Showing posts with label jokate. Show all posts
Showing posts with label jokate. Show all posts

Friday, October 25, 2013

Sijawahi vua nguo na kufanya mapenzi na mwanaume yeyote tangu niachane na Diamond"...Jokate Mwegelo





MTANGAZAJI wa Channel O mwenye mvuto wa aina yake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amefunguka na Weekly Star Exclusive na kuanika kuwa tangu amwagane na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ hajawahi kuanguka dhambini na mwanaume mwingine.
Penzi la Jokate na Diamond lilichanua kwa takriban miezi miwili mwaka jana wakati Kidoti alipomwagana na aliyekuwa mpenzi wake, mcheza kikapu wa Ligi ya NBA ya Marekani, Hasheem Thabit.
Akizidi ‘kutema madini’ mbele ya kinasa sauti cha Weekly Star Exclusive, Jokate alisema kwa kuwa alikuwa na mapenzi ya dhati na Hasheem, ndiyo maana alimwagana na Diamond ndani ya muda mfupi na tokea hapo amekuwa bize na kazi zake.
“Daah! Nipo bize sana na kazi zangu, ninaimba, ninaigiza, nina kampuni yangu ya urembo ya Kidoti huku bado natakiwa kutangaza Channel O basi kazi kwelikweli hata muda wa huyo mwanaume nakosa,” alisema Jokate.
Alipoulizwa anamudu vipi hisia za matamanio ya kibaiolojia, Jokate alisisitiza kuwa kazi pekee ndiyo silaha kubwa ya kumuepusha na vishawishi ingawa anatambua upo umuhimu wa kuwa na mpenzi.
“Akitokea mkweli, nipo tayari ingawa hadi sasa hata sijajua nani anaweza kuwa kama alivyokuwa Hasheem, nilimpenda sana,” alisema.

Monday, October 21, 2013

VIDEO:JOKATE AFICHUA MAZITO KUHUSU UHUSIANO WAKE NA DIAMOND...



KUMEKUWA na maneno mengi juu ya uhusiano wa kimapenzi kati ya staa mwenye vyeo vingi Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kisha staa wa kikapu wa NBA ya Marekani, Mtanzania Hasheem Thabeet Manka.
Kwa mara ya kwanza mwanadada huyo amefunguka kupitia mahojiano maalum (exclusive interview) na gazeti bora la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda na kufichua mazito nyuma ya pazia.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipozi na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Jokate ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07. Ana kofia nyingi kama mtangazaji wa Channel O, mwigizaji, mwanamitindo, MC, mwanamuziki na video queen wa nyimbo za Bongo Fleva.

DAKIKA 150
Katika mahojiano hayo ya dakika 150 (saa 2 na nusu) yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, pamoja na uhusiano wake na mastaa hao, Jokate anayependa kucheka na kuachia tabasamu pana, alifunguka mambo mengine mengi;
Ijumaa Wikienda: Jokate kuna taarifa kuwa uliwahi kuwa na uhusiano na Hasheem Thabeet. Je, ni kweli?
Jokate: Ni kweli. Nakumbuka ilikuwa baada ya Miss Tanzania 2006. Ilikuwa kitu kama 2007 au 2008.
Ijumaa Wikienda: Uhusiano wenu ulidumu kwa muda gani?
Jokate: Miaka miwili…mitatu (kicheko).
Ijumaa Wikienda: Ulikutana wapi na Hasheem na ilikuwaje?
Jokate: Tulikutana kwenye maonesho ya mavazi kwenye Ukumbi wa Water Front, Stesheni jijini Dar. Mwanzoni tulisalimiana lakini hakukuwa na chochote kwani nilikuwa nikikutana naye nacheka vile alivyo tall (mrefu). Naye alicheka tu.
Hasheem Thabeet Manka katika pozi na Jokate.
PENZI LA HASHEEM
Ijumaa Wikienda: Ilikuwaje hadi mkaingia kwenye mapenzi?
Jokate: Baada ya kuwa washkaji tukiendelea kuchati, tulijikuta tumependana sana. Mimi nilijikuta nikimpenda sana Hasheem na bado nampenda sana lakini kuna mambomambo tu yalitokea kila mtu akawa kivyake.
Ijumaa Wikienda: Maisha yako ya kimapenzi na Hasheem yalikuwaje?
Jokate: Aisee usipime…nakumbuka tulikuwa tunanunua matunda tunakaa kwenye gari tunakula. Tunatoka wote sehemu mbalimbali japo hakupenda kujianika.
Ijumaa Wikienda: Una kumbukumbu yoyote mbaya kwa Hasheem?
Jokate: Wala…japokuwa kuwa watu walikuwa wananiona nimeharibika. Labda namfuata Hasheem kwa sababu ya fedha au vyovyote walivyosema lakini mimi nilimpenda sana.
Ijumaa Wikienda: Kabla ya Hasheem kulikuwa na mwanaume mwingine?
Jokate: Yaah…lakini sipendi kabisa kumzungumzia. Namchukulia Hasheem kama mwanaume wangu wa kwanza.

