Showing posts with label nyingine. Show all posts
Showing posts with label nyingine. Show all posts

Wednesday, October 2, 2013

MGANGA WA KIENYEJI AGAWA IRIZI ZENYE VYURA WANAOPUMUA KUWALINDA WAHAMIAJI HARAMU WASIKAMATWE MKOANI KIGOMA

Mganga akamatwa na hirizi zenye chura wanaopumua akizitumia kuwauzia wahamiaji haramu wasiweze kukamatwa katika Operesheni Kimbunga.

 Kampeni ya kitaifa ya kuwaondoa wahamiaji haramu nchini iliyopewa jina la “Operesheni Kimbunga”, imezidi kuibua mambo mazito baada ya mganga wa kienyeji, kugundulika akitumia uchawi ili kuwalinda wahamiaji hao wasikamatwe.
  .   Mganga huyo aliyefahamika kwa jina la Bw. Bahalaye Gwenda (60), ameifanya kazi hiyo tangu kuanza kwa operesheni hiyo kwa kuwalipisha wahamiaji haramu sh. 200,000 kila mmoja wasiweze
 kukamatwa na vyombo vya dola vinavyofanya kazi hiyo.

Tukio hilo la kustaajabisha, limetokea katika eneo la Kigaga, Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma ambapo mganga huyo hutumia hirizi ambazo ndani yake kuna dawa za kienyeji na vyura wanaopumua kuwauzia wahamiaji hao.
 
Taarifa za mganga huyo, ziliifikia Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo ambapo Mwenyekiti wa kamati hiyo Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. Venance Mwamotto, aliongoza kikosi kazi cha wajumbe wa kamati, polisi hadi nyumbani kwa mganga.

Kamati hiyo ilipata malalamiko hayo kutoka kwa wahamiaji ambao walikamatwa mbali ya kupewa dawa na mganga huyo ambaye ni raia wa nchi jirani ya Burundi.
 
Mazingira ya kamati kufika nyumbani kwa mganga huyo yalikuwa kama sinema ambapo wajumbe wa kamati wakiwa na askari polisi, baada ya kukaribia nyumba yake mganga akiwa ameshika mzizi mkononi na kibuyu kilichofungwa hirizi, aliwapa ishara ya kutosogelea nyumba hiyo.

“Wakati tukiwa mbele yake tukimfuata, alituambia tusisogelee nyumba yake kwani uchawi alionao una nguvu kubwa hivyo unaweza kutudhuru, hatukumsikiliza tuliendelea kumfuata hivyo alitupa vifaa vyake chini na kukimbilia ndani.
 
  “Baadhi yetu walikuwa waoga katika eneo husika wakiogopa kudhurika, alipoingia ndani, alitokea mlango wa nyuma na kukimbia na sisi baada ya kuingia ndani, tulichukua vifaa vyake kama ushahidi,” alisema Bw. Mwamotto.

 Aliongeza kuwa, kikosi kazi alichokiongoza kiliamua kwenda nyumbani kwa mganga huyo kwa lengo la kumkamata kutokana na malalamiko waliyopata kutoka kwa wateja wake ambao walidai kutumia fedha nyingi kumpa mtaalamu huyo hivyo walitaka kurudishiwa fedha zao.
 
 Alisema baada ya kuzipasua hirizi walizozikuta, vibuyu na pembe, walikuta dawa za kienyeji pamoja na chura wazima wanaopumua. Vitu vingine walivyovikuta ni vitambaa vyeusi, vyeupe, vyekundu na vitu vingine vya ajabu.

   Akizungumzia operesheni hiyo wilayani humo, alisema wamefanikiwa kukamata sare za Jeshi la Burundi na kofia vilivyokuwa vikitumika katika matukio mbalimbali ya uhalifu na wahamiaji haramu.“Tunaendelea na operesheni yetu kwa kushirikiana na viongozi ili kuhakikisha wahamiaji wote haramu wanarejeshwa nchini mwao tuweze kurudisha amani na usalama,” alisema.
 
   Awali Mkuu wa Mkoa huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Issa Machibya, alisema wahamiaji haramu wengi walikuwa wakijihusisha na matukio ya ujangili na biashara ya silaha zikiwemo za kivita.

  Alisema Mkoa huo pekee umewakamata wahamiaji haramu 4,365 kutoka nchini Burundi katika awamu ya kwanza ya operesheni iliyosambaa katika mikoa mbalimbali nchini na kuwataka wakazi wa Kigoma, kushiriki kikamilifu katika vita hiyo.
 
  Kwa mujibu wa kiongozi wa timu ya Habari na Mawasiliano ya Operesheni Kimbunga, Zamaradi Kawawa, alisema katika operesheni hiyo awamu ya pili iliyofanyika Mikoa ya Geita, Kigoma na Kagera, bunduki moja aina ya SMG, bastola moja, magobole 17 na risasi 115 zikiwemo za bunduki aina ya SMG 102 na 13 za bastola vilikamatwa.
 
