Showing posts with label ney wa mitego. Show all posts
Showing posts with label ney wa mitego. Show all posts

Sunday, October 27, 2013

NEY WA MITEGO APIGWA MARUFUKU NA BASATA KUVAA “MLEGEZO........


 Ney wa Mitego

ney wa Mitego ni msanii wa Hip-Hop.Sifa yake kubwa aliyonayo ni pamoja na “kusema chochote”. Kwa lugha za mjini wanasema Ney anakuchana tu. Haogopi. Nyimbo zake mbili ambazo hivi sasa zinamuweka kwenye chati ni Muziki Gani alioshirikiana na Diamond pamoja na ule wa Salamu Zao.
Pamoja na kuwa msema chochote, Ney wa Mitego anayo pia sifa ya kuwa msanii mvaa mlegezo mkubwa. Kwako wewe msomaji ambaye yawezekana hujui mlegezo ni nini; ni hii style ya vijana wa siku hizi kuvaa suruali na kuzishusha kwa nyuma na kuacha chupi au boxers zao zikionekana. Mlegezo una historia ndefu na ambayo imeshazungumziwa mara nyingi katika vyombo mbalimbali vya habari.Historia yake inasemekana kuanzia nchini Marekani katika jela. Hiyo ni makala nyingine inayojitegemea.
Sasa inaelekea Ney Wa Mitego naye kapata mtu ambaye anaweza kumwambia chochote. Ni Baraza La Sanaa La Taifa(BASATA) ambao, kwa mujibu wake mwenyewe Ney wa Mitego na taarifa iliyoripotiwa katika vyombo mbalimbali vya habari, wamemwandikia barua wakimtaka kuacha mara moja tabia yake ya kuvaa mlegezo.BASATA, bila shaka, wanaona mlegezo wa Ney kama uchocheaji wa anguko la kimaadili miongoni mwa wasanii. Binafsi nimewahi kujiuliza maana halisi na uzuri wa fasheni hii ya mlegezo na sikupata jibu. Ningempata Ney ningemuuliza kwa undani zaidi kuhusu hili.
Wakati nikisubiri kwa hamu kuona jinsi Ney Wa Mitego atakavyotekeleza amri au ombi hilo la BASATA, nabaki na swali moja au mawili kichwani. Vipi wasanii wengine (ambao ni wengi tu) wanaovaa pia mlegezo BASATA litawaandikia pia barua?Na Je,BASATA watamfanya nini NEY endapo atakaidi agizo hilo?
Kisha lipo suala pana zaidi la maadili miongoni mwa wasanii nchini wakiwemo wale wa kike ambao pamoja na kutovaa mlegezo kama wa Ney,wao wana “mlegezo” wa nguo fupi kupita kiasi au zile zinazoacha asilimia 80-90 ya miili yao wazi. Sijui hili BASATA wanaliangaliaje. Kuna mengi.Tutaongea siku moja…

Friday, October 25, 2013

NEY WA MITEGO AWEKWA SERO KWA KOSA LA KUTUMIA SARE ZA POLISI

Rapper Ney Wa Mitego ameniambia kuwa hii picha hapo juu tukio hilo limetokea Jana wakati wana shoot video ya wimbo wake Unaofanya vizuri kwa sasa kwenye radio stations ' Salam Zao'.

Ney Wa Mitego Amesema ' Nikweli nilituwa sero jana baada ya raia wasio julikana kuleta fujo eneo la kazi yangu  kwasababu kulikuwa na waigizaji waliokuwa na sare za polisi. Watu hao sijuani nao na walijitambulisha kama askari na kutaka kujua kwanini natumia sare za polisi kwenye video yangu bila kibali. hicho ndio kitu kilichopelekea nikapelekwa polisi. 

Mitego ameendelea kusema kuwa baada ya kukaa sero kwa dakika kama 15 mkuu wa kituo alikuja na kusikiliza tatizo hilo na ndio aliachiwa huru baada ya kutoa maelezo kuhusu tukio hilo na sare hizo kuoneknaA uraiani. 


