Showing posts with label RAY. Show all posts
Showing posts with label RAY. Show all posts

Thursday, December 5, 2013

MAINDA AZIDI KUWAVUA NGUO RAY, JOHARI. HOFU YA RAY KUHISIWA MGUMBA NAYO YAANZA KUSAMBAA MTAANI KWA KASI





Hapo majuzi kupitia mtandao mmoja wa kijamii mwanadada Mainda aliamua kuvunja ukimya baada ya kuamua kuwachana live ‘wabaya’ waka Chuchu hans, na Johari kuhusu sakata linaloendelea la wao kumgombania mwigizaji Vicent kigosi ambaye anadaiwa alikuwa mpenzi wa mrembo huyo. Bila kupoteza muda soma hapo chini alivyofunguka mwanadada huyu… "...Hizi salamu zako Johari, ni hivi naomba usinitaje kwenye huo upumbavu wenu, Huyo mwanaume mnae mzungumzia mimi kwangu namuona mtu wa kawaida tu ndio maana nikatupa kule. Nadhani umenipata alafu sitaki kumpandisha mtu jina sawa?. Ni hivi mimi si mpinzani wako, nadhani mpinzani wako unamjua mliopiganana (Sakata la Johari na Chuchu hans kupigana)  mkataka kutoana roho kisa shingo ya kuku mlivyokuwa wajinga na malimbukeni wa mapenzi wanaume hapawiganiwi. Nimewakalia kimya naona wewe mwenye kilanga umejitoa kimasomaso ukaenda kiu ukasema Mainda amebip wewe unataka kumpigia, ni hivi usiniweke kwenye upumbavu wenu, mimi huyo mwanaume wenu kwangu ni kuku kama kumtafuna nimemtafuna mpaka mifupa alafu nikatupa kwenye shimo la taka, sasa nyiyni mbwa koko mlio kosa wafugaji ndio mnaruka ovyo hamjui mle nini, pumbavu kabisa wewe na mke mwenzio sindio amkauki kunisema me mgonjwa, sasa kama me mgonjwa huyo bwana wenu ni hivi wewe mwenye shape kama ubao usiejielewa nakushauri achaha na mimi nenda sinza…..(Itaendelea)

Tuesday, November 12, 2013

VIDEO: MAINDA HATOSAHAU SIKU ALIYOTOA MIMBA YA RAY

HILI ndiyo Risasi bwana! Sikia, kama ulikuwa hujui ni kwamba msanii mkongwe katika filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ ameibuka na kueleza mengi ikiwemo kutoa mimba ya mpenzi wake wa siku nyingi, Vincent Kigosi, tulia hapohapo.
Ruth Suka ‘Mainda’.
Mbali na uhusiano wao huo uliokuwa ukifanywa siri, Mainda ameeleza kwa machungu jinsi Ray alivyomtesa kwa kumchanganya na wasanii wenzake, Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans ambaye ni mke wa mtu.
Risasi Mchanganyiko lilipata wasaa wa kufanya naye mahojiano ‘exculusive’ kwa saa moja na dakika tano, wikiendi iliyopita, makao makuu ya gazeti hili, Mwenge – Bamaga, jijini Dar.
Hata hivyo, alisema uhusiano wao kwa sasa umevunjika rasmi huku akibainisha jinsi alivyonyooshewa vidole na watu wakiamini kwamba aliambukizwa Ukimwi na aliyekuwa mpenzi wake kabla ya Ray, marehemu Said Maulid Banda  ‘Maxi’.
Soma mwenyewe mahojiano yalivyokuwa mstari kwa mstari, neno kwa neno:

 
Vincent Kigosi 'Ray'.
Risasi: Baada ya kifo cha Maxi, Ray alijitokeza na kukutongoza au siyo?
Mainda: Hapana, nakumbuka ilikuwa Siku ya Valentine’s Day mwaka 2004...sikumbuki kama tulitongozana ama vipi lakini ilitokea tukajikuta kwenye uhusiano.
Risasi: Umedumu kwa muda gani katika uhusiano wako na Ray?
Mainda: Miaka tisa, nilimpenda sana hata yeye alikuwa akinipenda na kuniheshimu sana.
Risasi: Kwa nini mmeachana?
Mainda: Hajaniacha wala hatujaachana. Miye ndiye nimemwacha.

