Showing posts with label wolper. Show all posts
Showing posts with label wolper. Show all posts

Monday, December 16, 2013

NA HIKI NDIYO KIASI ANACHOPATA KWA KILA MOVIE MOJA ... JACKLINE WOLPER..!!!






Inawezekana ukawa unajua but in real sense unahitaji kujua zaidi na Swahilitz ipo kukupa exclusive, mkali wa movie kwa sasa Jackline Wolper , mwanadada hustler aliyezaliwa tarehe 6 December huko mjini A- town, ni ukweli usiofichika kwamba Wolper ndio msanii bize wa kike mwenye kazi nyingi zaidi katika Bongo movie kwa mwaka huu.
Jacklin aliyewahi kwenda kwenye audition ya Planet bongo ya host Salama J hii inaweka wazi kama ni real hustler and that has no doubt kama hakuja Dar kupiga picture kwa bahati mbaya hakuweza kufanikiwa lakini hiyo haikumrudisha nyuma na ndio ilikuwa sababu ya yeye kujituma zaidi na zadi na hivi sasa Jackline Wolper ndio msanii busy wa kike kuliko wote East Afrika akiwa ameshafanya movie kumi na moja toka feb 22 mpaka oct 20 mwaka huu. Hicho ni kiwango kikubwa kuweza kufikiwa kwa wasanii wa kike hapa nchin ambao wanafanya vizuri with high pay.
Curently ukitaka kuongea deal na Wolper ujipange, kama Diamond alivyofika dau la Million kumi per show Jackline Wolper ameweza kufikia mpaka Million tano per movie

Friday, November 22, 2013

HUU NDIO MUONEKANO MPYA WA MWANADADA "JACKLINE WOLPER"......




Sunday, November 10, 2013

HII NDIYO SABABU ILIYONIFANYA NITOKE KWENYE "UISLAMU" NA KURUDI "KANISANI"....... WOLPER AFUNGUKA..!!!

Hatimaye  Jacqueline Wolper afunguka baada ya kubadili Dini kwa mara ya pili. Hichi ndicho alichokisema
Hatimaye mwanadada Jacqueline Wolper ameamua kuweka wazi kilichotokea mpaka kuamua kubadili Dini yake ya Uislamu na kurudi kwenye ukristo tena. Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii mwanadada huyu wa bongo movies ametoa ujumbe ufuatao kwa mashabiki wake.
“…mambo mashabiki zangu.sikua na njia nyingne yakulikwepa hili nanaamini kua kwa wale mashabk zangu waislam amtomaind maana akuna mtu wakumsikiliza chin ya hanga zaidi yawazazi so imenipasa kurudi kanisani kwakauli yawazazi wangu.naamin kama aujaolewa ata uwe na miaka mingap bado unatakiwa kua chin ya imaya ya wazazi ata ukifa ujue unazikwaje na mimi ni binadam sijui saa wala dakika.muhm nikuwajuza nakuwaelewesha mashabk zangu stak maswal nawapenda wote…”
Hapo awali iliripotiwa kuwa mwanadada huyu ameamua kuwa mkristo tena baada ya penzi lake lililosababisha abadili dini na kuwa muislamu na jamaa aitwaye 'Dallas' kuvunjika hivi karibuni.
Swali ni je, atabadili dini tena akitokea mwingine wa dini aliyo tofauti na sasa?

Wednesday, November 6, 2013

PICHA: HIVI NDIVYO "JACKLINE WOLPER" ALIVYODHALILISHWA FACEBOOK.., AWAOMBA MASHABIKI KUWA NA HURUMA KIDOGO


Akionyesha kusikitishwa na kile kinachoendelea facebook, leo hii muigizaji bongo movie,Jackline Walper ameanika maongezi yaliyokuwa yakiendelea katika akaunti ya Walper fake kupitia facebook ikionyesha chati iliyoonekana Walper akiomba sh 20,000 kwa ajili ya kununua umeme mara baada ya kutaikiwa na umeme huku akifanya kazi zake kwenye computer. 


Walper aliweka maongezi hayo yakiambatana na manenoo haya kwa chini

wolpergambemashaniki zangu haya ndo mambo ya fc bk dah hvii kweli ndo wanavyonidhalilisha plz nisaidien ata kuamdika huko kwa fc bk zenu situmii jina lolote zaidi ta wolper gambe real .siyoo vzuri jamani muwe na roho ya huruma kdogo dah

BAADA YA MIEZI KADHAA YA KUSILIMU NA KUWA MUISLAMU...WOLPER AAMUA KUREJEA TENA KANISANI

STAA anayefanya vyema katika tasnia ya filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameamua kurudi katika imani yake ya awali ya Kikristo ikiwa ni miezi michache tangu alipotangaza kubadili dini na kuwa Muislamu.

Novemba 3, mwaka huu (Jumapili iliyopita) paparazi wetu alimnasa Wolper katika Kanisa la KKKT lililopo Kijitonyama jijini Dar, akisali sambamba na waumini wa kanisa hilo.

