Wednesday, November 6, 2013

DIAMOND AFUNGUKA:"NAFANYA NGONO BILA KINGA ... ILI NIPATE MTOTO....

HUWEZI kumkwepa Diamond katika ulimwengu wa habari! Staa huyo wa muziki wa Bongo Fleva ambaye jina alilopewa na wazazi wake ni Nasibu Abdul, ameibua mengine mapya, akidai hapendi kabisa kutumia kinga awapo faragha.
 
Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz'.
Akizungumza kwa njia ya simu wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Diamond katika maelezo yake, alionesha wazi suala la afya yake siyo ishu sana, muhimu kwake ni mtoto.
Penniel Mungilwa ‘Penny’.
KILIO CHA MTOTO
Diamond alisisitiza kwamba kwa sasa kiu yake kubwa ni kupata mtoto na siyo vinginevyo.
“Nashukuru maisha yanakwenda vizuri lakini nitakuwa mwenye furaha zaidi kama nitabahatika kupata mtoto. Mwanamke atakayenizalia, atakuwa amekamilisha furaha yangu,” alisema Diamond.
Staa huyo wa singo ya Number One inayosumbua kwenye chati mbalimbali za muziki, alisema siku akiitwa baba, atakuwa amefungua ukurasa mpya kabisa kwenye maisha yake.
“Ni furaha yangu kuitwa baba. Unajua huwa naangalia... kuna baadhi ya marafiki zangu tayari wamepata watoto. Hata Wasafi kuna madensa wangu wana watoto. Nahisi nami nikipata nitakuwa na amani zaidi,” alisema.

 
Wema Sepetu.
VIPI MAGONJWA?
Pamoja na kiu yake hiyo ya kupata mtoto, kutokutumia kinga kunamuweka mtu kwenye hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa hatari ukiwemo Ukimwi, kuhusu hilo Diamond alisema, hana wasiwasi, anajiamini.
“Kwanza mimi huwa napima Ukimwi mara kwa mara, nipo sawa. Najiamini kwa asilimia mia moja lakini pia siyo kiruka njia. Sina maana kwa sababu natafuta mtoto, basi kila mwanamke nakutana naye tu. Hapana.
“Mimi nawaamini wanawake wangu... isitoshe wanajulikana. Kifupi tunaaminiana na ninatafuta mtoto ndani ya hao, siyo vinginevyo,” alisema.

 
Jokate Mwegelo.
MTOTO NJE YA NDOA?
Kuzaa kabla na nje ya ndoa haikubaliki katika jamii yetu lakini pia hata imani anayoiamini Diamond inakataza, alipoulizwa alisema haoni tatizo, anataka mtoto.
“Kaka, kaka, kaka...mbona huelewi? Hayo yote nayajua lakini cha msingi hapa mimi nimesema nahangaikia mtoto na ninatamani sana kupata mtoto ambaye naamini atakamilisha furaha yangu,” alisema.

Rehema Fabian.
MAMA WA MTOTO ATAOLEWA?
Hata hivyo, Diamond alisema mwanamke atakayemzalia mtoto siyo lazima ndiye awe mke wake wa ndoa kwa sababu suala la ndoa ni jingine na kuzaa ni jingine.
“Wangapi wanazaa na wanaheshimiana bila kufunga ndoa? Suala la ndoa ni kubwa, siyo la kukurupukia. Inawezekana mwanamke akanizalia na akiwa na tabia ninazopenda akawa mke wangu lakini inawezekana tukaishia kuzaa tu.
“Kifupi suala la ndoa ni mipango. Ikiwa sawa basi nitaoa lakini kwa sasa ninachozungumzia ndugu yangu ni kupata mtoto, baaasi!” alisisitiza Diamond.
WALIOPITA KWA DIAMOND
Diamond amewahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na wasichana kadhaa, kati yao wengine walikubali na wengine walikana uhusiano huo huku baadhi mapenzi yakiwa ya siri.
Baadhi ya wasichana waliowahi kuwa penzini na Diamond ni pamoja na Jacqueline Wolper, Wema Sepetu, Rehema Fabian, Jokate Mwegelo, Pendo Mushi na Penniel Mungilwa ‘Penny’ ambaye mpaka sasa yuko mikononi mwake.
Wema wakati penzi lao likiwa motomoto, ilisemekana ana ujauzito lakini ghafla ikawa kimya, ilikuwaje? Diamond anafafanua: “Alisema ilitoka, sasa ningefanyaje? Lakini pia sipendi kuzungumzia sana mambo hayo yaliyopita. Tuongee kuhusu yajayo.”
Kuhusu mimba ya Penny? Huyu hapa Diamond: “Ni kweli aliwahi kusema kuwa ana mimba yangu lakini baadaye alisema imeharibika. Siwezi kusema zaidi ya hapo.”
KUTOKA
Kila mmoja ana uhuru wa kupanga na kuamua maisha aliyoyachagua. Wazo la kuwa na mtoto ni zuri lakini ni vyema Diamond akawa makini ili kiu yake hiyo isije ikazima ndoto zake katika maisha
.