Chuchu Hans.
Risasi: Jeuri ya kumuacha Ray umeitoa wapi?
Mainda: Siyo jeuri, ni kujiamini na kujitambua tu.
Risasi: Chanzo cha kumuacha nini labda?
Mainda: Nilipojihakikishia kwamba anatoka na Chuchu Hans na Johari, nikafanya uamuzi.
Risasi: Lini ulipata uhakika huo?
Mainda: Ni hivi karibuni. Niliumia sana (analia).
Risasi: Pole sana, jikaze tafadhali. Siku zote ulikuwa hujui?
Mainda: Nilikuwa nasikia tu maneno, lakini nilipothibitisha nikaamua kukaa pembeni.
Risasi: Uhusiano wako na Ray ulifikia hatua gani?

Blandina Chagula ‘Johari’.
Mainda: Mwaka 2009 miye na Ray tulienda kanisani kwa ajili ya kutaka kufunga ndoa. Kwa sababu  mwenzangu ni Mkatoliki ilibidi aokoke na kunifuata kwenye wokovu ili tuweze kufunga ndoa yetu, nashangaa amebadilika tena.
Risasi: Ulibadili dini kwa ajili yake?
Mainda: Big no! (Hapana kabisa) ulikuwa ni uamuzi wangu binafsi.
Risasi: Mipango yenu ya ndoa ilikuwaje?
Mainda: Tulipanga kufanya private wedding (ndoa ya siri).
Risasi: Unauzungumziaje uhusiano wako na Ray? Namaanisha ni nini hasa ambacho hakitaweza kufutika kirahisi katika kumbukumbu zako?
Mainda: Daah! (anavuta pumzi ndefu kisha anazishusha) Nilimpenda sana Ray. Ilifikia hatua nikapata mimba yake. Mapenzi yetu yakaongezeka lakini kwa bahati mbaya ilitunga nje ya kizazi na ilinitesa sana, tena kwa kuwa ilikuwa ni mimba ya kwanza sikuwa nimejitambua mapema. Madaktari wakashauri niitoe, nikakubaliana nao.
Risasi: Ilikuwa ni mwaka gani?
Mainda: Sikumbuki, ila ni kipindi tulipokuwa tukirekodi filamu iitwayo Johari (kwa kumbukumbu za Risasi ni mwaka 2005).
Risasi: Kuna madai kwamba wewe hukubaliki kwa mama yake Ray, ambaye anadaiwa anamkubali zaidi Johari, ni kweli?
Mainda: Siwezi kumsema vibaya yule mama, namheshimu sana lakini inawezekana kuna maneno ya uongo ambayo ameambiwa na watu.
Risasi: Kama yapi?
Mainda: Kuhusu miye kuwa na Ukimwi. Ngoja nikuambie kitu kaka’ngu, baada ya kifo cha Maxi, watu wengi walininyooshea vidole kwa kuamini kuwa Maxi amekufa kwa ugonjwa huo jambo ambalo siyo la kweli. Nakumbuka mwaka 2003, nilienda na Maxi Mwananyamala (Hospitali), alitolewa vipimo vingi (kikiwemo cha VVU), akabainika kuwa na kansa ya damu.
Akatakiwa kwenda Ocean Road (Hospitali) ambako walipendekeza akatwe mguu uliokuwa umeathirika na ugonjwa huo lakini alikataa. Alisema ni heri afe kwa ugonjwa huo kuliko kuzikwa akiwa na upungufu wa viungo mwilini mwake.
Risasi: Kuna tiba alishaanza kuitumia Ocean Road kabla ya kifo chake?
Mainda: Yeah! Alikuwa akichomwa mionzi, hadi kifo kilipomfika.
Risasi: Pole sana.
Mainda: Ahsante... ila baada ya kifo chake, watu wengi walihisi amekufa kwa Ukimwi na wakaamini nami pia ni mwathirika... hiyo hali ilinitesa sana (anaangua kilio).
Risasi: Pole sana, usilie...jikaze tafadhali.
Mainda: Kama kweli Maxi angekuwa amekufa kwa Ukimwi, Ray asingekubali kuwa na mimi kwa sababu  alikuwa rafiki yake na alishiriki kumuuguza kwa kiasi kikubwa.
Risasi: Kwa hiyo unaamini kwamba mama Ray alipandikizwa sumu hiyo?