‘USICHANA’
Ijumaa Wikienda: Unaposema hivyo ina maana Hasheem ndiyo alikutoa ‘usichana’.
Jokate: Nisingependa kujibu hilo lakini hadi natoka kwenye Shindano la Miss Tanzania 2006, nilikuwa sijamjua mwanaume. Nafikiri nikisema hivyo inaeleweka.

KWA NINI ALIACHANA NA HASHEEM?
Ijumaa Wikienda: Umesema ulimpenda sana Hasheem. Je, kwa nini mliachana, kumwagana au kupeana likizo?
Jokate: Ilitokea tu halafu akatokea mwanaume aliyenikuta kwenye msongo wa mawazo akawa ananiliwaza nikaona yees…nijipoze moyo.
Ijumaa Wikienda: Kabla ya kuachana mliwahi kugombana?
Jokate: Kugombana ni sehemu ya mapenzi. Ni kuonesha kuwa mnapendana. Ilitokea hivyo kwangu kwa sababu Hasheem alikuwa na heshima tofauti na wanaume wengine. Nahisi hakuna kama yeye, alinionesha alikuwa ananijali kwa kiasi gani.
Diamond akimpatia Jokate T-shirt. katika shoo ya Diamond are Forever ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar mwaka jana.
DIAMOND ALIMTIBULIA
Ijumaa Wikienda: Inasemekana mwanaume huyo ni Diamond.
Jokate: Yap…ni yeye lakini kulikuwa na vitu vingi akatumia nafasi au fursa kama wanavyosema siku hizi.

ANGEMTONGOZA MWAKA HUU ANGEKULA ZA USO
Ijumaa Wikienda: Ilikuwaje?
Jokate: Sijui…ilitokea tu. Nilikuwa kwenye hali fulani akatumia nafasi hiyo lakini angenitongoza mwaka huu nisingemkubali.
Ijumaa Wikienda: Jokate haukuwa mtu aliyetegemewa kugombea mwanaume na Wema Sepetu. Huoni kuwa uliharibu mtazamo wa watu juu yako?
Jokate: Kama nilivyosema sijui nini kilitokea.
Ijumaa Wikienda: Kwani ulikutana wapi na Diamond?
Jokate: Nakumbuka nilimwalika kwenye maonesho ya mavazi yangu. Watu wengi walikuwa wakisema kuwa nimemtoa uswahilini hadi ushuani. Sikupendezwa na watu walivyokuwa wanaponda.
Naye ni binadamu, anahitaji kila kitu anachohitaji binadamu mwingine. Ukweli ni kwamba yaliibuka maneno mengi mno. Baada ya hapo kweli alikuwa ananijali sana.
Jokate akiongea na GPL.
HAMKOSI MWANAMKE
Unajua jamaa anajua kuimbisha na ndiyo maana anawapata wanawake wengi. Mara ananiletea chakula, zawadi, nikitaka kwenda sehemu ananipeleka. Alikuwa anataka kwenda na mimi kila sehemu.
Ijumaa Wikienda: Vipi kuhusu kufumaniwa na Wema ukiwa na Diamond hotelini?
Jokate: Nakumbuka siku moja nilikutana na Diamond hotelini kuzungumzia kazi kabla sijaingia kwenye uhusiano naye, mara Wema akatokea, alipotuona akaondoka zake. Sasa sikujua nini kinaendelea. Huku na huku nikasikia eti Wema kanifumania jamani…hahahaa…
Ijumaa Wikienda: Ulidumu na Diamond kwa muda gani?
Jokate: Kama miezi miwili hivi...
Ijumaa Wikienda: Wakati unaingia kwenye mapenzi na Diamond hukujua kama yupo na Wema?
Jokate: (akiweka uso wa kazi) Nimesema sijui nini kilichotokea na nilikuja kujikuta najuta kuwa na Diamond japo naye ni binadamu.
Ijumaa Wikienda: Uhusiano wako na Wema ukoje?
Jokate: Simchukii Wema. Sina tatizo naye. Unajua lilipotokea lile tatizo la yeye kunikashifu niliona nikiendeleza malumbano haitakuwa busara.
Ijumaa Wikienda: Kwa nini uliachana na Diamond?
Jokate: Unajua Diamond ni mtu wa kujitangaza kuwa sasa nipo na huyu na mimi sipo hivyo so hata hapo sijui nini kilitokea lakini nitafanya naye kazi. Kuna wakati nilimwambia aniandikie wimbo ‘so’ tupo kikazi zaidi.
Ijumaa Wikienda: Unajuta kuwa na Diamond?
Jokate: Najuta. Ndicho kipindi ambacho kuliibuka mambo mengi sana.

