Showing posts with label lulu. Show all posts
Showing posts with label lulu. Show all posts

Wednesday, August 27, 2014

GARI JIPYA LA LULU LAIBUA MAKUBWA NA MAZITO ...PATA STORY KAMILI HAPA

MAKUBWA! Mambo yamekuwa mambo, kadi ya gari jipya la staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ imeibua mazito kufuatia Jeshi la Polisi Dar es Salaam kubaini kuwa namba ya Sanduku La Posta (SLP) iliyoandikwa kwenye kadi hiyo ni Wizara ya Mambo ya Ndani Tanzania. 
Gari ya staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ aina ya Toyota Rav 4 New Model
 IMEVUJAJE?!
Hilo lilibainika baada ya gazeti dada na hili, Ijumaa toleo la Ijumaa iliyopita kuandika habari yenye kichwa kisemacho; LULU AANDIKA HISTORIA. 


Katika habari hiyo, Lulu alipewa shavu kwa vile alinunua gari aina ya Toyota Rav 4 New Model kwa pesa zake mwenyewe tofauti na baadhi ya mastaa wa Bongo ambao huhongwa magari na wanaume. 

SIMU YAPIGWA
Wakati gazeti hilo likiwa mitaani, mtu mmoja aliyedai kuwa ni afisa wa jeshi la polisi jijini Dar es Salaam alipiga simu kwenye chumba cha habari cha Global Publishers na kusema kuwa S.L.P ya 9140 iliyotumika kwenye kadi ya gari la Lulu ni ya jeshi hilo. 

NI KOSA LA JINAI

Ofisa huyo aliliambia gazeti hili kuwa raia wa kawaida haruhusiwi kutumia sanduku la barua la jeshi kitu alichodai kinaonesha jinai ilifanyika wakati wa usajili ya gari hilo.
“Haiwezekani Lulu atumie Postal Office Box (P.O.Box au S.L.P) ya jeshi kwenye kadi ya gari lake ikizingatiwa kuwa yeye ni raia wa kawaida.
 
'Lulu’ akipozi.
 “Ukiachana na hilo hata sisi maofisa wa jeshi la polisi hatuwezi kuitumia hiyo anuani kwa shughuli zetu binafsi labda kuwe na kibali maalum,” alisema afisa huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa vile yeye si msemaji wa jeshi hilo. 

LULU ANASEMAJE?
Baada ya kupata maelezo hayo, gazeti hili lilimtafuta Lulu ili kujibu madai hayo yenye utata ambapo alisema kuna mtu alimtengenezea namba yake ya TIN (Taxpayer Identification Number) ndiye aliyemwekea anuani hiyo bila yeye kujua. 

Huku akisita kumtaja kwa jina mtu huyo lakini akimtaja kwa cheo ambacho kiko wazi na mapaparazi wetu wakamjua, Lulu alifunguka hivi: 
“Namiliki gari langu kihalali kabisa na nina kila kitu, niko tayari kwenda kokote kuonesha uhalali wa umiliki wangu. Kuhusu hiyo anuani, mtu aliyenitengenezea TIN Number ili nipate leseni ya udereva ndiye aliyetumia hiyo anuani, mimi sijui chochote jamani.” 

AOMBA AHIFADHIWE SIRI

Katika hali ya kushangaza, Lulu aliwaambia mapaparazi wetu wasimtaje jina gazetini mtu huyo aliyemsajilia TIN akisema asitiriwe siri yake.
 
Kadi ya gari la ‘Lulu’ yenye anuani za jeshi la Polisi (S.L.P ya 9140).
 POLISI NAO WANENA
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, ambako ndiko usajili wa gari hili ulifanyika katika ofisi za TRA, Zakaria Sebastian, alisema jeshi lake halina taarifa za kuwepo kwa jambo hilo lakini watalifuatilia kwa karibu. 


“Huenda ni mke wa askari au mwanafamilia. Unajua kuna baadhi ya maofisa wana msamaha, huenda alitumia hivyo, lakini tutafuatilia,” alisema kamanda huyo ambaye alielezwa kuwa, Lulu hajawahi kuwa mke wala mwanafamilia ya mwajiriwa wa jeshi la polisi. 

“Kama hajawahi kuwa mwenye kustahili kutumia anuani hii, basi tutafuatilia ili kujua wakati akiitumia, je alikuwa anakusudia kufanya jinai? Tukijiridhisha hivyo bila shaka sheria itafuata mkondo wake.” 

