Showing posts with label MANDELA. Show all posts
Showing posts with label MANDELA. Show all posts

Monday, December 16, 2013

KWELI MANDELA HAKUWA MTU KAWAIDA, MAAJABU YATAWALA KWENYE MAZISHI YAKE, MIZIMU YAONEKANA LIVE MAHALA ALIPOZIKWA!





 Hapa Mwili wa Mandela baada ya kufariki.









 

Hatimae Nelson Mandela amepumnzishwa kwenye makao yake ya milele na kimsingi hatutomuona tena hadi siku ya mwisho kwenye ufufuo.
Afrika Kusini na dunia zilikuwa kweye majonzi mazito ya kifo cha shujaa huyo wa karne ambae dunia inamfahamu kwa mambo mema aliyoyafanya

Sunday, December 15, 2013

UPDATES:MAZIKO YA NELSON MANDELA KIJIJINI QUNU

 
Jeneza lenye mwili wa Mandela likiwa makaburini.
 
Jeneza lenye mwili wa Hayati Nelson Mandela likipelekwa makaburini tayari kwa maziko.
 
Hapa ndipo Hayati Nelson Mandela atakapozikwa.
 
Oprah Winfrey naye ni miongoni mwa waombolezaji. Hapa akielekea eneo la makaburi.
 
Askofu Desmond Mpilo Tutu ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa marehemu Mandela naye akielekea eneo la makaburi.
 
Jeneza baada ya kuwasili eneo la makaburi. Hapa likifunguliwa kutoka kwenye gari maalum.

Saturday, December 7, 2013

MACHANGUDOA AFRIKA KUSINI WAPIGA PESA KAMA HAWANA AKILI NZURI KUTOKANA NA MSIBA WA MANDELA,VIONGOZI WANAOKWENDA HUKO WATAHADHARISHWA,

 Kazi kazi: Hapa Changudo wa Afrika Kusini akiwa mzigoni na mteja wake.
 Machangudoa hawa nao walifumwa wakiwa na maua kama ishara ya kuomboleza kifo cha Mandera.







Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua maelfu ya wakina dada wanaoujiuza nchini Afrika Kusini wameugeuza msiba wa Rais huyo mwenye heshima kubwa Duniani kuwa mchongo wa kupigia pesa,
Mwandishi wa Xdeejayz nchini huko ambae yuko kwenye mitaa mbalimbali nchini humo akishuhudia mambo yanvyoendelea alijionea ongezeko la wakina dada hao maaruu kwa jina la Changudoa wakipioga pesa ndefu kufuatia ongezeko la watu wanaendelea kutua huko kwa ajili ya kushiriki kwenye zoezi hilo la mwisho la kuuaga mwili wa shujaa huyo wa karne.
Hata hivyo mwandishi amesema Airpor kubwa ya nchini huko sasa hivi imeimarishwa ulinzi mkali ambapo maraisi mbalimbali toka Dunia kote wanaendelea kuwasili

CREDIT:XDEEJAYZ

Thursday, December 5, 2013

TWEET ZA WANAMUZIKI WAKUBWA DUNIANI BAADA YA KIFO CHA NELSON MANDELA


Mwanamuziki Robert Sylvester Kelly "R. Kelly" akiwa na Nelson Mandela enzi za uhai wake.

Tuesday, July 9, 2013

MANDELA BASI TENA

Johannesburg, Afrika Kusini
MADAKTARI wanaomtibu Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, wanakubali kuwa kiongozi huyo basi tena kwani hali yake ni tata na sasa wanasubiri kiungo kimojawapo cha mwili wake kishindwe kufanya kazi ndipo wazime mashine inayomsaidia kupumua.
Nelson Mandela.
Kutokana na subira hiyo madaktari hao sasa wamebadili msimamo wao wa awali wa kuiondoa mashine hiyo inayomsaidia kupumua.
“Madaktari hao, wameishauri familia yake kuachana na ushauri wa awali wa kuiondoa mashine hiyo hadi tu pale moja ya kiungo chake muhimu cha mwili kitakaposhindwa kufanya kazi,” alisema rafiki wa Mandela, Denis Goldberg ambaye alikuwa mpigania uhuru aliyewahi kufungwa pamoja na Mandela.
Amesema madaktari hao waligusia kuhusu suala la kuondoa mashine lakini baadaye walikataa kwa kuwa kiongozi huyo aliweza kusogeza baadhi ya viungo na kutambua sauti.
“Ni kweli kuwa hali ya Mandela ni mbaya lakini si kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika,” alisema Goldberg.
Juzi vyombo vya habari vya hapa nchini vilitoa hati ya kiapo ya mahakama, ikionyesha kuwa madaktari hao waliishauri familia ya Mandela kuondoa mashine ya kumsaidia kupumua kwani asingeweza kuendelea kuishi.
Hata hivyo, msemaji wa Rais Jacob Zuma,Mac Maharaj alikataa kuzungumzia kuhusu hati ya mahakama ambayo ilieleza kuwa Mandela mwenye miaka 94 yupo mahututi.

Friday, July 5, 2013

MJUKUU WA MANDELA AFICHUA 'UCHAFU' WA FAMILIA YAO AWATUHUMU NDUGU ZAKE KWA UZINZI



Mjukuu wa mzee Mandela...Mandla Mandela alipokuwa akiongea na vyombo vya habari kijijini Mvezo jana.

Chuki miongoni mwa familia ya Nelson Mandela imeongezeka na kuchukua sura mpya jana pale mjukuu wa kiume na mrithi Mandla kuwatuhumu ndugu zake kwa uzinzi na kuukamua umaarufu wa kiongozi huyo anayeheshimika wa kupinga ubaguzi wa rangi.

