Showing posts with label aunt ezekiel. Show all posts
Showing posts with label aunt ezekiel. Show all posts

Sunday, November 10, 2013

AUNT EZEKIEL: NILIKWENDA KWA DEMONTE KUSAKA MTOTO

Sura ya mauzo katika sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amefunguka kuwa alikwenda Dubai kwa mumewe Sunday Demonte kwa ajili ya kusaka mtoto kwani kwa sasa hatumii kinga kwa sababu anahitaji kuitwa mama.
Aunt Ezekiel akiwa na mumewe Sunday Demonte.
Akistorisha na Ijumaa Wikienda mara tu baada ya kutia maguu kwenye ardhi ya Jakayaland mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo alilazimika kurudi mapema kutokana na msiba wa rafiki yake kipenzi aliyemtaja kwa jina moja la Sofia, Aunt alisema kuwa kwa sasa muda umefika wa kuzaa.
“Hata mume wangu anatamani sana mtoto, tumekaa na kukubaliana juu ya ishu hiyo hivyo muda wowote naweza kuwa mjamzito, japo siwezi kuweka wazi kama ni tayari au bado kuepuka wanga,” alisema Aunt.

Thursday, October 31, 2013

AUNT EZEKIEL APOST PICHA MTANDAONI AKIWA CHUMBANI NA MUMEWE....!!!


STAA kunako tasnia ya filamu Aunt Ezekiel amepost picha za chumbani mtandaoni akiwa amelala kitandani na mumewe Sunday Demonte huku picha moja ikiwa imeandikwa happy birthday 2u my lvly wife,the lv ov ma life! ours is an everlasting.

Aunt amepost picha hizo kupitia mtandao wa instagram akiwa na mumewe huyo huku akiandika Thanx ma lv… Ma Mume akeee.. huku watu wakitoa coment wakimsifia kwa kumtunza mume wake hadi amenenepa tofauti na alivyokuwa mwanzo.
Angalia coment za watu baada ya Aunt kupost picha hizo
• saphyipsah Wawaaaache mlaleeeeeeeeeeee 2d
• lin_libra Shemeji ananenepa.. Hongera kwa matunzo 2d
• fettybihaki Hatareeeee 2d
• 23eclat mnapwndeza 2d
• amandaposhy Hapana chezea..miaka 1000000000 @auntezekiel 2d
• gorgeoucminer Aunty na auncle ake.... 1d
• coplosalum Mpo juu 16h

Saturday, September 28, 2013

"SINA NUKSI KAMA WATU WANAVYODAI".....AUNT EZEKIEL


STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amesema hana mkosi kama watu wasiomtakia mema wanavyoeneza maneno mitaani.

Akipiga stori na paparazi wa Ijumaa juzikati, Aunt alisema kuna baadhi ya watu wasioitakia mema ndoa yake wamekuwa wakieneza maneno kwamba ana mkosi ndiyo maana kila mwanaume anayekuwa naye hupatwa na balaa.
Staa huyo aliongeza kuwa haumizwi kichwa na maneno hayo kwa kuwa anaamini kila kinachotokea katika maisha yake ni mipango ya Mungu.
Maneno yao ni imani potofu na siwezi kumfikiria mwanaume niliyewahi kuwa naye huko nyuma kabla ya kuolewa na mume wangu Demonte kwani hakuna baya lililomfika tangu tulipooana,” alisema Aunt.

Monday, September 23, 2013

ALIYE MJERUHI AUNT EZEKIEL NA CHUPA HATIMAYE AFIKISHWA KORTINI

Hatimaye yule mbaya wa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel aitwaye Yvonne Maximilian (22) amenaswa na kuhenyeshwa kortini kisa kikiwa ni kumpiga chupa mwigizaji huyo.

Yvonne aliburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya kukamatwa maeneo ya nyumbani kwake Kinondoni-Manyanya.

Habari za ndani kutoka kortini zilieleza kuwa awali kesi hiyo ilikuwa isikilizwe na hakimu Agustino Mbando lakini baadaye kulitokea mabadiliko ambapo ilisomwa na Fundi Fimbo.


Akiwa mahakamani hapo huku Aunt naye akihudhuria kama mlalamikaji, Yvonne alishuhudiwa akipelekwa puta na polisi.

