Showing posts with label sinta. Show all posts
Showing posts with label sinta. Show all posts

Wednesday, September 11, 2013

SINTAH YAMKUTA-HABARI YA UONGO ALIYOIANDIKA NA KUIWEKA KWENYE BLOG YAKE YAMTOKEA PUANI POLISI WAANZA KUMFUATILIA



Msanii zilipendwa kwenye sanaa ya filamu Sintah amefanya madudu mengine baada ya kuandika habari ya uongozi na uchochezi na kukipakazia kituo cha redio time fm cha Jijini Dar kuwa kilishindwa kujipanga kwenye shoo yao iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye suala la ulinzi hadi kupelekea wasichana kubakwa na kuporwa mali zao.


Habari hiyo iliwashangaza waandaji wa tamasha hilo pamoja na jeshi la polisi Kanda ya Kinondoni ambalo lilikuwepo uwanjani usiku kucha wakingozwa na mkuu wa kituo cha Polisi Oysterbay Wilbrod Mtafungwa hadi asubuhi bila kushuhudia matukio mabaya.
Katika habari hiyo ya Sintah iliyokuwa inasema kuwa Wasichana wabakwa usiku kucha na wahuni kwenye shoo ya Azonto bila msadaa wowote jambo ambalo Jeshi la Polisi Kinondoni limekanusha vikali madai hayo huku ikisema kuwa hadi leo Jumanne hakuna taarifa yoyote kuhusiana na madai hayo ya Sintah.

Akiongea mmoja wa askari wa kituo cha Oysterbay ambae aligoma kutaja jina lake kwa madai kuwa yeye si msemaji alisema" Tumeshangazwa sana na taarifa ya Sintah aliyoiandika jana Jumatatu mapema kuwa kuna wasichana walibakwa usiku kucha hii habari naona ilikuwa na mlengwa wa kushoto kwa kuchafuliana habari hiyo haina ukweli wowote kwani hadi sasa sisi kama Polisi tuliopewa jukumu la kulinda wananchi ziku zile hatuna taarifa hizo" Alisema afande huyo

Hata hivyo jeshi hilo lilikuwa na mpango wa kuhitaji ushahidi wa vielelezo juu ya habari hiyo ambavyo Sintah angetakiwa kuviwakilisha polisi ili waweze kuwasaka wabakaji hao vinginevyo habari hiyo ingemletea matatizo Sintah kwani ni ya uchochezi na unafiki.
 Siku ya shoo hiyo ya mwanamuziki Azonto toka nchini Ghana mwenye makazi yake nchini Uingereza ilikuwa na ulinzi mkali sana kulikuwa na Mbwa wa polisi 15, Polisi wasiopungua 90 wakiwemo wale wenye siraha ambao walikuwa wanazunguka viunga vya uwanja wa Ustawi wa Jamii.
Aidha baadhi ya mashabiki wengi walisema kuwa huenda Sintah bado ana hasira na kituo hicho cha redio times baada ya kupigwa chini kwenye kipindi alichokuwa anatangaza kutokana na kukosa sifa ya kuendesha kipindi hali iliyosababisha Sintah kuwawekea bifu.
Hata hivyo Sintah aliitoa haraka habari hiyo kwenye blog hiyo baada ya kutonywa na wasamalia wema kuwa ingemletea matatizo makubwa kwani kama hana ushahidi wa vielelezo ni heri akaitoa na mara moja alifanya hivyo.

Xdeejayz iliwasiliana na uongozi wa redio times lakini bahati mbaya simu zao zote zilikuwa bize kila walipopigiwa simu, hata hivyo tunawaahidi wasomaji wetu kuwa itamtafuta mkurugenzi wa kituo hivho Rehure Nyaulawa kuzungumzia suala hilo na kama kuna hatua zozote wameshaanza kuzichukua juu ya Blog hiyo kwa kuandika habari hiyo ya uongo

Friday, August 2, 2013

SINTAH "SISI MASTAA WENYE MASTERS DEGREE HATUWEZI PIGIZANA KELELE NA MASHOROKO MAGENI"


Sintah leo kaja na haya : jisomee mwenyewe

"Ukifungua gazeti la babkubwa toleo jipya ,kurasa ya katikati shurti utakutana na kichwa cha habari MASTAA Ambao shule imelala kichwani, seriously kuna siku mdau alinitumia comment maana mimi na magazeti ni hasi na chanya, 
kilichoandikwa ni ukweli mutupu jamani khaaa sasa mtu mwenye MA apigizane kelele na mashoroko mageni aaaah wapiii??

though babkubwa mmejichanganya sana maana mmeandika ndivyo sivyo one n only CEO anayetambulika ana MA International Relations and Diplomacy naomba ieleweke hivyo, sijui kwa wengine mliowaja kama ni sawa ama ila me mmenimixia sana na ma post graduate ya nini mieee?

