Showing posts with label DIAMOND. Show all posts
Showing posts with label DIAMOND. Show all posts

Thursday, November 20, 2014

OFFICIAL VIDEO: DIAMOND PLATNUMZ - NITAMPATA WAPI

d2Alhamisi ya Nov 20 Diamond Platnumz  ameibariki siku hii kwa kuachia video na audio ya wimbo wake mpya unaoitwa Nitampata wapi,kwenye radio station,tv na kwenye mitandao.
Video hii ambayo kwa mara ya kwanza ilianza kuonyeshwa Nov 19 kupitia kituo cha MTV BASE,kama hukufanikiwa kuiona unaweza kuiona kwa kubonyeza play hapo chioni.

Monday, October 6, 2014

USHAHIDI HUU HAPA:NYIMBO YA MWANA YA ALIKIBA NI DONGO KWA DIAMOND////

BONGOCLAN.CO.TZ DIAMOND

HUU HAPA UTHIBITISHO.
Mali ni nyingi nyumbani, kipi kimekukimbiza,
Hapa Alikiba, anamwambia Diamond, nyumbani ( SHAROBARO RECORDS) kuna kila kitu, beats kali, management nzuri and all that, kitu gani kilimkimbiza SHAROBARO RECORDS?

Ona babio mamio wote wanakulilia,

HAPA ALIKIBA ANAMAANISHA, SHAROBARO RECORDS, WAKIONGOZWA NA BOB JUNIOR, WOTE WANAMLALAMIKIA DIAMOND KWA KITENDO CHAKE CHA KUKIMBIA KUFANYA KAZI SHAROBARO. (BOB JUNIOR ALIPIGA KELELE SANA DIAMOND ALIPOKIMBIA SHAROBARO RECORDS )

Mtoto pekee ako nyumbani, kipi kimekukimbiza,
HAPA ALIKIBA ANASEMA, DIAMOND ALIKUWA NDO ARTIST PEKEE MKALI ALIYEKUWA CHINI YA SHAROBARO RECORDS. HAKUKUWA NA UPINZANI WOWOTE NDANI YA SHAROBARO, KITU GANI KILIMFANYA AONDOKE ?

Ona babio mamio wote wanakulilia
 
Ndani ya Dar es salame ulikuja bure
HAPA ALIKIBA ANAMKUMBUSHA DIAMOND, KUWA SIKU ALIPOKWENDA SHAROBARO RECORDS KWA MARA YA KWANZA, HAKUWA NA HATA SENTI TANO NA ALIREKODIWA WIMBO WAKE BURE KABISA.NENO DAR ES SALAME, LIMETUMIKA KUMAANISHA SHAROBARO RECORDS AU MUSIC INDUSTRY.
(KAMA ULIKUKUWA HUJUI, ALIKIBA NI MMOJA KATI YA WANAHISA WA SHAROBARO RECORDS, NA NDIO ALITOA IDHINI KWA BOB JUNIOR, AREKODI BURE WIMBO WA DIAMOND. ILIKUWA HIVI DIAMOND ALIENDA KWA BOB JUNIOR NA KUMWAMBIA ANA WIMBO WAKE ANAOMBA UREKODIWE LAKINI HANA UWEZO WA KIFEDHA, BOB JUNIOR AKAOMBA KUMSIKILIZA, ALIPOMSIKILIZA AKAGUNDUA KIPAJI CHA DOGO, BUT HAKUWA NA MAMLAKA YA KUREKODI WIMBO HUO BURE BILA IDHINI YA BOSS, ALIKIBA, SO IKABIDI AENDE KWANZA KUOMBA IDHINI KWA ALIKIBA, ALIKIBA AKAMWAMBIA BOB JUNIOR KAMA DOGO ANAJUA KUIMBA VIZURI, MREKODIE TU, HAKUNA SHIDA. ALIKIBA ALIYASEMA HAYA AKIWA ANAYAFANYA MAHOJIANO KWENYE KIPINDI CHA MKASI HIVI KARIBUNI.
kiba

Tena kimwana, kimwana hujui kuchuna
 
WAKATI DIAMOND, ANAENDA KUOMBA KUREKODI KWA BOB JUNIOR, ALIKUWA TAYARI KUFANYA SHOW ZAKE HATA BURE ILIMRADI TU AWEZE KUJITANGAZA..DIAMOND ALIWAHI KUMUOMBA ALIKIBA, APANDE NAYE KWENYE SHOW YA ALIKIBA, BILA MALIPO YOYOTE ILI WATU WAMUONE AKIWA NA ALI KIBA. SO ALIKIBA AMETUMIA NENO “KIMWANA ASIYE JUA KUCHUNA” AKIMAANISHA ‘MSANII UNDERGROUND ALIYE TAYARI KUIMBA HATA BILA MALIPO.

