HABARI ZAIDI ZITAWAJIA HAPAHAPA
Showing posts with label ajali. Show all posts
Showing posts with label ajali. Show all posts
Friday, September 5, 2014
AJALI MBAYA YA BASI YASABABISHWA FIESTA KUAHIRISHWA MKOANI MARA...PICHA ZAID HAPA
HABARI ZAIDI ZITAWAJIA HAPAHAPA
Thursday, July 31, 2014
WALIOKUFA AJALI YA DODOMA WAONGEZEKA,DEREVA ALIKUWA ANAONYESHA MWANAFUNZI HAWEZI KUMPITA
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Polisi David Misime amesema tukio hilo la Pandambili Wilayani Kongwa
katika barabara ya Dodoma – Morogoro limesababisha vifo vya watu 18
wanaume watu wazima 11 na mtoto mmoja wa kiume na Wanawake watu wazima 5
na mtoto 1 wa kike.
Majina ya Marehemu hao ambao wametambuliwa na ndugu zao na kusafirishwa kwenda makwao kwa maziko ni:-
1. Christina d/o Dickson, Miaka 35, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Mpwapwa
2. Omari s/o Mkubwa, Miaka 32, Muhaya, Kondakta wa bus, Mkazi wa Morogoro
3. Malick s/o Masawe, Miaka 42, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mpwapwa
4. Wilson s/o Paul @ Suda, Miaka 63, Mgogo, Mstaafu Red Cross, Mkazi wa Mpwapwa.
5. Said s/o Lusogo, Miaka 44, mluguru, dereva wa bus, Mkazi wa Kihonda Morogoro.
6. Gabriel s/o Meja @ Chiwipe, Miaka 50, Mgogo, Mkazi wa Mpwapwa
7. Gilbert s/o Lemanya, Miaka 53, Mgogo, dereva wa Lori, Mkazi wa Makole Dodoma
8. Mikidadi s/o Zuberi @ Omari Miaka 22, Mbondei, Tingo wa Lori, Mkazi wa Morogoro/Ilala Dar es Salaam.
9. Justine s/o Makasi, Miaka 24, Mgogo, Mkulima wa Mpwapwa
10. Alice d/o Masingisa, Miaka 24, Mgogo, Mkazi wa Mpwapwa
11. Merina d/o Doto @ Marcel, Mgogo, Miaka wa Mji mpya Mpwapwa
12. Nasibu s/oSeif, Miaka 48, Mkazi wa Morogoro
13. Nicholaus s/o Raymond Kileo Miaka 51, Mkazi wa Mpwapwa
14. Stella d/o Mdako, Miaka 60, Mkazi wa Mpwapwa
15. Erick s/o Lucas,Miaka 10, Mkazi wa Morogoro
16. Nazaret s/o Deremsi @ Kasuga, Miaka 45, Mhehe, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kibakwe Mpwapwa.
17. DArini d/o Dickson, Miaka 2, Mgogo, Mkazi wa Mpwapwa
18. Magreth d/o Nyanzi, Miaka 35, Mgogo, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mwananyamala Dar es Salaam.
Aidha majeruhi waliokuwa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya
Wilaya ya Kongwa wametibiwa na kuruhusiwa na wengine kuhamishiwa katika
Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma.
Waliobaki
katika Hospitali ya Mkoa wakiendelea na matibabu ni 32 na wanaendelea
vizuri isipokuwa walio katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi
wa karibu wa madaktari (ICU) ambao ni George s/o Mjelwa, Miaka 40,
Daktari wa Wilaya ya Mpwapwa na mke wake aitwaye Getrudar s/o Kombe,
Miaka 37, Mfamasia wa Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.
Jana
kamanda alisema ajali hiyo baada ya uchunguzi zaidi inaonyesha
kusababishwa na madereva wote wawili kwa maana ya dereva aliyekuwa
anaendesha lori namba T 820 CKU/T390 CKT GILBERT S/O LEMANYA kwa kupita
gari lingine bila kuwa mwangalifu na magari yaliyokuwa yanatokea mbele
yake na kuwa katika mwendo kasi.
Dereva
wa bus namba T 858 AUH SAID S/O LUSOGO kulingana na mashuhuda hasa
abiria wanaeleza alikuwa mwendo kasi na ndiyo maana ajali hii imeleta
madhara makubwa kiasi hicho kwani kama angelikuwa kwenye mwendo wa
kawaida unaotakiwa madhara yangekuwa siyo makubwa kiasi hicho pamoja na
dereva wa lori kufanya aliyofanya.
Wito
kwa madereva na watumia barabara wengine waache mwendo kasi na ushabiki
wa ushindani kwani kulingana na ushahidi uliokusanywa unaonyesha dereva
wa Moro best alikuwa akiendesha kwa mwendo kasi kutaka kwenda kulipita
bus la AL-SAEDY lililokuwa limeondoka mbele yake kwa kigezo kuwa dereva
wa bus hilo ni mwanafunzi wake hivyo hawezi kufika Morogoro kabla yake.
Wamiliki
wa Ma bus na magari mengine wawaonye madereva wao kuhusiana na mwendo
kasi na kuwataka wazingatie sheria za usalama barabarani ili kuepusha
ajali mbaya kama hii.
Aidha
abiria wasiwe wanakaa kimya kama walivyofanya wa bus la Moro best
wanapoona dereva anaendesha kwa mwendao wa kasi watoe taarifa Polisi ili
wakamatwe na kuepusha madhara kama yaliyotokea.
Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
Saturday, July 26, 2014
MWIMBAJI BAHATI BUKUKU APATA AJALI MBAYA YA GARI
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba, mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili hapa nchini, Bahati Bukuku amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali mbaya katika eneo la Kongwa, mkoani Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, mwimbaji huyo alipata majeraha makubwa sehemu mbalimbali mwilini na kwamba chanzo cha ajali hiyo kinadhaniwa kuwa ni mwendokasi.
Chanzo hicho hakijaweza kueleza zaidi kwamba Bukuku alikuwa akielekea ama kutoka mkoani Dodoma na kama ndani ya gari hilo kulikuwamo na abiria wengine.
Pia haikuweza kufahamika mara moja kama mwimbaji huyo alikuwa akiendesha mwenyewe gari hilo, ingawa kilithibishwa ajali hiyo na kwamba Bukuku alijeruhiwa vibaya.
Thursday, July 24, 2014
NDEGE YA ALGERIA IMEANGUKA NCHINI MALI

