MSANII wa filamu nchini Rose Ndauka kwa mara ya kwanza amefanya shoo
ya aina yake ya nyimbo ya bongo fleva aliyoshirikiswa na kundi la TNG,
katika tamasha la sikukuu ya Iddi lililofanyika Dar Live jijini Dar es
Salaam.
Msanii huyo sasa ameamua kufanya muziki ambapo ameweza kushirikishwa
single inayoenda kwa jina la 'Crazy Love ' na kundi hilo ambapo siku
hiyo ilikuwa maalumu kwake kwa ajili ya kutambulisha nyimbo hiyo.
Akizungumza na mwaandishi wa habari hii baada ya kumaliza kufanya
shoo hiyo, Rose aliweka wazi kuwa kuimba 'live' jukwaani kunatofauti na
kazi ya filamu ambayo ameizoea.
Alisema upande wa filamu ni rahisi kurekebisha makosa endapo ukihisi
kukosea tofauti na kuimba live jukwaani kwani ukikosea hauwezi kupata
nafasi ya kurekebisha hivyo umakini unahitajika katika kazi hiyo.
"Mimi ni msanii na kuimba ni kipaji changu kingine, lakini kwenye
uimbaji inahitajika umakini zaidi tofauti na nilikokuzoea" alisema
Ndauka.
Aliongezea kuwa anamshukuru mtayarishaji wa muziki P Funk kwa kuweza
kutambua kipaji chake hicho cha uimbaji na kuweza kumpa nafasi ya
kushiriki katika nyimbo hiyo.
Kundi la hilo linaundwa na wasanii wawili akiwemo Chiwaman pamoja na
'Latino Man', ambapo wameachia single yao ikiambata na uzinduzi .