Showing posts with label ray c. Show all posts
Showing posts with label ray c. Show all posts

Friday, September 27, 2013

RAY C ASHINDWA KUJIZUIA,ADONDOKEA KWENYE PENZI LA HUYU SHUJAA WA MAGAIDI WA KENYA


Abdul Haji ni miongoni mwa mashujaa ambao hawatasahaulika nchini Kenya kutokana na kuamua kuhatarisha maisha yao ili kuokoa watu waliokuwa wamekwama ndani ya jengo la Westagate baada ya kushambuliwa na Al-Shabaab Jumamosi iliyopita.
Tangu asimulie namna alivyopambana na magaidi hao, Haji ametokea kuwa kipenzi cha watu wengi hasa wasichana na mmoja wa watu aliowagusa ni Rehema Chalamila ambaye amesema anatamani mwanaume mjasiri kama yeye ambaye watazaa naye watoto.
“In love with ths Soldier!i want a soldier like him to marry me,” ameandika Ray C kwenye picha ya gazeti aliyoipost kwenye Instagram ikimuonesha Abdul Haji.
“I love You Abdul Haji,You are my Heroooooooo,” aliandika Ray C kwenye picha nyingine.
Kwenye picha nyingine Ray C aliongeza, “My soldier,My Prince,My Love….Love You Abdul Haji.”
Kijana huyo ni mtoto wa waziri wa zamani wa ulinzi nchini Kenya ambaye alienda kwenye mall hiyo baada ya kupata ujumbe kutoka kwa rafiki yake kuwa kaka yake alikuwa ndani ya Westgate wakati watu hao wenye silaha walipovamia.

Akiongea na NTV, Haji ambaye sio mwanajeshi, alisema alifundishwa kutumia bunduki na baba yake ili kulinda mifugo yao isiibiwe na wezi.

Ujuzi huo ulimsaidia Jumamosi hiyo kuwasaidia wafanyakazi wa Red Cross wafanye kazi yao kwa usalama kwa saa tatu na kusaidia kuokolewa kwa watu wafikao 1,000 nje ya mall hiyo

Thursday, September 19, 2013

RAY C ARUDI KWA KASI KWENYE GEMU LA MUZIKI....HILI NDIO GARI JIPYA ALILONUNUA



STAA wa Bongo Fleva Rehema Chalamila‘Ray C’  ameamua kuianika  gari  yake  ambayo anatembelea kwa sasa ...

Gari  hilo  ni aina ya Jaguar ambalo namba zake za usajili hazionekani vizuri ila mwishoni zinasomeka T…CHL,huku akiandika kwenye instragram kuwa… Jaguar don't care...CHL means Chalamila Family..... 

Friday, September 13, 2013

Ray c na Zamaradi Mketema waingia katika bifu zito....Kisa ni PENZI la mwanaume

 
So Rehema Chalamila aka Ray C na mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema haziivi? Katika kile kilichoacha wazi midomo ya watu wengi, warembo hao leo wameingia kwenye vita vya maneno kwenye mtandao wa Instagram. Alianza Zamaradi aliyepost picha yenye maneno ya mafumbo: 
aae8fb521c4a11e3842d22000a1f9ada_7 Picha hiyo aliiandikia maneno haya:
Huwezi amini sikuchukii ila nimezidi kukudharau!!!! Katika watu wa mwisho kabisa ambao siwezi kupanic nao hata siku moja ni WEWE.. Dont waste your energy.. you have so much to accomplish ndugu.. mi hunipi tabu kabsa, kabsaa, kabisaaaaaaaaa yani sanasana unanichekesha tu na vituko visivyoisha.. lol!! Ila sikulaumu sana sio kosa lako maskini… 
 
ungekuwa una akili usingefanya hayo ya kitoto tena hasa KWA KIPINDI HIKI.. na huenda hiyo sio akili yako mwaya.. NIMEKUSAMEHE BURE maana hapo ulipo hujielewi bado.. 