 CEO's 
MA International Relations n Diplomacy
BA Public Administration and Management  (kwa wale ambao mme cram  BA hamkawii kusema Business Admin khaaaa ni Bachelor of Arts in PAM muelewe sasa.

hope tumeelewana ila sivibaya nikawataja na wenzangu ambao tuna hadhi ya kipekee (sio mchezo,, sonyaa, kwanini ilikushinda kama ni rahisi?? ukipata jibu utakuwa umenielewa chezeyaa kufanya research weweee)

Mwegelo Jokate 
Black Rhino
Dj Fetty
Nikki wa Pili
Hamisi Mwinjuma
Ally Remtullah
na mwenyewe CEO wa ukweeeh 

UJUMBE
unaweza ukawa kama  hao hapo juu ila acha majungu, umbea, fitina, hela unazozipata kama ni mwanadada usijipeleke kununua lace wig, sijui Galaxy zichange mdogo mdogo ujitupe kile chuo kinaitwa V*** fasta .

The roots of education are bitter, but the fruit is sweet.

okaybyeeee..
Swaum Maqbul" Sintah

Tuesday, July 30, 2013

SINTAH " NASUBIRI KUPIGWA NA SHILOLE KAMA ALIVYO AHIDI-SAFARI ZA UKUBWANI MAJANGA


"Heee aliposema Sintah akarukiwa kwenye media zote nini na nini mbuta nanga.
Nothing personal to be honest ila watanzania tusipende kudanganyana jamaniii, juzi tu tulikuwa na kampeni za kwenda World Cup 2014 Brazil na kamati zikaundwa za kutosha tu, leo hakuna hata anayejua ndoto zimefia wapi now heeee.



Mtu anayekupenda lazima akwambie ukweli, truth sets a person free sasa sielewi kwa nini sie watanzania hatupendi critics rather tunapenda urahisi wa maisha vitu vitokee tu pap ndo maana mabinti wanaamua kubeba madawa e.t.c TUSIPENDE KURAHISISHA MAISHA


Joke of the year ni pale mtu hana hata album, nyimbo mbili/tatu tu za mdumange anakuja kutuambia eti Jenifer Lopez kafurahi anataka kufanya naye nyimbo kiruuuuuu. Charity begins at home, hujawagusa hata kina Lady Jaydee sogeasogea mpaka kwa kina Wahu na Juliana Kanyomozi kwanza ndo at least uje utudanganye Lolest. Kuna tofauti gani sasa kati ya huyu na wale waliotuambia tutaenda Brazil 2014?????



Tukijipanga timu yetu ya taifa itashiriki World Cup. Why not?
Msanii ukijipanga hakuna kinachoshindikana, nini JLO unaweza fanya featuring hata na Jay Z lakini sio kutuletea mambo ya mfalme njozi kwa kuwa umepata sponsor kakusafirisha basi mburula mwanzo mwisho. 


kuwa exposed ukubwani linaelekea kuwa janga la taifa sasa....Dont hate critics, you can learn a lot from them!


I had to say that because nasumbuliwa sana na media kila mara simu na interviews, I got nothing to hate on nothing... Im always honest nasubiri kupigwa now kama alivyoahidi Lolest.

Thx kwa wale mliokuwa mna mtazamo kama mie coz sio wanafiki, Mungu anapenda sana wasema ukweli.



sitaki tena media yeyote sasa iniulize hili swala that's it, huu ndio ukweli wangu na sipendi kupigiwa simu kwasababu sitaki kumpa mtu hypes za kumtajataja, got better things to do than discuss issues that aint no valuable.

Good Day. Xo Xo

Unstoppable" 

Sintah"

Sunday, July 28, 2013

SIJAWAHI PIGA PICHA ZA UCHI...NIMEMFAHAMU SINTAH KUPITIA SKENDO YA KUGAWA PENZI KWA NATURE"...RAYUU AFUNGUKA TENA

Jana, Bongomovies.com imefanya interview kwa njia ya simu na mwanadada msanii Rayuu alaice Bungenzi kuhusiana na mambo mablimbali yanayoandikwa kwenye mitandao na tovuti mbalimbali nchini.