Mainda: Binafsi nilikuwa simfuatilii ila mwanaye alijitahidi kuniweka karibu na mama yake.
Risasi: Kivipi?
Mainda: Mara kadhaa Ray alikuwa akinipigia simu na kunitaka niongee na mama yake au ndugu zake, aliniweka karibu sana na familia yake.
Risasi: Umewahi kupima Ukimwi?
Mainda: Siyo mara moja, baada ya maneno hayo,  mwanzo nilipima kwa hofu kwa kuhisi labda wale madaktari wa Mwananyamala walinidanganya kwa vile nilikuwa mdogo.
Risasi: Majibu yako yanasomekaje?
Mainda: Namshukuru Mungu, nipo negative (hana uambukizo).
Risasi: Ulijisikiaje ulipogundua kuwa Ray anatembea na Johari na Chuchu?
Mainda: Awali sikujua na kila nilipomuuliza Ray alinikatalia.
Risasi: Kwa hiyo ulimwamini Ray?
Mainda: Sana, tena nilipokuwa naye alikuwa akiwapigia na kuweka loud speaker kisha kuwauliza kama walikuwa wapenzi, walikataa.
Risasi: Unawachukuliaje Johari na Chuchu?
Mainda: Kwangu nawaona wapumbavu na wasiojiamini katika mapenzi. Mfano kama Ray angenipigia simu na kuniuliza kama natembea naye, ningekubali bila ya wasiwasi. Walikuwa wakijua kama miye natembea na Ray lakini kwa nini wao walifanya mapenzi yao na Ray kuwa ya siri? Mfano Chuchu alikuwa akiniita first lady na aliniambia kuwa Ray ananipenda sana, kumbe kuna kitu alikuwa akinificha.
Risasi: Chuchu alikuwa rafiki yako?
Mainda: Hapana ila alikuwa akipenda kunipigia simu na kujiaminisha kwangu kwamba alikuwa na Ray na hakuna kibaya kitakachotokea.
Risasi: Ulijuaje kama Ray anatambea na Chuchu?
Mainda: Inasikitisha kwa kweli, kwanza Chuchu ni mke wa mtu, (jina la mume kapuni) kisha amezaa na mumewe mtoto mmoja lakini anatangaza mtoto huyo ni wa Ray. Anamuweka kwenye mitandao, unadhani baba yake wa kweli anajisikiaje?
Halafu inasemekana walipokwenda Mbeya na Bongo Muvi, Chuchu alilala chumba kimoja na Ray.
Risasi: Uliambiwa na nani?
Mainda: Kuna msanii mmoja anaitwa (jina kapuni) ambaye naye alikuwa akitembea na Chuchu, ndiye aliyeshuhudia Chuchu akiingia chumbani kwa Ray. Pia ndiye aliyemfumania Chuchu na Ray Msasani hivi karibuni.
Risasi: Inadaiwa siku Ray na Chuchu walipofumaniwa, ulikuwepo na ukapandisha mashetani, ni kweli?
Mainda: Siyo kweli, sikuwepo ila siku hiyo (anamtaja jina huyo jamaa) aliniletea simu za Chuchu ambazo zilikuwa na meseji alizokuwa akichati na Ray. Halafu Chuchu ndiye mwenye tabia ya kupandisha mashetani.
Risasi: Meseji za Ray kwa Chuchu zilikuwa zinasemaje?
Mainda: Mambo ya mapenzi tu, tangu hapo niliamini kwamba Ray alikuwa akitembea na Chuchu. Nikaamua rasmi kumuacha Ray aendelee na Chura wake!
Risasi: Kwa nini unamwita Chuchu Chura?
Mainda: Wenyewe ndivyo wanavyojiita yaani ni kifupi cha Chuchu (Chu) na Ray (Ra) badala ya RJ (Ray na Johari).
Risasi: Ray alijiteteaje kwako?
Mainda: Alidai kwamba simu yake ilikuwa ikitumika na rafiki yake mwingine ambaye ni mume wa mtu (jina tunalo) akidai kwamba ndiye aliyekuwa akitembea na Chuchu lakini si kweli.
Risasi: Kama leo hii Ray akikufuata na kukuomba radhi utakubali kurudiana naye?
Mainda: Ameshaomba radhi sana, hata Chuchu alishaniomba radhi na kudai kutorudia lakini mambo ni yaleyale.