SIRI YA DIAMOND KWA WANAWAKE
Ijumaa Wikienda: Diamond ni mwanaume wa aina gani?
Jokate: Mcheshi sana. Anajua kujali. Anajua kuzungumza na mwanamke kwa maneno matamu ndiyo maana akimtokea mwanamke hamkosi.
Ijumaa Wikienda: Diamond na Hasheem nani akikurudia unakubali?
Jokate: Hakuna lakini ukweli nilimpenda sana Hasheem.
Diamond akicheza na Jokate.

ZAWADI
Ijumaa Wikienda: Kati ya Diamond na Hasheem nani zaidi kwa zawadi?
Jokate: Naona sasa unataka kumkasirisha Diamond!
Ijumaa Wikienda: Tangu ulipoachana na Diamond una zaidi ya mwaka. Je, huna mpenzi mwingine?
Jokate: Nipo singo au unanishauri nani ananifaa?
Ijumaa Wikienda: Siwezi kuingia kwenye moyo wako wakati umesisitiza kuwa unampenda Hasheem!
Jokate: Yap…nilimpenda na ninampenda sana.

MWANA-FA VIPI?
Ijumaa Wikienda: Mbali na Hasheem, Diamond na huyo jamaa wa zamani, vipi kuhusu habari za wewe kutoka na mwanamuziki Hamis Mwinjuma ‘Mwana-FA’?
Jokate: Afadhali mnisaidie kwa sababu sijui hicho kitu kilianzia wapi. Ni uzushi tu uliosambazwa na mtu mmoja

source:GPL

Friday, October 18, 2013

KWA ZAIDI YA MWAKA MMOJA SIJAFANYA MAPENZI,SIJAWAHI NA MTU AMBAE NIMEWEZA KUMUITA.....MY BOYFRIEND" JOKATE



Hii  ni  mara  ya  kwanza  kwa  Jokate  Mwegelo  kuongelea  mambo  ya  chumban...


Maongezi  hayo  yalifanyika  kati  yake  na   Millard  Ayo   ambaye  ni  mtangazaji   wa  Clouds  FM.Katika  maongezi  hayo, Jokate  naye ameeleza  jinsi  anavyosumbuliwa  kutongozwa  na  mamia  ya  wanaume  kwa  siku 



Yafuatayo ni maongezi  yao: 

Millard Ayo: Nini kimekufanya ufunguke na hizi info ambazo hujawahi kuzizungumzia na mara nyingi umekua ukigoma kuziongelea kwenye media?

Jokate: Nahisi kwa sababu watu wanazidi kuizungumzia na wanaizungumzia sivyo, hawazungumzii kiuhalisia na kiukweli inanisumbua ndio maana nimeamua kusema kitu kidogo alafu niufunge huu ukurasa.
 
Millard Ayo: Imekua ikikusumbua kwa mda gani?
Jokate: Kwa muda mrefu, toka mwaka jana… kwenye facebook watu wanatoa comment na najua kabisa watu hawajaelewa hili swala na mimi sipendi mashabiki wangu kutokunielewa.

Millard Ayo:  umewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond pamoja na Hasheem?
Jokate: Hahahahahhaha !!!! Yeah..
 
Millard Ayo: Uhusiano wa nani kati ya hawa wawili ulidumu kwa muda mrefu?
Jokate: Wa Hasheem.. karibia miaka miwili mitatu
 
Millard Ayo: Na wa Diamond?
Jokate: Oooh kipindi kifupi sanaaa, sijui mwezi sijui miezi miwili… kidogo alinipa tabu, ila kiukweli nilitaka tu kwa sababu kuna watu wengi walikua wanasema Jokate yani vurugu, unajua sio kila kitu unachokisikia ndio chenyewe na media saa nyingine inapenda kuandika vitu ambavyo sio vya ukweli au wanaviwasilisha sivyo.
 