Bila ya kificho, Wolper ambaye alipokuwa Muislamu alikuwa akitumia jina la Ilham alisimama na kujitambulisha kama muumini mpya wakati mchungaji wa kanisa hilo alipowataka waumini wapya kufanya hivyo.
 

Wolper akiwa katika ibada kanisani hapo.
 Wakati ibada hiyo ikiendelea, Wolper alionekana kuimba pambio kwa hisia kali na ibada ilipoisha, alitoka kanisani huku mkononi mwake akiwa ameshika Biblia.
 

Wolper (kulia) akiwa na muumini mwenzake nje ya kanisa.
 Nje ya kanisa hilo, Wolper alionekana akiongea na wazee wa kanisa pamoja na baadhi ya waumini ambapo wote walimkaribisha kwa furaha.
 


Jacqueline Wolper akiwa katika vazi la Kiislamu wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan mwaka jana.
 Paparazi wetu alimfuata Wolper na kumuuliza kilichomfanya arudi kwenye dini yake ya awali, naye alisema kwamba amefanya hivyo kutokana na msukumo wa wazazi wake ambao kwa muda mrefu walikuwa wakipinga kitendo chake cha kuwa Muislamu.
 “Nimeamua kuurudia Ukristo kwa kuwa wazazi wangu kwa muda mrefu walikataa mimi kuwa Muislamu, kwa hiyo kuanzia sasa siyo Ilham tena, niite Jacqueline kama zamani,” alisema Wolper.
 

 Mwaka jana, Wolper alibadili dini na kuwa Muislamu kutokana na kuwa na uhusiano na Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
 Dallas akiwa nje ya nchi akamtaka Wolper kubadili dini ili akirudi wafunge ndoa ya Kiislamu, Wolper alikubali na kufanya hivyo katika Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni jijini Dar na kuchagua jina la Ilham.
 

Gari aina ya BMW X6 alilonunuliwa Wolper na Dallas baada ya kuwa muislamu.
 Dallas alirudi nchini lakini wawili hao  hawakufunga ndoa bali penzi lao likaingia doa na kumwagana, Wolper akaendelea na msimamo wa imani yake hiyo mpya na mara kwa mara alikuwa akidai kwamba hataiacha dini hiyo pamoja na kumwagana na Dallas.

Friday, August 16, 2013

JACK WOLPER"SI KILA MWANAUME ANAJUA KUHONGA, KUHONGA KIPAJI BWANA"

 STAA katika tasnia ya filamu Bongo, Jackline Wolper amefungukia kipaji cha wanaume kuhonga na kusema kuwa, si kila mwenye pesa nyingi anafanya hivyo bali inategemea na hulka ya mtu

Akifafanua juu ya madai kuwa wauza unga wengi Bongo wanaongoza kwa kuwahonga mastaa, Wolper alisema siyo kweli kwani mtu unaweza kuwa na mpenzi mfanyabiashara mwenye pesa nyingi lakini akawa mbahili.

“Si kweli kuwa wauza unga ndiyo wanahonga sana wanawake au sisi mastaa, unaweza kuwa na bwana mfanyabiashara na mwingine kaajiriwa lakini huyo aliyeajiriwa akawa ana kipaji cha kuhonga, akakupa hata asilimia 75 ya mshahara wake na yule mwenye pesa nyingi akawa mbahili sana, ni kipaji tu,” alisema

Tuesday, July 9, 2013

JACK WOLPER HANA KAZI HAPA MJINI ZAIDI YA KUJIUZA ".....BABY MADAHA

MWIGIZAJI wa kike na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Baby Madaha Joseph amemshukia mwigizaji mwenzake wa kike Jack Wolper kwa kudai kuwa amekuwa akitumia vyombo vya habari kumsema na baadae kujifanya anamuomba msamaha huku hana dhamira ya kweli.

Akiongea na FC , msanii huyo amesema kuwa  Jack  Wolper anatumia jina lake ili apande na kuwa Maarufu (nyota ).

“Mimi ni mwanamke mpigaji na ninajua ninachofanya katika maisha yangu...

"Kuna wanawake hawajui misingi ya sanaa.Ni wanawake ambao  wamevamia fani na kutuharibia  sifa  zetu  kama  wasanii..

"Mimi siwezi kugombana na mtu mwenye fani moja ,tena  ya kubebwa . Jack hana cha kufanya akifeli kuigiza labda arudie kazi yake ya kuuza vipodozi...Atafanya nini kingine hapa mjini zaidi  ya  kujiuza?,”alisema Baby Madaha  na  kuongeza:

“Jack anataka kukiki kwa kunichafulia jina langu, lakini mimi ni Star mwenye vision na najua nafanya nini katika Industry..


"Mimi ni kiongozi mtarajiwa .Nategemewa niongoze watu , sasa nikianza kugombana na watu itaniharibia  ndoto zangu za kisiasa,”