UCHUNGUZI WA RISASI MCHANGANYIKO
Katika uchunguzi wa gazeti hili, anuani hiyo imeshatumika na Jeshi la Polisi Magomeni na Mkoa wa Polisi wa Ilala jijini Dar. Namba hiyo inatofautiana tarakimu moja na ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam

Tuesday, February 18, 2014

LULU ATIKISA MAHAKAMANI, KESI YAKE YAAHIRISHWA MASHABIKI WAMSHAURI KUACHA MBWEMBWE MJINI ATULIE KWANZA KUSIKILIZIA KESI

Lulu, Dr.Cheni na mama mzazi wa Lulu wakipitia gazeti wakati wakisubiri kuanza kwa kesi

Lulu akiwa na mama yake mzazi

Lulu akiwa na Dr.Cheni
Dr.Cheni na mama yake Lulu



Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabiri muigizaji wa kike, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu imesikilizwa leo (February 17) katika mahakama kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Lulu alikiri mbele ya Jaji Rose Temba kuwa alikuwa na uhusiano wa mapenzi na marehemu Steven Kanumba na kwamba walikuwa na ugomvi, lakini alikana mashitaka ya kumuua bila kukusudia.
Mbali na kukiri kuwa na uhusianano wa mapenzi, muigizaji huyo pia alikiri kuwa baada ya tukio hilo alitoka nje ya chumba walichokuwepo na kwenda kumwambia mdogo wake marehemu Kanumba, Setti Bosco kuwa Kanumba ametangulia mbele ya haki.
Akisoma hati ya mashitaka, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Monica Mbogo, alidai kuwa Aprili 7, mwaka 2012, Sinza Vatikani, Mkoa wa Dar es salaam, mshitakiwa alimuua bila kukusudia Stevin Kanumba.
Wakili Kombo, alidai kuwa pamoja na mambo mengine, marehemu Kanumba baada ya kufa, mwili wake ilipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo majibu yanaonyesha kwamba kifo chake kimesababishwa na uvimbe ndani ya ubongo.
 Upande wa serikali una mashahidi watano pamoja na vielelezo wakati upande wa utetezi pia unatarajia kuwa na mashahidi watano na vielelezo.

 

Friday, December 13, 2013

Lulu na Young D wakutwa “wakivunja amri ya 6”ndani ya gari ya LULU Usiku mzito wa manane...!!!

HATARI! “ETI” Lulu na Young D wakutwa “waki-nanii amri ya 3+3 ” ndani ya gari ya LULU Usiku mzito wa manane
HATARI! “ETI” Lulu na Young D wakutwa “waki-nanii amri ya 3+3 ” ndani ya gari ya LULU Usiku mzito wa manane

Jana kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha clouds FM chini ya bwana Sudi Brown ama Gossip Cop kulikuwa na FUNUNU kali iliyokuwa inamuhusu mwanadada wa bongomovies Elizabeth Bin Michael a.k.a LULU na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Young D al-maarufu kama Young Dar es salaam kama mwenyewe anavyojiita ya wawili hao kukutwa kwenye gari wakifanya lile tendo linaloruhusiwa kufanywa mara baada ya mdada na mkaka kufunga ndoa.
Kwa mujibu wa Sudi Brown = Gossip cop, wawili hao walikutwa maeneo ya Mbezi beach ndani ya gari aina ya Hyundai ya mwanadada lulu na polisi wa doria wakivunja amri hiyo iliyokatazwa na vitabu vyote vitakatifu kwa maana ya biblia, Quran na vitabu vingine vya dini ulimwenguni.
Habri zainasema Baada ya wawili hao kukutwa eneo hilo na polisi walipelekwa pembeni gizani na kuongeana polisi kabla ya wao kutokomea wasipojulikana na gari hilo.
Alipopigiwa simu mwanadada LULU alipokea na kukata muda mfupi na baadaye Young D alipopigiwa simu alitoa majina ya utata kama alivyoongea mwenyewe kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha clouds fm. MSIKILIZE MWENYEWE HAPA

Monday, December 2, 2013

LULU Awahamasisha vijana juu ya Upimaji wa Virusi vya Ukimwi..


Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael aka Lulu amesema vijana wanatakiwa wawe mstari wa mbele katika kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
 
Akizungumza na mwandishi wetu jana katika usiku wa Red Ribbon Fashion Galla iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam, Lulu alisema siku ya Ukimwi duniani inatukumbusha kuangalia tumetoka wapi na tunakwenda wapi na kuangalia wangapi wamepoteza maisha kwaajili ya gonjwa la Ukimwi.
 
Najumuika na Watanzania leo ,siku ya Ukimwi duniani ambayo hufanyika kila mwaka, kwa kuangalia wangapi wamepoteza maisha, pamoja na kuwahamasisha zaidi vijana Wakitanzania kutumia kinga ili kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi ambavyo vinapoteza nguvu ya Taifa,” alisema Lulu.
 
Pia Lulu alisema amekuwa akipima Ukimwi mara kwa mara ili kuangalia afya yake,huku akiwashauri vijana kwenda kupima ili kujua afya zao.
 
