Showing posts with label MASOGANGE. Show all posts
Showing posts with label MASOGANGE. Show all posts

Wednesday, November 6, 2013

BAADA YA KUTOKA LUPANGO..... MASOGANGE APIGA ZA NUSU UTUPU ...........

SIKU chache baada ya kutoka lupango kwa msala wa madawa ya kulevya, ‘video queen grade one’ Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ametupia picha za utupu mtandaoni.
Agnes Gerald ‘Masogange’ katika pozi.
Masogange na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu wakidhaniwa kuwa na madawa haramu ya kulevya na baadaye mahakama kuu ya nchini humo ikawaachia kwa dhamana ikidai unga waliokutwa nao si madawa ya kulevya bali ni mali ghafi zijulikanazo kama Methamphetamine.
Baada ya kuachiwa huru, Masogange anayesifika kwa kuwa na figa matata, alitupia picha hizo katika mtandao wa Instagram akiwa amevalia sidiria na nguo ya ndani pekee hali iliyowafanya wafuasi wa mtandao huo wamshangae huku wengi wakimlaumu kuwa alichokifanya hakifanani na maadili ya Mtanzania.

 
Video queen grade one Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’.
“Sasa huu upuuzi gani unatuwekea humu, kwani kila kitu unachofanya ni lazima sisi tuone? Hivi kwa nini mastaa wa Bongo wanapenda kujirahisi kiasi hiki?” alihoji mmoja wa wafuasi wa mtandao huo.
Pamoja na wadau wengi kuonesha kukerwa na picha hizo, Masogange hakujali, aliwajibu kuwa kama hawataki kuziona picha hizo wamuondoe kwenye listi ya marafiki mtandaoni humo kwani siyo lazima.
“Hii ni akaunti yangu, nina uhuru wa kuweka picha za aina yoyote. Kama mtu anaona nimemkera basi ‘aniblok’ maana hapa nimevaa mavazi ya kuogelea sasa mlitaka nivae pensi niogelee nayo? Simuogopi mtu…,” aliandika Masogange

Friday, November 1, 2013

TANZANIA YAPINGA HUKUMU YA "MASOGANGE" ILIYOTOLEWA AFRIKA KUSINI.....


MAKAMANDA wa vitengo vya kudhibiti madawa ya kulevya kwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamemaliza kikao chao jana kujadili mustakabali wa uhalifu ikiwemo hukumu iliyotolewa kwa Mtanzania Agness Gerald ‘Masogange’ aliyekamatwa na malighafi haramu aina ya Ephedrine, Julai 5, 2013 nchini Afrika Kusini kwamba ni ndogo.
Agness Gerald ‘Masogange’.
Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi Tanzania zimeeleza kuwa makamanda wa nchi hizo 15 walikutana jijini Arusha kuanzia Jumatatu iliyopita lengo kubwa likiwa kutokubaliana na adhabu zinazotolewa na baadhi ya nchi wanachama kwa wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’.

WALICHOJADILI
Kwa mujibu wa chanzo kilicho ndani ambacho kiliomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji, makamanda wa nchi hizo walikuwa na kibarua kizito cha kujadili mbinu mbalimbali za kukabiliana na uhalifu pamoja na hukumu inayotolewa kwa watu wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na unga.
“Walijadili matukio mengi ya uhalifu likiwemo suala la madawa ya kulevya, wakajadili mbinu za kukomesha biashara hiyo haramu ili waweze kupata suluhisho la kudumu,” kilisema chanzo hicho.
                                                                                  Kamanda Nzowa.
WATAKA HUKUMU KWA NCHI WANACHAMA IWE MOJA
Ilidaiwa kuwa, malighafi aliyokamatwa nayo Masogange na mwenzake kwa nchi nyingine kifungo chake kinafanana na kile cha mtu aliyekamawa na madawa ya kulevya, lakini kwa Afrika Kusini ni cha chini sana.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, miongoni mwa masuala yaliyokuwepo kwenye ajenda ni pamoja na umoja katika suala zima la hukumu hususan kwa watuhumiwa wa madawa ya kulevya kwani kumekuwa hakuna uwiano baina ya nchi moja na nyingine ndani ya Jumuiya hiyo.
Rais Dk. Kikwete.
“Tumeona ilivyokuwa kwa Masogange, nchi nyingi zimepinga kabisa ile hukumu kwani ilikuwa haifanani na kosa husika. Mtu anatozwa faini ya shilingi milioni nne na laki nane (Sh. milioni 4.8) kitu ambacho hakiingii akilini kabisa, makamanda wengi wameonesha kupinga hukumu ile,” kilisema chanzo hicho.

MASOGANGE AJIFICHA
Wakati makamanda wa nchi hizo wakimaliza kikao chao, habari zenye utata zimesambaa kwamba, Masogange alitua Bongo katikati ya mwezi uliopita lakini anaishi Dar au Mbeya kwao kwa kujificha.
Baadhi ya watu, wakiwemo marafiki zake wamekuwa wakisema kwa mkato staa huyo yupo Dar huku wengine wakisema baada ya kutua Dar alikwenda kwao Mbeya kwa sababu hataki kujulikana kuwa amesharudi Bongo.
Mwenyewe anapopatikana kwenye simu na kuulizwa amekuwa akijibu bado yupo Afrika Kusini lakini siku yoyote atatua Dar.

