Habari zimetujia sasa hivi zinasema abiria kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa wamenusurika kifo, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuwa pasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa Arusha leo mchana.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la precision aina ya ATR ilipata
ajali hiyo wakati ikitua, ambapo Matairi yote manne ya nyuma yalipasuka
na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria. Ila hakuna mtu aliyedhurika
katika ajali hiyo.
"Yaani
Mungu ni mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi
chetu Lowassa...Mungu atamlinda jamani...siamini" alisikika akisema mama
mmoja miongoni mwa abiria hao wakati akishuka.
Mh
Lowassa ni mbunge wa Monduli, jimbo ambalo anatoka Waziri Mkuu
aliyekuwa kipenzi Cha mwalimu Nyerere na watanzania hayati Edward
Moringe Sokione.Sokoine aliyefariki katika ajali ya gari mwaka 1984