Johari Blandina Chagula ambaye ni star mkongwe Swahiliwood amesema kuwa
anamshukuru Mungu kwa kuutunza muonekanio wake na kuwa kama kijana licha
ya umri wake kuwa mkubwa tofauti na baadhi ya waigizaji wenzake wa kike
ambao hujiachia na kuonekana wazee licha ya umri wao kuwa mdogo.
Akizungumza na Filamucentral Johari alisema "“Wasanii
wa kike wengi ni watoto wadogo lakini kwa sababu ya kujiachia
wanaonekana kama watu wazima lakini ukweli ni watoto wadogo sana,
namshukru Mungu nimeanza sanaa kitambo lakini mwili wangu upo fiti,”
Johari alimtolea mfano Irene Uwoya ambaye ni shoga'ke wa karibu kuwa
anaonekana mkubwa kwasasa sababu ya kujiachia licha ya kwamba amempita
miaka kadhaa. Vile vile Johari amesema kuwa kawasasa amerudi kwa moto wa
kasi kama muigizaji kama awali baada ya kuwa upande wa producer kuwapa
nafasi chipukizi ambao wengi amesema wameshindwa so amerudi mwenyewe
kwenye game
CREDIT:SWAHILI WORLD
“Napenda kuchukua nafasii hiii kuomba samahan
kwa wote nilio wakosea...napia mim nimewasamehe...nataka nimaliza mwaka
kwa amani na upendo...nawapenda wote sina kinyongo na mtu...asante
mwenyez mungu kwakunipa nguvu
Irene Uwoya ameamua kuanza mazoezi ya kupunguza unene na kujiweka fiti na kurudisha mvuto wake wa awali ambao unadaiwa kupotea mara baada ya kujifungua huku media na wataalamu wa fashion wakimuandama mara kwa mara kuwa kapoteza mvuto wa mwanzo kwa kujiachia kunenepeana kiasi cha kupoteza mvuto. Owoya yupo chini ya mwalimu wake wa mazoezi Rashid Matumla ambaye ni bondia maarufu nchini na pia wanakuja na filamu wakiwa pamoja ambayo inaitwa Raundi Ya 8.
akizungumza na Filamucentral "Nimejipanga kwa kufanya mazoezi ya nguvu chini ya mwalimu wangu Rashid Matumla na nipo fiti kwa ajili ya kujifua najua kuigiza ndio ajira yangu lakini nikijiachia na kunenepa bila mpango nitaanza kucheza nafasi za akina bibi muda si mrefu na najiona mwili
unavyoninyemelea sitaki manyama uzembe"
Filamu hiyo imeshutiwa Tanga, Dar es salaam na Morogoro huku waigizaji wengine wakiwa ni Francis Cheka na Lumolwe Matovolwa.
Uwoya akiwa na Rashid Matumla....................
Siku za Hivi karibuni kumekuwa na tetesi zisizo rasmi kuwa mastaa wawili
wa filamu Swahiliwood Yobnesh Yusuph(Batuli) na Irene Uwoya hawana
maelewano mazuri chanzo kikidaiwa ni Irene Uwoya kutaka kumpoteza Batuli
kwenye tasnia ya filamu ili asifurukute. Habari hizo zinaenda mbali
zaidi zikidai kuwa kuna kipindi Batuli alikuwa anaumwa maeneo ya kifuani
lakini baadhi ya watu
wakiwemo wasanii wenzake wakiamini Uwoya ndiye
kamfanyia mambo ya kilozi(ushirikina).
Tetesi hizo tulizipuuza mwanzoni lakini zinaonekana kurudi tena kwa kasi hivyo Swahiliworldplanet
iliamua kuwatafuta mastaa hao wawili ili watoe ufafanuzi wao wenyewe na
wa kwanza kuulizwa alikuwa Uwoya hata hivyo namba yake ilionekana
kutokuwa hewani alipotafutwa juzi na jana alipotumiwa ujumbe namba yake
ilionekana bado haipo hewani. Batuli nae alitumiwa ujumbe juzi kuhusu
issue hiyo lakini hakujibu mpaka jana usiku ndiyo alijibu akisema
alikuwa busy sana. Batuli alisema "sina ubaya na msanii yeyote na moyo
wangu ni mweupe na nina mapenzi na wasanii wenzangu wote, nawapenda sana
anayeniwinda kwa ubaya Mungu atanipa ulinzi wake, sipendi uadui na mtu
namuachia Mungu atanilipia yote"
Hata hivyo bado SWP inamsaka Uwoya kwa namba yake nyingine ili atoe
ufafanuzi wake kuhusu issue hiyo na pindi akitoa maelezo yake basi
utayasoma hapa hapa SWP.