Ndege ya shirika la ndege la Air Algerie ikiwa na watu 116 imeanguka kaskazini mwa Mali. Ilikuwa ikisafiri kutoka Burkina Faso kwenda mji mkuu wa Algeria, Algiers. Kulikuwa na hali mbaya ya hewa katika eneo hilo wakati ilipopoteza mawasiliano na waongoza ndege. Abiria 51 kati ya waliokuwemo ni raia wa Ufaransa. Ndege mbili za kijeshi za Ufaransa zimepelekwa katika eneo hilo kufanya uchuguzi zaid
Thursday, July 10, 2014
BASI LA AMANI LAPATA AJALI MAENEO YA SALANDA MKOANI TABORA, MTOTO MMOJA AFARIKI DUNIA

Basi la Amani Express likitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam limepata ajali usku wa kuamkia leo maeneo ya Salanda mkoani Tabora, ambapo mtoto wa miaka mitatu amepoteza maisha na abiria kadhaa wamepata majeraha. Mashuhuda wanahisi kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi. Pichani abiria wakitafuta vitu vyao


Baadhi ya abiria walionusurika katika ajali hiyo wakisubiri msaada wa usafiri

Basi la Amani likiwa limepinduka

Kikosi kazi cha Michuzi TV kilicho katika ziara ya kikazi mikoani kikihojiana na baadhi ya abiria asubuhi hi
Monday, December 16, 2013
BASI LA CHAMPION LAPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI 29 WA CHUO KIKUKU CHA ZANZIBAR KATIKA MLIMA CHIMWAGA LIKITOKEA CHUO KIKUU DODOMA (UDOM)
Gari lenye namba za usajili T 704 ADR aina ya Scania bus la kampuni ya CHAMPION likiendeshwa na dereva ALLY RAMADHANI, mnyaturu, umri kati ya 35 - 40, mkazi wa Kisasa Dodoma likiwa limebeba wanamichezo/wanavyuo wa vyuo vikuu vya Zanzibar na State University Zanzibar likitokea chuo kikuu Dodoma (UDOM) likielekea kituo kikuu cha mabasi Dodoma lilipinduka na kusababisha majeraha kwa abiria wapatao 43 kati yao Majeruhi 29 waliotibiwa na kuruhusiwa na majeruhi 14 wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma, wote wakiwa ni wanaume.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Kamishna msaidizi wa Polisi SUZAN S. KAGANDA amesema ajali hiyo imetokea tarehe 15/12/2013 majira ya saa 06:15 hrs huko eneo la mlima wa Chimwaga UDOM Kata ya Makulu Dodoma mjini.
Kamanda KAGANDA amewataja majeruhi katika ajali hiyo ambao ni:-
1. Hamisi Hamisi, miaka 28, mshirazi, mwanachuo Zanzibar University. Amelazwa word namba 1.
2. Bashiru Yusuph, miaka 26, sukuma, mwanachuo Zanzibar University. Amelazwa word namba 1.
3. Abdallah Juma, miaka 28, mshirazi, mwanachuo State University. Amelazwa word namba 1.
4. Ally Sharifu, miaka 24, mshirazi, mwanachuo. Amelazwa word namba 1.
5. Mussa Mkanga, miaka 21, mzanzibari, Mwanachuo. Amelazwa word namba 1.
6. Seifu Fakii juma, miaka 27, mshirazi, mwanachuo State University. Amelazwa word 1
7. Ahamed Mohamed Hassani, miaka 23, Mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University. Amelazwa word namba 11.
8. Richard Mwasonga, miaka 36, mnyiha, Tingo wa bus, Miyuji Dodoma. Amelazwa word namba 1.
9. Juma Nasoro, miaka 23, mshirazi, mwanachuo State University Zanzibar. Amelazwa word namba 1.
10. Hemedi Mohamed, miaka 29, Mzanzibari, mwanachuo State University Zanzibar. Amelazwa word namba 1.
11. Mussa Mtaugana, miaka 24, mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University
12. Adam Mwale Bonifasi, miaka 24, mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University.
13. Amelazwa word namba 1.
14. Mohamed Ally Mohamed, miaka 23, mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University.
15. Nassoro Mohamed Saidi, miaka 25 -30, mwanachuo State University Zanzibar. Hali yake si nzuri sana na amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Aidha Kamanda KAGANDA amesema Chanzo cha ajali ni mteremko mkali wenye kona iliyosababisha dereva kushindwa kulimudu gari lake na kusababisha ajali ya gari kupinduka upande wa kulia na kulala kiubavu. Mara baada ya ajali hiyo dereva alikimbia kwenda kusikojulikana na juhudi za kusaka dereva huyo zinaendelea. Pia uchunguzi unaendelea kubaini iwapo gari hilo lilikuwa na tatizo lolote.
Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma linatoa Wito kwa madereva kila mara wawe makini barabarani hasa kipindi hiki cha mvua na kuwa makini hususani kwa barabara zenye milima
Friday, December 13, 2013
UPDATES:Lowassa anusurika katika ajali ya ndege jijini Arusha leo
Habari zimetujia sasa hivi zinasema abiria kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa wamenusurika kifo, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuwa pasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa Arusha leo mchana.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la precision aina ya ATR ilipata
ajali hiyo wakati ikitua, ambapo Matairi yote manne ya nyuma yalipasuka
na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria. Ila hakuna mtu aliyedhurika
katika ajali hiyo.
"Yaani
Mungu ni mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi
chetu Lowassa...Mungu atamlinda jamani...siamini" alisikika akisema mama
mmoja miongoni mwa abiria hao wakati akishuka.
Mh
Lowassa ni mbunge wa Monduli, jimbo ambalo anatoka Waziri Mkuu
aliyekuwa kipenzi Cha mwalimu Nyerere na watanzania hayati Edward
Moringe Sokione.Sokoine aliyefariki katika ajali ya gari mwaka 1984
Tuesday, October 29, 2013
AJALI MBAYA YATOKEA MLIMA WA MZALENDO IGAWILO JIJINI MBEYA