  Wahamiaji haramu waliokamatwa wengi wao ni kutoka nchi za Burundi ambapo raia wake 114 walikamatwa wakiishi nchini kinyume na sheria na raia 20 wa Rwanda ambao nao walikamatwa katika kipindi hicho
 
Majira.

Tuesday, October 1, 2013

PICHA: SHEIKH PONDA ALIVYOFIKISWA MAHAKAMANI MOROGORO LEO

 Sheikh Issa Ponda akishuka kwenye basi la Magereza tayari KuingiaMahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro leo ambapo leo Mahakama Ilikuwa inatoa Maamuzi kuhusu Kufutiwa shitaka moja kati ya matatu yanayomkabili Sheikh Ponda katika Mahamama hiyo.Mahakama Imetupilia Mbali Ombi hilo na kesi itaendelea Kusikilizwa katika Mahamama hiyo.Kesi hiyo imeahiriswa Mpaka tarehe 7 November mwaka huu ambapo mahakama itaanza kusikiliza Mashahidi wa kesi hiyo.Sheikh Ponda Amerudiswa Rumande.

 Sheikh Issa Ponda Akiingia katika viwanja vya mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa morogoro
 Sheikh Issa Ponda akishuka kwenye basi la Magereza tayari KuingiaMahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro leo ambapo leo Mahakama Ilikuwa inatoa Maamuzi kuhusu Kufutiwa shitaka moja kati ya matatu yanayomkabili Sheikh Ponda katika Mahamama hiyo.Mahakama Imetupilia Mbali Ombi hilo na kesi itaendelea Kusikilizwa katika Mahamama hiyo.Kesi hiyo imeahiriswa Mpaka tarehe 7 November mwaka huu ambapo mahakama itaanza kusikiliza Mashahidi wa kesi hiyo.Sheikh Ponda Amerudiswa Rumande.

 Sheikh Issa Ponda Akiingia katika viwanja vya mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa morogoro
 Sheikh Issa Ponda akishuka kwenye basi la Magereza tayari KuingiaMahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro leo ambapo leo Mahakama Ilikuwa inatoa Maamuzi kuhusu Kufutiwa shitaka moja kati ya matatu yanayomkabili Sheikh Ponda katika Mahamama hiyo.Mahakama Imetupilia Mbali Ombi hilo na kesi itaendelea Kusikilizwa katika Mahamama hiyo.Kesi hiyo imeahiriswa Mpaka tarehe 7 November mwaka huu ambapo mahakama itaanza kusikiliza Mashahidi wa kesi hiyo.Sheikh Ponda Amerudiswa Rumande.

 Sheikh Issa Ponda Akiingia katika viwanja vya mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa morogoro
morogoro..

Sheikh Ponda akiwa mahakamani akimsubiri Hakimu tayari kusikiliza Kesi yake katika Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa morogoro
 Mke wa sheikh Ponda akiwa mahakamani 
 Ulinzi ukiwea umeimarishwa mahakamani hapo leo wakati kesi hiyo ikiendelea katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wsa morogoro

MAPENZI YA JINSIA MOJA YASHAMIRI AFRIKA MASHARIKI.