Na zile lawama za wale walokuzoeza,
HAPA ALIKIBA ANAZUNGUMZIA LAWAMA ZA MADEMU WANAO TOSWA NA DIAMOND



Ulikuja jana na leo tofauti sana.
HAPA ALIKIBA ANAZUNGUMZIA NAMNA AMBAVYO DIAMOND AMEBADILIKA KITABIA BAADA YA KUPATA MAFANIKIO KIMUZIKI.

Tena bora Yule wa jana, wa leo tofauti sana,
HAPA ALIKIBA ANAWAZUNGUMZIA WEMA SEPETU NA PENNY, ANASEMA BORA HATA PENNY KULIKO WEMA AMBAYE NDIO YUPO NA DIAMOND KWA SASA

Dakika mbili mbele nyuma, kichwa kinauma
HAPA ALIKIBA ANAZUNGUMZIA TABIA TABIA ZA WEMA SEPETU. MKOROFI(DAKIKA MBILI MBELE NYUMA), NA MWINGI WA HABARI, AMA PASUA KICHWA ( KICHWA KINAUMA) AMA KICHECHE.

Tena bora Yule wa jana, wa jana leo wa jana,
HAPA ALIKIBA ANASISITIZA ANACHO KIMAANISHA, KWAMBA ANAMZUNGUMZIA WEMA, ” tena bora yule wa jana, wa jana leo wa jana ” YANI YULE AMBAYE UPO NAE LEO, NA AMBAYE ULIWAHI KUWA NAE ZAMANI. NI WA JANA, UPO NAE LEO, LAKINI ULIWAHI KUWA NAYE JANA. HUYO NI WEMA SEPETU, ALIWAHI KUWA NA DIAMOND, WAKAACHANA, WAMERUDIANA TENA. ( ‘WAJANA LEO WA JANA = WEMA SEPETU )

Dakika mbili mbele nyuma, kichwa kinauma
HAPA ALIKIBA ANAKUTOLEA UFAFANUZI ZAIDI KWAMBA, HUYU ” WA JANA LEO WA JANA” SI MWINGINE ILA NI WEMA SEPETU. ANAFANYA HIVYO KWA KUELEZEA TABIA YA WEMA SEPETU AMBAZO NI “UKOROFI” (DAKIKA MBILI MBELE NYUMA ), NA UKICHECHE A.K.A PASUA KICHWA (KICHWA KINAUMA)..KAMA UMESAHAU WEMA SEPETU ALIWAHI KUMTUKANA BOB JUNIOR MATUSI YA NGUONI, KESI IKAENDA MAHAKAMANI..UNAKUMBUKA HIYO?

Oyayee , mbona unawatesa sana,
HAPA ALIKIBA ANAMWAMBIA DIAMOND MBONA UNAWATESA SANA HAO WASICHANA UNAO WABADILISHA BADILISHA ?

Omamee, omame oya mame, omame oya mamee
Mbona unajitesa sana
 
HAPA ALIKIBA ANAMWAMBIA DIAMOND “WHAT GOES AROUND COMES AROUND”. ANAVYO WATESA HAO WSICHANA, NI SAWA NA KUJITESA MWENYEWE TU. UKICHECHE WA DIAMOND UNAMTESA KIASI CHA KUMFANYA ASHINDWE KUJUA AMPENDE NANI KATIKA MAISHA YAKE, KWA SABABU WANAWAKE KARIBU WOTE ANAO TOKA WANAKUWA NA KASORO ZISIZO VUMILIKA.
Omamee, oya mame, omame oya mamee
Ukaanza kulewa
 , madawa kuvuta kwa sana.