“Nimekuwa nikipima HIV kila mara katika hatua za maisha yangu,kuangalia kuhakikisha najiweka katika usalama wa afya yangu,pamoja na kupanga matarajio ya maisha.Sio kuwa ukipima ukagundulikana una HIV utashindwa kupanga malengo yako hapana! ukipata ushauri nasaha, ukajua uishi vipi kwa kuboresha afya yako, maisha yataendelea kama kawaida. Kwahiyo kinachotakiwa vijana ni kujua afya zetu mapema

Wednesday, November 27, 2013

PICHA:HUU NDIO MUONEKANO MPYA WA MWANADADA "ELIZABETH MICHAEL" A.K.A LULU

You simply look beautiful Lulu

Saturday, November 23, 2013

Siwezi kumvulia Diamond Chupi yangu...Hana hadhi ya kutembea na mimi Kabisa"....LULU

Msanii wa filamu bongo,na mwenye jina kubwa kuliko umri wake,Elizabeth Michael aka LULU, ameonesha msimamo mkali baada ya msanii wa bongo fleva mwenye jina la madini expensive Naseeb Mohamed au DIAMOND kufanya kila aina ya mbinu ikiwemo ile ya kutaka kumuagizia msanii huyo gari expensive aina ya nissan murrano yenye thamani ya shiling million zaidi ya 60,ambapo hata hivyo mbinu yake iyo imeonekana kugonga mwamba baaada ya Lulu kukataa kata kata kutoka na staa huyo anayetamba na ngoma ya my number one.

Kwa kumaanisha kuwa hataki kutoka na staa huyo, Lulu alilazimika kubadilisha namba ya simu yake ya mkononi ili kuepuka usumbufu kutoka kwa bwana mdogo huyo ambaye kila kukicha amekuwa akiwindwa na wasichana warembo ili tu waonje sukari yake.

Pia inasemekana lengo la diamond kutaka kutoka na Lulu ni kutaka kukuza jina lake(kiki) kwa kuwa anaamini staa huyo ana jina kubwa na lenye mvuto hivyo kumfanya na yeye aogelee kwenye dimbwi la umaarufu na kuongelewa zaidi na watu,na kuwa ishu iyo ndo itakuwa habari ya mujini yaan yeye kutoka na lulu.

Baadhi ya watu wameonyesha kushangzwa sana na msimamo mkali wa binti huyo,kwa kuwa waliamini hakuna staa yeyote bongo mwenye ubavu wa kupindua kwa diamond,kama ilivyokuwa kwa Wema,Jokate,Aunt,Wolper na baadhi ya mastaa ambao dogo huyo aliwamega kiulaini.

Watu wanahaha kumjua mwanaume anayempa jeuri Lulu hadi kufikia hatua ya kuchomoa kwa diamond.

Tuesday, November 19, 2013

HIZI NDIZO TWETTS ZA" LULU MICHAEL" AKIMTONGOZA JUSTIN BIEBER....!!!


Kupitia  ukurasa  wake  wa  twitter, Lulu  Michael  amekuwa  akieleza  jinsi  anavyokosa  usingizi  kwa  sababu  ya dume  hilo,  hali  inayomfanya  akonde  na  kukongoroka.
 


Pamoja  na  maneno  mazuri  ya  kumtongoza  mwanaume  huyo, tweet  za  Lulu  zimeonekana  kutokuwa  na  msaada  wowote  kwake  kutokana  na  ukweli  kuwa  Justine  Bieber  ni  mtu  ambaye  hajui  kiswahili...

Mbali  na  kutoijua  lugha  ya  kiswahili, Bieber  ni  mtu  mwenye  followers  wengi  sana  (  47,180,637   followers ), hivyo  ni  ngumu  sana  kutambua  kwamba  kuna  mtu  anayeitwa  Lulu  Michael.



Zikiwa  zimepita  wiki  kadhaa  tangu  Johari  atimkie Canada  kumfuata  mpenzi  wake, Lulu  Michael  naye  ameanza  kujipendekeza  kwa  msanii  Maarufu  Justine  Bieber   kiasi  cha  kudiriki  kumtongoza  mtandaoni.

Friday, November 15, 2013

Lulu kuweka taarifa za filamu zake kwenye simu



Mwigizaji Bora wa Kike kwa mujibu wa tuzo za Tamasha la Majahazi la mwaka huu, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu,  amesema anatarajia kuanza kutoa taarifa zote zinazohusiana na filamu zake kupitia simu za mkononi.
Akizungumza na Mwananchi jana Lulu alisema taarifa hizo zitapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini. “Shabiki wangu pia anaweza kuangalia filamu zangu kupitia mitandao ya kijamii yaani Tigo, Zantel, Vodacom na Airtel. Bado haijawa rasmi hivyo nitakapozindua ndipo nitakapotoa mwongozo halisi,” alisema Lulu.
Kwa mujibu wa Lulu bado hajajua ni lini bidhaa yake hiyo itaanza kurushwa hewani ila kwa sasa yupo katika mazungumzo ya mwisho na wadau wa mitandao ya simu za mikononi.
“Hii ni moja ya mafanikio katika tasnia ya filamu hivyo siwezi nikasema ni lini mpango huu utaanza kurushwa hewani na mashabiki kupata huduma hii, ila natarajia kesho (leo) nitaweza kutoa taarifa rasmi ni lini sasa mashabiki waanze kujiunga na huduma hii.”
Miezi michache iliyopita Lulu alizindua filamu yake mpya Foolish Age katika ukumbi wa Mlimani City, filamu inayofanya vizuri sokoni kwa hivi sasa. Hata hivyo Lulu ni kati ya hazina na vipaji vilivyokuzwa tangu utotoni ambapo anaonyesha kuliteka soko kwa sasa na huenda anaweza kuwapiku wasanii wakubwa wa kike hapo baadaye.