MAPENZI ya jinsia moja ni moja ya biashara inayozidi kushamiri katika nchi za Afrika Mashariki na kuchangia maambukizi makubwa ya Ukimwi. Kutokana na hali hiyo, nchi za Afrika Mashariki zimetakiwa kuangalia namna ya kuokoa maisha ya mashoga, ili wasiendelee kuteketea na ugonjwa hatari wa Ukimwi badala ya kuwanyanyapaa.
Akizungumza jana katika mkutano unaojadili masuala ya afya kwa watu wanaosafiri, wahamiaji na watu wanaozunguka sehemu mbalimbali, Mratibu wa Chama cha Watu wanaofanya biashara ya ngono nchini Kenya, John Mathenge alisema jambo la hatari ni kwamba hata viongozi wakubwa serikalini wanapenda kufanya mapenzi na mashoga.
Katika mkutano huo ulioandaliwa na Asasi ya Kimataifa ya Wahamiaji (IOM), Mathenge alisema pamoja na desturi za kiafrika kukataza vitendo vya ushoga na usagaji, lakini wapo watu katika jamii wanaofanya mapenzi hayo kama biashara ya kuwapatia kipato au kujifurahisha.
Alisema shirikisho la watu wanaofanya kazi za mapenzi lina wanachama wengi hapa nchini wapatao kama 40,000.
"Unajua biashara hii ya kuuza mwili ni kazi sawa na kazi zingine, mtu anaweza kuamua atumie mwili wake kuwa mkimbiaji, mwingine kuwa kahaba au shoga zote hizi ni kazi na wanaofanya kazi hiyo hawapaswi kulaumiwa na jamii bali wasaidiwe ili wasiambukizwe Ukimwi," alisema.
Alisema kwa kuwa watu hao wako katika jamii yetu na wanafanya mapenzi na viongozi na watu wa kawaida, maambukizi ya Ukimwi yanazidi kuongezeka hivyo kuna haja ya Serikali kukubali kuzungumza na mashoga na makahaba wengine ili kuangalia namna ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi.
"Tuache tabia ya kuwanyanyapaa, tukienda hospitali tunanyanyapaliwa tunaambiwa twende na wapenzi wetu, tutawatoa wapi wakati mtu umekutana naye kwa siku moja tu? Ukweli ni kwamba kila mtu hapa duniani anafanya biashara ya ngono ila katika mfumo tofauti.
"Wewe wakati unataka kuoa mke wako ulitoa mahari ili aje kwako, au kuna watu wana vimada wanawapelekea zawadi ili waendelee kupewa mapenzi, hawa nao wanafanya biashara ya ngono, sasa iweje sisi ambao tumejitokeza tuanze kunyanyapaliwa? Alihoji Mathenge.
Alisema hata kuongezeka kwa wahamiaji haramu kumetokana na kuwepo biashara hiyo ya ngono ambayo inafanywa na maofisa wa Serikali kama Uhamiaji ambao wanapewa ngono na wasichana na kuwaachia waingie kwenye nchi husika bila kuwa na vibali vinavyotakiwa kisheria.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Mohamed Sharrif Abdukadir, alisema urasimu uliopo kwenye mipaka katika kushughulikia nyaraka za mizigo ndizo zimekuwa zinachangia madereva wanaosafiri kwenda nchi jirani kuingia katika vitendo vya ngono.
Alitoa mfano wa mpaka wa Tunduma kuwa unaongoza kwa kuwa na urasimu kutokana na mfumo uliopo wa kushughulikia nyaraka hali inayomfanya dereva wakati mwingine akae wiki mbili eneo hilo hivyo kujikuta anafanya vitendo vya ngono.
Hata hivyo alisema asasi ya IOM kwa kushirikiana na Chama cha Madereva wa Masafa Marefu imewasaidia kuwapa ushauri wa namna ya kujikinga na maambukizi ya Ukimwi wakati wanapokuwa safarini.
Abdukadir alisema tayari kumejengwa vituo vijulikanavyo kama One Stop Border Posts ambavyo vinatumiwa na madereva kwenda kupata ushauri na kupima afya zao.
Alisema vituo hivyo viko chini ya IOM vinatoa semina kwa madereva na hata kama mtu anakutwa ameambukizwa anapewa dawa za kurefusha maisha. Eva Mwai ambaye ni Mratibu wa Asasi ya North Star Alliance katika ukanda wa Afrika Mashariki, anasema asasi yake imekuwa inatoa msaada wa kiafya kwa watu wanaozunguka kwa vile hawana muda wa kwenda kupimwa hospitalini.