NZOWA ATOA UFAFANUZI
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alipoulizwa kwa njia ya simu juzi kuhusu mkutano huo alijibu kuwa yupo safarini kikazi akiwa katika mazingira mazuri atatoa ufafanuzi.
“Nipo safarini kikazi, naomba unitafute siku nyingine nitakupa ufafanuzi mzuri sana,” alisema Kamanda Nzowa ambaye naye ilidaiwa alikuwepo kwenye kikao hicho.
Mellisa Edward.
KUMBUKUMBU
Masogange na Mellisa Edward walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg  nchini humo wakidaiwa kuingiza madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Hata hivyo, mahakama kuu nchini humo ilidai madawa hayo si ya kulevya bali ni malighafi haramu iitwayo Ephedrine ambapo kwa sheria za Afrika Kusini mtu akipatikana na hatia ya kuyaingiza nchini humo ni kifungo cha miezi 32 jela au faini ya shilingi milioni 4.8 kama alivyohukumiwa Masogange ambayo ni ndogo

Sunday, September 22, 2013

NIKIRUDI TANAZANIA SITAKI MAPOKEZI KWASABABU WATANZANIA NI WANAFIKI"...AGNESS MASOGANGE


 




Mtanzania Agnes Gerald, maarufu Masogange, ameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, baada ya kulipa faini ya R30,000 (Sh4.8 milioni) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumika 
kutengeneza dawa za kulevya.

Lakini hata hivyo kwa mujibu chanzo chetu toka kwa mtu wa karibu na familia yake, Masogange amesema hatohitaji mapokezi yoyote pindi atakapowasili nchini kwa vile hao wanaopanga mapokezi ndio wanafiki wakubwa ambao walikuwa wanashangilia alipokuwa jela

Saturday, September 21, 2013

MASOGANGE, MELISA WAACHIWA HURU RASMI KWA KUTOA FAIN YA SH MILIONI 4

maso aca5c
Johannesburg. Mtanzania Agnes Gerald, maarufu Masogange, ameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, baada ya kulipa faini ya R30,000 (Sh4.8 milioni) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya
Wakati Masogange akitozwa faini hiyo mwenzake, Melissa Edward ameachiwa huru na mahakama hiyo, baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.
Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini(Hawk), Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya, bali kemikali aina ya ephedrine.

Hata hivyo, Mahakama ilibaini kuwa, Melissa hana hatia kwa kuwa ilionekana kuwa amemsindikiza Masogange, ambaye alimwomba amsaidie kubeba mzigo huo.
"Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kumsaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini hayakuwa yake. Mizigo yote iliandikwa jina la Agness Gerald na si Melissa," alisema Kapteni Ramaloko.
Kapteni Ramaloko alisema, Melissa alijitetea kuwa hakuwa amesafiri pamoja na Masogange bali walikutana ndani ya ndege na Masogange alimwomba amsaidie kubeba mizigo hiyo, kwani ilikuwa mikubwa.
Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria, hivyo mahakama iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela kwa miezi 30 (miaka miwili na miezi mitano) au alipe faini ya R30, 000 (sawa na Sh4.8 milioni).
Hata hivyo, Kapteni Ramaloko alisema mdhamini wa Masogange alilipa nusu ya fedha na kwamba zinazobaki amalizie baadaye.
Alisema kutokana na kutomalizia kulipa fedha hizo ataendelea kubaki nchini humo hadi atakapomaliza kulipa nusu ya faini iliyobaki.
Masogange na mwenzake walipokamatwa na SARS ilielezwa walikuwa wamebeba dawa za kulevya aina ya
Methamphetamine, lakini Mahakama juzi ilithibitisha walikamatwa na kemikali aina ya Ephedrine, ambayo siyo dawa za kulevya.
Wakati Kamishna Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Geofrey Nzowa alipoulizwa na Mwananchi Jumamosi juzi alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa ni dawa za kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya, lakini Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS), Marika Muller alieleza kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5 ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine.Jana, Muller alipoambiwa kuwa Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kulipa faini na mmoja kuachiwa huru kwa kuwa Mahakama imeridhika kuwa hazikuwa methamphetamine bali kemikali aina ya Ephedrine, alirudia tena na kueleza kuwa, mamlaka hiyo ina uhakika na kazi yake na iwapo mahakama imewaachia huru basi yeye hana la kusema zaidi.
"Kazi yetu kubwa ni kukamata mizigo haramu inayopitishwa uwanja wa ndege, kama Mahakama imeona kuwa si dawa za kulevya, hatuna la kuongeza. Kikubwa tumemaliza kazi yetu," alisema Muller kwa kujiamini.
Hata hivyo, Nzowa jana akizungumzia kuachiwa huru kwa Watanzania hao, alionyesha kushangazwa jinsi Mahakama ilivyotoa adhabu ndogo.
"Hii ni ajabu sana. Kama watu wamebeba mzigo wenye thamani ya Sh6.8 bilioni wanapigwa faini ya milioni nne, hawataogopa kufanya hiyo biashara. Hao watu ni hatari sana," alisema Nzowa.
Alipoulizwa iwapo wakirudi Tanzania wanaweza kushtakiwa, Nzowa alisema kitengo chake hakitaweza kuwashtaki tena kwa sababu wanaweza kujitetea kuwa tayari walishahukumiwa, isipokuwa Mwendesha Mashtaka aliyekuwa akisimamia kesi yao anaweza kukata rufaa.
"Iwapo Mwendesha Mashtaka wa huko akikata rufaa kwa kuona adhabu aliyopewa mhalifu huyo ni ndogo, anaweza kufanya hivyo," alisema Nzowa.
Nzowa alisema, inasikitisha kuwa wakati mapambano ya biashara hiyo yakiwa yanaendelea Tanzania, watuhumiwa hao wanaachiwa.
"Adhabu waliyopewa ni ndogo hasa wakati huu ambao Tanzania tunachafuka kwa tuhuma hizi. Lazima kitu kifanyike kubadili hali halisi hapa nchini," alisema.
Nzowa alieleza kuwa alikwenda Afrika Kusini tangu Septemba Mosi kuwahoji wasichana hao ambao hata hivyo hawakuweza kusema lolote la kuisaidia polisi.
Masogange aliandika kwa maandishi kuwa ni kweli mzigo ulikuwa wa kwake, lakini akasema mdogo wake, ambaye ni Melissa, hajui lolote na alikuwa amemsaidia.
Julai 5, mwaka huu Masogange na Melissa walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo wakidaiwa wamebeba kilo 150 zilizodaiwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine zenye thamani ya Sh6.8 bilioni.
Dawa hizo zilizokuwa zimepakiwa katika mabegi makubwa sita, zinatajwa kuwa ni kiwango kikubwa kukamatwa katika historia ya SARS ndani ya uwanja huo unaotumiwa na mataifa makubwa duniani.Taarifa za kukamatwa kwa wasichana hao zilipamba kurasa mbalimbali za magazeti ndani na nje ya Tanzania, jambo lililosababisha Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kuchukua hatua za kuusafisha Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.
Baada ya uchunguzi wa Dk Mwakyembe ambao ulibaini kuwapo mchezo mzima uliochezwa wakati Masogange na Melissa walipokuwa uwanja wa ndege.
Agosti 17 alitoa agizo la kufukuzwa kazi, Koplo Juliana Thadei, Jackson Manyoni, Yusuph Daniel Issa, Koplo Ernest na Mohamed Kalugwan.
Mwakyembe alisema katika hali isiyokuwa ya kawaida mfanyabiashara ambaye hakuwa na tiketi ya kusafiri siku hiyo, baadaye alibadili mawazo hapohapo na kuamua kuondoka siku hiyo kwenda Afrika Kusini na kulipia faini ya dola 60 (Sh96, 000) ili kupata tiketi.
Pia Mwakyembe aliliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kumkamata mfanyabiashara anayedaiwa kumsaidia Masogange kusafirisha dawa za kulevya ambaye alitoweka na mabegi matatu ya dawa hizo huko Afrika Kusini:
chanzo mwananchi