Millard Ayo: Sasa hivi uko single?
Jokate: Yeah, kwa muda mrefu tu niko mwenyewe alafu saa nyingine wananisumbua sana  tena  wengi  tu, lakini nafurahia kwa sababu naweza kufocus kwenye kazi zangu mfano wiki ijayo nakwenda kushoot movie na JB, muziki na biashara zangu kwa hiyo inanipa fursa nzuri kufanya vitu vyangu, yani mwenyewe kujiamulia asubuhi nakwenda kufanya vitu vyangu hivyo bila kusumbuliwa si unajua Wanaume wanaweza kusema wanataka attention nini… sio kitu kibaya atleast kwa sasa hivi.
 
Millard Ayo: Umekaa single kwa muda gani sasa hivi? zaidi ya mwaka?
Jokate: Yeah, kwa zaidi ya mwaka mmoja sijafanya  mapenzi… sijawahi na mtu ambae nimeweza kumuita like oohh this is my boyfriend… najua ni ngumu lakini nabusubusu watu wengi…. hahah a hah natania hapo, basi tu imetokea hivyo pengine bado sijapata mtu ambae nimeona ataweza kuwa kama wale

Monday, September 16, 2013

BAADA YA MANENO MANENO KUHUSU LUCCI NA JOKATE, HATIMAYE LUCCI AVALISHA PETE MWANAMKE AMPENDAE

Mtu wangu wa nguvu unaweza kujiuliza huyu shemeji yetu alikuwa na hali gani kipindi kifupi kilichopita wakati Kaka Dada,Lucci Jokate ndiyo headline kila sehemu. Lucci anaongezea,”Unajua ukishakuwa kwenye mapenzi na mtu anayejitambua na anafahamu kazi yako. Basi atafahamu kabisa entertainment inahitaji vitu tofauti ili kufanikisha. So mimi na yeye tuliongea kwamba muda huu tunaitoa kazi ya kaka dada na plan nzima alikuwa anaijua. So hakukuwa na tatizo lolote”
Kama unataka kujua upande wa pili wa Lizzyblazzer, Lucci anatuelezea kuhusu mchumba wake,”Lisa ni director wa kampuni yetu mimi na yeye inaitwa  Tsere. Kazi tunayofanya ni creative and marketing, pia anafanya kazi ya HR kwenye hii kampuni”

Oky, so kumaliza mawazo mengi ambayo watu walikuwa nayo kuhusu Jokate na Lucci. Kaka Dada ni kaka na dada kweli, ule ulikuwa wimbo tu.
Tunasubili Jokate na yeye atuwekee wazi shemeji yetu…JUST KIDDIN’
Yanayoendelea twitter…




Friday, September 13, 2013

JOKATE ATOA SABABU ZINAZOWAFANYA MIDUME KUMTOLEA MACHO NA KUMTONGOZA KILA SIKU

 MREMBO anayefanya vizuri katika mambo mengi nchini, Jokate Urban Mwegelo (pichani) ametaja sababu nne zinazowafanya wanaume kumzimikia, akiwemo nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’. 

Akiandika katika mtandao wake wa Kidoti Life Style, Jokate, mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2006, alizitaja sababu hizo kuwa ni kujiamini, kujitegemea, kupendeza na tabasamu muda wote.
 

Kujiamini ndiyo sababu kubwa ya kwanza inayonifanya nipendwe zaidi, hamna kitu kinachowavutia watu hasa wanaume kama kujiamini,” anaandika Jokate.

Kujitegemea ni sababu ya pili, binafsi naamini kwamba hakuna kitu kinachowaboa wanaume kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume wewe unapenda kutafuta vyako, basi jua atakupenda zaidi.”
  
Jokate alisema sababu nyingine inayomfanya kuwa kivutio kwa wanaume ni kupendeza katika mavazi, hasa kwa kuvaa nguo zenye rangi ya kuonekana.

Sababu nyingine aliyoitoa ni tabasamu, akiweka wazi kuwa tabasamu linamfanya aonekane mrembo zaidi.

Tuesday, September 10, 2013

JOKETE AFUNGUKA INSTAGRAM KUHUSU UHUSIANO WAKE NA LUCCI.


