Showing posts with label kikwete. Show all posts
Showing posts with label kikwete. Show all posts

Thursday, September 11, 2014

JK AKUTANA NA MBUNIFU WA MAVAZI WA KIMATAIFA SHERIA NGOWI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Mbunifu wa mavazi wa kimataifa Sheria Ngowi(kulia)alipokutana na Rais Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam alipomtembelea na kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na tasnia hiyo jana.Rais Jakaya Kikwete akizungumza  na ujumbe wa mbunifu wa mavazi wa kimataifa Sheria Ngowi (wa kwanza Kulia) Ikulu jijini Dar es Salaam jana. Rais Jakaya Kikwete akipitia baadhi ya sample za vitambaa vya nguo vinavyotumiwa na mbunifu wa mavazi wa kimatafaifa Sheria Ngowi (kulia)IKULU Jijini Dar es Salaam jana. Mwenye suti ya bluu kushoto ni Makamu wa Rais wa Sheria Ngowi Brand Bw. Haki Ngowi ambaye pia ni blogger maarufu nchini. Rais Jakaya Kikwete katika picha ya kumbukumbu  na Ujumbe wa  Mbunifu wa mavazi wa kimataifa Sheria Ngowi (wa pili kushoto) Ikulu jijini Dar es Salaam jana

CREDITS:GPL

Wednesday, August 27, 2014

JK:Nipo tayari kukutana na UKAWA



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, amesema yeye hana tatizo kukutana na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
 “Wanajua jinsi ya kukutana nami, ili tuweze kutafuta namna ya kumaliza tofauti hizi,”alisema wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Morogoro, viongozi na wakazi wa vijiji jirani na chuo.
Aidha alisema ana matumaini kuwa mchakato wa katiba unaoendelea utaweza kuwapatia Watanzania katiba mpya.
“Mimi naishi kwa matumaini. Naamini kuwa tutafika mwisho vizuri. Mchakato ni mgumu lakini barabara ndefu haikosi kona. Tukidhamiria kweli tutafika tuendako vizuri,” alisema.
Aliwambia mamia ya wanachuo, watumishi wengine wa chuo hicho: “Maoni yenu ndiyo maoni yangu. Ni jambo la kusikitisha kuwa tofauti hizi za viongozi wa siasa zinaleta mfarakano wa namna hii. Tokea mwanzo niliwaambia kuwa wakiruhusu kushindana na kuviziana katika mchakato huo watakwama.”
 “Aidha, niliwaambia kuwa Katiba inayotafutwa siyo katiba ya CCM, ama ya CHADEMA, ama ya NCCR, ama ya CUF. Niliwaambia kuwa hii ni katiba ya wananchi wa Tanzania. Ni vyema tukakubaliana kuwa yenye kutugawa tukayaacha kwa sasa na kukubali kwa yale ambayo hatuna tofauti,” alisema.
Mapema wanafunzi wa chuo hicho waliunga  mkono mchakato wa Bunge Maalumu la Katiba wakisema wanaridhishwa na hatua iliyofikiwa na mwendo mzima wa bunge hilo na kuwa mwafaka unawezekana kuhusu vipengele viliyobakia na kupatikana kwa theluthi mbili za kupitisha katiba mpya.
Katika risala hiyo iliyosomwa na Rais wa Chama cha Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Boniface Maige Juma, wanafunzi hao walisema ni vyema mchakato huo ukaungwa mkono na kila Mtanzania ili kuuwezesha kuleta neema na matarajio yanayokusudiwa.

 “Tunaridhishwa na hatua iliyofikiwa na Bunge Maalum la Katiba. Tunaamini kuwa mwafaka unawezekana kwa vipengele vingine vya rasimu ya katiba. Aidha, tunaamini kuwa theluthi mbili za kupitisha katiba mpya zinawezekana kupatikana,” alisema.