Friday, September 20, 2013

USHAHIDI KUWA AGNESS MASOGANGE YUKO HURU.... HUU HAPA



Picha hizi Amezipiga akiwa Gym leo asubuhi zinazidi kutoa ushahidi kuwa yupo Mtaani ...au jela za South Mambo ndio hivi ? We unasemaje?

Wednesday, September 18, 2013

UJUMBE ALIYO ANDIKA AGNESS MASOGANGE FACEBOOK WAZUA MASWALI..JE KAACHIWA HURU?
















Hii ni post aliyoiweka Agnes Masogange kwenye ukurasa wake wa FB na imeanza kusambaa kwa kasi kupitia wasanii mbalimbali na mm nimeinasa  muda huu.
Je yawezekana wametoka?Au ndio zile fununu kuwa wanapiganiwa kesi yao irejee nchini?
Tungoje kama ni kweli au la!


Monday, September 16, 2013

Melisa, Masogange kortini Jumatano



Watanzania, Agnes Masogange na mwenzake Melisa Edward,  wanatarajiwa kupandishwa tena  kizimbani Septemba 18 mwaka huu  katika mahakama moja nchini, Afrika Kusini.
Wanawake hao watasomewa mashtaka ya  kukutwa na kilo 150 za kemikali za kutengenezea  dawa za kulevya aina ephedrine, zenye thamani ya Sh7bilioni.
Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifika katika mahakama hiyo ya mjini Johannesburg Septemba 13 mwaka huu.
Hata hivyo wote walikana mashtaka hayo na kurudishwa rumande  kwa sababu upelelezi wa kesi hiyo  ulikuwa haujakamilika
Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, aliliambia gazeti jana   kuwa washtakiwa watapandishwa kizimbani kwa mara ya pili  na kwamba wao  wanasubiri maamuzi ya mahakama kwa mara nyingine.

 “Kama upelelezi wa kesi yao utakamilika huenda  wakaachiwa kwa dhamana kama watatimiza masharti lakini dhamana hiyo siyo kurudi hapa nchini watabaki huko huko, Afrika ya Kusini kama sheria zao zinavyoeleza,”  alisema Kamanda Nzowa.
MWANANCHI:

Monday, September 9, 2013

MASTAA BONGO WAMFANYIA SHEREHE YA BIRTHDAY AGNESS MASOGANGE


So guys kama mnavyojuajuz ilikuwa birthday ya Miss FineAss AGNES MASOGANGE, Na kwakutambua mchango naurafiki wao Jackline Wolper akaamua kuangusha boonge la dinner kwa ajili ya kusherehekeasiku ya kuzaliwa ya kipenzi chao uyo ambaye yuko jela kwa tuhuma za madawa ya kulevya huko South Africa... hivi ndivyo hali ilivyokuwa...
Enjoy!!