Maoni yake hayo yamekuja wakati mabaki ya miili ya watoto watatu wa kiongozi huyo mwenye miaka 94 ikizikwa upya kwenye eneo la makaburi ya awali kufuatia amri ya mahakama kuirejesha baada ya Mandla kuwa amehamisha miili hiyo.

Katika mkutano na vyombo vya habari uliorushwa moja kwa moja kwenye televisheni ambao umewafadhaisha wananchi wa Afrika Kusini, Mandla alithibitisha tetesi kwamba mtoto wake mdogo wa kiume, Zanethemba, alikuwa ni mtoto wa uhusiano haramu kati ya kaka yake Mbuso na mke wa Mandla ambaye sasa wametengana, Anais Grimaud.

Huku Mandela akiwa kwenye mashine ya kupumulia hospitalini mjini Pretoria, chuki hiyo inayoongezeka imeiduwaza na kuishitua Afrika Kusini kwa uwiano sawa.

"Mbuso alimpa ujauzito mke wangu," alisema Mandla huko Mvezo, kijiji kilichoko Eastern Cape kilomita 700 (maili 450) kusini mwa Johannesburg ambako Mandela alizaliwa na mahali ambako Mandla anatumikia akiwa kama chifu rasmi wa ukoo huo.

Mandla, mwenye miaka 39, kwanza aliibua maswali kuhusu ubaba wa mtoto wake mwaka jana wakati alipotengana na Grimaud anayezungumza Kifaransa, ambaye tangu wakati huo alirejea kwao katika kisiwa cha Reunion kilichoko kwenye Bahari ya Hindi. Pia alibainisha wakati huo kwamba hakuwa na uwezo wa kupata watoto.

Juhudi zake kuipata familia hiyo kujibu maswali hayo ya ubaba wa Zanethemba yaligonga mwamba kwa lengo la kuhifadhi mfanano wa umoja katika familia hiyo maarufu kabisa nchini Afrika Kusini," alisema Mandla.

"Jambo hili halikuwahi kabisa kujadiliwa na wanaoitwa ndugu wa familia hiyo ambao wanasema kwamba wanataka kuhakikisha kwamba kuna utulivu katika familia hii," alisema, akiwapa changamoto waandishi wa habari kufanya vipimo vya DNA kuthibitisha madai yake hayo.

"Ukweli uko pale. Unaweza kwenda na kubaini, fanya vipimo vya muhimu vinavyohitajika," alisema. Kaka yake Mbuso amekana kuwa baba wa mtoto huyo.

Vyombo vya habari vimepachika vichwa vya habari 'Mandela vs Mandela' kwenye kurasa zao za mbele na tahariri zimesikitikia ukatili wa mgawanyiko wa chuki ndani ya familia hiyo ya mtu aliyetikisa dunia nzima kama mfano wa mapatano kati ya pande zinazopingana.

Sunday, June 23, 2013

HALI YA MANDELA NI TETE...ASHINDWA KUFUMBUA MACHO KWA SIKU KADHAA...

Mzee Nelson Mandela ameendelea kuwa katika hali mbaya hospitalini jana baada ya kubainika kwamba gari la wagonjwa lililombeba Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini kwenda hospitali limeharibika.

Gari hilo la wagonjwa mahututi liliharibika wiki mbili zilizopita wakati Mandela alipokuwa akikimbizwa kwenye hospitali moja mjini Pretoria, na kumwacha 'njiapanda' kwa dakika 40.


Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini alihamishiwa kwenye gari jingine la wagonjwa la hospitali ya kijeshi kumalizia safari iliyobaki ya dakika 50 kati ya Johannesburg na Hospitali ya Moyo ya Medi-Clinic.

Msemaji wa Rais Mac Maharaj alisema: "Tahadhari zote zimechukuliwa kuhakikisha kwamba hali ya kiafya ya rais wa zamani Mandela haiathiriki na tukio hilo."


Madaktari wanaomtibu Mandela waliridhika kwamba hakupata maumivu yoyote katika kipindi hiki, aliongeza Maharaj.

Taarifa ya jana kuhusu afya ya Mandela inaonesha kwamba kuna mabadiliko kidogo katika hali ya shujaa huyo wa kupinga ubaguzi wa rangi tangu alipopokelewa hospitalini hapo.
 
Mandela, ambaye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini mwaka 1994, alikimbizwa hospitali moja ya Pretoria mapema Juni 8 kufuatia maambukizi kwenye mapafu.
Ilidaiwa jana kwamba Mandela hajitingishi na familia yake sasa inajadili uwezekano wa kusitisha matibabu.

Amekuwa hospitalini kwa wiki mbili akipambana na maambukizi hayo, lakini taarifa zilizopita zimeashiria kwamba afya ya Mandela inaimarika.

Kwa mujibu wa vyanzo vipya, ufanyaji kazi wa ini na figo za Mandela umeshuka hadi asilimia 50 na hakufungua macho yake kwa siku kadhaa.
 
Pia alitakiwa kufanyiwa oparesheni mbili hivi karibuni, moja kutibu vidomda vya tumbo zilivyokuwa vikichuruzika damu na nyingine kuchomeka mpira mwilini mwake, imeripotiwa.
Taarifa hizi zinaashiria kwamba suala la Mandela ni kubwa kuliko inavyoripotiwa na mamlaka za Afrika Kusini.

Historia ya matatizo ya mapafu ya Mandela ilianzia tangu alipokuwa kwenye gereza la Kisiwa cha Robben karibu na Cape Town. Aliachiwa huru mwaka 1990 baada ya miaka 27 na akaendelea kutumikia nchi kama Rais kuanzia mwaka 1994 hadi 1999.

Kulazwa kwake hospitalini ni mara ya nne tangu Desemba, mwaka jana.