HAPA ALIKIBA ANATHIBITISHA NAMNA AMBAVYO HALI YA KUWATESA WANAWAKE INAMRUDIA DIAMOND MWENYEWE. BAADA YA KUUMIZWA NA MWANAMKE/WANAWAKE, DIAMOND AKAONA HAKUNA NJIA NYINGINE YA KUPAMBANA NA MAUMIVU YA KUUMIZWA NA MWANAMKE, ZAIDI YA KULEWA. DIAMOND ALITOA WIMBO, ” NATAKA KULEWA” AMBAO ULIKUWA BASED ON TRUE STORY.
Ndani ya Dar Es salaam, mambo matamu hayakukwisha hamu
HAPA ALIKIBA ANAELEZEA NAMNA AMBAVYO DIAMOND HAJAISHIWA NA HAMU YA KUTEMBEA NA WANAWAKE AMBAO ANAWAPATA BAADA YA YEYE KUWA MAARUFU KUPITIA MUZIKI.
We bado mtoto wa mama hujayajua mengi
HAPA ALIKIBA ANAUA NDEGE WAWILI KWA JIWE MOJA., KWANZA ANATOA UFAFANUZI WA MTU ANAYE MZUNGUMZIA. ALIKIBA ANATAKA UJUE KUWA ANAMZUNGUMZIA DIAMOND NA SIO MTU MWINGINE YOYOTE YULE, SO ANAELEZEA JAMBO LINALO ASHIRIA MTU ANAYE MZUNGUMZIA HAPA ” we bado mtoto wa mama “ DIAMOND NI MTOTO WA MAMA, YUPO KARIBU ZAIDI NA MAMA YAKE NA HANA MAWASILIANO MAZURI NA BABA YAKE. ( UKISIKILIZA VIBAYA HAPO UNAWEZA KUDHANI ALIKIBA ANA MAANISHA “MTOTO KWA MAMA”, BUT KIUKWELI ANAMAANISHA “MTOTO WA MAMA” )
NA ANAPOSEMA HUJAYAJUA MENGI, ANAELEZEA MTAZAMO WAKE KUHUSU UPEO WA DIAMOND, KUHUSU MAISHA YA MWANADAMU. ALIKIBA ANA AMINI KUWA DIAMOND BADO HAJAJUA MENGI KUHUSU MAISHA, NDIO MAANA ALIWADHARAU SHAROBARO RECORDS WALIO MTOA PAMOJA NA BABA YAKE MZAZI.

Mwenda tezi na omo marejeo ngamani
HAPA ALIKIBA ANAMKUBUSHA DIAMOND ASISAHAU ALIPOTOKA.

Amesema sana mama, dunia tambala bovu

Kuna asali na shubiri ujana giza na nuru
 
HAPA ALIKIBA ANAMSHAURI DIAMOND, ASICHEZE NA UJANA WAKE NA AKUMBUKE KUWA KUNA WAKATI WA KILA JAMBO, LEO YUPO JUU KIMUZIKI NA KIMAISHA LAKINI KESHO ATAKUWA CHINI. SO AKUMBUKE ALIPOTOKA, ASIJISAHAU.
We mwana wewe mwana, mbona jeuri sana
 
HAPA ALIKIBA ANA ELEZEA NAMNA AMBAVYO DIAMOND AMEKUWA JEURI BAADA YA KUPATA MAFANIKIO YA KIFEDHA NA KIMUZIKI.
Ulichokifata hukupata , umekosa ulivyo achaa

Kwa baba yako mwana, na mama yako mwana
 
Kwa vicheche ulivyo vitaka , ni vingi ulivyo achaa,
 HAPA ALIKIBA ANAMWAMBIA DIAMOND ” UMEKIMBIA SHAROBARO RECORDS NA KWENDA KWINGINEKO ILI UPATE UPATE MAFANIKIO ZAIDI YA KIMUZIKI NA HATIMAYE UPATE FURSA YA KUN’GOA MADEMU, LAKINI UMEISHIA KUPATA VICHECHE TU KAMA AKINA WEMA SEPETU NA JOKATE. WAKATI VICHECHE KAMA HAO ULIKUWA NA NAFASI YA KUWAPATA HATA KAMA UNGEBAKI SHAROBARO RECORDS. MATOKEO YAKE SASA, WALE MADEMU AMBAO ULIKUWA UNAWATAKA WAKATI UPO SHAROBARO RECORDS ( AMBAO WALIKUWA NA AFFILIATION NA SHAROBARO RECORDS) UMEWAKOSA NA MADEMU AMBAO ULITARAJIA UNGEWAPATA UKIWA NJE YA SHAROBARO RECORDS HUJAWEZA KUWAPATA. 
Oyayee, mbona unajitesa sana

Mbona unawatesa sana
 
( IMESHAELEZEWA JUU )

UNALETA LAWAMA, UNALETA LAWAMA X 2
 
Uchungu wa mwana aujuaye mzazi.
 
Uchungu wa mwana aujuaye mzazi, siku zote leilee
 
Analiaa oooh oooh oooh oooh
 
Kutwa nzima analalamika
 
Obaba baba na mama yako yako, oooh mwana rudi eeeh
 
Watafurahi wakikuona umerejea salama.
 