Friday, September 6, 2013

HATIMAYE MASOGANGE NA MELISA WAAMUA KUWATAJA WALIOWATUMA UNGA A.KUSINI BAADA YA ADHABU KALI.



BAADA ya warembo hao kukamatwa ilielezwa kuwa walikuwa wakigoma kueleza mzigo huo wa kilo 150 wa unga ulikuwa wa nani hivyo ikabidi polisi wa upelelezi watafute njia nyingine ya kuwalainisha kwa kuwabembeleza kuwa wakieleza ukweli wataachiwa.

Chanzo hicho kilisema kuwa baada ya mbinu hiyo kushindikana ndipo wawili hao wakaingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ikiaminika kuwa watasema aliyewatuma.

“Unajua Sauzi (Afrika Kusini) huwa hawana utani na ishu za madawa ya kulevya. Jamaa (polisi) wana kila aina ya mbinu ya kumfanya mtu aeleze ukweli.
“Katika kutesa unaweza kuingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ambayo nayo huwa yana steji zake.
“Kwanza utaanzia kwenye chumba kilichojazwa siafu wakubwa na huko unaweza usijue kuwa kuna siafu zaidi ya kuona kitu kama red carpet (zuria jekundu) kuanzia sakafuni, ukutani hadi kwenye dari, kumbe wale wote ni siafu.
“Wakishakuingiza mle ndipo utashangaa wale siafu wanacharuka na kuanza kukung’ata mwili mzima, zoezi hilo hufanyika kwa saa 24. Lazima useme ukweli.
“Kama bado ukijifanya mbishi au nunda ndipo unapelekwa hatua nyingine ya kulazimishwa kujisaidia haja ndogo kwenye waya wa umeme.

“Si unajua tena waya wenye umeme na maji vikikutana nini kinatokea? Lazima itatokea shoti ya kutisha kwani ule waya hufuata sehemu yale maji yanapotokea.
“Kinachofuata ni mtu kupigwa shoti kali ya umeme ambapo lazima utasema tu.
“Hicho ndicho kilichowapata akina Masogange kama wanavyofanyiwa Wabongo wengine wanaokamatwa Mitaa ya Rissik hapa Johannesburg.

“Baada ya mateso hayo, waliwataja waliowatuma mzigo huo wa unga aina ya crystal methamphetamine wenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8,” kilisema chanzo hicho ambacho ni Mbongo ambaye kwa sasa ni mkazi wa Mtaa wa Rissik, Johannesburg, wanapoishi Wabongo kwa kuungaunga aliyewahi kukumbwa na mkasa kama huo.

Habari za ndani zilidai kuwa baada ya kupitia mateso hayo, mabinti hao waliwataja watu wawili waliowatuma kusafirisha mzigo huo, mmoja akiwa ni mtoto wa kigogo ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania (jina lipo).

Ilidaiwa kuwa mtoto huyo wa mkubwa ni mjanja wa mjini ambaye alihusika kushughulikia kusafirisha mwili wa msanii Albert Mangweha ‘Ngwea’ aliyefia Johannesburg Juni, mwaka huu.

Ilivuja kuwa mwingine aliyetajwa na akina Masogange ni mfanyabiashara maarufu Bongo anayesafiri nje mara kwa mara huku jina la ‘mtoto wa mjini’ Mangunga likitajwa zaidi hata na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe.

Kamanda wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa, alikiri kupewa majina hayo lakini akaliomba gazeti hili kutoyachapisha kwa sasa kuepuka kuvuruga ushahidi.

Baada ya polisi wa upelelezi na wale wa kimataifa (Interpol) kujiridhisha na maelezo ya mabinti hao, walipandishwa kizimbani kwa mara ya pili Agosti 19, mwaka huu chini ya ulinzi mkali kama ule ‘anaowekewaga’ Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda anapofikishwa kwenye mahakama mbalimbali nchini kwa kesi zake za madai ya uchochezi.

Habari kutoka Sauzi zilieleza kuwa akina Masogange walipandishwa tena kizimbani hivi karibuni ambapo tayari kesi yao imeanza kuunguruma ikielezwa kuwa endapo watakutwa na hatia watakula mvua ya kifungo si chini ya miaka 10 kwa sheria za nchi hiyo.

Masogange na Mellisa walinaswa nchini humo Julai 5, mwaka huu wakiwa na mabegi sita yaliyokuwa na mzigo huo wa unga

Thursday, September 5, 2013

SAKATA LA AGNESS MASOGANGE. AINGIZWA CHUMBA CHA MATESO ATAJA ALIYE MTUMA MADAYA HAYO YA KULEVYA



IMEVUJA! Staa muuza nyago kwenye video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu za Kibongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ na shosti wake, Mellisa Edward kabla ya kupandishwa kizimbani kwa msala wa dawa za kulevya ‘unga’ Afrika Kusini waliingizwa kwenye chumba cha mateso kwa saa 24 ili kutaja waliowatuma.
Habari kutoka kwa chanzo chetu kilichopo jijini Johannesburg nchini humo zilidai kuwa baada ya kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, walipelekwa polisi ambapo walichukuliwa maelezo.
Ilielezwa kuwa mwanzoni waligoma kueleza mzigo huo wa kilo 150 wa unga ulikuwa wa nani hivyo ikabidi polisi wa upelelezi watafute njia nyingine ya kuwalainisha kwa kuwabembeleza kuwa wakieleza ukweli wataachiwa.
MATESO SAA 24

Chanzo hicho kilisema kuwa baada ya mbinu hiyo kushindikana ndipo wawili hao wakaingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ikiaminika kuwa watasema aliyewatuma.