Risasi: Hebu fafanua?
Mainda: Ninaujua msururu mrefu wa wanawake wa Ray, (akaanza kuwataja majina - wamo wanenguaji na wasanii wa filamu na wengine), mmoja kwa sasa ni mke wa mtu huyo sitakutajia jina lake.
Risasi: Jambo jingine?
Mainda: Sijui kama ulisikia, Ray alipata ajali na Chura wake hivi karibuni?
Risasi: Nilisikia!
Mainda: Hiyo nayo inatosha kuthibitisha ninachokisema. Hizi zote ni laana, tukio lingine ni lile la Johari kumfumania Ray akiwa na Chura.
Risasi: Hata hilo nililisikia na liliripotiwa, vipi kuhusu Johari?
Mainda: Johari naye alikuwa akinifuatilia nyendo zangu, kuna wakati nilivaa pete ya uchumba, alihaha kutaka kujua nimevalishwa na nani?
Risasi: Alijua Ray amekuvisha?
Mainda: Nadhani!
Risasi: Ni kweli?
Mainda: Tuyaache hayo.
Risasi: Kwa nini?
Mainda: (Akionesha msisitizo) tafadhali hilo tuliache kaka.
Risasi: Uliwahi kumsaliti Ray?
Mainda: Katika maisha yangu miye ndiye huumizwa kila siku. Baada ya kuwa na Maxi mwanaume mwingine ni Ray, sikuwahi kuwa na mwingine kabla na baada ya kuwa na uhusiano naye.
Risasi: Mwanaume gani alikuingiza katika dunia ya mapenzi?
Mainda: Aaah! Sitapenda kumtaja ilikuwa kabla sijakutana na Maxi.
Risasi: Unazungumza vizuri na Johari na Chuchu?
Mainda: Sina ugomvi nao, ila sikupenda kitendo cha kuchanganywa nao kwa mwanaume mmoja. Imeniuma sana, kwa kweli sipendi kuishi mitala.
Risasi: Unaionaje Bongo Muvi baada ya miaka mitano?
Mainda: Kwanza naomba Mungu aiangamize... unafiki mwingi sana. Kuna siku nilimuuliza Ray kama yeye ndiye mwenyekiti anafanya uchafu kama huu, anaweza kumkemea msanii mwingine? Hakunijibu kitu. Mengi mabaya yanayosemwa kuhusu Bongo Muvi  ni ya kweli, tena uongozi umeoza kuanzia juu mpaka chini.
Risasi: Baada ya kuachana na Ray una mwanaume mwingine?
Mainda: Wengi wamenipigia simu kunitongoza nikawachomolea wakiwemo wasanii waliokuwa wakijua uhusiano wangu na Ray.
Risasi: Kwa nini?
Mainda: Miye huwa sitongozwi kwenye simu.
Risasi: Unatongozwaje?
Mainda: (kicheko), sikia ninaye mtu wangu lakini hatujafikia hatua ya kufanya mapenzi, tunachunguzana ili kujuana tabia kwanza.
Risasi: Ni msanii wa filamu au?
Mainda: Siyo msanii, ni mtu anayejiheshimu.
Risasi: Mara yako ya mwisho kufanya mapenzi ilikuwa lini?
Mainda: Siku chache baada ya msiba wa Albert Mangweah (msanii wa Bongo Fleva).
Risasi: Unaamini iko siku utaolewa?
Mainda: Yeah! Tena nitajifungua watoto.
Risasi: Kitu gani ambacho huwezi kukisahau maishani mwako?
Mainda: Kifo cha Kanumba na marehemu Maxi  (anaangua kilio…) vifo vyao viliniuma sana na vimeshindwa kuondoka akilini mwangu kirahisi.
Risasi: Ahsante sana kwa ushirikiano wako Mainda. Karibu tena Global Publishers.
Mainda: Nashukuru sana lakini nasema hivi; kama  Ray, Johari na Chuchu watakanusha haya niliyoyasema, nipo tayari nikutanishwe nao tena hapahapa ofisini kwenu nitazungumza mbele yao. Naahidi nitaongea mengi zaidi.
Risasi: Sawa, nashukuru sana Mainda.
Mainda: Nanyi pia… ndiyo maana nayapenda magazeti yenu.
Risasi: Kwa nini unasema hivyo?
Mainda: (Kicheko)



