HABARI zilizochimbuliwa kwa undani zinadai kuwa tayari vigogo wawili waishio nchini wamebanwa na Jeshi la Polisi Tanzania wakituhumiwa kumtuma Masogange kupeleka madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa habari hizo, vigogo hao (majina tunayo) walidakwa wiki
iliyopita kila mmoja kwa wakati wake na kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha
Polisi (Central), jijini Dar ambako walihojiwa kwa saa sita.
“Hawa vigogo walikamatwa wiki iliyopita na kuhojiwa kwa masaa sita,
waliachiwa lakini waliambiwa wakihitajika tena wataitwa,” kilisema
chanzo hicho.
Chanzo kikaongeza kuwa, licha ya kuhojiwa na kuruhusiwa kuondoka, vigogo
hao, mmoja alinyang’anywa ‘paspoti’ yake huku mwingine akaunti zake za
benki zikifungwa kwa muda usiojulikana.
Habari zinasema kuwa, kigogo ambaye akaunti zake zimefungwa amekuwa
akihaha kila kukicha kuhakikisha zinafunguliwa kwa sababu hana njia
nyingine ya kuingiza kipato.
Juzi, Ijumaa liliwasiliana na Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kupambana na
Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa ili kujua uhakika wa madai hayo ambapo
alisema:
“Sisi (polisi) tumekuwa tukifanya mambo yetu kwa siri kubwa, si rahisi
kusema. Tukisema kunakuwa na ugumu kwa sababu mnaandika kwenye magazeti,
matokeo yake uchunguzi unavurugika.
“Mfano wale wasichana (akina Masogange) waliokamatwa Afrika Kusini
wamekuwa wagumu kuwataja waliowatuma kwa sababu hao waliowatuma ndiyo
wanaowategemea kuwawekea dhamana.”
Agnes Gerald na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa Julai 5, mwaka huu
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park
nchini humo wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine
yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
via-GPL