USHUHUDA
“Unajua Sauzi (Afrika Kusini) huwa hawana utani na ishu za madawa ya kulevya. Jamaa (polisi) wana kila aina ya mbinu ya kumfanya mtu aeleze ukweli.
“Katika kutesa unaweza kuingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ambayo nayo huwa yana steji zake.
“Kwanza utaanzia kwenye chumba kilichojazwa siafu wakubwa na huko unaweza usijue kuwa kuna siafu zaidi ya kuona kitu kama red carpet (zuria jekundu) kuanzia sakafuni, ukutani hadi kwenye dari, kumbe wale wote ni siafu.
“Wakishakuingiza mle ndipo utashangaa wale siafu wanacharuka na kuanza kukung’ata mwili mzima, zoezi hilo hufanyika kwa saa 24. Lazima useme ukweli.
“Kama bado ukijifanya mbishi au nunda ndipo unapelekwa hatua nyingine ya kulazimishwa kujisaidia haja ndogo kwenye waya wa umeme.
“Si unajua tena waya wenye umeme na maji vikikutana nini kinatokea? Lazima itatokea shoti ya kutisha kwani ule waya hufuata sehemu yale maji yanapotokea.
“Kinachofuata ni mtu kupigwa shoti kali ya umeme ambapo lazima utasema tu.
“Hicho ndicho kilichowapata akina Masogange kama wanavyofanyiwa Wabongo wengine wanaokamatwa Mitaa ya Rissik hapa Johannesburg.
WALIOWATUMA
“Baada ya mateso hayo, waliwataja waliowatuma mzigo huo wa unga aina ya crystal methamphetamine wenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8,” kilisema chanzo hicho ambacho ni Mbongo ambaye kwa sasa ni mkazi wa Mtaa wa Rissik, Johannesburg, wanapoishi Wabongo kwa kuungaunga aliyewahi kukumbwa na mkasa kama huo.
MTOTO WA KIGOGO ATAJWA
Habari za ndani zilidai kuwa baada ya kupitia mateso hayo, mabinti hao waliwataja watu wawili waliowatuma kusafirisha mzigo huo, mmoja akiwa ni mtoto wa kigogo ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania (jina lipo).
Ilidaiwa kuwa mtoto huyo wa mkubwa ni mjanja wa mjini ambaye alihusika kushughulikia kusafirisha mwili wa msanii Albert Mangweha ‘Ngwea’ aliyefia Johannesburg Juni, mwaka huu.
Ilivuja kuwa mwingine aliyetajwa na akina Masogange ni mfanyabiashara maarufu Bongo anayesafiri nje mara kwa mara huku jina la ‘mtoto wa mjini’ Mangunga likitajwa zaidi hata na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe.
Gazeti hili lilipozungumza na Kamanda wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa, alikiri kupewa majina hayo lakini akaliomba gazeti hili kutoyachapisha kwa sasa kuepuka kuvuruga ushahidi.
ULINZI KAMA SHEHE PONDA
Baada ya polisi wa upelelezi na wale wa kimataifa (Interpol) kujiridhisha na maelezo ya mabinti hao, walipandishwa kizimbani kwa mara ya pili Agosti 19, mwaka huu chini ya ulinzi mkali kama ule ‘anaowekewaga’ Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda anapofikishwa kwenye mahakama mbalimbali nchini kwa kesi zake za madai ya uchochezi.
WAPANDISHWA TENA KORTINI
Habari kutoka Sauzi zilieleza kuwa akina Masogange walipandishwa tena kizimbani hivi karibuni ambapo tayari kesi yao imeanza kuunguruma ikielezwa kuwa endapo watakutwa na hatia watakula mvua ya kifungo si chini ya miaka 10 kwa sheria za nchi hiyo.
Masogange na Mellisa walinaswa nchini humo Julai 5, mwaka huu wakiwa na mabegi sita yaliyokuwa na mzigo huo wa unga.

Thursday, August 22, 2013

FAMILIA YA MASOGANGE WAAMUA KUMWACHIA MUNGU ISHU YA MTOTO WAO

 FAMILIA ya Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ inadaiwa kumwachia Mungu ishu ya binti huyo kukamatwa na madawa ya kulevya Julai 5, mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa ndugu mmoja wa familia hiyo aliyeomba jina lake lisitiriwe, wameamua kumwachia Mungu ishu hiyo kwani ndiye anayejua ukweli.

“Unajua baba wa Masogange (mzee Gerald Waya) ni mlokole, sasa amekabidhi ishu nzima mikononi mwa Mungu kwa hiyo hayuko tayari kusemasema maneno ambayo hayatakuwa na faida,” alisema ndugu huyo.
Habari zinazidi kudai kwamba, mzee huyo aliwahi kuchukizwa na kitendo cha binti yake huyo kujiingiza kwenye sanaa, hadi kuonekana akinengua kwenye muziki.