Wednesday, September 18, 2013

JOHARI AKIRI KUZICHAPA NA HANSI CHUU KISA PENZI LA RAY...PATA MKANDA MZIMA HAPA

 Waigizaji wenye majina makubwa Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans wanadaiwa kuchapana kisa kikidaiwa kuwa ni penzi la mwigizaji ‘kaka mkubwa’, Vincent Kigosi ‘Ray’,
TUHUMA
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho ni rafiki wa karibu wa wasanii hao, tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ofisi za RJ Productions, zinazomilikiwa kwa ubia wa Ray na Johari zilizopo Sinza-Mori jijini Dar ambapo Johari alikuwa akimtuhumu Chuchu mambo mazito ya kimapenzi kwa Ray.
Shushushu huyo alitonya kuwa, siku ya tukio Johari na wasanii wenzake walikuwa wakirekodi filamu ndani ya hoteli moja (jina tunalo) iliyopo jirani na ofisi hizo ndipo alipofikishiwa umbeya kuwa Chuchu yuko kwenye ofisi hizo ‘akijiachia’ na bosi mwenzake (Ray), jambo lililotia ganzi moyoni mwa mdada huyo.
MCHEZO MZIMA
‘Kikulacho’ huyo aliendelea kudai kuwa baada ya Johari kupata habari hizo, bila kujiuliza wala kuvuta subira, ‘alisaga soli’ hadi maeneo hayo.
“Alipofika aliingia ndani moja kwa moja na kumvamia Chuchu huku akimshushia kipigo chenye ujazo,” kilidai chanzo hicho.
Alidai kuwa katika timbwili hilo, Chuchu naye alifurukuta ndipo wakazichapa laivu kabla ya Ray aliyekuwa nje kusikia na kuwahi kuokoa jahazi.
“Unajua kilichomshtua Ray ni kilio cha Chuchu aliyekuwa akiomba msaada baada ya kuzidiwa na Johari,” kilidai.
Chanzo kilidai kuwa aliingia ndani akiwa amefura na kufoka lakini alikuwa ameshachelewa kwani tayari Johari alikuwa ameshaugeuza bucha mwili wa Chuchu.
Ilidaiwa kuwa baadaye Ray alimtoa nje Johari akimtaka kuwa mbali na Chuchu.
SINEMA YA BURE
“Ilikuwa ni bonge la soo, watu walijaa sana, baadaye Ray alimtoa Johari nje huku akimfokea.
“Unaambiwa Johari alikuwa akikimbia na Ray kumfukuza, jambo lililovutia watazamaji wa sinema hiyo ya bure,” alisema mpashaji wetu.
JOHARI, CHUCHU WASAKWA
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo, gazeti hili liliwasaka Johari na Chuchu kwa nyakati tofauti.
JOHARI AKIRI
Kwa upande wake Johari alikiri kutokea kwa kasheshe hiyo.
“Ni kweli lakini nani amekuambia? Unajua kilichoniudhi mimi ni maneno machafu ya huyu dada (Chuchu) anavyotamba kwa watu kuwa amenipokonya mume, wakati hakuna ukweli juu ya hilo, nilishikwa na hasira sana ndiyo maana nikaamua kumpa somo kidogo.
“Inaniuma kwa sababu mimi na Ray tumetoka mbali sana hadi kuisimamisha RJ. Tulikuwa hatuna kitu kabisa tukaungaunga huku na kule hivyo Chuchu anapaswa kutambua hilo. Asitake kunikumbusha vitu vingi kwa sababu tuliteseka sana,” alisema Johari kwa uchungu.
VIPI BADO ANAKWENDA RJ?
“Tangu ile ishu itokee sijaenda RJ kwa sababu Ray alinifukuza eti kisa Chuchu. Usiniulize muafaka wa hili jambo kwa sababu hadi sasa sina majibu ya moja kwa moja kuna vitu naviweka vizuri,” alisema mwanadada huyo.
HUYU HAPA CHUCHU