Alisema wanafanya utafiti katika maeneo mbalimbali ambako ni hatarishi kwa madereva na wanajenga kliniki maalumu kwa ajili ya kutoa afya na ushauri kwa madereva na watu wengine ambao wana maisha ya kuzunguka.
Alisema wana vituo vya afya huko Mombasa, Tunduma, Kahama na Mwanza kwa ajili ya kufanya upimaji kwa watu wanaozunguka.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil aliwataka washiriki wa mkutano huo ambao wanatoka nchi mbalimbali kubadilisha uzoefu wa namna ya kushughulikia afya kwa watu wanaozunguka, wahamiaji mbalimbali hasa katika eneo hili la ukanda wa Afrika Mashariki

Friday, September 27, 2013

UPDATES":Barabara Tanzania zapitisha biashara haramu


BARABARA za Tanzania zimekuwa zikitumika kupitisha biashara haramu ya binadamu. Kauli hiyo imetolewa na Rais Jakaya Kikwete, ambapo alifafanua kwamba hakuna shughuli za biashara haramu ya binadamu inayofanywa Tanzania.
Hata hivyo, Rais Kikwete amesema Serikali yake itaendelea kushirikiana na nchi jirani kuhusu chimbuko la biashara hiyo, na katika kuchukua hatua za kukomesha vitendo hivyo haramu.
Alitoa msimamo huo wa Tanzania juzi, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wake, Daniel Yohannes.
Ujumbe huo ulikutana na Rais Kikwete mjini New York, ambako amefikia kwa ziara yake ya kikazi nchini Marekani.
Yohannes na wenzake walikuwa wanamwelezea Rais Kikwete maendeleo ya ombi la Tanzania la awamu ya pili ya misaada ya maendeleo, baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza.
Katika mazungumzo hayo, Yohannes alitaka kujua hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Rais Kikwete, kukabiliana na baadhi ya mambo yanayojitokeza kuwa changamoto katika utekelezaji wa miradi ya MCC, kupitia Akaunti ya Milenia Tanzania (MCAT).
Baadhi ya changamoto ambazo Yohannes amezitaja ni pamoja na nini kinafanyika kuhusu Shirika la Umeme (TANESCO), juhudi za kupambana na rushwa na jinsi gani ya kukabiliana na biashara haramu ya binadamu.
Rais Kikwete ametoa majibu ya changamoto zote tatu na kumweleza Yohannes kuwa biashara haramu ya binadamu haifanyiki wala kuanzia katika Tanzania na kuwa inaanzia Ethiopia inapitia Kenya, Tanzania, Malawi na kwenda hadi Afrika Kusini.
“Wanakusanya watu katika Ethiopia na kuna mtu anapewa fedha na watu hao wanaokusanywa. Wanakuja Kenya na kuna mtu wa kuwapokea na kuwahudumia, wanakuja Arusha na hatimaye wanaingia Malawi na Afrika Kusini.Katika Tanzania wanapita tu na kuna wakati tulipata kukamata Waethiopia kiasi cha 19,000 na tukawarudisha kwao kwa gharama yetu,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Kutoka Ethiopia watu hawa wamekuwa kama mto usiokauka maji. Hivyo, sisi katika Tanzania tunafanywa kama njia ya kupitia tu. Ni kweli wako mawakala lakini kwa hakika biashara hii haifanyiki katika Tanzania. Inafanyika kwingine na nchi yetu inafanywa kama njia tu. Kuna wakati nilipata kuzungumza na viongozi wa Ethiopia na Kenya kuhusu suala hilo lakini bado tutaendelea kulifuatilia.”
Rais Kikwete aliendesha kikao chake cha kwanza kama Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Nchi za Umoja wa Afrika Kuhusu Mazingira (CAHOSCO).
Rais aliendesha kikao hicho Jumanne wiki hii, katika Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU), katika Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.
Ubalozi wa Kudumu wa AU una hadhi ya watazamaji UN. Alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Nchi Wanachama wa AU kuhusu Mazingira mwanzoni mwa mwaka huu, baada ya kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Waziri Mkuu wa zamani wa Ethiopia, Meles Zenawi, aliyefariki Septemba mwaka jana.
source:habari leo