Hata hivyo, baada ya kesi hiyo kusomwa iliahirishwa hadi Oktoba 17, mwaka huu, itakaposikilizwa tena.


Agosti 26, mwaka huu, Yvonne anadaiwa kumjeruhi Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, Posta jijini Dar.

Tuesday, September 17, 2013

JB AWATAHADHARISHA WEMA SEPETU,IRENE UWOYA,AUNT EZEKIEL NA JOHARI WAKAZE BUTI LA SIVYO WATAPOTEA

   
Muigizaji maarufu Swahiliwood Jacob Stephen(JB) amewatahadharisha mastaa wenye majina makubwa katika tasnia ya filamu nchini kuwa wakaze buti baada ya kuanza kupotea kisanii licha ya kuwa na majina makubwa ambapo kwasasa chipukizi kadhaa wanaibuka na kufanya vizuri kuliko wao.
JB aliwataja wazi wazi baadhi ya mastaa wa kike kama vile Wema Sepetu, Irene Uwoya, Aunt Ezekiel na Blandina Chagula(Johari) ambao amesema wameanza kupotea kwenye fani tofauti na mwanzoni huku wengine wakibaki na majina yao tu lakini hawana filamu zozote sokoni kwa muda mrefu.
    JB aliyazungumza hayo hivi karibuni katika kipindi cha Take One kinachorushwa NA Clouds Tv. "mimi nimewataja na siogopi, kwani hawa dada zetu wamepotea na kubaki na majina yao tu, nawaomba kama wanataka kutoka kwasasa waendane na mazingira ya sasa" alisema JB
JB alisema kuwa wasanii hao wamekalia kuvaa nguo fupi tu huku wakishindwa kubadilika kutokana na wakati ambapo chipukizi wengi wanaonekana kuwa wabunifu na kuwapita licha ya ukongwe wao.
 
 


Aliongeza kwa kusema kuwa wakati wasanii hao wanaanza kuigiza katika filamu yeye alianza kuigiza kama baba wa lakini kwasasa anafanya vizuri katika sanaa sababu ya juhudi zake kubwa ambazo zimemfikisha alipo sasa.


"mimi kusema kweli kila filamu nilikuwa naigiza kama baba, lakini nikawa najifikiria nitaigiza kama baba mpaka lini, lakini nikajichanganya na nimetoka" alisema star huyo wa filamu za Shikamoo Mzee na Nakwenda Kwa Mwanangu.

Thursday, September 5, 2013

AUNT EZEKIEL YUPO HATARINI KUKATWA MKONO...



Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa’ yupo hatarini kukatwa mkono kutokana na jeraha la chupa alilolipata hivi karibuni.

Tukio la Aunt kupigwa chupa na mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Yvonne nje ya Club Bilicanas, Posta jijini Dar, lilitokea Agosti 26, mwaka huu wakati staa huyo alipokwenda kujiachia na mshosti zake.

Baada ya kupigwa chupa siku hiyo, Aunt alikimbizwa katika Hospitali ya Aga Khan lakini bahati mbaya alikosa daktari wa kumtibu hivyo akalazimika kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Dk. Mvungi, Kinondoni ambapo alishonwa nyuzi sita pamoja na dawa za kukausha kidonda. 
Kwa mujibu wa chanzo makini, Aunt ni muoga wa dawa na wakati kidonda kikiwa bado hakijapona vizuri aliacha kumeza dawa alizopewa.

Chanzo hicho kilisema tatizo la staa huyo kukatisha dozi lilisababisha kidonda kishindwe kupona na badala yake kikaanza kutengeneza usaha na taratibu mkono ukaanza kuoza.

“Mkono ulifikia hatua ukaanza kuoza kwani licha ya kushonwa lakini kilibadilika rangi ndipo alirudi hospitali.

Imeelezwa kuwa mapema wiki hii, Aunt alirudi tena katika Hospitali ya Dk. Mvungi na kusafishwa upya kidonda baada ya madaktari kugundua tatizo lilizidi kuongezeka.
 

Kwa mujibu wa nesi wa hospitali hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, hali ya Aunt ilimshtua daktari, akamwambia aombe Mungu kwani kidonda kilichimbika sana na tatizo kama hilo huweza kusababisha mtu kukatwa mkono. 