Wednesday, November 6, 2013

LULU AKANUSHA HABARI KUWA AMECHUMBIWA.

Star mkubwa wa filamu Swahiliwood Elizabeth Michael(Lulu)
 amekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la udaku "Filamu" kuwa amechumbiwa. Lulu alisema hajachumbiwa na haelewi habari hizo zimetoka wapi " mimi sijachumbiwa na hakuna mtu yeyote aliyenichumbia na kama ikatokea siku nikachumbiwa kila mtu atajua na mimi mwenyewe ndiye nitakayesema" alisema Lulu akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds fm.

Star huyo aliyejipatia umaarufu tangu akiwa mdogo aliongeza kwa kusema "lakini sasa sijajua wao wamepata hiyo habari kutoka kwenye chanzo gani, by the way kumekuwa na habari kila kukicha kila mtu anayejisikia kuandika anaandika, anaamka anaandika kwa hiyo leo wameandika nimechumbiwa kesho wataandika nimeolewa, kwa hiyo inategemea na mood ambayo wao waliamka nayo kwamba leo Lulu tumchumbie, tumuozeshe, tumuachishe i don't know"

Lulu Alimalizia kwa kusema "kuchumbiwa, kuolewa, kuwa mke ni vitu ambavyo tumeumbiwa binadamu, vipo kama ukiwa mpango wa mwenyezi Mungu nitachumbiwa na nitaolewa"

                                                                    Lulu

Friday, November 1, 2013

LULU ATOA MSAADA WA PESA HOSPITALI YA OCEAN ROAD.

 

Actress Elizabeth Michael(Lulu) ametoa msaada wa pesa katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam ili ziwasaidie wagonjwa wa kansa. Haijajulikana star huyo wa filamu ametoa kiasi gani na aliambatana na mama yake mzazi katika hospitali hiyo. Kupitia Instagram Lulu ameandika "naamini mimi sio mwema sana mpaka Mungu akaniwezesha kuona mwezi huu nikiwa mzima na mwenye afya. Kwa kutambua hilo nimeanza mwezi huu kwa kupita katika hospitali ya Ocean Road na kutoa mchango ili kuwasaidia wagonjwa wa cancer na tuwe na utaratibu wa kuwakumbuka wahitaji kwa chochote tulichonacho"
Mungu awe upande wako na akuzidishie zaidi Lulu

Lulu akiwa na mama yake mzazi akitoa msaada wa pesa katika hopspitali ya Ocean Road...

Wednesday, October 30, 2013

LULU AFURUMUSHA MVUA YA MATUSI KATIKA MSIBA WA BABA YAKE WEMA SEPETU



MSANII nyota wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amejikuta akiporomosha mitusi mizito ya nguoni kwenye msiba wa baba wa Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, mzee Isaac Abraham Sepetu hali iliyowafanya baadhi ya waombolezaji kumkodolea macho ya mshangao.
 
 Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa msibani kwa marehemu Balozi Sepetu.
Tukio hilo lililotawaliwa na hasira lilijiri Oktoba 28, 2013 kwenye msiba huo uliokuwa ukiombolezwa nyumbani kwa marehemu, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.
KISA NA MKASA
Ilikuwa wakati Lulu akitinga msibani hapo, ghafla alimfuata mmoja wa waandishi wa habari hii na kuanza kumporomoshea matusi hayo kwa kile alichodai kukerwa na habari iliyowahi kuandikwa juu ya kitendo chake cha kula chakula sahani tatu katika hafla moja iliyofanyika hivi karibuni huko Kunduchi Beach Hotel, Dar.

TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Katika tukio hilo la awali, Lulu alikuwa mmoja wa waalikwa wa harambee ya kuchangia kansa ya matiti kwa akina mama iliyofanyika kwenye hoteli hiyo.

Wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya wachangiaji wote, Lulu alionekana akirudia kuchukua msosi kwa zaidi ya mara tatu (alikula sahani tatu).
TURUDI MSIBANI
Baadhi ya watu waliokuwa msibani hapo walimshangaa Lulu kwa kuporomosha matusi hayo ya nguoni wakati akijua kuwa yeye ni kioo cha jamii na baadhi ya maneno machafu aliyoyatamka hadharani hayaandikiki gazetini wala mtandaoni.