Friday, August 22, 2014

INAPENDEZA:RAIS KIKWETE ASAFIRI KWA TRENI YA TAZARA KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA MOROGORO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika kituo cha Kisaki baada ya kusafiri kwa treni katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera, Mbunge wa Morogoro Kusini Mhe Innocent Kalogeris na KAtibu wa Rais Bw. Prosper Mbena wakiongea ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki mkoani Morogoro.
Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli, Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA Bw. Ronald Phiri (kulia) na viongozi wengine ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa Morogoro.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa Morogoro.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA Bw. Ronald Phiri zawadi ya picha ya jengo la makao makuu ya TAZARA akiwa ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa Morogoro.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na viongozi wengine ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa Morogoro.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipanda treni ya TAZARA kuelekea Kisaki Mkoani Morogoro akiwa katika ziara yake ya mkoa huo.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na umati mkubwa wa watu baada ya kuwasili katika kituo cha Kisaki baada ya kusafiri kwa treni katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Wananchi waliojitokeza kwa wingi kumlaki baada ya kuwasili katika kituo cha Kisaki baada ya kusafiri kwa treni katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika mkoa wa Morogoro. 

Thursday, July 17, 2014

RAIS KIKWETE AZINDUA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU ZA NHC MJINI SONGEA


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi nyumba zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC huko Mkuzo, wilayani Songea mjini mkoani Ruvuma leo. Kutoka kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof.Anna Tibaijuka, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Bwana David Misonge Shambwe, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Said Mwambungu.
Ris Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe la msingi wakati wa ufunguzi wa nyumba zilizojengwa kwa gharama nafuu na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) huko Mkuzo wilayani Songea mjini Mkoani Ruvuma leo.Kushoto ni kaimu Mkurugenzi wa NHC Bwana David Misonge Shambwe na wwapili kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na makazi Prof.Anna Tibaijuka

Tuesday, July 15, 2014

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WASAANI NYOTA WA FILAMU NA MUZIKI KUTOKA NCHINI MAREKANI JIJINI DAR LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa filamu na muziki kutoka  Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni na  Terrence J. Jenkins, mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment (wa pili kulia) Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records (wa pili kushoto)  na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitumia simu yake ya mkononi kuwaonesha vivutio vya kitalii wasanii nyota wa muziki na filamu wa Kimarekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni   Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group. Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa muziki na filamu kutoka Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni   Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group. Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.PICHA NA IKULU.
wakiwa katika picha ya Pamoja

Sunday, July 13, 2014

KIKWETE: UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KUSOGEZWA MBELE


RAIS Jakaya Kikwete amesema uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ulikuwa ufanyike mwezi Oktoba mwaka huu, huenda ukasogezwa mbele kutokana na kutokamilika kwa mchakato wa rasimu ya mabadiliko ya Katiba.
Kauli hiyo ameitoa kwenye mkutano wa majumuisho ya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tanga.
Alisema kulingana na hali ilivyo hivi sasa ambapo Bunge la Katiba halijakamilisha kazi zake, ni dhahiri kwamba uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi huo kwa kutumia Katiba mpya haupo.
“Kwa mfano, wabunge endapo wataamua wapitishe kwamba katiba itambue serikali 3 ni lazima kwanza itungwe katiba ya Tanganyika ambayo itaainisha taratibu zitakazotoa mwongozo wa uchaguzi…hata kama itabaki kama ilivyo …. bado muda wa kuandaa huo utaratibu wa uchaguzi wa serikali za mitaa hautatosha kwa sasa”, alisema.
 
Aidha aliongeza, “Nimeona niliseme hili japo kwa ufupi kwamba uchaguzi huu huenda utalazimika kusogezwa mbele kutokana na kutokamilika kwa mchakato wa Rasimu ya mabadiliko ya Katiba“, alisema.
 
Katika hatua nyingine, Rais amewataka Maofisa Kilimo kwenye halmashauri kujiendeleza kitaaluma na kuwa mabingwa waliojikita katika taaluma ya mazao yanayostawi kwenye maeneo yao badala ya kuyashughulikia kwa ujumla mazao yote yanayolimwa na wananchi.
 
Alisema utekelezaji wa agizo hilo utaongeza mavuno kwa zao husika, utapanua wigo wa uzalishaji pamoja na utaalamu katika kushughulikia zao, aina ya zao na kuleta tija katika sekta ya kilimo.
 
Alisema hatua ya maofisa kilimo kuendelea kujishughulisha kwa ujumla na mazao yote yanayostawi bila kuwa na lengo la kusimamia mazao maalumu, kunaifanya sekta hiyo kudumaa na hivyo kushindwa kuwakwamua kiuchumi wananchi.
 