Kwa upande wake Chuchu aliruka kimanga kuwa hakuna ishu kama hiyo.
“Aaah, jamani sina cha kusema juu ya hilo, nikiwa tayari nitawaambia.
“Kinachonishangaza kila Johari na Ray wakigombana huwa natajwa mimi. Yaani sijui hata haya mambo yanatokea wapi,” alisema Chuchu.
RAY

Ray kutaka kujua ukweli wa ishu hiyo, bila kujibu ndiyo au hapana, alimjia juu mwandishi:
“Sikia Brighton (mwandishi), hili jina nimelitafuta kwa miaka mingi. Nakuomba usiandike habari hiyo, sielewi chochote.
“Ugomvi wao siujui na wakigombana waache kunitaja, waeleze sababu zao za kugombana siyo kunitajataja mimi,” alisema Ray na hata alipoulizwa uhusiano wake na wanawake hao aliishia kujiumauma bila kutoa majibu ya kueleweka

Tuesday, August 6, 2013

PICHA:RAY KIGOSI AINGIA LOCATION KUSHOOT MOVIE MPYA 'CHICKEN HEAD'...


Ray ambaye ni CEO wa RJ Company inayoisimamia filamu hiyo, ameshare baadhi ya picha za behind the scenes za filamu hiyo ambayo tafsiri yake kwa Kiswahili ni ‘Kichwa cha Kuku

21921fa6fdb311e28deb22000ae911d0_7
Ray akiwa na msichana aliyeigiza mke wake kwenye filamu hiyo

c76fbf34fdca11e28a0c22000a9d0ded_7
76c093e2fdcf11e2996f22000a1fbc6f_7
d470d52cfddb11e2ba6522000aaa0486_7
f533c41efdda11e2974122000a9e2969_7
f74020befdca11e2986122000a9f194c_7 
Mke wa Ray wa kwenye filamu hiyo

Monday, July 15, 2013

Ray asheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kumkumbuka kanumba











MWIGIZAJI, mtayarishaji na muongozaji mahiri wa filamu Swahiliwood Vincent Kigosi ‘Ray the Greatest’ hivi karibuni aliangusha bonge la sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kuwakaribishwa rafiki zake na wadau wa filamu katika moja ya Hotel, siku hiyo pia aliweza kumkumbuka swahiba wake marehemu Kanumba na kuhisi uenda angekuwepo siku hiyo.
                                
“Ni siku ambayo nimesheherekea siku yangu ya kuzaliwa na ndugu zangu wa karibu na wasanii wenzangu, ni siku ambayo nimekumbuka mambo mengi sana katika maisha yangu, mara nyingi swahiba wangu marehemu Kanumba siku kama ya leo ningekuwa naye katika sherehe kama hii, lakin ndio mambo ya Mungu huwezi kulaumu kilichobaki ni kumuombea Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani Amen,” alisema The Greatest.

Katika sherehe hiyo iliyopambwa na vinywaji na malaji kibao ilijumuisha wasanii nguli katika tasnia ya filamu kama Bonge la bwana, JB, Maya, Odama, Chikoka na wasanii wengine kibao huku kukiwa na michezo kadha wa kadhaa ni jambo jema kwa marafiki kukumbuka katika matukio kama hayo.