MSIKILIZE LULU
“Siwapendi nyinyi waandishi hasa wewe (akamtaja jina). ‘I don’t want your f**** story dude, go to hell with you’re f**** shit,” alisikika Lulu akitamka matusi hayo. (hatuwezi kuyatafsiri kwa sababu za kimaadili).

WAOMBOLEZAJI SASA
Mamia ya waombolezaji waliokuwepo eneo la msiba huo walionesha kushangazwa na kitendo cha binti huyo aliyejipatia umaarufu kutokana na kuigiza kwake.

Baadhi yao walidai hali hiyo haikuwa ya kawaida na huenda alikuwa ‘amepata kiburudisho’ (alikunywa pombe).
“Sasa binti si uende ndani ukakae? Hapa ni msibani halafu wewe unasema maneno kama hayo, huoni kama unasumbua akili za wenzako?” mzee mmoja alisikika akisema wakati Lulu anaondoka.

“Unajua hawa mastaa wa Bongo mimi nimeshawajua kwani nawafuatilia sana, wakiandikwa kwa mazuri meno thelathini na mbili nje, wakiandikwa kwa mabaya timbwili kama hili.
“Hiyo habari anayoilalamikia mimi niliiona kwenye gazeti tena ilikuwa na picha sasa alichokereka ni nini, si kweli au?” alisikika mwombolezaji mwingine.
Mwombolezaji mwingine alisema Lulu anaweza kuwa na hoja lakini inakufa kwa vile kama habari ilimkera alipaswa kumtafuta paparazi huyo kwa wakati wake au afike Ofisi za Global badala ya kujianika hadharani huku akidai siku hizi amebadilika.
KWA NINI ALIKEREKA?
Habari zilizopatikana baadaye zilisema kuwa, Lulu alihamaki kumwona mwandishi huyo aliyeandika habari zake hizo za kula sahani tatu, kwani tangu kutoka kwa stori hiyo amekuwa akitaniwa na mastaa wenzake wakimwambia ‘yeye ni mbaya sana kwenye mechi za ugenini’.
Tafsiri hiyo ni kwamba, Lulu amekuwa akila kupitia kiasi kwenye ‘minuso’ (minuso ni vyakula vya bure kwenye shughuli).

AJITENGA NA BONGO MOVIE
Wakati huohuo, Imelda Mtema anaripoti kuwa, baada ya kufika ndani ya nyumba ya akina Wema, Lulu alionekana kutotaka kujihusisha na baadhi ya wasanii wenzake wa Klabu ya Bongo Movie Unity ambapo alijitenga.

Lulu alijitenga kwa kukaa na mama yake mzazi, Lucresia Karugila na mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
Wasanii wa Bongo Movie waliokuwepo ambao hawakupata nafasi ya kupiga stori na Lulu kama zamani ni Jacqueline Wolper, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Jennifer Kyaka ‘Odama’,  Rachel Haule, Kajala Masanja na Eshe Buheti.   

Baadhi ya waombolezaji waliokuwemo walinong’ona kuhusu kitendo cha staa huyo kujitenga wakidai kweli sasa amekua.
 “Mh! Lulu sasa amekua jamani, naona hataki kabisa ushoga na watu, alipofika akasalimia na kwenda kukaa na wazazi wake, ni maajabu,” alisikika akisema mmoja wa waombolezaji ambaye jina lake halikufahamika.

Mwombolezaji mwingine alisikika akisema kuwa mabadiliko yote yanayoonekana kwa Lulu kwa sasa ni kazi ya mama Kanumba.
TUJIKUMBUSHE
Mzee Isaac Sepetu alifariki dunia Oktoba 28, 2013 katika Hospitali ya TMJ, Dar alikokuwa amelazwa kwa matatizo ya kisukari.

MAZISHI YA MZEE SEPETU
Mwili wa marehemu ulitarajiwa kuzikwa jana saa kumi jioni Mjini Zanzibar baada ya kusafirishwa kutoka jijini Dar es Salaam alikofia.
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina

Monday, October 21, 2013

KAMA ULIKOSA KUCHECK MAHOJIANO YA "LULU" KWENYE MKASI..., ANGALIA HAPA




 CHECK HAPO CHINI



Saturday, October 19, 2013

LULU DUA ZANGU ZIKO PAMOJA NA MZEE NGUZA,PAPII KOCHA


“Ninaamini Mungu yupo...anasikia,anaona na ndiye mwenye kuhukumu kwa Haki...!!!!Dua zangu ziko pamoja na Mzee Nguza na Papii Kocha...!hakuna linaloshindikana mbele ya Mwenyezi Mungu...Kama anaweza kutoa Jaribu basi yeye pia ndo mwenye Uwezo wa kufanya Njia ya kutoka ktk jaribu Hilo...!Mwenyezi Mungu awasimamie katika rufaa yenu...!AMEN”
Hayo ni maneno ya mwanadada Elizabeth Michael (LULU) aliyoyaandika kupitia kwenye mtandao akiwaombea kheri Mzee Nguza na mwanawe Papii Kocha wanaosubiria kusikilizwa kwa rufaa yao ya kesi ya ulawiti inayowakabili

Toka atoke jela, mwanadada lulu ameonekana kubadilika sana kitabia tofauti na alivyokuwa akionekana hapo awali.