HAPA ALIKIBA AMEFANYA KAMA KUPOTEZA MABOYA VILE ILI ASIONEKANE KAMA ANAMPIGA MADONGO DIAMOND MOJA KWA MOJA.

Tuesday, September 23, 2014

PHOTOS:Ashley Toto Uso Kwa Uso Na Diamond Platnumz Nchini Ujerumani

Diamond na Ashley Toto
Msanii wa filamu za kiswahili nchi za Scandinavia Ashley Toto ambaye ni mkenya lakini akiwa na makazi yak nchini Denmark amekutana uso kwa uso na superstar wa muziki wa Bongofleva Tanzania Diamond Platnumz ambaye alikuwa nchini Ujerumani juzi kwa aja=ili ya show.


Wawili hao walikutana ambapo Ashley alikuwa akimsaidia kwa ukaribu mwandaaji wa show hiyo mnigeria kutokana na Ashley kuwa na uzoefu wa mabo ya u-promota.

Friday, September 5, 2014

DIAMOND ACHAGULIWA TENA KUWANIA TUZO ZA CHANNEL O,YUPO KWENYE CATEGORY 4






Tuesday, September 2, 2014

PROMOTER BRITTS EVENTS WAFUNGUKA JUU YA KASHIFA NZITO YA KUHARIBU SHOO YA DIAMOND NCHINI UJERUMANI

1384142_505866609511143_1668869613_n
Awin Williams Akpomiemie.
MY PEOPLE FIRST OF ALL, I WOULD LIKE TO EXPRESS MY HEART BY TELLING THE GENERAL PUBLIC AND THE FANS OF DIAMOND PLATNUMZ, THAT WE FROM BRITTS EVENTS MANAGEMENT IS VERY SORRY FOR WHAT HAPPENED LAST NIGHT, DURING THE CONCERT OF DIAMOND PLATNUMZ. IT WAS NEVER PLANNED FOR THE CONCERT TO BE DELAYED OR FOR THE ARTIST NOT TO PERFORM. 
HERE I WOULD TELL YOU ALL THE TRUTH OF WHAT REALLY HAPPENED ABOUT THIS EVENT FOR YOU ALL TO KNOW THE TRUTH.
THE PROJECT OF DIAMOND CONCERT WAS A VERY EXPENSIVE PROJECT,
BECAUSE THE BRITTS EVENTS MANAGEMENT WANTED EVERYTHING TO BE PROFESSIONAL, AS A COMPANY WE DECIDED TO LOOK OUT FOR INVESTORS WHO WOULD INVEST IN THIS PROJECT, THEN WE APPROACHED THREE INVESTORS WHO INVESTED BUT ONE OF THEM DID’NT INVEST TOO MUCH AS HE SAID HE WONT BE IN THE COUNTRY.
THE TWO INVESTORS ARE WELL KNOWN PEOPLE LIVING IN STUTTGART
ONE WORK WITH THE USA MILITARY THE SECOND ONE OWNS A SHIPPING COMPANY IN STUTTGART, THESE WERE THE TWO MAJOR INVESTORS THAT WE GOT, WE GAVE THEM A CONTRACT TO SIGN AND ONE OF THEM SIGNED BUT THE SHIPPING GUY REFUSE TO SIGN THE CONTRACT OF THE PROJECT THAT HE WANTS TO HAVE A PRIVATE CONTRACT WITH THE USA GUY, THEN I TOLD MR.USA THAT WAS A WRONG MOVE BUT MR.USA SAID BRITTS DO NOT WORRY,ALL WILL BE FINE,

MY PEOPLE THE PROJECT STARTED AND THEN THE TWO INVESTORS THEN NOTICE THAT DIAMOND IS A BIG ARTIST AND HE WOULD PULL LOTS OF CROWD AND PEOPLE LOVE HIM, THEN THEY TEAMED UP AGAINST BRITTS WHO INVITED THEM AS INVESTORS ON THIS CONCERT AND WANTED TO TAKE THE PROJECT AWAY FROM BRITTS BECAUSE THEY ARE THE ONE WHO BRINGS PART OF THE MONEY FOR THIS PROJECT WHILE BRITTS IS THE ONE WHO OWNS THE ARTIST AND THE PROJECT,.

