mdada

Siku chache tu baada ya kuanza kurushwa hewani kwa kipindi halisia cha televisheni(Reality Show) yake, muigizaji, mrembo maarufu nchini Tanzania (Miss Tanzania 2006),Wema  A. Sepetu, amepatwa na msiba mkubwa. Amefiwa na Baba yake mzazi,Balozi Isaac Abrahamu Sepetu.

Taarifa ambazo BLOG imezipata zinapasha kwamba Mzee Sepetu ambaye kwa muda wa miezi kadhaa sasa amekuwa akiugua na kusumbuliwa na maradhi ya kiharusi,. Mzee Sepetu alikuwa pia akisumbuliwa na kisukari.Amefariki jijini Dar-es-salaam. Mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar.



Wema2Wema katika picha ya pamoja na baba yake mzazi,Balozi Abraham Sepetu. Pembeni ni rafiki wa karibu wa Wema,Petitman
Balozi Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Kambarag Nyerere.  Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere.
Pia, Machi 27, mwaka huu, Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais wa Zanzibar, Dr Mohammed Shein,  kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitegauchumi ya Zanzibar (ZIPA).
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.

Tuesday, October 22, 2013

UPDATES:WAKAZI WA JIJI LA DAR WALIVYOJITOKEZA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS KWA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA JULIUS NYAISANGA ...



 Msafara wa Magari ambao moja wapo (la mbele) likiwa limebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Julius Nyaisanga ukiingia kwenye viwanja vya leaders muda huu kwaajili ya wakazi wa jiji la Dar kuweza kutoa heshima zao za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga kabla ya Kusafirisha Kwao Tarime Mkoani Mara



Baadhi ya Ndugu, Jamaa na marafiki wakibeba jeneza lenye Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga Kwaajili ya kupeleka sehemu husika tayari kwa kutoa heshima za mwisho kwa wakazi wa jiji la Dar waliofika katika viwanja vya leaders muda huu


Sehemu Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga litakapowekwa kwaajili ya wakazi wa jiji la dar kuweza kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Tarime Mkoani Mara
 Baadhi ya wakazi wa jiji la dar waliojitokeza katika viwanja vya leaders muda huu
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar wakisubiria Kutoa Heshima zao za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga Kabla haujasafirishwa kupelekwa Kwao Tarime Mkoani Mara