“Iligundulika mkono ulikuwa unaoza, daktari alimwambia amuombe Mungu kwani hatua iliyokuwa imefikia ni mbaya hivyo asipokuwa makini tatizo hilo litamfanya akatwe mkono,” alisema nesi huyo.

Aunt alipigwa chupa akigombania  penzi  la  mwanaume  na  Yvone  .

-Gpl & Aman

Tuesday, September 3, 2013

SIRI YAFICHUKA: KISA CHA AUNT EZEKIEL KUPIGWA CHUPA NI PENZI LA JEFF LINALOGOMBANIWA NA WAREMBO


Siri  ya  Aunt Ezekiel  kupigwa  chupa  club  na  kujeruhiwa  mkono wake imefichuka.Habari  za  uhakika  zinadai  kwamba  Aunt  alipigwa  chupa  na  mrembo  wa  kike  katika  harakati  za  kugombea  penzi  la  mwanaume...

 Mwanaume  aliyekuwa  akigombaniwa  ni  Jeff  ambaye  anadaiwa  kuwa  ni boyfriend  wa  Yvonne ( aliyempiga  aunt  chupa )..

Kutokana  na  aibu  hiyo, mastaa  kadhaa  wameongea  na  E.S.L kwa  nyakati  tofauti  na  kueleza  masikitiko  yao  dhidi  ya  aunt  Ezekiel  ambaye  ni  mke  wa  mtu... 

Katika  maongezi  hayo, mastaa  hao  walidai  kwamba  mambo  anayofanya  aunt  hayaendani  na  matendo  ya  mke  wa  mtu. Aunt amekuwa  ni mtu wa baa, club  na  madanguro  mengine  ya  usiku, hali  inayotia  shaka  uhai  wa  ndoa  yake. 

" Aunt  kapata mume mwelewa sana  ambaye  kakiheshimu sana  kipaji  chake  kwa  kuto-mbana.

"Cha  ajabu yeye ameanza  kufanya  mambo ya aibu  kwa kuendekeza ngono  nje  ya  ndoa  yake" alisema star mmoja wa kike aliyekataa kuwekwa wazi jina lake ..

Muigizaji mwingine wa kike ambaye hakuwa  tayari  kuchorwa  mtandaoni  alisema:
  
 "Aunt ajiangalie sana.Yeye  ni mke wa mtu kwa  sasa. Kitendo  alichokifanya kimemchafua mpaka ukweni na asipokuwa makini  atampoteza mume wake... 

"Yvonne alikuwa anamlinda bwanake, mi  siwezi kumlaumu sana ila nyie wanaume ni watu wabaya sana pia"

Friday, August 30, 2013

ALIYEMPIGA CHUPA AUNT EZEKIEL NDIYE ALIYEMCHANA LULU VIWEMBE


Mtuhumiwa aliyempiga chupa mwigizaji Aunt Ezekiel Jumapili iliyopita nje ya Ukumbi wa Bilicanas ndiye aliyewahi kumchana viwembe mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ mwaka 2011.

Kumbukumbu  zinaonesha kuwa, mwaka 2011 Lulu alivamiwa na wadada wa mjini baada ya kunaswa katika pozi tata na mwanaume wa watu maeneo ya Kariakoo, jijini Dar. Alipoulizwa juu ya sakata hilo, Lulu alitiririka hivi:

“Naweza kumkumbuka mwanamke mmoja, namfahamu kwa jina la Yvonne, alinivamia na kuanza kunishambulia huku mkononi akiwa ameshika wembe...”
 Mwishoni mwa wiki iliyopita, Yvonne huyohuyo ndiye aliyedaiwa kumpiga chupa mkononi Aunt ambapo haikubainika mara moja sababu za kufanya tukio hilo.

Aunt alipelekwa katika Hospitali ya Dokta Mvungi, Kinondoni na kushonwa nyuzi sita huku mtuhumiwa akishikiliwa na polisi.

Wednesday, August 28, 2013

HUYU NDO MDADA ANAYE DAIWA KUMJERUHI AUNT EZEKIEL KWA CHUPA







AUNT EZEKIEL APIGWA CHUPA USIKU AKIWA CLUB


MWIGIZAJI wa  sinema za kibongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa’ amenusurika kupasuliwa paji la uso kwa chupa baada ya kupigwa mkononi...
 