Wednesday, September 25, 2013

MHAMIAJI HARAMU AKUTWA NA LESENI NA KITAMBULISHO CHA KUPIGIA KURA

                      Leseni ya udereva.
Baadhi ya wahamiaji haramu, wamekuwa wakitumia mbinu ya kupiga picha na viongozi wa juu wa Serikali na kuzitumia kama ‘kibali’ cha kukaa nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari na kuonya kuwa mbinu hizo zimebainika na hazikubaliki.
“Kuna watu wasio raia ambao wamekuwa wakipiga picha na viongozi… hiyo haitakuwa dawa, hata mimi niliingia katika mtego na raia wa India ambaye katika kusalimiana, alipiga picha kumbe ni mhamiaji haramu, mtu huyo tulimwondoa mara moja,” alisema. 
Alitaka wahamiaji haramu waliojificha, kurejea kwao au kuhalalisha ukaaji wao nchini kwa kufuata utaratibu wa kimataifa.
“Tunawapenda sana majirani zetu na tunawapenda marafiki zetu, lakini watu wanaotaka kuishi nchini ni lazima wazingatie utaratibu wa kimataifa. Vivyo hivyo kwa Watanzania wanaokaa nchi zingine,” alisema.
Alisema wakifuata utaratibu wa kimataifa, watasaidia kuongeza usalama wa nchi kujua ina raia wa nchi gani na hata nchi zao, kujua raia wake walio nje ya nchi.
Alionya Watanzania wanaopokea na kuhifadhi watu wasiowafahamu, kuwa mbali na matatizo ya kisheria yanayoweza kuwakuta, lakini pia wanahatarisha amani ya nchi.
“Kila mtu anatakiwa kuwa macho na wageni ambao hawawafahamu hasa katika kipindi hiki ambacho usalama wa dunia uko shakani,” alisema.
Nchimbi alitolea mfano wa gaidi wa Kingereza, ambaye  aliishi nchini kwa kubadili majina na alipenya hadi kupewa kadi ya mpiga kura.
“Pamoja na kupongeza watendaji kwa kumkamata gaidi huyo, lakini ukweli tutakuwa  tunashangaza… mpaka huyo mtu kapewa leseni ya Tanzania na kadi ya kupigia kura?” Alishangaa.
Nchimbi pia alitaka viongozi wa serikali za mitaa nchini watimize wajibu wao wa kuhakikisha wanakuwa macho na wahamiaji haramu katika maeneo yao.
 “Sasa tutaanza kuulizana na kuchukuliana hatua na wenyeviti na watendaji wa mitaa, kwani haiwezekani eneo moja tukamate wahamiaji haramu 30 au 40 na kuwachukua wao tu, wanatakiwa kuwajibika kwa hili,” alisema.
Wakati huo huo, ugomvi wa wapenzi, umesababisha raia   wa Tanzania, Martina Pius, kutoboa siri kuwa baba mtoto wake, Fidele Ndayiragijimana (25) ni mhamiaji haramu kutoka Burundi.
Akisimulia kisa hicho jana, Kaimu Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dodoma, Naibu Kamishna Proches Kuoko, alisema kwa sasa Ndayiragijimana ambaye alikuwa akiishi kijiji cha Itiso wilayani Chamwino, anashikiliwa katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma.
Kwa mujibu wa Kuoko, Ndayiragijimana alikuwa akiishi katika kijiji hicho tangu mwaka 2009 na katika mapenzi yao na Martina, walibahatika kupata mtoto.
Alisema Ndayiragijimana alikuwa akifanya kazi kwa mkulima  na amekuwa akijitambulisha kwa bosi wake kuwa mzaliwa wa Kigoma.
Kuoko alisema baada ya kusikia Operesheni Kimbunga imeanza, Ndayiragijimana alirudi Burundi akachukue pasipoti na kuingia nchini na kuishi kihalali.
Hata hivyo, Ndayiragijimana alipata hati ya muda ya Burundi, ambayo Kuoko alisema aliitumia kuingia nchini kupitia mpaka wa Manyovu, Kigoma na kupata kibali cha mwezi mmoja cha kuingilia  nchini.
Hata hivyo, kibali hicho kilimaliza muda wake Septemba 6 na alipaswa kurejea kwao, jambo ambalo hakulifanya na kuendelea kuishi kwa siri, mpaka  Martina alipofichua siri hiyo.
Mhamiaji mwingine aliyekamatwa ni Husna Zekwana (26), raia wa Uganda, aliyekutwa na mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja aliyeingia nchini akitoka Kampala kwa kupitia mpaka wa Horohoro, Tanga.
Ofisa Uhamiaji huyo alisema Husna alikutwa na hati ya kusafiria isiyo yake, bali alipewa na kondakta wa basi la Smart ili avuke na kisha amrudishie baada ya kufika  Dodoma.
Akizungumzia Operesheni Kimbunga Awamu ya Pili, Dk Nchimbi alisema wanapanga upya ratiba, lakini nguvu ya kamatakamata inaweza kupungua kwa asilimia 70.
Katika awamu ya kwanza, kwa mujibu wa Dk Nchimbi, wahamiaji haramu 12,604 walikamatwa na kati yao, Wanyarwanda ni 3,448, Warundi 6,125, Waganda 2,496, Wakongo 589, Wasomali 44,  Myemeni mmoja na raia wa India mmoja.
Alisema watuhumiwa 212 wa unyang’anyi wa kutumia silaha walikamatwa, pia mabomu 10 ya mkono, silaha tofauti 61, risasi 665 na mitambo miwili ya kutengeneza   magobori.
“Tulifanya msako hata katika hifadhi za Taifa ambako ng’ombe 8,226 walikamatwa na zaidi ya Sh milioni 32.5 kupatikana kama tozo kutokana na faini ya ng’ombe walioachwa katika hifadhi ya Taifa,” alisema.
Nchimbi alisema pia walikamata nyara za Serikali ikiwamo ngozi ya duma, mbili za swala na vipande 10 vya nyama vinavyodhaniwa kuwa nyara za Serikali. Pia walikamata mbao 2,105, magogo 86, bangi kilo 77 na vipande viwili vya meno ya tembo.
Kuhusu wakimbizi wa Burundi zaidi ya 200,000 ambao wako nchini tangu mwaka 1972, Nchimbi alisema kazi ya kutoa uraia kwa watu hao ilisitishwa.
Sababu ya kusitishwa, ni hatua ya baadhi ya wabunge na wakuu wa mikoa kukataa kuwapokea baada ya kutokea vitendo vya uhalifu maeneo ya Kaskazini.
“Pamoja na kuwa tulikubaliana na Shirika la Kimataifa la Wakimbizi (UNHCR), tulisitisha kazi hiyo na sasa Serikali inatafakari njia mwafaka kwa kuwa kama mpango huo ungeendelea, basi ingekuwa Serikali yenye kiburi,”  alisema.

Monday, September 23, 2013

HUYU NDIYE SIMBA ALIYE UWAWA BAADA YA KULA MBUZI ZAIDI YA 47 HUKO MOROGORO

Simba huyo ambaye amesumbua kwa muda mrefu Mkoani humo maaskari Wanyamapori Mkoani Morogoro wamemwinda na kumuua simba huyo aliyetafuna mbuzi 47 katika Mlima Uluguru eneo la kijiji cha Bagilo kata ya Kinole, Tarafa ya Mkuyuni Mkoani humo.
Askari wanyamapori Wakimchuna ngozi simba