Thursday, October 17, 2013

LULU AKATAA KUOLEWA ...

STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekataa kabisa suala la kuolewa kwa sasa akidai moyo wake haupo tayari kwa tendo hilo.
Lulu alifunguka hayo Jumatatu iliyopita katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa kupitia Runinga ya East Africa ambacho humpa nafasi staa kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu maisha yake na sanaa kwa jumla.
Wakati mahojiano hayo yakiendelea, mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho anayefahamika kwa jina la Muba, alimtupia Lulu swali ambalo lilimtaka aeleze utayari wake endapo mtu akijitokeza na kutaka kumuoa.
“Sitaki kuolewa kwa sasa, muda wa kuolewa haujafikia. Ukifika nitafanya hivyo lakini kwa sasa sipo tayari kuolewa,” alisema Lulu.
Aidha, Lulu alikiri kuwa licha ya kutokuwa tayari kuolewa lakini amekuwa akipata usumbufu mkubwa wa kutongozwa na wanaume. Aliainisha kuwa alikuwa akitongozwa kabla na baada ya kutoka Segerea alipokuwa akishikiliwa kwa kesi ya kifo cha aliyekuwa mpenzi wake, marehemu Steven Kanumba.

“Watu wananitongoza sana, walikuwa wakifanya hivyo kabla hata sijaingia China (gerezani Segerea) na wameendelea kufanya hivyo hata baada ya kutoka,” alisema Lulu na kuongeza:
“Siwezi kuwakubalia sababu sipo tayari kuolewa kwa sasa…muda wa kufanya hivyo haujafika.”
Kuhusu suala la kudaiwa kutembea na bosi wa Kampuni ya Proin Promotion ambayo inamsimamia kisanii kwa sasa, Lulu aliruka viunzi na kudai taasisi hiyo inamlea kama mtoto wa familia na siyo vinginevyo.
Alisema hata madai yanayoelekezwa kwake kuwa Proin wamempa gari na nyumba kama sehemu ya kuhongwa na bosi wa kampuni hiyo, hayana ukweli wowote kwani yeye anafanya kazi kama msanii chini ya kampuni hiyo na hakuna kitu cha ziada.
“Hahahaha! Salama (mtangazaji) acha mambo yako bwana… mimi nipo chini ya Proin kwa sasa kwa kipindi flani ambacho nimesaini nao mkataba. Wananilea kama msanii wao, hakuna cha ziada,” alisema Lulu.
Akiendelea kubwabwaja maneno ndani ya kipindi hicho, Lulu aliweka wazi kuwa alikuwa akishindwa kuanika penzi lake na marehemu Kanumba kwa kuwa muda muafaka ulikuwa haujafika na kudai waliishi kama mtu na baba yake kabla hawajawa wapenzi, wakawa wapenzi na mauti yakamkuta Kanumba kabla hawajalianika penzi lao.

Thursday, September 12, 2013

LULU APATA VITISHO

Elizabeth Michael ‘Lulu’.

KUFANIKIWA kwa uzinduzi wa filamu ya Foolish Age ya msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, kumemfanya kinda huyo anayetingisha katika tasnia hiyo kupata vitisho kutoka kwa mastaa wenzake.
Habari kutoka vyanzo mbalimbali ndani ya fani hiyo zinasema katika uzinduzi huo, msanii huyo alifunika na kuonyesha dalili zote za kuwazima mastaa wenzake ambao kwa muda mrefu wamekuwa juu.
Taarifa hizo zinasema staa huyo wa Bongo Muvi anatafutwa kwa kila namna, usiku na mchana ili kuhakikisha nyota yake inafifia.
Madai hayo yamekuja zaidi baada ya uzinduzi huo kufana kwani pamoja na mambo mengine, hata jinsi alivyokuwa amejipanga kwa walinzi wake, lilikuwa ni jambo kubwa ambalo linafanana na inavyotokea katika shughuli za mastaa mbalimbali wa majuu.
Mwandishi wa gazeti hili aliamua kufunga safari hadi maskani kwao pande za Tegeta, lakini msanii huyo hakupenda paparazi afike kwao hivyo mazungumzo yao kufanyika kama ifuatavyo kwa njia ya simu ya kiganjani.
Mwandishi: Mambo vipi Lulu?
Lulu: Salama tuu za kwako?
Mwandishi: Salama, vipi umesikia vitisho vyako kutoka kwa mastaa wa Bongo Muvi wanaodai kuwa umekuja kuwapita kisanii?
Lulu: Hapana sijasiki, lakini kama wanatoa vitisho lazima wakubaliane na ukweli kwamba lazima awepo wa kwanza na wa mwisho, wakaze buti.
Mwandishi: Umejipangaje kukabiliana na hilo?
Lulu: Najipanga kufanya kazi mimi kama mimi na wao wafanye kama wao, wakijifanya kuwa kama mimi haiwezi kuwa hivyo, mbona mastaa wa ughaibuni kama Beyonce na Rihanna wako tofauti? Lazima awepo wa kwanza mpaka wa 10 hatuwezi kulingana.
Mwandishi: Kuna lolote la kuongeza juu ya hilo ama wito kwa wasanii?
Lulu: Wajipange kufanya kazi kwa nguvu zote, wasifanye kama mimi wafanye kama wao,
Mwandishi: Asante Lulu nakutakia siku njema
Lulu: Ok, sawa kazi njema.