JUST BECAUSE BRITTS IS A NEW COMPANY IN STUTTGART MR. SHIPPING GUY DECIDED TO TEAM UP WITH THE USA GUY AND DJ -WANTED, TO TAKE OVER THE PROJECT, WHEN BRITTS SITS DOWN AND HOLD MEETINGS WITH THEM, THEY WOULD DO THEIR OWN MEETING AND THEN,CHANGE ALL THE PLANS BEHIND BRITTS MANAGEMENT, SO THEY WERE OPPRESSING AND PUSHING THE PROJECT BEHIND BRITTS.

, BRITTS HAVE AGREEMENT WITH THEM THAT WHEN THE ARTIST ARRIVE GERMANY THEY WOULD GIVE HIM THE BLANCE OF 3.250 EUROS, AND THEY AGREED TO THIS TERM BECAUSE DIAMOND MADE IT CLEAR THAT WITHOUT THE MONEY HE WOULD NOT FLY, THEY ASKED ME TO TALK TO DIAMOND THAT THEY WOULD GIVE HIM THE MONEY RIGHT AT THE AIRPORT, BUT DO YOU KNOW WHAT? BEFORE DIAMOND ARRIVED, MR.USA AND MR.SHIPPING GUY TOGETHER WITH DJ WANTED, ARRANGED FOR THUGS TO STEAL THE ARTIST FROM BRITTS EVENTS BUT BRITTS WAS SMARTER AND TOOK AWAY THE ARTIST BEFORE THEY COULD MAKE ANY MOVE, THAT WAS WHERE THE TROUBLE STARTED FROM, IN ESSEN BEFORE BRITTS ARRIVED THERE, USA GUY AND SHIPPING GUY ,ALREADY BRING IN NEW WORKERS AND
SECURITY TO TAKE OVER THE SHOW, AND DROVE AWAY THE ORIGINAL WORKERS .
THEN BRITTS WAS FIGHTING WITH THEM THAT THEY ARE JUST INVESTORS AND NOT THE COMPANY MANAGER, WHY DO YOU WANT TO STEAL THE EVENT BECAUSE YOU WANT TO MAKE MONEY AND NOT CARING ABOUT THE PEOPLE, BRITTS THEN NOTICE THAT THE WORKERS THEY BROUGHT WERE THEIR EX-GIRL FRIENDS AND RELATIVES.
10649568_792593844095765_1264697582686012878_n
THE REASON WHY THEY DID THIS WAS TO STEAL THE MONEY AND NOT TO FOLLOW THE CONTRACT WITH BRITTS, SO WHEN DIAMOND ARRIVED STUTTGART LATE NIGHT AT 11.PM, HE WAS NOT TOO FINE BUT THE TWO INVESTORS DO NOT CARE.
THEY WERE ONLY THINKING ABOUT HOW THEY WOULD GET THEIR MONEY BACK,DIAMOND SAID HE NEEDS HIS MONEY BUT SHIPPING GUY REFUSE USA GUY TO GIVE DIAMOND THE MONEY , THINKING THAT BRITTS EVENTS WANTS EXTRA MONEY .
THEN WHEN IT WAS ALREADY TOO LATE THEY MANAGED TO BRING OUT 3.000 EUROS THEN IT WAS 3.30AM ALREADY , BUT DIAMOND REFUSED TO STILL PERFORM BECAUSE HE SAID THEY MUST GIVE HIM HIS BLANCE OF 250 EUROS , WHICH IS RIGHT CAUSE THAT WAS THE AGREEMENT.
BY THE TIME MR SHIPPING GUY AND MR USA GUY REALISED THAT BRITTS WAS DOING THE RIGHT THING BY ASKING THEM TO PAY UP THE MONEY TO DIAMOND IT WAS ALREADY TOO LATE CAUSE PEOPLE HAVE STARTED FIGHTING,WHILE DIAMOND WAS RIGHT INSIDE THE CAR IN FRONT OF THE VENUE,IF I LET HIM OUT THEY WOULD KILL HIM, AS WE ARE TALKING RIGHT NOW, MR. USA SAID THE MONEY WE MADE FROM THE WHOLE EVENT WAS STOLEN BY THE PEOPLE, SO BRITTS EVENTS CAN’T GET MONEY FROM THE EVENT WE ORGANISED AND OWNED .
THESE WHERE THEIR PLANS TO TAKE OVER ANOTHER MANS BUSINESS DUE TO GREED.