Saturday, September 21, 2013

BINTI WA MIAKA 6 ABAKWA NA MFUGA NGURUWE HUKO KITUNDA BAADA YA KUMRUBUNI KWA KUMNUNULIA PIPI



PEPO la ubakaji linazidi kutikisa jamii ambapo hivi karibuni watoto wawili wanaripotiwa kubakwa kwa nyakati tofauti jijini Dar.
Mtoto mmoja, mkazi wa Kitunda (jina linahifadhiwa) amebakwa na mfanyakazi wa kufuga nguruwe aishie maeneo ya jirani baada ya kumrubuni binti huyo mwenye umri wa miaka 6 kuwa atamnunulia pipi.
Akizungumza kwa uchungu, baba wa mtoto huyo, Joseph Isaac alisema mwanaye alibakwa na mfanyakazi huyo wa nguruwe aliyemtaja kwa jina la Fabiano baada ya kumuahidi kuwa atampa pipi.
“Siku hiyo nilirudi nyumbani nikamkuta mwanangu anachemka homa kali, nikamwambia mama yake amuogeshe tumpeleke hospitali kwani tulikuwa tumeshampatia dawa ya kutuliza lakini haikumsaidia,” alisema baba huyo.
Mama wa mtoto huyo aliyetajwa kwa jina la Elizabeth, alimuogesha mwanaye na kugundua kuwa alikuwa amevimba sehemu za siri kutokana na majeraha aliyopata na alipombana ndipo alipomtaja mfanyakazi huyo wa nguruwe.
“Nilimwambia mume wangu tukachukue PF3 (fomu ya uthibitisho wa polisi) kisha tukatibiwe. Tulienda Kituo cha Polisi Stakishari na  kuandikisha RB No KIT\RB\2804\2013 KUBAKA ndipo tukaenda Hospitali ya Amana kwa ajili ya matibabu,” alisema mama huyo.
Walipofika katika Hospitali ya Amana, walilazimika kulazwa kwa siku tatu kutokana na majeraha makubwa aliyokuwa nayo mtoto huyo wakati huohuo polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa (Fabiano).
Ilielezwa kuwa, pamoja na mtuhumiwa kukamatwa lakini alitolewa kwa dhamana hivyo wazazi wa mtoto huyo kuhoji kulikoni aachiwe.
Waandishi wetu walikwenda kwa mjumbe wa eneo hilo, Anna Kosmas ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuambatana na waandishi hadi nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo walielezwa kuwa ametoweka.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha Minangi aliahidi kufuatilia suala hilo kwani limesharipotiwa kituoni hapo na atahakikisha mtuhumiwa anakamatwa.
Unyama haukuishia hapo, mtoto mwingine mkazi wa Makabe, Dar aliyejulikana kwa jina la Sara (10) amesimulia jinsi alivyokuwa akibakwa mara kwa mara na mlinzi wa baa anayejulikana kwa jina la Athuman.
Akizungumza kwa masikitiko, mtoto huyo alisema kila siku huwa anaenda kuangalia video kwenye Pub ya Jack anayolinda mlinzi huyo ambapo wakati wa kurudi inakuwa ni usiku ndipo mlinzi huyo anapotumia muda huo kumaliza haja zake.
Alisema mlinzi huyo alikuwa akimkamata kwa nguvu na kumfunga kamba mkononi, miguuni na kumziba mdomo huku akimtishia kuwa akipiga kelele, atamchoma mkuki kitendo ambacho kilimsababisha mtoto aogope kumwambia hata mama yake.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa baada ya kugundulika kwa mchezo huo mchafu, polisi walimkamata mtuhumiwa na kumfikisha katika Kituo cha Polisi cha Kwa Yusuf, Mbezi Beach, jijini Dar kukamilisha taratibu za kipolisi kisha kumpeleka mahakamani.

