Showing posts with label Rose ndauka. Show all posts
Showing posts with label Rose ndauka. Show all posts
Sunday, August 25, 2013
Monday, August 12, 2013
ROSE NDAUKA AANZA KUPETA ANGA ZA MUZIKI.
MSANII wa filamu nchini Rose Ndauka kwa mara ya kwanza amefanya shoo
ya aina yake ya nyimbo ya bongo fleva aliyoshirikiswa na kundi la TNG,
katika tamasha la sikukuu ya Iddi lililofanyika Dar Live jijini Dar es
Salaam.
Msanii huyo sasa ameamua kufanya muziki ambapo ameweza kushirikishwa
single inayoenda kwa jina la 'Crazy Love ' na kundi hilo ambapo siku
hiyo ilikuwa maalumu kwake kwa ajili ya kutambulisha nyimbo hiyo.
Akizungumza na mwaandishi wa habari hii baada ya kumaliza kufanya
shoo hiyo, Rose aliweka wazi kuwa kuimba 'live' jukwaani kunatofauti na
kazi ya filamu ambayo ameizoea.
Alisema upande wa filamu ni rahisi kurekebisha makosa endapo ukihisi
kukosea tofauti na kuimba live jukwaani kwani ukikosea hauwezi kupata
nafasi ya kurekebisha hivyo umakini unahitajika katika kazi hiyo.
"Mimi ni msanii na kuimba ni kipaji changu kingine, lakini kwenye
uimbaji inahitajika umakini zaidi tofauti na nilikokuzoea" alisema
Ndauka.
Aliongezea kuwa anamshukuru mtayarishaji wa muziki P Funk kwa kuweza
kutambua kipaji chake hicho cha uimbaji na kuweza kumpa nafasi ya
kushiriki katika nyimbo hiyo.
Kundi la hilo linaundwa na wasanii wawili akiwemo Chiwaman pamoja na
'Latino Man', ambapo wameachia single yao ikiambata na uzinduzi .
"JAPO NILITUHUMIWA KUGAWA PENZI GESTI, LAKINI NIMEPIMA NA SINA UKIMWI.... NANI MJANJA??"...ROSE NDAUKA
Baada ya kukabiliwa na skendo ya kugawa uroda kwa msanii Nasry ndani ya Gesti, Rose ndauka ameamua kukimbilia hospitalini ili kuchukua vipimo vya gonjwa hatari la Ukimwi.....
Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii, Ndauka aliposti picha ya majibu ya vipimo vya UKIMWI vilivyochukuliwa katika hospitali ya TMJ iliyopo jijini Dar es salaam....
Majibu ya vipimo hivyo yalionesha kuwa Rose Ndauka yuko NEGATIVE.
Baada ya picha hiyo, comment kibao zilianza kumiminika toka kwa mashabiki wake.Wapo waliompongeza na wapo waliomponda.....
Waliomponda walihoji ni kwa nini kawahi kupima na kuyaanika majibu mtandaoni wakati MIEZI MITATU TANGU ATUHUMIWE HAIJAISHA??????.
Kwa kawaida, hawa wadudu huonekana katika mzunguko wa damu baada ya siku 90 tangu ufanye tendo la ndoa.