Hilo liliwahi kubainishwa na Masogange mwenyewe miaka ya nyuma alipohojiwa na gazeti ndugu na hili (Ijumaa) kupitia safu ya Ten Questions (Maswali Kumi) ambapo ilikuwa hivi:
TQ: Inasemekana umetokea kwenye familia ambayo imeiva kidini, walokole, wao wanachukuliaje suala la wewe kuingia kwenye mambo ya kuuza sura tena wakati mwingine kwenye mavazi ya kimitego?

Agnes: Mh! Baba yangu hataki kabisa kusikia mambo ya muziki na niliwahi kukosana naye lakini nalazimisha kwa kuwa ni moja ya ajira.
Jitihada za kumpata baba wa Masogange ziligonga mwamba baada ya namba iliyotolewa na ndugu huyo kutokuwa hewani.
Masogange na nduguye, Mellisa Edward walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakiwa na ‘unga’ kilo 150 aina ya crystal methamphetamine wenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.

Monday, August 19, 2013

Huyu ndo Mangunga aliyewatoroka akina Masogange baada ya polisi kuwanasa


Waziri wa uchukuzi Prof. Harrison Mwakyembe alimtaja mshukiwa mmoja wa dawa za kulevya aitaye Nassoro Mangunga  na  kuwataka  polisi  wamtie  nguvuni  popote  atakapoonekana....

Hata  hivyo, mshukiwa huyu pamoja na picha zake alishaandikwa na gazeti la SANI katika toleo lake la Agosti 7-9, 2013 (toleo la 1042) pamoja na namna alivyosafirisha mzigo pamoja na akina Masogange.

Hii  ni  taarifa  ya  gazeti  hilo:


Unaweza kukimbia lakini huwezi kujificha. Msemo huu unaonekana kutimia kwa kijana anayedaiwa kuambatana na watuhumiwa wa dawa za kulevya waliokamatwa Julai 5 mwaka huu nchini Afrika Kusini, Agness Gerald 'Masogange' (25) na Melisa Edward (24), kunaswa na gazeti hili.

 
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, wasichana hao, Masogange na Melisa walisafiri ndege moja na kijana anayejulikana kwa jina la Nassoro Mangunga wakitoka Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini, wakisafiri na ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA), yenye namba SA 189.


Wakiwa katika ndege hiyo Mangunga, Agness na Melisa walikaa kwenye viti vilivyo jirani kabisa huku Mangunga akiwa katikati yao, kwani Agness alikaa kiti namba 23B, Mangunga alikaa kiti namba 23D na Melisa alikaa kiti namba 23A.


Mangunga ambaye ni rafiki mkubwa wa wanamuziki wa Bongo Flava, Rashidi Abdallah Makwiro 'Chid Benz', Mgaza Pembe 'M2theP' na Albert Keneth Mangweha 'Mangwair', wakati akisafiri na mabinti hao walikuwa na jumla ya mabegi tisa kama kumbukumbu za nyaraka za shirika hilo la ndege zinavyoainisha.


Licha ya nyaraka za kusafirishia mabegi hayo kuonesha jina la Agness Gerald ambaye ni mpenzi wa Mangunga tangu mwanzoni mwa mwaka jana, kuwa ndiye aliyelipia mabegi hayo, ila kwenye sehemu ya anuani ya waraka pepe, imeandikwa  Mangunga.


Aidha, mabegi hayo, yalikuwa na kilo 150 za dawa za kulevya lakini kila mmoja alitakiwa kusafiri na kifurushi cha kilo ishirini kama mzigo wa mkononi ambao husafiri bila malipo, hivyo watatu hao kwa pamoja walikuwa na kilo sitini wote kwa pamoja, hivyi kubaki kilo 90 ambazo walizozilipia Dola za Marekani 94 badala ya Dola 450.


Mangunga ambaye licha ya kuishi zaidi nchini Afrika Kusini, lakini pia ni mkazi wa maeneo ya Ilala jijini Dar es Salaam.


Agness na Melisa, walikamatwa Julai 5, 2013 katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Thambo, Afrika Kusini wakiwa na dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya Sh bilioni 6.8 za Kitanzania, na walipotiwa mbaroni, walikuwa na mabegi sita tu kati ya tisa waliyokuwa nayo wakati wanapanda ndege jijini Dar es Salaam.


Inasemekana mabegi hayo matatu yaliondoka na Mangunga na kutokomea kusikojulikana....