Daktari FEKI akamatwa Muhimbili

DAKTARI anayedaiwa kuwa bandia amekamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, akiwa na vitambulisho bandia vya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) akisomea Shahada ya Pili.
‘Daktari’ huyo ambaye amekuwa akitafutwa na uongozi wa chuo kwa zaidi ya mwaka alikamatwa jana asubuhi akiwa hospitalini hapo karibu na jengo kilimo kitengo cha meno.
Katika kitambulisho chake cha kupigia kura anatambulishwa kwa jina la Dismas John Macha aliyezaliwa mwaka 1979 Kilimanjaro na anaishi maeneo ya Upanga Magharibi, Dar es Salaam.
Mkazi wa Dar es Salaam aliyejitambulisha kwa jina la Dismas Macha, akiwa chini ya ulinzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini jana, baada ya kukamatwa akidaiwa kujifanya daktari. (Picha na Theopista Nsanzugwanko).Mkazi wa Dar es Salaam aliyejitambulisha kwa jina la Dismas Macha, akiwa chini ya ulinzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini jana, baada ya kukamatwa akidaiwa kujifanya daktari. (Picha na Theopista Nsanzugwanko).
Gazeti hili, lilimshuhudia mtuhumiwa huyo akiwa katika kituo cha usalama cha Muhas na kupekuliwa na askari Polisi wa Muhimbili, Anthony Mwamatepela na kukutwa akiwa na vifaa vya udaktari .
Baadhi ya vifaa alivyokutwa navyo ni pamoja na koti jeupe la udaktari na stetoskopu ambacho ni kifaa cha kusikilizia mapafu yanavyofanya kazi na mapigo ya moyo.
Pia alikuwa na begi jeusi lenye aina mbalimbali za dawa, vitambulisho na karatasi nyingi, lakini alipoulizwa alidai kuwa hizo ni dawa zake.
Macha alikutwa pia na vitambulisho vitatu tofauti, kimoja kikimtambulisha kuwa mwanafunzi wa Muhas wa Shahada ya Pili ya Udaktari (Masters of Medicine ) yenye jina la Macha Dismas kikionesha kusajiliwa kwa namba 60520/2011 na kumaliza muda wake Septemba 30 mwakani. Kitambulisho kingine kilimtambulisha kwa jina la Macha Rogers anayesoma Shahada hiyo hiyo ikionesha kuwa anamaliza masomo yake mwakani.
Alikutwa pia na kitambulisho kinachomwonesha kuwa mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza na kadi ya anuani yenye jina la Amos Nnko ambaye ni Ofisa Rasilimaliwatu wa Chuo hicho.
Akizungumzia alivyomkamata askari wa chuo hicho, Fulgence Semfukwe alisema walimkamata baada ya kupata taarifa za yeye kuwa maeneo hayo na kupanga mbinu za kumkamata.
Alisema saa 4.45 asubuhi jana alimkuta kwenye jengo la meno na kumwomba kwa nafasi yake ya udaktari amsaidie tatizo lake na hivyo waongee pembeni, naye bila wasiwasi akakubali. Alimwuliza anatibu magonjwa gani naye kumjibu anatibu maradhi ya aina nyingi na kumwomba kitambulisho na yeye kumpa cha kwake.
Baada ya hapo alishituka na kudai kuwa ni daktari wa Mwananyamala na amekuja hapo kwa ajili ya kuona wagonjwa wake wa dharura ndipo alipokamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi.
Alisema amekuwa akiwachenga kwa muda mrefu kutokana na kuwa kila walipopewa taarifa yuko wodi au sehemu Fulani hawakumkuta kwani walipishana naye baada ya kuvua koti na kuweka kwenye begi lake jeusi.
Akizungumza na gazeti hili, Macha limweleza mwandishi wa habari hizi kuwa yeye ni mwanafunzi ambaye anaelewa masuala yote ya matibabu, lakini alifeli chuoni hapo mwaka jana.
Alidai kuwa dawa alizokutwa nazo ni zake kwani ana matatizo katika njia ya mkojo na kifua huku akiamua kufanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.
“Uwezo wa kutibu ninao na nimesoma katika chuo hiki, lakini mwaka jana nilifeli ndiyo maana nikaamua kuwa hivi,” alisema.
Ofisa Uhusiano wa Muhas, Hellen Mtui alisema kutokana na kukamatwa na nyaraka akijitambulisha kuwa mwanafunzi wa ‘Masters of Medicine’, ambaye anaweza kutibu watu hawana uhakika na idadi ya watu ambao ameshatapeli hospitalini hapo.
Kuhusu kusoma Muhimbili, Mtui alikana akisema baada ya kupekua nyaraka za chuo hawakubaini jina la mwanafunzi wa aina hiyo na katika vyeti vyake bandia vinaonesha kusainiwa na Mkuu wa Chuo aliyekuwapo kabla chuo hakijapanda hadhi na kuwa chuo kikuu.
Mtui alisema baada ya kumkamata na kumpiga picha akiwa na mavazi ya udaktari, kumpekua na kumhoji walimpeleka katika kituo cha Polisi cha Selander Bridge kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
-Habari Leo

TAZAMA PICHA NYINGINE 200 PAMOJA NA VIDEO ZA UCHI LIVE ZA MANAIKI SANGA:ANGALIA KWA MAKINI HUENDA NDUGU YAKO AKAWEMO....

 





  Katika hali ya kushtua msanii chipukizi Manaiki Sanga “The Don” aliyejipatia umaarufu mkubwa nchini na duniani baada ya picha zake za utupu akiwa na wanawake zaidi ya 400 wakiwemo wazungu akifanya nao ngono nzembe na baadae kusambaa kwenye mitandao yote duniani na kuonwa na mamilioni ya watu hasa wale wanaopata habari kupitia mitandao ya kijamii, sasa ameamua kutengenezea filamu halisi ya matukio hayo akiwa na wanawake walewale aliofanya nao ngono





Friday, September 20, 2013

WAKE WENZA WASHIKANA UCHAWI HUKO KIMARA

WANAWAKE wawili walioolewa katika familia moja ‘wake wenza’, mama Hashimu na mama Fadhila, wakazi wa Kimara King’ong’o jijini Dar, hivi karibuni walifikishwa serikali za mtaa kwa kosa la kutukanana matusi ya nguoni pamoja na kushikana uchawi.
Inadaiwa kuwa wanawake hao ‘walimwagiana’ matusi hayo usiku wa manane na kusababisha watu wengine kukosa usingizi na kukusanyika kuwasikiliza.
Mara baada ya kufikishwa serikali ya mtaa, wake wenza hao walitakiwa kueleza ugomvi wao na kila mmoja kuanza kushusha tuhuma kwa mwenzake.
Mapaparazi wetu waliwashuhudia wakati wake wenza hao walipokuwa wakijieleza mbele ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King’ong’o, Demetrius Mapesi na Mtendaji wake Amina Rashid.
Mama Hashimu alianza kuelezea kisa kizima na kufuatiwa na mama Fadhila ambaye wakati akijieleza alipandisha mori kiasi cha kumfanya atake kumrukia mwenzake.
Unajua nasikia hasira sana kwa sababu mama Fadhila ameniita mchawi huko mtaani unadhani mimi nitaelewekaje? Ukweli kauli hiyo inaniuma sana,” alisema mama Hashim na kuangua kilio.
Hata hivyo, baada ya kila mmoja kueleza ya moyoni, mwenyekiti wa serikali za mtaa pamoja na mtendaji wake, waliwaamuru wake wenza hao kupeana mkono na kuombana msamaha. 

