Wednesday, November 6, 2013

BAADA YA MIEZI KADHAA YA KUSILIMU NA KUWA MUISLAMU...WOLPER AAMUA KUREJEA TENA KANISANI

STAA anayefanya vyema katika tasnia ya filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameamua kurudi katika imani yake ya awali ya Kikristo ikiwa ni miezi michache tangu alipotangaza kubadili dini na kuwa Muislamu.

Novemba 3, mwaka huu (Jumapili iliyopita) paparazi wetu alimnasa Wolper katika Kanisa la KKKT lililopo Kijitonyama jijini Dar, akisali sambamba na waumini wa kanisa hilo.

Bila ya kificho, Wolper ambaye alipokuwa Muislamu alikuwa akitumia jina la Ilham alisimama na kujitambulisha kama muumini mpya wakati mchungaji wa kanisa hilo alipowataka waumini wapya kufanya hivyo.
 

Wolper akiwa katika ibada kanisani hapo.
 Wakati ibada hiyo ikiendelea, Wolper alionekana kuimba pambio kwa hisia kali na ibada ilipoisha, alitoka kanisani huku mkononi mwake akiwa ameshika Biblia.
 

Wolper (kulia) akiwa na muumini mwenzake nje ya kanisa.
 Nje ya kanisa hilo, Wolper alionekana akiongea na wazee wa kanisa pamoja na baadhi ya waumini ambapo wote walimkaribisha kwa furaha.
 


Jacqueline Wolper akiwa katika vazi la Kiislamu wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan mwaka jana.
 Paparazi wetu alimfuata Wolper na kumuuliza kilichomfanya arudi kwenye dini yake ya awali, naye alisema kwamba amefanya hivyo kutokana na msukumo wa wazazi wake ambao kwa muda mrefu walikuwa wakipinga kitendo chake cha kuwa Muislamu.
 “Nimeamua kuurudia Ukristo kwa kuwa wazazi wangu kwa muda mrefu walikataa mimi kuwa Muislamu, kwa hiyo kuanzia sasa siyo Ilham tena, niite Jacqueline kama zamani,” alisema Wolper.
 

 Mwaka jana, Wolper alibadili dini na kuwa Muislamu kutokana na kuwa na uhusiano na Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
 Dallas akiwa nje ya nchi akamtaka Wolper kubadili dini ili akirudi wafunge ndoa ya Kiislamu, Wolper alikubali na kufanya hivyo katika Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni jijini Dar na kuchagua jina la Ilham.
 

Gari aina ya BMW X6 alilonunuliwa Wolper na Dallas baada ya kuwa muislamu.
 Dallas alirudi nchini lakini wawili hao  hawakufunga ndoa bali penzi lao likaingia doa na kumwagana, Wolper akaendelea na msimamo wa imani yake hiyo mpya na mara kwa mara alikuwa akidai kwamba hataiacha dini hiyo pamoja na kumwagana na Dallas.