Okay leo nimeamua kupitia page yangu ya Instagram ku-address the following pressing matters kwenye ulimwengu wa majungu. 1. Luciano Gadie Tsere is NOT my LOVER and noooo hatumegani kisela. Na hata kama it were true inakuhusu nini. Sioni ishu. Kwenye Sanaa kuna kitu kinaitwa kuweka uhalisia. And that's what we did na KAKA DADA. I respect Lucci. Ni kaka yangu na tunafanya kazi nyingi sana zinakuja. Kuna watu wanefungua mpaka BBM group to discuss me and Lucci and this so called affair. Jamani kuliko maneno tufanyeni Kazi kuendeleza nchi yetu 2. Sijifanyi mtakatifu. Ila najitahidi kufanya matendo yanayompendeza Mungu. Na kwasababu kama binadamu sina ukamilifu basi only God can really judge me cause ndio anajua moyo wangu kuliko binadamu yoyote yule. Ila I'm a pretty good girl to be honest. Najaribu. Kwa nyinyi walimwengu don't be fooled by my PRETTY BABY FACE I know what I want, am fierce and I don't take trying to tarnish my image easily. So kindly don't mess with KIDOTI. Msione mtu mkimya mkajua ndio wa kumuonea. Still waters run deep 3. Yes there's some guy I'm checking out. Like any other female I deserve love cause I got so much love to give hey. So whoever it is tafadhali tusiharibiane kwa maneno maneno. Have a blessed evening!!

Saturday, August 24, 2013

i check video ya Lucci and Jokate – Kaka Dada

Hatimaye video iliyokuwa ikingojewa kwa hamu wiki nzima, Kaka Dada imetoka. Ni video ya wimbo wa kwanza wa Jokate Mwegelo akiwa na Lucci Da Don aliyeutengeneza. Video ilifanyika tangu February mwaka huu jijini Nairobi na kampuni ya Ogopa.


Thursday, August 22, 2013

JOKATE ATOBOA SIRI ZA KUZIMIKIWA NA WANAUME WENGI....DIAMOND ATAJWA



Mrembo anayefanya vizuri katika mambo mengi sana nchini Jokate Mwegelo amezungumza na kutaja Mambo manne yanayomfanya apendwe sana na wanaume wengi hapa nchini.
1. Kujiamini
Hii ndi sababu kubwa ya kwanza aliyoitaja jokate. Ansema hamna kitu kinachowavutia watu, hasa wananume kama kujiamini. Mwanaume anapenda msichana anayejiamini. Zaidi ya yote hamna kitu kinachosema kuwa “I’m sexy” Zaidi ya mwanamke anayejiamini
2. Kujitegemea
Hii ni kama sababu ya kwanza hapo juu,  Jokate anasema hamna kitu kinachowaboa wanaume kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume wewe unapenda kutafuta vya kwako basi jua atakupenda sana
3. Kupendeza
Jokate anasema ni muhimu kwa wadada kuvaa nguo nzuri ambazo zitakupendeza kulingana na mwili wako hasa hasa nguo zenye rangi ya kuonekana.
4. Tabasamu
Tabasamu kila saa kwani tabasamu linakufanya unaonekana mzuri Zaidi.

Wachunguzi wa mambo wamesema kuwa sababu hizi ndio pia zilichangia Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini Diamond platnumz kumpenda mwanadada huyu kwani sifa hizi hazipo kwa wadada wengi wa mjini

Thursday, July 25, 2013

JOKATE, MUSSA KIPANYA WAZUA JAMBO


MWANAMITINDO na mtangazaji maarufu Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Mtangazaji Mussa wa runinga wamezua jambo kufuatia picha zinazodhihirisha urafiki wao uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi kunaswa.
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ katika pozi na Mtangazaji Mussa.
Awali paparazi wetu aliinasa picha ya wawili hao ambayo kwa mujibu wao, walipiga miaka kumi iliyopita na walipokutana tena mwaka huu wakapiga mpya.
Baadhi ya wadau walioziona kwa mara ya kwanza, waliibua minong’ono kuwa urafiki wao ni wa siku nyingi hivyo kuna uwezekano wakafikia hatua ya ndoa.

 
Musa na Jokate katika picha ambayo inadaiwa kupigwa miaka kumi iliyopita.
“Urafiki wao ni wa kitambo, wanaweza kuja kuoana kabisa sababu aina ya maisha yao ni ya usiri sana,” alisema mdau mmoja ingawa wenyewe wamesema hawana cha kuzungumza juu ya hilo.