“Sasa hapa hakuna kesi, kwani wote mna makosa, hebu niambieni mnawafundisha nini watoto wetu kwa matusi 
mliyotukanana hadharani?” alihoji mwenyekiti na kuwataka wayamalize mambo hayo.
Aidha, mwenyekiti huyo aliahidi kuwafuatilia ili kuona kama watakuwa wamebadili tabia zao.
Kama vile haitoshi aliwaahidi kama watarudia atawahamisha mtaa pamoja na waume zao kwani mtaani kwao hawahitaji watu wanaotukanana ovyo na kuzushiana mambo ya kichawi.
Baada ya tamko la mwenyekiti, mtendaji wake aliwaamuru wake wenza hao kuandika matusi waliyotukanana kisha akawapiga faini ya shilingi 20,000 kila mmoja.
“Kutokana na matusi yenu nalazimika kuwapiga faini ya shilingi elfu ishirini kila mmoja, ingawaje kwa mujibu wa sheria ya Tanzania mtu akikutwa na hatia ya kutukana anatakiwa kutozwa faini ya shilingi elfu hamsini au kufungwa jela miezi sita,” alisema mtendaji huyo.
Kila mmoja alilipa nusu ya faini na kuahidi kumalizia huku wakisema kuwa hawatarudia kufanya kosa hilo tena

Thursday, September 19, 2013

AIBU: WEZI WA MTANDAO WAKAMATWA KATIKA OFISI ZA TIGO BUGURUNI ...CHEKI VIDEO NA PICHA ZA TUKIO ZIMA HAPA

mrembo huyu ni mmoja wa watuhumiwa wa kesi hii ya wizi wa mtandao baada ya kutumia kitambulisho chake na kutaka kuja kurudisha line ambaye sio yake kwa kuahidiwa kupewa pesa kidogo kama ujira wake na katika melezo yake akasema hawatambui wahusika wenzake kwani amekutana nao tu sinza na wakampa dili hilo na kuamua kuchukua bajaji ambao iliwaleta mpaka ofisi za tigo buguruni rozana
 

huyu ndio staring mwenyewe aliyechonga mchongo wote na kumshawishi huyu mwanamke kutumia jkitambuluisho chake kufanyia wizi huo wa kimtandaO 
Ads not by this site
mrembo akijitetea kuwa hahusiki kabisa katika wizi huu na pia kujitetea kuwa kaacha mtoto mdogo nyumbani 
 
hapa ni mmoja wa watuhumiwa akitoa maelezo kuwa yeye si mwizi na hafahamu kabisa wahusika wenzake na yeye ni mfanyabiashara wa vipodozi 
 
watuhumiwa wenzake wakificha sura zao huku wakitoa maelezo kwa wafanyakazi wa tigo na walinzi waliowatia chini ya ulinzi baaada ya kuweka mtego mzuri wa kuyanasa mataperli haya ya kimtandao 
 
hiki ndio kitambulisho alichoktaka kutumia huyu mwanamke kuswap line ambayo sio yake lakini aliweka jina la mhusika wa line na namba alizokuwa anapiga maranyingi lainmi sura yake bahati mbaya kwa umakini wa mfanyakaiz mmoja wa tigo kwa jina octavian rweyendera alifanikiwa kubaini udanganyifu huo na kuamuru awekwe chini ya ulinzi mara moja 
 
aliyesimama hapo yeye alibiwa kiasi cha milioni moja kwa njia ya sim banking ya NMB baada ya line kuharibika ghafla kumbe mmoja wa watuhumiwa alirenew na kuiba pesa

 
hiki pia ni kitambulisho cha mteja huyo hapo juu aliyeibiwa pesa kwenye acount yake ya NMB kiasi cha milioni moja kwa njia ya sim banking baada ya mmoja wa hawa watuhumiwa kuja kurudisha yake hii kwa kutumia kitambulisho hiki ambacho kimetengenezwa kwani si halisi na hatimaye kufanikiwa kuiba pesa kwa sim banking baadae 

hapa mtuhumiiwa mmoja akiwan kajilaza chini kwa kugoma kutoa maelezo kwa walinzi waliowaweka chini ya ulinzi 

hapa huyu binti KILIA kwa uchungu na kuomba asamehewe

wakiwa ndani ya gari ya polisi kuelekea kituo cha polisi buguruni

umati wa watu uliofurika kushuhudia tukio hilo la aina yake 

mmoja ya wafanyakazi mahiri wa tigo bw octavian rweyendera amabaye alifanikisha kukamatwa kwa watuhum,iwa hao akitoa maelezo kwa baadhi ya maafande wa polisi jinsi wathumiwa walivyotaka kufanya wizi huo wa kimtandao 

Askari polisi wakisikiliza kwa makini jinsi watuhumiwa hao walivyokamatwa

TIZAMA VIDEO YA TUKIO ZIMAHAPA CHINI