Friday, August 9, 2013

VIGOGO WALIOMTUMA AGNESS MASOGANGE KUPELEKA MADAWA YA KULEVYA AFRIKA KUSINI WABANWA....MMOJA AFUNGIWA ACCOUNT ZAKE




HABARI zilizochimbuliwa kwa undani zinadai kuwa tayari vigogo wawili waishio nchini wamebanwa na Jeshi la Polisi Tanzania wakituhumiwa kumtuma Masogange kupeleka madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa habari hizo, vigogo hao (majina tunayo) walidakwa wiki iliyopita kila mmoja kwa wakati wake na kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), jijini Dar ambako walihojiwa kwa saa sita.
“Hawa vigogo walikamatwa wiki iliyopita na kuhojiwa kwa masaa sita, waliachiwa lakini waliambiwa wakihitajika tena wataitwa,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo kikaongeza kuwa, licha ya kuhojiwa na kuruhusiwa kuondoka, vigogo hao, mmoja alinyang’anywa ‘paspoti’ yake huku mwingine akaunti zake za benki zikifungwa kwa muda usiojulikana.
Habari zinasema kuwa, kigogo ambaye akaunti zake zimefungwa amekuwa akihaha kila kukicha kuhakikisha zinafunguliwa kwa sababu hana njia nyingine ya kuingiza kipato.
Juzi, Ijumaa liliwasiliana na Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa ili kujua uhakika wa madai hayo ambapo alisema:
“Sisi (polisi) tumekuwa tukifanya mambo yetu kwa siri kubwa, si rahisi kusema. Tukisema kunakuwa na ugumu kwa sababu mnaandika kwenye magazeti, matokeo yake uchunguzi unavurugika.
“Mfano wale wasichana (akina Masogange) waliokamatwa Afrika Kusini wamekuwa wagumu kuwataja waliowatuma kwa sababu hao waliowatuma ndiyo wanaowategemea kuwawekea dhamana.”
Agnes Gerald na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park nchini humo wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
via-GPL


Monday, July 29, 2013

AGNESS MASOGANGE AFUTIWA DHAMANA YAKE NA KURUDISHWA RUMANDE



HUKU  akiwa hajui nini hatima ya kesi inayomkabili ya kunaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini, Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’ amepata balaa jipya

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo nchini humo,Masogange na mwenzake aliyekamatwa naye, Melisa Edward wamefutiwa dhamana hivyo wamerudi tena rumande.

Habari zinadai kuwa, dhamana za wawili hao zimefutwa kufuatia kuhisiwa kwamba wana mpango wa kuondoka nchini huko kinyemela na kurejea Tanzania, jambo ambalo limetafsiriwa kama jaribio la kuikimbia kesi hiyo.


“Unajua huku Sauzi si kila mtu anawaonea huruma Masogange na Melisa kwa tatizo lililowapata, sasa utakuta maskani mtu anaropoka vitu vya ajabu pengine vya uongo bila kujua kuwa si kila mtu anayesikiliza atayaachia hapohapo, wengine ni ‘mainfoma’ wanayafikisha mbele.



“Hicho ndicho kilichomtokea Masogange, wakati baadhi ya watu wakiwa kwenye mchakato wa kumsaidia ili kujua jinsi gani kesi yake itakwenda haraka, wengine wanakwenda kuongea mambo ya ajabu kwa watu wao wanaowatuma kuwapelekea taarifa, eti kuna watu wanajipanga kuwatorosha, si sheria ikafuata mkondo wake.
 

“Hii inatupa wakati mgumu sisi tuliokuwa tumsaidie, mara kwa mara tunaitwa na kuhojiwa na jeshi la polisi. Ndiyo maana dhamana yao imefungwa, ukiangalia nini kilichosababisha ni maneno ya uongo yanayotokea maskani,” kilisema chanzo hicho ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake.


Licha ya kukumbana na kesi ya madawa ya kulevya, Masogange aliendelea kutumbukiza picha zake kwenye mitandao ya kijamii na kuzielezea, lakini baada ya kufutiwa dhamana amekauka mitandaoni kwa picha za karibuni.
 
“Nyie si mnaona, siku hizi haposti tena picha zake mpya kama palepale katikati baada ya kukamatwa. Siku zile alikuwa nje kwa dhamana, sasa yupo rumande hawawezi kumwachia akacheza na simu,” kilisema chanzo.  

Baada ya staa huyo kutiwa nguvuni Julai 5, mwaka huu, baadhi ya Watanzania waishio Bongo na kule Afrika Kusini walidaiwa kuchanga fedha kwa lengo la kumsaidia mrembo huyo lakini kufuatia kuvuja kwa taarifa za kufungwa kwa dhamana yake, wamekosa nguvu na kusikitikia kitendo hicho.

Inadaiwa kuwa, nchini Afrika Kusini mtu akikamatwa na ‘unga’ anaweza kuwa nje kwa dhamana wakati kesi yake ikiendelea kusikilizwa mahakamani, Tanzania mtu akinaswa na unga kesi inasikilizwa akiwa rumande
  

Friday, July 26, 2013

"NILIJUA TU KWAMBA WANAFIKI WATAFURAHIA MATESO YANGU" ....AGNESS MASONGANGE


VIDEO Queen ambaye hivi karibuni alidaiwa kukamatwa na madawa yanayosadikiwa ni ya kulevya ‘unga’ nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’, Agness Gerald ‘Masogange’ amefunguka kuwa alijua watu wengi watafurahia kilichompata kwa kumuongelea kila wakati.

Akizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu akiwa Sauzi, Masongange ‘alishauti’ kuwa watu wengi wanamuongelea vibaya bila kujua nini kilichompata  hivyo anaamini hata marafiki zake wa karibu wamefurahia tatizo alilopata.


“Najua kabisa kuna watu wengi wamefurahia tatizo nililopata lakini watambue kuwa kila mtu anaweza kupata tatizo hivyo wapunguze kuongea sana bila kujua ni kitu gani kilichotokea juu yangu,” alisema Masogange ambaye atapanda kizimbani kwa mara ya pili mwezi ujao.

Monday, July 22, 2013

AGNESS MASOGANGE ATAPANDISHWA KIZIMBANI TENA TAREHE 13 AGOSTI MWAKA HUU

Hatima ya msanii anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, waliokamatwa Afrika Kusini na dawa za kulevya kesi yao inatarajiwa kusomwa tena tarehe 13 Agosti mwaka huu nchini humo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliweka wazi kuwa wanadada hao wawili tayari walishapandishwa kizimbani wiki iliyopita.