“Nimegundua kwamba watu wetu wengi hawana utaalamu uliobobea…hata maofisa kilimo wetu hawana taaluma maalumu zilizojikita kwenye aina ya mazao mengine zaidi ya mpunga na mahindi, hatua ambayo inawasababisha washindwe kusimamia vizuri uzalishaji wa mazao mengine ambayo yangeweza kuwakwamua kiuchumi wakulima kwenye halmashauri husika,” alisema.
 
Aliongeza, “Kwa hiyo ni jukumu lenu viongozi wa halmashauri kuwachukua maofisa kilimo wenu na kuwapeleka SUA kwa ajili ya ku-specialize (kujikita) kulingana na vipaumbele vyenu vya mazao kwa sababu sio wote wanao ubingwa katika kila zao…tukifanikiwa kwenye hilo tutapata mafanikio zaidi”, alisema.
 
Aidha aliwataka viongozi kwenye mkoa wa Tanga kuhakikisha shughuli za kilimo zinajikita kwenye uzalishaji endelevu wa mazao ya matunda na mboga, kwa kuwa mkoa huo uko katika fursa nzuri kiuzalishaji zaidi ya mazao ya nafaka

Sunday, July 6, 2014

RAIS KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA AICC SABASABA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye viwanja vya Sabasaba
Rais Dkt. Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje
Rais Kikwete (Mwenye Koti la Blue) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Taasisi zake.
Mtumishi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mbwana Msingwa akiweka saini katika kitabu cha wageni alipokuja na familia yake kwenye banda la Mambo ya nje lililopo kwenye viwanja vya sabasaba
Ankal akisalimiana na Afisa Mawasiliano Ally kondo, alitembelea Banda la Mambo ya Nje katika Viwanja vya Sabasaba. Picha na Reginald Phili

Saturday, November 30, 2013

Rais Kikwete awasili jijini Kampala kuhudhuria mkutano wa EAC....Maada kuu watakazoongelea ni pamoja na Sarafu moja ya jumuiya ya Afrika Mashariki

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama wa Uganda muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.
*****************

Wakuu wa nchi zinazounda jumuiya ya Africa Mashariki wanakutana leo tarehe 30 Novemba huko Kampala, Uganda.

 Wakuu hao ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Yoweri Mseveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkuruzinza wa Burundi na Uhuru Kenyatta wa Kenya.
 
 Masuala watakayozungumzia leo ni pamoja na soko la pamoja, umoja wa forodha, shirikisho la kisiasa na umoja wa sarafu ambapo leo watatia saini mkataba wa kuwa na sarafu moja

Monday, November 11, 2013

RAIS KIKWETE AINGILIA KATI SAKATA LA MCHUNGAJI MWINGIRA KUDAIWA KUZAA NA DAKTARI AMBAYE NI MKE WA MTU


Dk. Philis Nyimbi anayedaiwa kuzaa na Nabii Mwingira.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ameingilia kati sakata la Mtume na Nabii Josephat Mwingira kudaiwa kuzaa na mke wa mtu. 


JK, aliingilia kati sakata hilo baada ya mume wa mtu, Dk. William T. Morris, kukamatwa na maofisa wa uhamiaji kisha kutakiwa kufukuzwa nchini kutokana na kile kinachodaiwa ni ‘shinikizo la mtu mwenye nguvu’.
Habari ambazo Tumezithibitisha ni kwamba baada ya Dk. Morris kufungua mashtaka akimtuhumu Mwingira kuzaa na mkewe, Dk. Philis Nyimbi, alikamatwa na maofisa wa uhamiaji kisha kupewa hati ya kutimuliwa nchini.
tumebaini kuwa JK ndiye aliyezuia hati hiyo na mpaka sasa, Dk. Morris, raia wa Liberia, yupo nchini akiendelea na harakati zake za kusaka haki kisheria kuhusiana na madai yake hayo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
JK ALIMFIKIAJE?
Inaelezwa kuwa wakati Dk. Morris alipokamatwa, alitokea msamaria mwema (jina tunalo) anayejua ‘njia za kupita’ kufika Ikulu ambaye alimfikishia JK mkanda mzima wa sakata hilo la Mwingira.
“… (anataja jina la msamaria mwema), alimwambia JK kuwa nchi inaelekea katika aibu, Dk. Morris ni mtu anayetambulika Umoja wa Mataifa (UN) hasahasa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).
“JK baada ya kusimuliwa kila kitu, alichokifanya ni kuingilia kati na kuzuia Dk. Morris asifukuzwe nchini,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:

Mtume na Nabii Josephat Mwingira.
“Vilevile JK aliomba namba ya Dk. Morris kisha alimtumia SMS na baadaye wakaongea, akamhakikishia yupo salama nchini lakini kuhusu madai yake kuhusu mkewe, aendelee kufuata sheria.”
HATI YAKE BADO INASHIKILIWA NA UHAMIAJI
Habari zaidi zinaweka kweupe pamoja na JK kuzuia Dk. Morris asitimuliwe nchini, bado maofisa wa uhamiaji Mkoa wa Pwani, wanashikilia hati yake ya kusafiria (passport) mpaka leo.
Dk. Morris alipoulizwa kuhusu hilo, alikiri: “Ni kweli wanaishikilia. Niliwaomba wale maofisa wanipe nyaraka inayoonesha passport yangu wanaishikilia. Niliogopa wanaweza kunigeuka. Waliniandikia, kwa hiyo sina wasiwasi.”

Cheti cha ndoa ya Dk. Morris na mkewe Dk. Philis.
SAKATA LENYEWE LIPOJE
Toleo lililopita la gazeti hili, tuliandika habari yenye kichwa Mume: Mwingira amezaa na mke wangu.
Katika habari hiyo, gazeti hili lilisimamia tuhuma zilizofunguliwa na Dk. Morris kwenye Kituo cha Polisi Kati (Central), Kibaha, Pwani, akidai Mwingira amezaa na mkewe.
Shauri hilo lilifunguliwa kwa kichwa JALADA LA UCHUNGUZI, nambari KBA/PE/20/2011, mtuhumiwa akiwa Josephat Mwingira.
Habari yetu iliyopita, mke wa Dk. Morris, Dk. Philis, alidai alizaa nje ya ndoa baada ya kutekelezwa na mumewe, ingawa alikataa kumtaja mwanaume aliyezaa naye.
Zaidi ya hapo, Dk. Philis alisema Dk. Morris hakuwa mwaminifu kwenye ndoa, kwani alidiriki kumsaliti kwa binti mwenye umri chini ya miaka 18 ambaye wao kama mke na mume, wangeweza kumzaa.

Mtoto wa Nabii Mwingira aliyezaa na Dk. Philis.