Katika interview hiyo waliweza kupata mambo manne  kama  ifuatavyo:
 

1. Hajawai kupiga picha za utupu na kuzisambaza ili kupata umaarufu


Akiongea kwa msisitizo Rayuu amesema kuwa hajawai kupiga picha za utupu na kuzisambaza kwenye mtandao kwa ajili ya kupata umaarufu.


“Sijawai kusambaza picha za utupu ili nipate umaarufu, hizo picha kweli ni zangu na ukizitazama vizuri sio picha za utupu kama watu wanavyosema(?????), ni picha nilizopiga kwenye simu yangu kujiangalia tattoo yangu niliyochora kiunoni lakini kuna marafiki zangu waliochukua simu yangu na sijui ni nani ndio zilisambaa kutokea hapo na kila mtu kuandika stori anayoijua yeye” Alisema.



2. Hafahamiani na wala hajawai kuonana na sintah kwa zaidi ya miaka mingi sana

Rayuu amesema kuwa hajawai kuonana na sintah, wala hafahamiani naye personally na huwa anashangaa sana kwanini mwanadada huyu anamchafua kwenye blog yake.



“Kiukweli mi sifahamiani na Sintah, na wala hatujawahi kuonana kwa kipindi kirefu sana, sasa huwa nashangaa kwanini ananichafua na kunitukana kwenye blog yake. Kuna kipindi nilichoka nikaanza kumjibu lakini baadaye nikaona ni utoto bora ninyamaze kwanza nione kama ataacha lakini nashangaa hakui.


Huyu dada mi huwa simuelewi kwakweli,anagombana na kila mtu, nahisi anaweza kugombana hata na panya. Kwanza ni mtu mzima sana kwangu.


Nakumbuka mi nimemfahamu yeye wakati teyari kashakuwa maarufu na skendo za uroda kwa Juma nature na mimi nilikuwa bado mdogo sana. Sa sijui kwanini hakui. Kila siku anatukanwa kwenye blog yake lakini wala hajali.”…Alisema Rayuu


3. Marehemu Mzee Kipara ndiye haswa aliyemuingiza kwenye sanaa

Watu wengi hawajui kuwa marehemu mzee kipara ndiye aliyemuingiza Rayuu kwenye sanaa. Rayuu alisema kuwa anakumbuka siku moja kundi la kaole walienda kurekodi igizo  lao mitaa ya nyumbani kwa kina Rayuu na alipowaona alimfuata mzee kipara na kumueleza nia yake na ndipo alipompeleka na kumtambulisha kwenye kundi la kaole na kuanza kupata nafasi ya kuigiza na kufanya mazoezi kundini hapo.


4. Sio mtu wa kutoka sana na akila "bata" anaumwa sana kesho yake

Rayuu amesema yeye sio mtu wa kutoka na kupenda kwenda club kama wengi wanavyodhani bali hupenda sana kushinda ndani kwani akifanya hivyo kesho yake lazima aumwe siku nzima

-bongomovies.com 

Monday, July 22, 2013

SINTA AJIBU MAPIGO ASEMA ANASUBIRI KIPIGO KUTOKA KWA SHILOLE


Msanii wa muziki na maigizo nchini Shilole ambae ametangaza kumvulumushia makonde mazito Sintah popote atakapomuona.
Na Livingstone Mkoi
Msanii mkongwe kwenye tasnia ya afrika na kati Sintah amefunguka kuhusu vitisho anavyopewa na msanii mwenzake wa muziki na maigizo Shilole kuwa ajiandae kuchezea kipigo cha mbwa mwizi popote atakapomuona.
Akiongea kwa njia ya simu toka nyumbani kwake Sintah baada ya mtandao huu kutaka kueleza anachukuliaje vitosho hivyo vya Shilole ambapo alisema" Kaka naambiwa sana na watu hasa wanaofatilia mitandao eti natafutwa kupigwa na Shilole sasa ninacho shangaa huyo Shilole anapafahamu kwangu aje basi anipige au kwenye ofisi zangu anapajua namkaribisha vizuri sana jamani" Alisema Sintah