BRITTS EVENTS LOVE YOU GUYS, BRITTS EVENTS WANTED EVERYONE TO BE HAPPY, BRITTS EVENT HAVE NEVER PROMISED ANY ARTIST AND THE ARTIST DID’NT COME,.
AND TRUST ME WHEN WE DID BRACKET EVENT WE HAD THE SAME EXPERIENCE THE SAME THING FROM THE INVESTORS , AS SOON AS THEY SEE THAT THE EVENT WOULD BE A SUCCESS THEY STARTED ASKING FOR 50% OF THE COMPANY.
WELL AM NOT SUPPOSE TO SAY ALL THESE HERE AS ITS A MANAGEMENT ISSUE,BUT I DECIDED TO CLEAR THE AIR I CAN’T KEEP IT ANY MORE , WE HAVE LOTS OF GREEDY AFRICANS OUT THERE WHO WANTS TO TAKE AWAY PEOPLES BUSINESS JUST BECAUSE OF GREED.

OUR AIM IS TO MAKE YOU ALL HAPPY, NOT TO WASTE YOUR TIME AND MONEY , WE KNOW THAT YOU ALL CAME FROM FAR PLACES, LEFT YOUR KIDS AND FAMILY . BRITTS EVENTS MANAGEMENT IS REALLY VERY SORRY ABOUT THIS.

SO DO NOT BLAME THIS ON BRITTS EVENTS BUT BLAME IT ON THE GREED OF MR USA GUY AND MR. SHIPPING GUY. WE LOVE YOU AND WE PROMISE YOU A FREE SHOW EVENT WITH DIAMOND VERY SOON…. JUST LOOK OU

Monday, September 1, 2014

DIAMOND ADAIWA KUOKOLEWA NA POLISI WA UJERUMANI,KUFUATIA MASHABIKI WAKE KUSHIKWA NA HASIRA

 Gari ya Polili ilioibuka kumuokoa Diambond kufuatia sakata la mashabiki wake kupandwa na jazba
Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini stuttgart,ujerumani
UJERUMANI SI SHWARI KIMENUKA !!
POLISI UJERUMANI WAMUOKOA DIAMOND KUTOKA KWA WASHABIKI WENYE HASIRA ! KASHINDWA KUWIKA STUTTGART KISA ?

KAFIKA UKUMBINI SAA 10 ALFAJIRI ! WASHABIKI WANASURI SHOW TANGU SAA 4 USIKU

PROMOTA MNAIJERIA AINGIA MITINI ,DJ APATA KISAGO HETI VYOMBO VIBOVU ! HAIBU

Stuttgart,Ujerumani,
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show,washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki  Diamond na promota wake,Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muzikima-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.
Mmoja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ  Flor alipatwa shock mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo  DJ Drazee naye yupo hoi hospatal. Polisi nchini ujerumani wanamesema tukio hili la haibu alijawahi kutokea,kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwawanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara

Saturday, August 23, 2014

EXCLUSIVE:Diamond Platnumz Atangaza Kumuoa Wema Sepetu, Ndoa Kuhudhuriwa Na Mashabiki Uwanja Wa Taifa

Diamond amesema yupo mbioni kuoa hivi  karibuni, msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na Mwanaspotinyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo.


“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond.



Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.

“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.

“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.”

Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa. Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa.

Sunday, August 17, 2014

#TEAMDIAMONDTZ YAMPA MAKAVU WEMA..SOMA HAPA UJIONEE UONDO...



Friday, August 15, 2014

MENINAH AFUNGUKA ADAI KUWA DAIMOND SIO LEVO YAKE.....

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Meninah Abdulkareem ‘Meninah’ amefunguka juu ya tetesi zinazoeneo kuwa na uhusiano wa chinichini na Nasib Abdul ‘Diamond’ kwa kusema kuwa siyo levo yake.
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Meninah Abdulkareem ‘Meninah’ akiwa ndani ya studio za Global Tv Online.
Akichonga na paparazi wetu, Meninah anayetamba na ngoma ya Pipi ya Kijiti alikanusha na kusema kuwa, wote ni mastaa lakini wametofautiana kwa kiasi kikubwa na kwamba hawezi kuwa naye katika mahusiano ya aina yoyote.
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’
“Kwanza nilishawahi kukutana naye kwenye shoo tofauti na zote sikuwahi hata kuzungumza naye chochote, ni staa na mimi staa lakini tunatofautiana kuwa yeye yupo juu yangu,” alisema Meninah.

