Showing posts with label linah. Show all posts
Showing posts with label linah. Show all posts

Thursday, October 31, 2013

NGUO ZA NUSU UTUPU YA LINAH YACHANGANYA MIDUME

Linah akiwa jukwaani wakati wa shoo ya Fiesta 2013 jijini Dar.
Mavazi ya nusu utupu ambayo msanii Esterlina Sanga ‘Linah’ hupenda kuyavaa hasa kwenye matamasha yamekuwa yakiwadatisha wanaume na wengine kuomba kupiga naye picha kwa lengo la ‘kujipoza’ kama ilivyotokea kwenye Fiesta, Dar hivi karibuni.

 


 
Linah akipozi na baadhi ya wanaume walioomba kupiga naye picha.
 
Ijumaa limekuwa likimfuatilia Linah na kubaini kuwa kila mara hupenda kuvaa nguo zinazoacha wazi mapaja na kitovu chake na watu ambao amekuwa akipiga nao picha ni wanaume ambao wengi huonekana wakiwa wamemshika kimahaba.



Hata hivyo, licha ya mwenyewe mara kadhaa kueleza kuwa, hayo ni mvazi ya kikazi zaidi, baadhi ya mashabiki wamemponda na kumtaka kubadilika hasa ikifahamika kuwa ni mtoto aliyetokea kwenye familia iliyoshika dini na kwamba kuvaa hivyo ni kujidhalilisha

Tuesday, August 6, 2013

ANGALIA PICHA ZA LULU, MAMA KANUMBA NA LINAH NDANI YA FILAMU YA MAPENZI YA MUNGU

Muigizaji maarufu Swahiliwood Elizabeth Michael(Lulu) na mama Kanumba(Flora Mtegoa) kwa mara ya kwanza wanakuja na filamu inayoitwa Mapenzi ya Mungu. Katika filamu hiyo waigizaji wengine ni Linah Sanga ambaye ni mwanamuziki maarufu wa Bongofleva na Sudi Ali. Angalia baadhi ya picha za behind the scenes za filamu hiyo
Lulu na Linah

Mama Kanumba, Sudi Ali na Lulu wakiwa location
 

Sunday, July 21, 2013

LINAH AKANUSHA MADAI YA KUBAKWA USIKU BAADA YA KULEWA


Mrembo na mwanamuziki wa kike nchini, Linah Sanga amezikanusha ripoti zilizosambazwa leo kuwa amebakwa na rapper Kimbunga na kudai kuwa ameshangazwa mno na taarifa hizo. 

Taarifa hizo zimeanza kusambazwa leo mchana baada ya akaunti ya Facebook inayoonekana kuwa ya rapper Kalapina yenye jina ‘KalApina Kikosi Cha Mizinga’ kuandika: 
 
“Mtoto kimbunga amechamba ana leta usela mavi mambo ya kizamani hivi yupo chini ya ulinzi osterbay police kwa kosa la kumbaka msanii lina.” 

Mwandishi wetu amezungumza na Linah ambaye amesema amepigiwa simu na watu wengi wa karibu kumuuliza suala hilo wakiwemo, Barnaba, Ditto, Amini na mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown. 

 
Amesema Soudy alimwambia kuwa ameziona taarifa hizo kwenye Facebook kwenye akaunti ya Kalapina. 
“Sasa nikasema Kalapina ameandika hivi, kwasababu sijaingia mwenyewe kuangalia chochote. 

"Sikutaka kujipa stress kwasababu kuna kazi nafanya nisije nikaharibu kazi kwahiyo nikaona vitu vingine kama hivi ni vya kupotezea tu lakini sio vizuri kabisa yaani.

 "Kiukweli sijapenda, yaani bora mtu anizushie kitu kingine chochote lakini si suala kama hilo hapo, si suala zuri,” amesema Linah. 
 
Amesema jana usiku alitoka na mpenzi wake kwenda kwenye sinema na wakarejea nyumbani salama. 


“Sasa sielewi huko kubakwa nimebakwa saa ngapi na nilikuwa na boyfriend wangu labda yeye ndio kanibaka! Maana mtu wanayeniambia amenibaka Kimbunga, huyo Kimbunga hata simjui, namskia tu.
  
Nashindwa kuelewa, kwanini mtu azushe kitu kama hicho yaani ndo nataka kujua source ni nini. Niko fine yaani, kwasababu naelewa ‘it’s not true, lakini nafikiria huyo mtu mpaka kaamua kunifanyia kitu kama hicho, nimemkosea nini au kuna kitu gani, yaani hicho ndio kinaniumiza kichwa.”