Aidha Sintah aliongeza kusema kuwa" Mimi huwa sio mtu wa maneno yeye aje tu anipige na sio kutangaza kwenye mitandao kuwa ananitafuta anipige hayo mambo ya bifu siku hizi watu wanayachukulia upuuzi kutafuta pesa ndio mpango mzima hivyo mimi namshauri Shilole kama underground wa sanaa nchini aachane na bifu badala yake akazane kwenye mambo yake ya kutafuta pesa kwa ajili ya maisha yake na familia kwani uzee unakuja" Alisema Sintah
Chanzo cha ugomvi huo ulitokana na Sintah kuandika habari kwenye mtandao wake kuwa Shilole hawezi kuimba na Jennifer Lopez wa Marekani bora hata Linah wa THT anaweza kufanya hivyo kwa hiyo Shilole aache kuidanganya jamii. Mtandao wa Sintah uliandika hivyo

Aidha Mashabiki mbalimbali hasa wasomaji wa kwenye mitandao wamemuunga mkono Sintah kuhusu kauri yake" Ni kweli jamani Shilole hawezi kuimba na Jennifer Lopez hayo ni masihara jamani kwenda marekani ndio aje kuongea ulojo kiasi hicho kwanza ikumbukwe kuwa wasanii wote wa tanzania kule Marekani hawajulikani hata, hasa kwa sisi tunaofatilia tunajia" Alisema mfanyabiasha wa kimataifa aliyejitambulishia kwa jina la Hamu Juma.

Sunday, July 21, 2013

SHILOLE ATANGAZA BIFU LA NGUMI BAADA YA SINTAH KUMPONDA KUWA ANAUWEZO MDOGO KIMUZIKI


MWIGIZAJI wa kike wa filamu na muziki Bongo zuwena Mohamed ‘Shilole’ amemtangazia hali ya hatari msanii mwenzake wa filamu na mtangazaji wa televisheni Christina John ‘ Sintah’ kuwa popote atakapomkuta lazima amchape kwa kipigo ambacho hatasahau katika maisha yake...

Shilole  ametoa kauli hiyo kufuatia kuandikwa na mwanadada huyo katika mtandao wake akimbeza kwa kejeli. . 
“Ni kweli sisi wanawake hatupendani na kuwa na wivu wa kijinga, mtu anakurupuka anakotoka bila hata kufanya utafiti na kunibeza eti sina uwezo wa kuimba na JLO (Jenifer Lopez) ....

"Kuna mtu aliyetegemea mimi kwenda kufanya show Marekeni!Sasa ninachomwambia ninamtafuta nikikutana naye nimtapa kipigo cha Mbwa mwizi,”aliongea kwa hasira Shilole.

Katika mtandao wake Sintah aliandika kwa kusema Shilole ni sawa na mtu anayeota ndoto za mchana, na kumkejeli kwa kusema kuwa aendelee kuota anaweza baadae kurudi katika hali yake...

  Sehemu ya maneno yanayomkera Shilole ni haya: 
“Shilole bwana hii week katujia na kali kuliko eti ameongea na Benny Medina (Jlo’s Manager) ili aweze kufanya collabo na my sister, heee yes inawezekana maana hakuna lisilowezekana chini ya jua lakini swali ni?? wataimbaje?? yule dada yake na mie ni RnB na music wa Shilole bado sijaujua ni chakacha ama nini sasa naomba msaada kwenye tuta wadau wa music, hili linauwezekano??,”
 

“ Chakacha na RnB?? Kwa sababu Shilole nyimbo zake sawa na Snura wa majanga, kidogo Linah angeniambia ana collabo na my sisy ningeelewa sasa Shilole?? Ndoto za mchana ila si vibaya kuota maana ukishtuka unarudi ktk reality,” 

Shilole anasema kuwa hajawahi kumuona mwanamke mwenye roho dhaifu kama Sintah, anajifanya anambabaikia Jlo wakati hata hajulikani.... 

“Mimi sikuwa nimeenda Marekani kwa ajili ya kuomba kumshirikisha J-lo kuimba naye,  lakini baada ya meneja wake kuja kuniona na kumpelekea video za muziki wangu  JLO alikubali kufanya kazi na mimi...

"Ilitakiwa nionane naye siku ya Jumapili lakini ndio siku niliyoondoka na ninarudi huko kwa ajili ya kazi hiyo, sijui nikifanya naye kazi atajificha wapi?,” anasema Shilole. 

Shilole anasema Mungu ni mkubwa hata kama kuna mtu anayemchukia kwa mafanikio yake bado Mungu ana nafasi kubwa kuwazima watu wenye roho mbaya wivu kama Sintah ambaye anaonekana yupo tayari kwa ajili ya kuwaombea matatizo watu wanaojituma kwa ajili ya kuendesha maisha yao.