Usiku wa kuamkia Jumatatu, nje ya Ukumbi wa Billicanas, mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Yvonne alimpiga Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamedai  kuwa, wakati Yvonne anatekeleza ukatili huo, Aunt alikuwa amesimama na marafiki zake waliotajwa kwa jina moja moja, Sajenti na Rehema. 
 “Ndani ya ukumbi shoo ilikuwa ikiendelea, Aunt, Rehema na Sajenti walisimama nje, ghafla alitokea Yvonne akiwa na chupa mkononi, akailenga kwenye paji la uso la mwenzake, bahati nzuri Aunt aliiona na kukinga mkono,” kilisema chanzo.

Kikaendelea: Vurugu kubwa ilizuka, ilibidi shoo ndani isimame ili kushughulia suala hilo. Aunt alikimbizwa Aga Khan, Yvonne akapelekwa msobemsobe Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar ambapo anashikiliwa.

Baada ya taarifa hizo, juzi mchana, mwandishi wetu  alifika  nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala na kumkuta ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Ishu ni kweli kama mlivyosikia, lakini kule Agha Khan sikutibiwa, niliambiwa daktari hayupo mpaka saa mbili asubuhi na muda huo ilikuwa saa kumi alfajiri.

“Ilibidi niende kutibiwa kwa Dokta Mvungi, Kinondoni Hospitali ambako nilishonwa nyuzi sita.”

mwandishi: Madai ya Yvonne ni nini hasa?
Aunt: Yaani hata mimi sijui, nilishangaa sana. Kwanza lengo lake lilikuwa kunijeruhi kwenye uso, lakini niliiona chupa nikaikinga na mkono ndiyo maana ikaniumiza.

 mwandishi: Siku za nyuma uliwahi kuingia kwenye mzozo na Yvonne kwamba unamchukulia mpenzi wake aitwaye Joff, siyo kwamba ndiyo kisasi?
 

Aunt: Yale mambo yalipita, yeye ana maisha yake na mimi nina yangu.

-Risasi 

Monday, August 19, 2013

AUNT EZEKIEL AFANYIWA OPERESHEN YA TUMBO


MKALI wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefanyiwa oparesheni ya haraka kwa ajili ya kuondolewa uvimbe tumboni.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu na staa huyo, Aunt alikuwa akitembea na uvimbe huo siku nyingi pasipo kujijua hadi alipougua ghafla wakiwa katika mizunguko ya kila siku jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita. 
“Ghafla alibadilika, hakuwa katika hali ya kawaida kwani tulikuwa tukipiga stori lakini nikashangaa mwenzangu anabadilika kama mtu aliyepandwa na presha hivi.
“Tulilazimika kuahirisha misele yetu, ikabidi twende Hospitali ya Aga Khan na ndipo alipogundulika kuwa ana uvimbe tumboni kisha kufanyiwa upasuaji haraka sana kwani ulikuwa katika hatua mbaya za kuleta madhara,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo mtu huyo wa karibu ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alisema staa huyo anaendelea vizuri. 


Tuesday, August 6, 2013

AUNT EZEKIEL AFUNGA DIMBA LA KUFUTURISHA


Irene Uwoya ‘Mama Krrish’ akipata msosi wakati wa futari hiyo.
    Aunt Ezekiel akiongea jamba na marafiki zake wakati wa futari.
  Mcheza filamu mahiri Jacob Steven 'JB' akipata futari.
Yvonne Cherry 'Monalisa' akifurahia jambo wakati wa futari.
Chuchu Hans (kushoto) na Devota Mbaga wakipata msosi.
  Kajala akiwa na mtoto wake Paula wakipata futari.
Aunt Ezekiel akiwa na marafiki zake.
   Beautiful Onyinye Wema Sepetu akiwa na shosti wake Kajala katika futari hiyo.
    Wema, Kajala na Sajenti katia pozi.
  Kajala akiwa na Chuchu Hancs muda mfupi kabla ya kufuturu.
Kajala akiwa na mtoto wake katika picha ya pozi.
STAA mahiri wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel jana alifunga dimba la kufuturisha kwa mastaa baada ya kuwaalika watu mbalimbali nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kupata futari pamoja. Pichani juu ni baadhi ya taswira wakati wa zoezi hilo.