Lori baada ya kupata ajali katika eneo la mlima wa Mzalendo Igawilo jijini Mbeya wakati likielekea jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya majeruhi katika ajali hiyo wakipelekwa hospitali.
Saturday, October 5, 2013
PICHA:AJALI MBAYA MLIMA KITONGA
Ajali mbaya nyingine imetokea usiku huu katika mlima kwa Kitonga wilaya ya Kilolo mkoani Iringa katika barabara kuu ya Dar es Salaam -Iringa .
Katika ajali hiyo watu wawili wamekufa papo hapo huku
wa wawili wakijeruhiwa vibaya baada ya malori mawili kugongana uso kwa uso .
Ajali hiyo imetokea mida ya saa 12.50 jioni ya leo ikiwa ni dakika takribani 30 baada ya ajali ya basi la JM kupinduka eneo la Mazome wilaya ya Kilolo.
waliopoteza maisha katika ajali hiyo ambayo chanzo ni dereva wa lori la IT lililokuwa likisafirishwa kwenda nchi za kusini mwa Tanzania aliyekuwa akitaka kulipita gari la mbele mlimani na katika kona kali .
Hata hivyo dereva wa lori hilo IT aliyetambuliwa kwa jina la Gody amevunjika mguu wake ambao umetoka katika na dereva na utingo la fuso wamekupa papo hapo huku mwanamke aliyekuwa katika lori IT akisalimika .
Tuesday, September 24, 2013
AJALI:ABIRIA ZAIDI YA 50 WANUSURIKA KIFO IRINGA
Lori la Kampuni ya Ivory lililogongana uso kwa uso na Basi la Sai baba
Askari
wa usalama barabarani Iringa wakilitazama basi la kampuni ya Sai - baba
Express lenye namba za Usajili T 668 BCD ambalo liligongana uso kwa uso
na lori la kampuni ya Ivori lenye namba T 280 ADK eneo la Kibwabwa
katika barabara kuu ya Mbeya - Iringa jana na watu zaidi ya watatu
kujeruhiwa vibaya na wengine zaidi ya 50 ambao ni abiria wa basi hilo
kunusurika kifo
Wednesday, September 11, 2013
TAZAMA PICHA ZA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA JANA USIKU JIJINI ARUSHA
ARUSHA:Jana usiku majira ya saa moja ilitokea ajali mbaya iliyohusisha gari aina ya Escudo yenye nambari za usajili T600 AUC na Coaster yenye nambari za usajili T598 BNS. Ajali hiyo iliyotokea eneo la Makumira, wilayani Arumeru, jijini Arusha. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema chanzo cha ajali hiyo wamesema kuwa ni gari aina ya coaster iliyokua ikitokea jijini Arusha na ilipofika eneo la makumira ilitaka kupita gari iliyokuwa mbele lakini kabla gari hiyo haijamaliza kuipita gari hiyo, kumbe mbele kulikua kuna gari aina ya Escudo iliyokua ikitokea Moshi kuelekea Arusha ndipo zilipokutana uso kwa uso na kusababisha ajali mbaya.


Hii ndio coaster iliyopata ajali ambayo baada ya ajali ilihama barabarani na kuelekea vichakani.

Huu ni upande wa mbele wa garri aina ya Suzuki Escudo ambao unaonekana kuumia sana, na baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wakishangaa jinsi ambavyo gari hiyo imeharibika.

Huu ndio upande wa mbele wa coaster iliyopata ajali na abiria wote kutoka wakiwa wazima wa afya.
Katika ajali hiyo hakuna hata mtu mmoja aliyefariki ila dereva wa gari aina ya Escudo aliyefahamika kwa jina moja la Hussein maarufu kama Baunsa ndie aliyeumia sehemu za miguuni na kichwani lakini wasamaria wema waliweza kumtoa katika eneo la ajali na kumuwahisha hospitali
Friday, September 6, 2013
ANGALIA PICHA YA AJALI ILIYOWAPATA WAANDISHI NA MAAFISA WA BUNGE KARATU JANA
Gari lilivyopindukaMatukio ya picha baada waandishi na maafisa wabunge walivyonusurika katika ajari iliyotokea karatu jana.
Maafisa wa Bunge na waandishi walikuwa katika msafara wa Wabunge toka nchi za SADC waliokua wanaelekea ngorongoro
Afisa Habari wabunge Owen Mwandumbya akiwa amepumzishwa ili apate hewa kidogo baada ya ajari
Maafisa wa Bunge na waandishi walikuwa katika msafara wa Wabunge toka nchi za SADC waliokua wanaelekea ngorongoro
Sunday, September 1, 2013
BREAKING NEWS: NDEGE ZAGONGANA ZANZIBAR.
Ndege ya Oman air na Ethipian airlines leo jioni zimegongana katika kiwanja cha ndege cha Zanzibar wakati zikijitaarisha kuruka, ila ajali hii haikuwa kubwa, wakati hayo yakiendelea abiria wa Ehiopian airline wameshushwa na kuweka sehemu ya mapumziko.
Nawatakia kila la kheri wasafiri wote na inshaalah Mwenyezi
Mungu atawapa wepesi wa katika safari zao.
Wednesday, August 28, 2013
BREAKING NEWS: WATU 13 WAFA NA WENGINE 11 WAJERUHIWA VIBAYA KATIKA AJALI YA GARI HUKO SHINYANGA