Sunday, July 27, 2014

KAULI YA WEMA SEPETU BAADA DIAMOND KUSHINDA TUZO



Saturday, July 19, 2014

CHEKI BABA YAKE DIAMOND ANAVYO TESEKA...WATU WASEMA LAANA HIYO...ANATAKIWA AMSAMEHE

Oooh! Nooh! Wakati akimpa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ gari la Sh. milioni 38 huku akitawanya mamilioni ya fedha kwenye matukio mbalimbali, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anadaiwa kunyemelewa na laana kufuatia baba yake, Abdul Jumaa kuugua na kuvimba miguu bila msaada wowote.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akila ujana na mpenzi wake Wema Sepetu.
 Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa, baba wa staa huyo anayeishi Magomeni-Kagera jijini Dar, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu na hakuna msaada wowote anaoupata kwani chanzo cha mapato anachokitegemea ni kodi tu ya nyumba ambayo anaipata kutoka kwa wapangaji wachache alionao.
 BOFYA HAPA KUKISIKIA CHANZO
“Yaani tunashangaa kusikia Diamond ana fedha nyingi, juzikati tuliona katika gazeti kamnunulia mama yake gari la milioni 38 (Toyota Lexus-Harrier) sasa kwa nini asimthamini baba yake hata kidogo? 


“Ukweli ni kwamba baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba.

 “Amekuwa akilalamika mara kwa mara lakini Diamond hatujawahi kumuona,” kilinyetisha chanzo hicho na kuongeza:“Juzikati hapa baba Diamond alishikika kwelikweli miguu, akaugulia mwenyewe ndani pasipo kuwa na msaada wowote tena nasikia mzee huyo hataki hata kuongelea lolote kuhusu Diamond maana haoni umuhimu wa kufanya hivyo wakati amemsusa muda mrefu sana.”
 MATIBABU HAYAZIDI MILIONI
Katika aya nyingine, chanzo hicho kilidai kwamba ugonjwa wa miguu ambao unamsumbua mzazi huyo, gharama za matibabu haziwezi kufikia hata shilingi milioni moja za madafu achilia mbali mamilioni anayoyatapanya staa huyo.


Mama yake Diamond,Sanura Kassim ‘Sandra’ akilitesti gari alilokabiziwa na Mwanaye kama zawadi.
 “Ingekuwa tatizo kubwa sana, hapo sawa, kwa sababu miguu huwa inamvimba lakini akipata dawa za kutumia huwa inarudi katika hali ya kawaida, kwa nini lakini anamfanyia hivyo baba yake? Amemkosea nini?” Kilihoji chanzo hicho.
 UTAJIRI WAKE WAANIKWA
Wakati chanzo hicho kikiweka nukta hapo kwa muda, mapaparazi wetu walipewa malalamiko mengine kutoka kwa jirani mmoja wa baba Diamond ambaye alimsihi amsaidie mzazi wake kwani anaamini uwezo anao kupitia kumbukumbu ambazo Diamond mwenyewe alizithibitisha kupitia vipindi mbalimbali vya runingani kama Take One na Spora Show vya CloudsTV.

 Pia kwenye vyombo vingine vya habari zikiwemo redio na magazeti pendwa ya Global Publishers.
Jirani huyo alidai kwamba mwaka jana Diamond alitangaza kuwa ana utajiri wa Sh. bilioni moja ikiaminika kwamba mwaka huu umeongezeka mara dufu.

 “Nakumbuka mwaka jana kupitia Kipindi cha Spora Show na kile cha Take One, Diamond alikiri kuwa ana mkwanja usiopungua bilioni moja, hiyo ilikuwa kwa mwaka jana, sasa mwaka huu unadhani atakuwa na shilingi ngapi? Aache hizo bwana, amsaidie baba yake hata kwa kumpa mtaji mdogo wa biashara ambao unaweza kumsaidia,” alisema jirani huyo.
 MATANUZI  YA DIAMOND, WEMA
Katika kuendelea kuichimba habari hiyo, mapaparazi wetu walinasa malalamiko kutoka kwa jirani mwingine wa mzazi huyo ambaye alieleza masikitiko yake kwa kulinganisha starehe ambazo staa huyo anazifanya na asali wake wa moyo, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na maisha halisi ya baba yake.

 “Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa habari za mastaa, naona kila siku kwenye vyombo vya habari jinsi gani Wema na Diamond wanavyotumia fedha nyingi katika masuala ambayo hayana ulazima kiivyo.
“Sisi kama majirani hatupendezwi na hali hii, angekuwa anakuja angalau siku mojamoja kumuona baba yake kuliko kila siku kumhudumia mama yake pekee,” alisema jirani huyo.