Dramas Dramas Dramas… sizipendagi ila huwa zinanifata zenyewe.. lol!!! Mbona naandamwaga hivi jamani kwani kosa langu nini mimi mtoto wa watu… hahahahahaaaa majanga haya @wemasepetu anyways sorry to my good people jamani kwa mapost ya aina hii.. 
 
sometimes inabidi coz mwisho wa siku mi ni binaadamu tu wa kawaida.”
 
Wema naye aliongeza kwa kuchangia: Mbona majanga….. dont waste ur tym to fools maamy…. nawe utaonekana a fool… fanya yako… wanaokufatilia wanatamani wawe kama wewe… na si kingine its called ENVY.”
 
“Sina hata time nae mammy bado ana vichembechembe kwenye ubongo.. maana ghafla tu anaanza kuniparamia jamani.. lol!!! Kishafulia anatafuta kick kwa kugombana na watu.. mtu wa zamani,” aliongeza Zamaradi.
 
Japokuwa Zamaradi hakutaja wazi nani mlengwa wa ujumbe huo, ni Ray C mwenyewe ndiye aliyejibu kwenye maelezo ndani ya post yake kwenye mtandao huo akisema:
 
“Hihihi kazi kwelikweli mi naweza posts zangu watu wanajihisi au wanaumia. Tatizo skuliiiii shauri yako #uki skuli kdg wala matatizo hakuna ila km huja skuliii mweeeh unakua mbulula mama we hujui fanya yako achana na watu weusi,” aliandika Ray C.
 
Aliongeza tena, “Haswa anajiona kichwa kumbe mbulula haswaa Hana lolote,Watu wameanza shughuli hizo anazofanya wenzie tulishazifanya kitambooooooooo,tushauza sura sanaaaaaaaaaa zaid ya miaka. 12 namuangalia simmalizi maana haeleweki.”

Haukuishia hapo, Zamaradi aliongeza tena kwa kuweka post mpya.

886c292a1c5c11e383d722000a1f99fc_7
“Nashusha sana hadhi yangu kwakweli dealing with watu wenye hasira na maisha ya watu wengine… this is not ME kabisa. Una mengi ya kutukaniwa lkn mi ni binaadamu ninaejua baya na zuri.. maisha yashakushinda wewe sasa USIPANIC.. jipange. Ushafanywa yote ya dunia ntakuweza wapi mie mtu wa zamani,” aliandika Zamaradi kwenye picha hiyo.
 
Ray C alijibu kwa kupost video hii

Wednesday, September 11, 2013

Ray C alianika "shairi la penzi lake" instagram...Albam yake mpya iko jikoni inapikwa


Haya wale wenye kiu na ujio mpya wa Ray C mnaweza kuanza kuandaa makoo yenu sababu chakula kimeshawekwa jikoni na muda si mrefu mnaweza kukaribishwa mezani.

 Ray C ameshea picha kadhaa akiwa studio na wadau mbalimbali akiwemo Bab Tale na Said Fella, na kama haitoshi ameweka mashairi ya wimbo wake ambao unaonekana ndio aliokuwa akiurekodi wakati anapiga picha hiyo na kuandika “Mashairi ya my new song…,its a very beautiful song…am sooooooo happy..Thank you Lord”.
 Ray C lyrics
 Unaweza kuyapitia na kuanza kutengeneza taswira ya kile kinachokuja kutoka kwa Rehema Chalamila amabaye anasubiriwa kama nguo ya Christmas au Idd kwa watoto.

Pia Ray C amesema album yake inakuja hivi karibun

PICHA:HATIMAYE OMMY DIMPOZ KUFANYA COLABO NA RAY C WACHECK HAPA





Staa wa Ngoma ya Tupogo,Omary Nyembo,‘Ommy Dimpoz’na nguli wa muziki wa Bongo Fleva,Rehema Chalamila‘Ray C’wanatarajia kuachia ngoma yao? baada ya kupiga picha pamoja.Ommy Dimpoz alipost picha hicha hiyo kupitia mtandao wa instagram huku akiandika Studio Flowwww wit the Legendary her self ...Kiuno bila Mfupa...Huku mashabiki wao wakisema kuwa… haya madimpoziii poz na kiuno bila kidari..