BENKI
Kuu ya Tanzania(BoT)Kanda ya Kaskazini Arusha imewatahadharisha
wananchi kuchukua hatua mapema juu
ya wimbi la noti bandia hapa nchini kwakuwataka wawemakini wakati
wakutoa ama kupokea noti mpya ili kuepuka kufilisika na taifa kuyumba
kiuchumi,anaripoti
Richard Konga, Arusha.
Aidha
benki hiyo imeanzisha utaratibu
wakutoa elimu kwawananchi ili kutambua noti bandia na halali kupitia
alama halisi
zilizoko kwenye noti halali na kusisitiza kwa wananchi kuwa macho kwa
kuzitambua alama hizo ilikuepuka kuruhusu matumizi ya noti feki kuingia
kwenye mzunguko wa kawaida.
Akizungumza kwenye maonyesho ya wakulima
Nanenane , Kandaya Kaskazini, Meneja wa Fedha na Utawala wa Benki hiyo,Eve na
Ndesingo alisema kuwa BoT imeanza kutumia maonesho ya wakulima ya nanenane kutoa
elimu ya utambuzi wa noti zake.
Alisema maonyesho yaliyofanyika jijini Arusha wananchi zaidi ya 10,000 wamepatiwa elimu ya utambuzi wa alama za
noti mpya lengo ikiwa ni kuwafikia wananchi zaidi waliopo hapa nchini kupitia matawi
yake.
Hata
hivyo Ndesingo alibainisha kuwa matumizi ya noti bandia kwa jamii
yamekuwa yakipungua mwaka hadi mwaka kutokana na jamii kuwa na uelewa wa
noti halisi na bandia na hivyo kupunguza kasi ya
mzunguko wa noti bandia kwa kiasi kikubwa.
Aidha
alisema kuwa BoT kupitia matawi yake hapa nchini imejizatiti kuwa
elimisha wananchi juu ya utambuzi wa noti mpya na alama zake ili jamiii
zielewe na kutofautisha noti halali na bandia.
Alisema
noti bandia iwapo zitaachwa ziendelee kuwepo kwenye mzunguko wamatumizi
ya kawaida ipo hatari kwa jamii
kufilisika sanjari na taifa kupoteza uchumi wake, kwahiyo aliitaka jamii
kuwa makini sana pindi wanapokuwa wanapokea ama kutoa noti mpya kwa
kuangalia alama zake halisi zikiwemo zakificho .
Akizungumzia namna ya kutambua noti halali za shilingi500, 2,000,5,000 na10 ,000,alisema zina alama ya kificho
ambayo unaweza kuitambua kwakuipapasa kuangalia kwenye mwanga na kwamba alama hizo
kwenye noti bandia hazipo na wala noti hizo hazina ubora unaotakiwa .
Ndesingo aliitahadharisha jamii kuwa
makini pale inapofanya malipo ya noti mpya kwa kuchunguza kwamakini alama hizo kabla ya haijapelekwa kwa mtu mwingine.