Baba yake Diamond, Abdul Jumaa akitafakari jambo.
 TATIZO NI NINI?
Mapaparazi wetu waliingia mzigoni kusaka kiini halisi kwa nini Diamond amwage fedha nyingi kwa mama yake pasipo kumkumbuka japo kiduchu baba yake ambapo ilielezwa kuwa staa huyo wa Mdogomdogo hakuwa na ugomvi wowote na mzazi wake huyo.

 “Kama ni ugomvi ulikuwepo kati ya mama na baba lakini Diamond hahusiki, tunashangaa kuona kama staa huyo naye anaweza kumsusia baba yake,” kilieleza chanzo na kuongeza:
 “Mbaya zaidi nasikia Diamond amekuwa mzito kupokea simu za baba yake, sasa huoni kama siyo jambo la busara, mzazi ni mzazi tu hata iweje. Kwa mtazamo wangu kinachofuata ni laana.
 “Kuna mifano ya watu wengi ambao waliingia kwenye laana za wazazi wao na wakajikuta kama siyo kufulia kama (wanatajwa mastaa waliofulia wa muziki Bongo) au hata kukutwa na umauti.
“Jambo hili si la kibinadamu tu, kwa wale wanaosoma vitabu vitakatifu watakuwa na mifano mingi ya watu waliowakosea wazazi wao wakalaaniwa.”

 BABA DIAMOND ANASIKITISHA
Ijumaa lilipomtafuta baba Diamond kwa njia ya simu aliongea maneno ya kusikitisha huku akikataa katakata kumzungumzia kijana wake huyo.

 “Jamani naomba mumuache Diamond na maisha yake, sitaki kabisa kusikia habari zake maana hata nikiongea naonekana najipendekeza kwake.
 “Namshukuru Mungu, kama ni kuumwa kwa sasa naendelea vizuri na maisha yangu, niacheni nipumzike,” alisema mzee huyo kwa unyonge.
 DIAMOND ANASEMAJE?
Alipotafutwa Diamond ili kumsikia anazungumziaje madai hayo, simu yake iliita bila kupokelewa. Tunaamini atasoma habari hii hivyo si vibaya akatutafuta ili afunguke kwa upande wake.

MAONI YA MHARIRI
Diamond ni staa mkubwa kwa sasa ndani na nje ya Bongo, uwezo alionao kifedha unapaswa kuendana na baraka za wazazi wa pande zote mbili. Vitabu vya Mungu vinatufundisha kwamba wazazi ndiyo Miungu wetu hapa duniani hivyo hata kama kuna kosa amefanya, mzazi atabaki kuwa mzazi tu. Hatutakiwi kumkosoa!


Wednesday, July 16, 2014

Wanaigeria Wamtaka Diamond Nchini Germany, Ashley Toto Aitwa Kuweka Mambo Sawa.

Diamond
Superstar wa Bongo Fleva Diamond Platnumz anatarajiwa kufanya show mbili nchini Ujerumani mwezi wa nane mwaka huu. Kwa mujibu wa habari ilizopata SWP ni kuwa show hiyo inaandaliwa na promota wa Nigeria kupitia kampuni ya Britts Events. 
Tarehe 29 mwezi wa 8 Diamond atafanya show Essen na tarehe 30 atafanya show Sttutgart. Hata hivyo habari zaidi zinasema kuwa muigizaji wa filamu za kiswahili nchi za Scandinavia Ashley Toto ambaye anaishi Ujerumani ameombwa na waandaaji hao kuwasaidia katika show hizo kutokana na uzoefu wake kwenye mambo ya kuandaa shows za wasanii wa Afrika Mashariki.

                                                                Ashley Toto

                                                      Ashley na Diamond

Sunday, July 13, 2014

DIAMOND PLATNUMZ AHUDHURIA RED CARPET YA UZINDUZI WA FILAMU YA THINK LIKE A MAN

Msanii Diamond Platnumz akihojiwa wakati wa uzinduzi wa filamu ya THINK LIKE A MENjana.
Msanii Diamond Platnumz pamoja na wageni alioambatana nao akiwemo Mkurugenzi wa Ufundi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba wakati wakiwasili katika uzinduzi huo.
Terrence akizungumza kabla ya uzinduzi wa filamu ambayo naye ameshiriki kuanza.
Diamond akisalimiana na baadhi ya mashabiki baada ya uzinduzi.
Mtangazaji wa Television kubwa duniani ya E, Terrence J yupo nchini Tanzania, ambapo pamoja na mambo mengine, jana 'alihost' uzinduzi wa filamu ya THINK LIKE A MEN ambayo na yeye ni mmoja wa nyota walioigiza humo