Ney aliwekwa sero Kwenye kituo cha polisi Urafiki kilichopo Manzese na wiki ijayo video hii itaonekana kwenye vituo vya televison Tanzania

Sunday, August 25, 2013

NAJIONA MWENYE FAHARI KUTONGOZWA NA NAY WA MITEGO"...NISHA


MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema hata kama msanii Nay wa Mitego akiwa na mpenzi mwigine kwa sasa lakini anajivunia kupendwa na kijana huyo kwani alihangaika sana kumpata.

Akizungumza na mwandishi wetu, Nisha alisema Nay alimfuatilia kwa kipindi kirefu na alimzungusha kama miaka miwili kabla hata hajawa staa. “Nikivuta ile picha ya kumdengulia kiasi kile mpaka kuamua kumkubali, naamini alinipenda tu na hata kama hakunipenda lakini najivunia kwamba alihangaika kunipata,” alisema Nisha.
Wawili hao walidumu katika uhusiano wa kimapenzi kwa miezi kadhaa kabla ya kuachana na kila mmoja akichukua hamsini zake.

Monday, August 12, 2013

NIKIFA SIHITAJI KAMATI YOYOTE YA KUENDESHA MSIBA WANGU" NEY WA MITEGO

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Ney wa Mitego, ameweka wazi kuwa ikitokea amefariki dunia hatohitaji kamati kwa ajili ya kuendesha mipango ya msiba wake, kwa kile anachodai kuwa kamati hizo zipo kwa ajili ya kuvuna pesa.

Hayo aliweka wazi baada kupokea ujumbe mfupi kwenye simu yake wenye vitisho uliotokana na mashairi alioimba kwenye single yake mpya ya 'Salaam zao' .

Ujumbe huo wa vitisho ambao umepokelewa na msanii huyo umekuja mara baada ya msanii huyo kuachia single yake hiyo ambapo moja ya mashahiri ni juu ya hela za rambirambi zilizopatikana katika msiba wa msanii Ngwear pamoja na Kanumba kushindwa kuwafikia walengwa.

Akizungumza na jarida la Maisha, mara baada ya kutuma ujumbe alioupokea wa vitisho kwenye ukurasa wake wa 'Instagram', Ney wa Mitego aliweka wazi kuwa amepokea ujumbe wa vitisho mara baada ya kuachia nyimbo hiyo.

Alisema kuwa amepokea ujumbe mbalimbali ambazo zipo zinazowataja wahusika moja kwa moja wale waliohusika kula rambirambi, huku wengine wakimtumia ujumbe wa kumtisha kwa kile alichokiimba katika nyimbo hiyo.

"Mimi hata ikitokea nakufa leo sihitaji mtu yeyote wa  kuweka  kamati ya mazishi yangu kwani najua kitakachotokea siyo mazishi bali ni kula hela na rambirambi hizo kushindwa kutimiza malengo kama yalivyokusudiwa" alisema Ney wa Mitego.

Aliongezea kuwa hawezi kuacha kuimba ukweli hata kama ataendelea kupokea vitisho.

Tuesday, July 23, 2013

NAY WA MITEGO ATANGAZA KUMPIGIA KAMPENI LOWASA KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA 2015..!!



aya  ni  mashairi  aliyoyaandika Nay wa  mitego  kwenda  kwa  mtoto  wa  Rais  a.k.a Riz One  akimtaka  amwambie  baba  yake  kuwa  mtwara  hawataki  korosho, wanataka   gesi  na  pia Lowassa  asiache  kugombea  urais  maana  yupo  tayari  kumpigia  kampeni-2015
----------------
MASHAIRI YAKE:
Naongea na Riz one hey Riz One, we si mtoto wa raisi Riz one. Mwambie dingi yako Masela hawamuelewi wamakonde wa Mtwara hawataki tena Korosho, wanaitaka ges si mtawaua na mkong'oto?! Nani rafiki wa Lowasa anifikishie salam 2015 nataka agombee uraisi nitamfanyia kampeni wananchi wampe nafasi, 
# Salam zao# 
my new track coming soon.!!