Tuesday, September 10, 2013

LULU MICHAEL NA RAY WAULA WACHAGULIWA KUWA MABALOZI

Waigizaji Elizabeth Michael (LULU) na Vicenti Kigosi (Ray) wamechaguliwa kuwa mabalozi wa wasanii wenzao katika tamasha la filamu la Dar filamu Festival litakalofanyika kuanzia tarehe 24 – 26. Katika press Release iliyotolewa na kampuni inayoandaa tamasha hilo imesema kuwa pamoja na mambo mengi, tamasha hilolitatoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa Filamu Tanzania.



Soma press Release hiyo hapo chini.



Kampuni ya Haak Neel Production kwa kushirikiana na mtandao wa habari za filamu wa filamucentral inapenda kutambulisha kwenu Tamasha la filamu linaloitwa Dar Filamu Festival (DFF) 2013 litalofanyika katika uwanja wa CoICT- UDSM- Posta Kijitonyama, kuanzia tarehe 24- hadi 26, September,2013 Tamasha litaambatana utoaji wa Semina kwa wadau wa filamu, kuonesha filamu za kitanzania kwa watu wote bure kwa siku tatu.Kutakua na filamu nne kwa siku kuanzia saa kumi na mbili jioni mpaka saa tano usiku.



Tamasha hilo limelenga kutoa hamasa kwa watanzania kuziona filamu za kitanzania na zile zinazotumia Lugha ya Kiswahili pekee ili kutoa fursa ya ajili kwa vijana na jamii husika kwa ujumla, filamu zitakazoonyeshwa ni zile zinazotengenezwa na hapa nchini katika kutangaza Lugha yetu nzuri ya Kiswahili kupitia kazi zao ikiwa kampeni ya filamucentral kuitangaza lugha hiyo na kuwa ni bidhaa muhimu Ulimwenguni.

Kwa tamasha hili la awali tutaonyesha filamu za hapa Tanzania pekee ikiwa ni utambulisho wa Dar Filamu Festival kwa mara ya kwanza kwenu wanahabari, miaka ijayo Tamasha litahakikisha linashirikisha filamu kutoka sehemu mbalimbali zinazotumia Lugha ya Kiswahili kutoka popote Ulimwenguni.

Akiongea na Waandishi wa Habari mratibu wa Tamasha hilo Staford Kihore pia amesema kuwa katika kuzingatia maendeleo ya tasnia ya filamu siku tatu hizo kila siku imepewa jina kwa filamu zitakazoonyeshwa Tarehe 24th September, 2013 siku ya Jumanne ambayo ndio siku ya ufunguzi utakuwa ni usiku wa Bongo Movie Classics, 25th September, 2013 ni usiku wa Quality Nights.

Na ile siku ya mwisho tarehe 26th September, 2013 itakuwa ni Stars Nights siku ambayo kutakuwa na wasanii wetu mbalimbali ambao wanajenga soko hilo la Bongo movie filamu, Tamasha hili linapambwa na wasanii wote wakiwakilishwa na wasanii wenzao wawili ambao ni Vincent Kigosi ‘Ray’ kama Official Producer and Director for DFF 2013 na Elizabeth Michael ‘Lulu’ kama Official Actress for DFF 2013.

Pia tamasha litaambatana na utoaji wa semina kwa wadau wa filamu kwa asubuhi ambapo madarasa yataendeshwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sanaa tarehe 24 September, 2013 masomo ya Uandishi wa Muswada, Uigizaji na Uongozaji wa filamu yatafundishwa kwa washiriki, 25th September 2013 Siku nzima Makapuni ya Utengenezaji filamu yataonyesha na kutangaza kazi zao kwa wadau mbaliambali.

Tarehe 26th September 2013 ni siku muhimu sana kwani Taasisi kama vile TRA, Bodi ya Ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza, Wasambazaji wa filamu na taasisi nyingine watakutana katika jukwaa la majadiliano kuhusu mustakabali wa tasnia ya filamu, pia filamu kadhaa zitaonyeshwa na kujadiliwa na wadau watakaokuwepo matukio yote ya asubuhi yatafanyika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Idara ya Sanaa.