DK. MORRIS NA MWANDISHI WETU
Katika kumchimba zaidi Dk. Morris, mwandishi wetu alifanya naye mahojiano kama ifuatavyo;
MWANDISHI: Ni kweli ulimtelekeza mkeo ndiyo maana akaamua kusaliti na kuzaa nje ya ndoa?
DK. MORRIS: Si kweli hata kidogo, amenisingizia, naomba amuogope Mungu.
MWANDISHI: Una ushahidi wowote kuwa ulikuwa unamjali mkeo?
DK. MORRIS: Ushahidi upo wa kutosha. Anazungumzia kipindi cha kuanzia mwaka 2006 mpaka 2011, ni kipindi ambacho nilikuwa naishi Marekani kikazi WHO.
Kipindi hicho, nilikuwa namtumia mke wangu dola za Kimarekani 2500 (zaidi ya shilingi 4,000,000) kila baada ya wiki mbili lakini kuna wakati nilikuwa nampa zaidi ya hizo.
Gazeti hili lilioneshwa nakala ya karatasi za kibenki zikionesha jinsi alivyokuwa akimuingizia fedha mkewe aliyekuwa na akaunti katika Benki ya Standard Chartered Moshi (namba ya akaunti tunaihifadhi), yeye akiwa Marekani akitumia Bank of America kuanzia mwaka 2006.
MWANDISHI: Hebu niambie, Dk Philis bado ni mke wako? Yeye anasema wewe siyo mumewe.
DK. MORRIS: Ni mke wangu halali wa ndoa takatifu. Nilifunga naye ndoa katika Kanisa la St Alban, Dar Desemba 23, 2001, nikiwa na umri wa miaka 39 na yeye (mkewe) akiwa na miaka 30.
Ndoa hiyo niliigharamia sana tangu mavazi ya wapambe wangu na wa mke wangu. Ilikuwa siku ya furaha kabisa. Sikupenda wakwe zangu wapate shida.
MWANDISHI: Ukiwa Marekani ulipata habari zozote za kuwa mkeo ni mjamzito au kajifungua?
DK. MORRIS: Hapana, sikuwa na habari kabisa juu ya jambo hilo na ndiyo maana nilikuwa nikimtumia fedha za kutosha.
Kuna siku moja aliniambia anataka kwenda kufanya utafiti Afrika Kusini, akawa  anataka dola 2500 siku hiyohiyo aliyoniambia. Nilimwambia taratibu za fedha Marekani ni ngumu. Nilikwenda ofisini kwangu nikaomba malipo ya awali ya mshahara wangu, nikamtumia dola za Kimarekani 3,000 (shilingi milioni 4.8 kwa cheji ya sasa).
MWANDISHI: Uliporejea Tanzania, ilikuwaje ukajua mkeo amezaa nje ya ndoa?
DK. MORRIS: Nakumbuka usiku mke wangu alianza kulia. Nilishangaa nikamuuliza kwa nini unalia, akanijibu kwamba anaomba nimsamehe kwa sababu amezaa nje ya ndoa.
MWANDISHI: Baada ya kusikia hivyo ulijisikiaje?
DK. MORRIS: Niliishiwa nguvu kabisa, nikamuuliza kwa nini amefanya usaliti huo? Nilimuuliza ni nani amempa mimba, akaniambia ni mwanaume mmoja injinia ambaye alidai yupo Marekani kwa wakati huo.
MWANDISHI: Hayo ulikuwa unamuuliza mkiwa wapi Dar au Kibaha?
DK. MORRIS: Tulikuwa Moshi, nikiwa Marekani mke wangu aliniambia yupo Moshi anachukua shahada ya pili (Master) ya udaktari, na nilikuwa namtumia fedha za pango la nyumba, lakini pale nilimkuta hotelini, kesho yake tukarudi Dar.
MWANDISHI: Baada ya kufika Dar mambo yalikuwaje?
DK. MORRIS: Mke wangu aliniambia kuwa ni lazima nimsindikize kwa Nabii Mwingira ili akaombewe kwa ushetani alioufanya wa kuzaa nje ya ndoa.
MWANDISHI: Ulikubaliana naye?
DK. MORRIS: Nilimkubalia tukaenda kwa sababu wakati huo nilikuwa sijajua kuwa yeye ndiye mbaya wangu. Tulimkuta na akatukaribisha ofisini kwake.
MWANDISHI: Mambo yakawaje?
DK. MORRIS: Mwingira alituombea, wakati akituombea Mwingira mwenyewe alilia sana.
MWANDISHI: Ukaja kumtuhumu vipi tena Mwingira kuwa amezaa na mkeo?
DK. MORRIS: Subiri kwanza, kesi ikishakuwa mahakamani yote yatakuwa wazi. Nitataka pia tupimwe kila kitu, DNA  pamoja na Ukimwi.
MWANDISHI: Vipi madai ya wewe kutimuliwa nchini?
DK. MORRIS: Namshukuru sana Rais Kikwete, ni kiongozi mzuri, alinisaidia sana. Namuamini, nampenda na nawaomba Watanzania wampende kiongozi huyu, ni mpenda haki.
MWINGIRA BADO SHIDA
Jitihada za waandishi wetu kumpata Mwingira bado hazijazaa matunda, kwani kila njia inayotumika, wasaidizi wake hawataki kabisa kiongozi huyo wa Kanisa la Efatha, afikiwe na kuhojiwa kuhusu madai haya.
Hata hivyo,halijakata tamaa, litaendelea kumsaka mpaka apatikane na kujibu tuhuma hizo.

Monday, October 28, 2013

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WATOA POLE KWA MJANE NA FAMILIA YA BALOZI ISAAC SEPETU LEO


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  alipokwenda  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole. Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
 Mama Salma Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam. . Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mjane wa Balozi Isaac Sepetu, Mama Miriam Sepetu, alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kwa mjane huyo na familia ya Marehemu Sepetu aliyefariki jana jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa wanafamilia wa Balozi Isaac Sepetu alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kufuatia msiba Marehemu Sepetu aliyefariki jana  jijini Dar es salaam.

  Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimfariji mjane wa Balozi Isaac Sepetu alipokwenda  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kufuatia msiba Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
:Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji  mjane wa Balozi Isaac Sepetu, Mama Miriam Sepetu, alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kwa mjane huyo na familia ya Marehemu Sepetu aliyefariki jana jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU

Thursday, October 24, 2013

BALAA:MSAFARA WA RAIS KIKWETE WAKUMBWA NA BALAA LA MOTO MKALI .. HUKO IRINGA...!!!

Moto mkubwa ukiteketeza msitu wa Sao Hill Mufindi



 Msafara  wa rais Jakaya  Kikwete ukiwa  umesimama kwa muda eneo la  msitu wa  taifa  wa Sao Hill Mufindi  katika barabara kuu ya Iringa- Mbeya  kufuatia  moto mkubwa kuwaka katika msitu huo jana mchana.


 Askari polisi akimamisha  msafara  wa rais Kikwete kutokana na moto  mkubwa  kutanda  eneo hilo la Changalawe katika  msitu wa Taifa  wa Sao Hill umbali wa mita  mbili kuelekea  barabara  ya Ikulu ndogo mjini Mafinga


 Askari  wa FFU  wakishuka katika gari lao kwenda  kuangalia  usalama  wa rais Kikwete na  kulia gari la kwanza ni naibu waziri wa ujenzi gari la pili la la tatu ni magari ya Ikulu yakiwa  yamesimama


 hapa  askari  wakishuka  kuingia katika moshi mzito  kuangalia  usalama  wa rais katika eneo hilo ambalo moshi mzito  ulitanda barabarani


Msafara  ukipita  eneo hilo salama huku kulia ni askari wa JKT mafinga wakizima moto  huo



YAKIWA  ni masaa takribani mawili  kupita  kutoka Rais Jakaya  Kikwete kufanya  kikao chake  cha majumuisho   ya ziara  yake   na  viongozi wa mkoa wa Njombe na  kuwataka  kuchukua hatua  katika kuthibiti moto  ili  kuepusha ukame, moto  mkubwa umezuka katika msitu wa Taifa  wa Sao Hill Mufindi na kupelekea  msafara  wa  Rais kusimama kwa  muda  kiusalama kutoka na moshi mzito  uliotanda  barabara  kuu ya Iringa Mbeya .


Moto  ulio ulioanza  kuwaka  mida ya saa nane  mchana    ulizuia kwa  muda  kama dakika tatu hivi msafara  wa Rais Kikwete  kufimama katika eneo la Changalawe mjini  Mafinga umbali  wa mita 2  kufika  njiapanda  ya   kuingia ofisi ya mkuu  wa wilaya ya  Mufindi na Ikulu ndogo  ya  wilaya ya Mufindi.


Kutokana na tukio hilo la moto msafara  wa rais  Kikwete  ulisimama na baada ya maofisa  usalama  kushuka na kutazama usalama  zaidi wa msafara  huo ndipo  walioruhusu msafara  huo  kuendelea .


Hata  hivyo  jitihada  kubwa  zilionekana kufanywa na  kikosi  cha askari  wa  JKT Mafinga  pamoja na  wananchi ambao  walikuwa  wakizima  moto  huo .


Huku   vyombo  vya  usafiri  yakiwemo mabasi ya abiri yanayosafiri  kutoka Dar es Salaam kuwenda  mikoa ya  kusini na nchi  za kusini mwa Tanzania yakikwama  kuendelea na  safari  kutoka na moto  huo kushikakasi na  moshi  mzito  kutanda  barabara 


Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Dr  Christine Ishengoma  alisema kuwa  uongozi  wa  mkoa  tayari  umeagiza  mkuu wa wilaya ya Mufindi kuwasaka   waliohusika na  uchomaji  moto huo ili  kuchukulia  hatua  kali.



Mkuu  huyo  wa  mkoa alisema  kuwa mkoa  wa Iringa umekuwa  ukichukua hatua  kali  kwa wale wote wanaoanzisha  moto  kichaa kama  huo hivyo  kupitia  ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi wahusika  watasakwa  popote  walipo .


Mbali na  hilo mkuu  huyo amelipongeza  jeshi la JTK Mafinga kwa  kuchukua hatua  za haraka katika kukabiliana na moto  huo huku akisema madhara  zaidi  yatokanayo na moto  huo yatatolewa baada ya  moto  huo kuthibitiwa .