HABARI ZILIZOUFIKIA MTANDAO HUU HIVI PUNDE ZINASEMA KUWA WATU 13, WAMEFARIKI DUNIA NA 11 WAMEJERUHIWA KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA KIJIJI CHA NGONGWA MKOANI SHINYANGA KWENYE AJALI ILIYOHUSISHA GARI AINA YA HICE LENYE NAMBA ZA USAJIRI T 756 CHX NA GARI LILILOKUWA LIMEHARIBIKA LENYE NAMBA ZA USAJILI T 696 AMS.
AKIZUNGUMZA KWA NJIA YA SIMU KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA SHINYANGA, KIHEMA KIHEMA, ALISEMA KUWA MIONGONI MWA WATU WALIOFARIKI DUNIA NI PAMOJA NA DEREVA WA HICE, ILIYOKUWA NA ABIRIA HAO IKITOKEA KAHAMA KUELEKEA USHIROMBO AMBAYE ALIFARIKI PAPO HAPO, HUKU MAJERUHI WAKIPELEKWA KUPATIWA HUDUMA YA KWANA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA.
Thursday, August 22, 2013
WATU SABA WANUSURIKA KWA AJALI YA NDEGE ILIYOTUA ZIWA MANYARA
Ndege ndogo ya shirika la Tanzanair iliyokuwa ikitokea mjini Bukoba mkoani Kagera kwenda Dar ss Salaam imelazimika kutua kwa dharura katika ziwa Manyara baada ya injini yake moja kuzimika ghafla ikiwa angani.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria sita na rubani mmoja ambapo wote wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Seliani mjini Arusha kwa matibabu.
Chanzo: ITV
Tuesday, August 20, 2013
MSAFARA WA MBIO ZA MWENGE WAPATA AJALI...
Baadhi ya washiriki walikuwa katika msafara wa kwenda
kukabidhi mwenge kutoka wilaya ya Dodoma mjini na kuukabidhi katika
wilaya ya Mpwapwa wakiangalia moja ya magari yaliyoharibika baada ya
kutokea ajali hiyo Gari namba DFP.7178 TOYOTA LAND CRUISER (AMBULANCE)
ambayo ni mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.

Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Dodoma, Mrakibu wa Jeshi la
Polisi Bw. Bonventure Nsokolo Akikagua moja ya gari iliyoharibika katika
ajali iliyotokea katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya
Chamwino, ambapo takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara
wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye
makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa.

Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Bi. Suzzan Kaganda Akiongea na
waandishi wa Habari hawapo pichani, Katika ukumbi wa Mikutano wa Jeshi
la Polisi Mkoa wa Dodoma Kuhusia na ajali iliyotokea katika kijiji cha
Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, ambapo takribani magari matano
(5) yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya
Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa, ambapo Watu
wapatao tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo.
===============
Mnamo
tarehe 20/08/2013 majira ya 08.45 hrs. huko katika kijiji cha Fufu,
Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, takribani magari matano (5) yaliyokuwa
kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea
kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa, moja ya magari yaliyokua kwenye
msafara huo lilikutana na tuta huku dereva wake akishika ‘brake’ ghafla
na kusababisha magari yaliyokuwa nyuma yake kugonga gari la mbele kwa
kila moja lililokuwa likitimka kutokana na vumbi kubwa lililokuwa
likifuka wakati wa msafara huo kufuatia matengenezo ya barabara Dodoma –
Iringa yanayoendelea.
Katika ajali hiyo magari yaliyoathirika ni kama ifatavyo:-
1. STK 3007 TOYOTA LAND CRUISER
2. STK 3357 TOYOTA LAND CURISER yote ni mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa Katibu Tawala [M] Dodoma.
3. SM 5835 TOYOTA LAND CRUISER mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma
4. DFP.7178 TOYOTA LAND CRUISER (AMBULANCE) nayo ikiwa ni mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
5. T.627 BFJ TOYOTA LAND CRUISER mali ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma
6.
STK 4983 TOYOTA LAND CRUISER HARD TOP Mali ya Wizara ya Kilimo. Watu
wapatao tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo, kati yao wanne (4)
wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Dodoma na watano (5) walipatiwa
matibabu na kuruhusuiwa kurudi nyumbani.
Majeruhi waliolazwa ni kama ifuatavyo:
1. JUMA S/O ALLY @ SIMAI, Miaka 32, Mpemba, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mkazi wa Kusini Unguja.
2. CHARLES S/O MAMBA, Mgogo, Miaka 50, Mkazi wa Ipagala, Diwani wa Kata ya Ipagala
3. DATIVA D/O KIMOLO, Miaka 46, Mrangi, Afisa Mifugo, Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa Mailimbili.
4. AMINA D/O MGENI, Miaka 36, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area ‘C’ Manispaa ya Dodoma.
Majeruhi waliotibiwa na kuruhusiwa kurudi makwao ni kama ifuatavyo:-
1. JACKLINE D/O MAGOTI, Miaka 39, Mjita, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area C Manispaa ya Dodoma
2. RICHARD S/O MAHELELA, Miaka 51, Mgogo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Ipagala, Mkazi wa Ipagala Manispaa ya Dodoma
3.
JUMANNE S/O NGEDE, Miaka 58, Mrangi, Diwani Kata ya Chamwino/ Naibu
Meya wa Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa Chamwino Manispaa ya Dodoma.
4. ZAITUNI D/O VARINOI, Miaka 43, Mkazi wa Mbwanga, Manispaa ya Dodoma.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa wito kwa madereva na watumiaji wa
barabara hususan zilizopo kwenye matengenezo wanapokuwa katika misafara,
wanapaswa kuwa makini na wapeane nafasi kati ya gari moja hadi jingine
ili kuepusha madhara yanayoweza kuepukika
Saturday, August 17, 2013
Friday, August 16, 2013
WACHOMEWA NYUMBA WAKIDAIWA KUIBA KWENYE GARI LILILOPATA AJALI
NYUMBA sita katika eneo la Mbwewe wilayani Bagamoyo mkoani Pwani zimeteketezwa kwa moto na watu. Inaelezwa kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada ya kudaiwa kuwa wakazi wa nyumba hizo walihusika na wizi wa marobota na viatu yaliyokuwamo katika gari ya Fuso iliyopata ajali katika eneo hilo.
Gari hiyo ilipata ajali katika eneo la Mbwewe katika barabara ya Chalinze- Segera baada ya gurudumu la nyuma upande wa kushoto kupasuka na kusababisha ipoteza muelekeo na kuziba njia kwa saa kadhaa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Ulirch Matei, alisema gari hilo lilikiwa likiendeshwa na Zakayo Joseph akiwa na watu wengine wawili.
Alisema baada ya kupinduka wakazi wa eneo hilo waliiba marobota na viatu vilivyokuwamo na kutokomea navyo majumbani kwako.
Matei alisema dereva Joseph na wenzake wawili walifanya msako kwa kushirikiana na wasamaria wema kwa kupita nyumba hadi nyumba na ndipo walibaini kuwa marobota hayo yaliibwa katika nyumba hizo.
Alisema wenye nyumba hizo walipigwa na kuchomewa moto nyumba zao.
Watu waliopigwa na kuchomewa moto nyumba zao ni Athumani Seif, Togeza Motua, Mwajuma Adam, Mustafa Rajab, Shabani Rajab, Said Khalfan na Zuhura Adam ambao walikimbizwa katika Kituo cha Afya Mwewe kupatiwa matibabu.
Matei alisema uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea na amewaasa wananchi kuachana na tabia ya kuiba inapotokea ajali.


.jpg)
.jpg)