Pia tunatoa shukrani kwa taasisi za Serikali kutuunga mkono katika ufanikishaji wa tamasha hilli la Dar Filamu Festival (DFF) 2013, taasisi kama Bodi ya Filamu na ukaguzi wa michezo ya kuigiza Tanzania, Fine Perfoming Art – Udsm, Tanzania Film Federation (TAFF), MFDI, Swahiliwood na makapuni ya usambazaji wa filamu Steps Entertainment Ltd, Leo Media na kampuni mpya ya usambazaji ya Proin Promotion ambayo imeanza hivi karibuni na kuonyesha dhamira ya kusaidia tasnia ya filamu, pia leo tunazindua mtandao wa www.dff.or.tz

Kwa kutambua mchango wako kama mwanahabari tunaamini utaungana nasi katika kuhakikisha DFF inakuwa ni chachu ya maendeleo ya tasnia ya filamu Tanzania, huku tukisema kuwa Dar Filamu Festival2013 kwa kauli mbiuya ‘Ubora wa Filamu Zetu’ ikiwa ni njia ya kuwakutanisha wadau wote kwa pamoja na kuwa jukwaa linalojenga tasnia ya filamu inayokua kila siku. Pia tunaomba ushiriki wako katika kufanikisha hili.



Imetolewa na Mratibu wa Tamasha la DFF 2013 Staford Kihor

Monday, September 9, 2013

PENNY ATOA ONYO "MSICHANA ATAKAE MGUSA DIAMOND ATAJUA MIMI MTOTO WA KITANGA"

    Penny,Lulu na Wema enzi za mahusiano yao.


Mtangazaji nyota nchini ambae ni mchumba wa kupika na kupakua wa mwanamuziki Diamond Penny amevunja ukimya na kutoa onyo kali kwa wasanii wa kike na wasio wasanii kumlaia mbali baby boy wake Diamond.

Habari za uhakika toka kwa mtu wa karibu na Penny anaeishi nae maeneo ya Mwananyamala ambae pia aliomba hifadhi ya jina lake alisema “ Jamani Penny amejipanga kuolewa na Diamond kwani sasa hivi amecharuka na kutoa onyo kali kwa mwanamke yeyote atakae msogelea mchumbaake huyo la sivyo ataroka mtu” Alisema dada huyo ambae anafanyakazi nyumba ya jirani na anapoishi Penny

Penny amepiga mkwara huo hasa akimlenga zaidi msanii Lulu na Linah nk huku akitahadharisha kuwa anawaomba wote wenye tabia ya kuchukua wanaume za watu kwani yeye katika maisha yake hajawahi kuchukua mume wa mtu hivyo kama akihisi kuna ajenda yoyote ya siri kati ya mchumbaake na wasanii hao hakika ataroga mtu kwani yeye ni mtoto Mdigo halisi.

Aidha chanzo hicho kiliongeza kusema kuwa penzi la Penny na Diamond limefikia pazuri kiasi cha familia zao kutembelea na kula pamoja kama wakwe. Hata hivyo ilielezwa kuwa Familia ya Diamond imeshampa Baraka zote mtoto wao ili amuoe kabisa Penny na huku nae Penny akihimizwa kudumisha upendo wa dhati kwa Diamond ambae tangu aanze kuishi na mtangazaji huyo Diamond amebadilika sana kitabia kiafya nk.

CHECK TRAILER YA MUV YA LULU "FOOLISH AGE"







































 CHECK HAPA CHINI

Thursday, September 5, 2013

LULU KUIMBA TENA NA LADY JAY DEE @ NYUMBANI LOUNGE





BAADA ya kufanya vizuri katika uzinduzi wa filamu yake mwanadada Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameonekana kumvutia sana mwanamuziki Judth Wambura ‘Lady Jaydee’ na kuamua kuandaa Onyesho litalaowakutanisha pamoja na kuimba katika jukwaa moja na kuimba wimbo maalum wa Yahaya. 

Lulu siku ya uzinduzi wa filamu yake ya Foolish Age aliweza kuwashangaza waarikwa waliohudhuria show baada ya kuimba wimbo wa Yahaya sambamba na Anaconda na kushangiliwa na umati wa wapenzi wa filamu wanakutana tena na kuimba kwa mara nyingine.

Lady Jaydee na Machozi Band wakishirikiana na msanii mwarikwa Lulu watafanya bonge show kesho siku ya Ijumaa katika viwanja tulivu vya Nyumbani Lounge ni show ya Ladies Nite nyote mnakaribishwa.

Saturday, August 31, 2013

VIDEO:LULU AKIONGEA NA VYOMBO VYA HABARI KWENYE RED CARPET SIKU YA UZINDUZI