Alisema kuwa kutokana na ushahidi kutokukamilika ndiyo sababu ya akinadada hao kusubiri kupanda kizimbani tena tarehe 13 ya mwezi ujao.

Kamanda Nzowa aliweka wazi kuwa nchi zote mbili zinashirikiana kwa ajili ya kufanya upelelezi wa jambo hilo: "Nchi zote mbili tunategemeana kwa upelelezi, hivyo sisi huku tunafanya wa kwetu na wao wanafanya wa kwao mwishoni tunaulizana tulipofikia hivyo ndivyo tunavyofanya kazi," alisema Nzowa.

Wadada hao ambao walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu wakitokea Tanzania, walikutwa na dawa za kutengenezea dawa za kulevya, ambazo hazina matumizi nchini,  zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni sita.

Sunday, July 14, 2013

HAWA NDIO WALIMPA SHAVU MASOGANGE APITE NA 'UNGA' AIRPORT


HAKUNA sababu ya kumkamata ‘mchawi’  kwenye skendo ya Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ kudaiwa kukamatwa na madawa ya  kulevya nchini Afrika Kusini wakati ukweli upo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Watu mbalimbali ambao wamesoma sakata hili kwenye vyombo vya habari, walitoa maoni yao wakisema kuwa watu wanaotakiwa kuwajibishwa ni waliokuwa uwanjani hapo siku Masogange aliposafiri na kuruhusu mizigo ya mrembo huyo na mdogo wake, Melisa Edward ipite bila ukaguzi makini.

“Kuna uwezekano kabisa wa kuwajua watu hao,” alisema msomaji wetu, Mbande Kinaka, mkazi wa Kariakoo, Dar.
Risasi Jumamosi lilimtafuta Mkuu Kitengo cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Kamanda Godfrey Nzowa, alipopatikana na kuulizwa namna ya kuwabaini waliomruhusu Masogange akapenya na mzigo airport, alisema lazima watawapata.


Taarifa tulizozipata zinasema Agnes na mdogo wake Melisa Edward  waliondoka nchini Julai 5, mwaka huu kwenda Afrika Kusini.

Friday, July 12, 2013

JESHI LA POLISI TANZANIA LAAMUA KUMFUATA AGNESS MASOGANGE AFRIKA KUSINI...!!


Jeshi la Polisi litapeleka askari wake Afrika Kusini kuwahoji washiriki wa video za wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Agnes Gerald ‘Masogange’ na mwenzake Melisa Edward waliokamatwa nchini humo na dawa za kulevya.

Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa aliliambia gazeti hili kwa simu jana kuwa watawapeleka polisi kuwahoji na wanaamini wahusika watawaeleza wahusika wa mzigo huo.

Wasichana hao walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania wakiwa na kilo 150 za dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine.

“Tutawapeleka askari wetu kuwahoji, tumekwishaanza uchunguzi wa hili...wote watakaohusika katika hili tutawakamata, lakini tunakwenda polepole hatua kwa hatua kuhakikisha tunawanasa wahusika sahihi,” alisema Nzowa.

Naye Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, (JNIA), Moses Malaki alieleza kushangazwa na kiasi kikubwa kupitishwa kwenye uwanja huo licha ya kuwa wapo watu wenye dhamana ya kuangalia usalama.

“Sitaki kusema tutafanya nini, lakini ninachotaka kukwambia ni kwamba uchunguzi umeanza na suala zima tumewaachia polisi na sisi tutatoa ushirikiano kwa kila hatua watakayotutaka, lazima kukomesha hili.

Tutaangalia nani walikuwa zamu siku hiyo,” alisema Malaki.


Tuesday, July 9, 2013

HUYU NDIO "MELLIS EDWARD" ALIYEKAMTWA NA MADAWA YA KULEVYA AKIWA NA "AGNESS MASOGANGE" HUKO AFRIKA KUSINI...!!

Picha  ya  Mrembo Mellis Edward  aliyedakwa  na  madawa  ya  kulevya  Afrika  kusini  akiwa  na  Agness Masogange
Mellis Edward
Inahisiwa kuwa  huyu mwanamke wa pili aliyetajwa na Kamanda Nzowa kwa jina la “Melisa Edward”  ni mdogo wake na Agnes ambaye katika akaunti ya facebook anayo tumia jina la (MELLIS EDWARD) , Agnes amemuweka katika orodha ya family kama ‘sister’ katika akaunti yake ya Facebook.
 Kamanda  Gofrey  Nzowa - Kitengo  cha  Madawa ya Kulevya

 Agness Masogange  akiyahesabu  "MAPESA" yake.Picha  hii aliiweka  siku  chache  zilizopita

AGNESS MASOGANGE AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA AFRIKA KUSINI

 
HATIMAYE  wale Wanawake wawili walionaswa  na  madawa ya  kulevya  Afrika  kusini wametambuliwa kuwa  ni  mabinti  wa  KITANZANIA ..


Mabinti  hao  wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Akizungumza na mwandishi wetu  jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.

Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald (MASOGANGE)  ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.

Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.

Jumapili iliyopita mtandao huu  ulipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.

Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.

Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.

Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi. Tukio hilo linatoka takribani wiki moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu kutangaza kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini.

Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.

Pia alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.

Pinda alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.
 


Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.

Alisema vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani.