Showing posts with label kitaifa. Show all posts
Showing posts with label kitaifa. Show all posts

Thursday, October 2, 2014

MBUNGE WA CCM MH. VICKY KAMATA ATIWA MBARONI KWA KUWATUKANA WABUNGE WENZAKE!

MBUNGE wa Viti Maalumu, Vicky Kamatta (CCM), amekamtwa na Polisi Mkoa wa Dodoma kwa tuhuma za kuwatumia ujumbe mfupi wa simu za matusi wabunge wenzake.Chanzo cha kuaminika kutoka mjini Dodoma kiliambia MTANZANIA kuwa kwa kipindi cha miezi kadhaa Vicky amekuwa akituma sms za matusi kwa wabunge wenzake wa viti maalumu kupitia CCM, Catherine Magige na Lucy Mayenga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Uyui.
Taarifa zaidi zinasema kuwa wabunge hao walikuwa wakitumiwa sms za matusi kwa namba 0653 762 *** ambapo baada ya kuona hali imekuwa ikizidi waliamua kwenda kufungua jalada la malalamiko katika Kituo Kikuu cha Kati mjini Dodoma na kuomba ufanyike uchunguzi ili waweze kumbaini mwenye namba hizo.
 Kutokana na maelezo hayo, Jeshi la Polisi lilianza kufanya uchunguzi kuhusu sakata hilo na kubaini namba hiyo imesajiliwa kwa jina la mdogo wa kiume wa Vicky.
 
Baada ya Jeshi la Polisi kufuatilia, ilibainika namba hiyo ilikuwa ya mbunge huyo ingawa hakuisajili kwa jina lake.

Uchunguzi zaidi ukabaini kuwa sms za matusi alizokuwa anatuma, pia alikuwa akitoa taarifa kwa mwenye namba 0767 500***, akimweleza namna anavyopambana na wabunge wenzake kwa kuwatukana.
Habari zinapasha kuwa polisi wamekuwa wakifuatilia suala hilo kwa muda licha ya kuwa mara nyingi namba hiyo huwa imezimwa.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa Septemba 28, mwaka huu polisi waliokuwa wanachunguza suala hilo walifanikiwa kuipiga namba hiyo na kupokewa.
 
Chanzo cha habari kinaeleza kuwa baada ya namba hiyo kupokewa aliyepokea aliulizwa ni wapi alipo na kama inawezekana afike kwenye viwanja vya Bunge kuchukua mzigo wake.

“Aliambiwa hivyo kwa sababu SMS ya kwanza inasemekana kuwa ilitumwa na mtu aliyekuwa kwenye viwanja vya Bunge, na yule kijana aliyepokea simu bila kujua aliwaelekeza polisi nyumbani kwao akisema ndipo alipo mwenye simu.

“Polisi walipofika huko walimtaka kijana aliyekuwa nyumbani apige ile namba na akapokea yule kijana aliyewaelekeza polisi,” alisema.

Wakiwa wanafanya uchunguzi askari polisi waliipiga simu 0767 500*** ambapo ilipokewa na kigogo mmoja wa ngazi za juu serikalini ambaye baada ya mahojiano alitakiwa afike kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.

Kigogo huyo baada ya maelezo alimtaka askari anayefanya upepelezi wa kesi hiyo kuwa mvumilivu kwani muda ambao alikuwa akihitajika kituoni isingiwezekana kutokana na kuwa anapiga kura bungeni kuhusu Katiba Mpya.

Chanzo hicho kilisema pamoja na majibu hayo, mpelelezi huyo aliingiwa na hofu baada ya kutajiwa jina la kigogo huyo wa ngazi za juu serikalini.

CATHERINE MAGIGE
MTANZANIA ilipomtafuta mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Magige (CCM), alikiri kupokea matusi na kufungua kesi katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati mjini Dodoma.

Alisema Septemba 2, mwaka huu alipokea matusi kupitia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi hali iliyomshitua na kuamua kuizima ili isitumiwe tena kumpigia wala kutuma sms.

Alisema kuwa baada ya kuzungumza na baadhi ya watu walimshauri kufungua kesi polisi ili uchunguzi ufanyike na anayetuma matusi hayo akamatwe.

Alieleza kuwa Septemba 3, mwaka huu alikwenda Kituo Kikuu cha Polisi Kati Dodoma na kufungua jalada la kesi dhidi ya mtu huyo aliyekuwa akimtukana kwa sms.

“Nilipokuwa pale polisi sasa ndiyo nikaifungulia ile namba na kumbe kuna sms nyingine zilikuwa zimeshatumwa zikawa zinaingia kwa fujo.

“Ukijaribu kuangalia unaona sms ya kwanza ilitumwa na mtu akiwa kwenye eneo la viwanja vya Bunge, nyingine Naam Hotel na nyingine maeneo ya Uwanja wa Ndege hapa hapa Dodoma,” alisema Magige.

Alisema kuwa tangu hapo polisi waliendelea na uchunguzi wa suala hilo na jana alipata taarifa kuwa washukiwa wao wamekamatwa.

“Hii simu inaonekana kazi yake kubwa ilikuwa ni kututukana sisi na wakati mwingine kuongea na kutuma sms kwa (jina tunalihifadhi), kwa mfano usiku wa Septemba 28 inaonekana kwamba simu hiyo iliongea kwa sekunde zaidi ya 1,300 (dakika 21.6), na sijui walikuwa wanaongea nini.

“Kwa kweli mimi hata sielewi tumefika wapi kama viongozi tunaweza kuwa tunatumia simu kutukanana hivi,” alisema.

LUCY MAYENGA
Kwa upande wake Lucy Mayenga, alipoulizwa juu ya suala hilo, alisema amekuwa akitukanwa kwa njia mbalimbali za mtandao kwa takribani miezi minne sasa.

Alisema kuwa baadhi ya matusi yalipitishwa kwa watu wake wa karibu jambo ambalo lilimfanya aumie, lakini asijue cha kufanya.

Alisema kuwa Septemba mbili alivyoanzwa kutukanwa Magige, baadhi ya sms zilizokuwa na matusi zilimtaja pia Catherine.

“Sasa tukaongea na Lucy mimi wakati huo sikuwa Dodoma na tukashauriana pia na watu wengine ndipo alipoamua kufungua kesi.

“Nilivyokuwa natukanwa mimi nilikuwa sina muda wa kufuatilia na niliona ni kama nitu kitapita tu ndiyo maana sikufuatilia, sasa ilivyohamia kwa Catherine na huko nikawa natajwa na mimi pia, nikaona hapa sasa imefika mbali,” alisema.

KAULI YA VICKY
Akizungumza tuhuma hizo, Vicky alisema anashangazwa na taarifa za kukamatwa kwake kwani muda wote yeye alikuwa nyumbani kwake na hakuna jambo kama hilo.

“Mimi silijui suala hilo… Sijakamatwa na muda huu nipo hapa nyumbani kwangu na sasa ninajiandaa ili nirudi tena katika vikao vya Bunge,” alijibu kwa kifupi Vicky.

JESHI LA POLISI
Akizungumza sakata hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, awali alisita kidogo na baadaye alisema hakuna taarifa zozote katika mkoa wake za kukamatwa kwa mbunge huyo huku akitaka kujua taarifa hizo zimetoka wapi.


“Nani kakwambia masuala hayo… hakuna taarifa kama hizo, hatujamkamata mbunge yeyote usiku huo wa jana,” alisema Kamanda Misime

Tuesday, September 23, 2014

WACHUNGAJI ARUSHA MBARONI KWA ULAWITI WA WATOTO KANISANI

WATOTO sita, wakiwemo wawili wa kiume wenye umri wa miaka 8 hadi 14 wameharibiwa vibaya sehemu zao za siri baada ya kubakwa kanisani na watu wanaodaiwa ni wachungaji.
Watoto sita waliobakwa kanisani na watu wanaodaiwa ni wachungaji.
Wakiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru walikopelekwa kwa matibabu na kuangaliwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa, watoto hao walidai kufanyiwa mchezo huo kwa nyakati tofauti  na wachungaji watatu wa kanisa hilo lililopo eneo la  Feed Force, Kwamorombo jijini Arusha.
Mmoja wa watoto hao anayesoma darasa la 4 katika shule ya msingi alieleza kuwa yeye na wenzake wamekuwa wakifanyiwa mchezo mchafu katika kanisa hilo baada ya wachungaji hao kuwapatia shilingi 2,000 za kufungia mdomo.
“Siku moja nilipofika shuleni wenzangu wakaniambia niende pale kanisani tukapewe hela, nilipofika niliwaona wenzangu wengine wakifanyiwa mchezo mchafu na mimi mchungaji aliniambia niiname akanifanyia kitendo kibaya na kunipa shilingi 2,000, niliumia sana,’’ alisema mwanafunzi mmoja.
Mwanafunzi mwingine alisema amekuwa akitoroka shuleni na wenzake na kwenda kwa watumishi hao ambapo huwaingiza katika kanisa hilo na kujifanya wanawaombea baadaye huwafanyia mchezo mbaya.
Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema.
“Tukifika huwa wanatufungia ndani na kutuambia tuwanyonye, baadaye wanatubaka  na wakimaliza wanatuambia tukisema kwa mtu yeyote watatuchinja na kutuzika ndani ya kanisa lao,” alisema denti huyo.
Wanafunzi hao walieleza kuwa watumishi hao huwarubuni kwa kuwaeleza kuwa watawasaidia kuwasomesha iwapo watakuwa wakienda kwenye kanisa hilo na kuwaingilia.
Mzazi mmoja wa watoto hao, Julius, mkazi wa Kwamorombo alisema mtoto wake alimweleza kwamba amekuwa akifanyiwa mchezo mbaya na watumishi hao baada ya kupewa shilingi 2,000.
Alisema aligundua hilo kufuatia tabia ya mtoto wake kuchelewa kurudi nyumbani.
Naye Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema ambaye alifika hospitalini kuwajulia hali watoto hao alisikitishwa na kitendo hicho na kulitaka jeshi la polisi lifanye uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vipimo vya kidaktari ili kupata ukweli wa tukio hilo.
“Nimeongea na mkuu wa mkoa, Magesa Mulongo ambaye ameahidi kulifuatilia kwa kina suala hili na kujua undani wake,’’ alisema Lema.
Kamanda wa Polisi Arusha, Leberatus Sabas.
Hata hivyo, watoto hao baadaye walihamishiwa katika Hospitali ya Seliani kwa ajili ya vipimo zaidi huku taarifa za awali zikithibitishwa na daktari wa hospitali hiyo kuwa, baadhi yao walikutwa na michubuko na kupanuka sehemu za siri hali inayooneshwa kuingiliwa.
Watuhumiwa wa tukio hilo wanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapa  kwa uchunguzi zaidi na Kamanda wa Polisi Arusha, Leberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

CREDIT:GPL

Thursday, September 18, 2014

MAAJABU YA MTOTO WA MIUJIZA,MAMA YAKE AFUNGUKA MAZITO NA YA KUTISHA

Mtoto Happiness (10) anayedaiwa kuzua kizazaa mjini Zanzibar.
MTOTO Happiness (10) (pichani) ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita  alizua kizazaa mjini Zanzibar baada ya kuonekana akizungumza na viumbe wa ajabu na wanyama, ametua jijini Dar kufuatia kufika kisiwani humo kimaajabu.Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo, Sarah Zefania, mwanaye Happiness alianza kuonesha maajabu Zenji tangu alipoonekana kwenye uwanja wa ndege kisiwani humo wiki iliyopita.
Alisema maofisa wa uwanja huo walipigwa butwaa baada ya kumwona mtoto huyo uwanjani amepita sehemu zote za ukaguzi ambazo abiria asiyekaguliwa nyaraka zake za kusafiria na mitambo maalum ya kuangalia vitu mbalimbali vikiwemo kemikali hatari, silaha na madawa ya kulevya hawezi kupita.
Kwa mujibu wa mama huyo, aliambiwa na maofisa wa uwanja huo kuwa sehemu hizo zote mtoto wake alipita bila kuonekana na kamera za uwanjani hapo wala kuacha kumbukumbu yoyote hali iliyozidi kuwaumiza vichwa maofisa wa uwanja huo.

Zefania alisema wakati maofisa hao wakitafakari hayo, ndipo msamaria mwema mmoja alijitokeza na kumchukua kwenda kumuhifadhi nyumbani kwake.Mtoto Happiness akiwa na mama yake mzazi, Sarah Zefania.
“Akiwa nyumbani kwa msamaria mwema huyo, nimeambiwa mwanangu alianza kumfanyia maajabu mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wanyama na viumbe wengine wa ajabu au kutoka nje huku mlango umefungwa kwa ndani.
“Kuna muda alizungumza na viumbe wasioonekana ambapo aliwasiliana nao na kumletea vitu kadhaa alivyovitaka. Wakati mwingine alizungumza na wanyama wa mle ndani, kama kuku na paka ambao alikuwa akiwatuma kumfanyia yote aliyokuwa akiwaagiza.
“Hali hiyo ilimshtua yule msamaria mwema naye aliomba kupambazuke ili ampeleke mwanangu ustawi wa jamii. Yaani nahisi pengine angekuwa amemuokota sehemu bila kukabidhiwa mbele ya mashahidi pengine angemtupa usiku huohuo.
“Baada ya kushuhudia vituko hivyo, asubuhi iliyofuata alimkimbiza ustawi wa jamii ambako nako wameniambia alianza kuwafanyia vituko kama hivyo na kuwaambia kuwa angewatoroka muda wowote, kisha kuonekana akiparamia juu ya paa na kutaka kutoka.
“Yaani kwa muda mfupi waliokaa naye, maofisa wa ustawi wa jamii wanasema amewahenyesha vya kutosha ndipo walipofanya juhudi za kunitafuta na mimi nikaenda kumfuata,” alisema mama huyo muda mfupi baada ya kutua bandarini Dar.
Mtoto Happiness katika pozi.
Paparazi wetu alipomtaka mtoto huyo kuzungumza alikataa katakata na kujifanya bubu hali iliyomshangaza hata mama yake. “Nashangaa, sijui kwa nini hataki kuzungumza na wewe wakati ni mzungumzaji sana,” alisema mama Happiness.
Akizungumzia historia ya mtoto huyo, mama huyo alisema alimzalia Musoma, Mara na mwanaume mmoja aliyemtaja kwa jina la Juli ambaye walitengana na hawana mawasilino mazuri.
Mama huyo alisema alimpeleka mtoto wake shuleni lakini kila akifika harudi nyumbani na kutorokea anakokujua na kuonekana baada ya wiki mbili au tatu.
Kufuatia hali hiyo amewaomba wasamaria wema na viongozi wa dini kumwombea mtoto wake ili arudi katika hali ya kawaida kwani anajua kuna mkono wa mtu wa karibu uliyemharibu mtoto wake

Thursday, September 11, 2014

Waislamu wacharuka Mahakama ya Kadhi ndani ya bunge la katiba

Na Mwandishi wetu,Dodoma
Baadhi ya wajumbe wa Bunge la Maalum la  Katiba ambao ni waumini wa dini ya Kiislamu, wametaka suala la mahakama ya kadhi iingizwe kwenye katiba mpya. 

Mvutano huo ulijitokeza jana wakati wakichangia mjadala wa rasimu ya katiba baada ya kamati 12 za bunge hilo kumaliza kuwasilisha taarifa za mapendekezo yao.

Mmoja wa wajumbe hao, Shekh Hamid Jongo, aliitaka katiba itamke kwamba kutatungwa sheria ambayo  itaeleza kwamba masuala ya ndoa, mirathi na talaka  yataamuliwa kwa mujibu wa imani ya dini ya  kiislamu.

 Alisema katika sura ya 10 ibara ya 150 (3) ya rasimu ya mabadiliko ya katiba inaleza kwamba mahakama ndio chombo cha mwisho cha kutoa haki na katika dini ya kiislamu mambo ya ndoa, mirathi, wakfu na talaka  yanaamuliwa kidini, hivyo utoaji haki kwa mambo hayo ni ibada.

 Aidha alisema kutambulika kwa mahakama ya kadhi kisheria hakuzuii watu wa madhehebu mengine na wao kudai mambo wanayoyataka kuwemo katika katiba.

“Waislamu mambo ya mirathi, talaka, ndoa ni ibada yetu  na kamba yanakataliwa kuamuliwa katika mahakama ya kadhi,” alisema.


Naye mjumbe mwingine,Dk. Zainab Gama, alisema umefika wakati sasa kilio cha Waisalamu cha kutaka mahakama ya Kadhi kutambulika kisheria  kisikilizwe ili kunusuru amani iliyopo.

“Chonde chonde nchi yetu hii ina amani tusiruhusu watu kutumia udhaifu ulipo kuvunja sheria, pamoja na kwamba Waislamu wameruhusiwa kuanzisha mahakama za  kadhi lakini mahakama hizi hazitambuliki kisheria,”alisema.
Alisema mambo yanayoamuliwa na mahakama za kadhi yanapofikishwa katikamahakama za kawaida hutupiliwa mbali.

Kwa upande wake, Shamimu Khan, yeye alitaka kujua kigugumizi kiko wapi kutokana na kushindwa kuingiza mahakama ya kadhi katika katiba na  sheria za nchi.

Alisema kilichopo sasa Waislamu wanapigwa danadana kwamba suala la  mahakama ya kadhi litawekwa kwenye sheria na kusema jambo hilo  haliwezekani kama limeshindwa kutambulika katika sheria mama ambayo ni  katiba.

Mbwana Salum Mbanda yeye alitaka mahakama ya kadhi itambuliwe kikatiba na Serikali igharamie katika uendeshaji wake.

Mjumbe mwingine, Hamisi Ally Togwa, alisema pamoja na ibara ya 32  ya katiba kueleza uwepo wa uhuru wa imani ya kuabudu dini yoyote  lakini Waislamu wamekuwa wakiikosa haki hiyo kwa muda mrefu.

Baada ya kuchangia, suala hilo liliibua mvutano ambapo baadhi ya wajumbe walipinga mahakama hiyo kutambulika kikatiba akiwemo Ave Maria Semakafu na Jasson Rweikiza.

Rweikiza alisema ni makosa kwa Katiba kuzungumzia mahakama ya kadhi wakati serikali haina dini.

Suala jingine lililoibuka ni uraia pacha  ambapo baadhi ya wajumbe walipendekeza uraia pacha uruhusiwe kikatiba.

Aliyekuwa wa kwanza kuunga mkono uraia pacha  ni Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Zakia Meghji ambaye alisema Watanzania wenye uraia wa nchi za nje, walilazimika kufanya hivyo kutokana na sababu mbalimbali.


Mapendekezo hayo ya Meghji yaliungwa mkono na mjumbe mwingine ambaye ni Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu (CCM), aliesema suala la uraia pacha halipaswi kupigwa vita kwa kuwa ni jambo la kawaida duniani na kwamba Watanzania wenye uraia wa nchi za nje, walifanya hivyo kutokana na sababu  mbalimbali.

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA MTAMBO WA 10,000 WA BIOGAS KITAI

IMG_1607Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa CARMATEC Ndugu Elifariji Makongoro mara baada ya kuwasili kwenye Kijiji cha Kondo kilichoko katika kata ya Zinga wilayani Bagamoyo kushiriki katika siku ya kitaifa ya biogas iliyofanyika kijijini hapo na Mama Salma akiwa mgeni rasmi tarehe 10.9.2014.

IMG_1625Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitembelea maonesho ya biogas yaliyofanyika katika Kijiji cha Kondo tarehe 10.9.2014. Mkurugenzi Mkuu wa CARMATEC  Ndugu Elifariji Makongoro (kulia) akimpatia maelezo mbalimbali ya kazi zinazofanywa na shirika hilo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Mwantumu Mahiza.
IMG_1631Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Kijijini Kondo kwenye sherehe za kilele cha siku ya biogas kitaifa.
IMG_1648 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe huku akishirikiana na viongozi mbalimbali ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa mtambo wa wa 10,000 wa Biogas hapa nchini. Mtambo huo unaomilikiwa na Ndugu Bakari Seif na Mkewe Mwanaidi Said (wa pili na wa tatu kutoka kushoto). Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndugu Eliakim Maswi, kulia kwa Mama Salma ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Ndugu Mwantumu Mahizana. Aliyesimama kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kondo Ndugu Ramadhan Seleman akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa CARMATEC Ndugu Elifariji Makomgoro.
IMG_1660Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa CARMATEC  Ndugu Elifariji Makongoro kuhusu ujenzi wa mtambo huo na unavyofanya kazi.
IMG_1747Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akizungumza na wageni waalikwa na mamia ya wananchi waqliohudhuria sherehe ya siku ya biogas kitaifa iliyofanyika katika Kijiji cha Kondo huko Bagamoyo tarehe 10.9.2014.

Tuesday, September 9, 2014

DENTI AWATISHIO KWA UTAPELI KWA WAKAZI WA JIJI LA DAR

Nyuma ya tukio la denti wa darasa la tano kwenye shule moja ya msingi iliyopo Mbezi-Shamba, Dar, aliyejitambulisha kwa jina moja la Irene (11) la kunaswa akifanya utapeli kwa kuwaibia raia, mazito yameibuka.
Denti wa darasa la tano anayetambulika kwa jina moja la Irene (11) aliyenaswa akiwatapeli raia.
Katika tukio hilo lililojiri hivi karibuni maeneo ya Posta Mpya, Dar, denti huyo alikuwa akisimama nyakati za asubuhi akivalia sare za shule huku akiombaomba kwa madai kuwa hana nauli ya kuvukia katika kivuko cha Kigamboni kwenda shule anayosoma.
Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda, mtoto huyo alikuwa akisimama mbele  ya Kituo cha Daladala cha Posta mpya akijifanya ombaomba kwa madai kwamba hana  nauli.Ilisemekana kwamba siku nyingine mtoto huyo alikuwa akionekana akiuza simu kwa bei chee na alipohojiwa alikokuwa akizitoa alidai ameziokota.
Mwandishi wa Global na Global TV Online, Gabriel Ng'osha (kushoto) akipata undani wa habari katika tukio hilo. 
Dereva mmoja, Juma Hamis anayeegesha gari lake eneo hilo (Posta Mpya) alisema kuwa tabia ya mtoto huyo ilikuwa ni ya muda mrefu kwani alianzia Kariakoo, Dar akitapeli na kuiba madukani ambapo watu walimstukia hivyo akaamua kuhamia Posta.
“Mara kadhaa amenusurika kupigwa akidaiwa kuchomoa simu za watu kwenye mikoba ndani ya daladala.“Kukamatwa kwa Irene, watu wa maofisini na kwenye daladala wameshukuru kwani anafahamika na ni tishio kwa utapeli na ndiyo waliomchoma kwa polisi akadakwa baada ya kukutwa akijidai ni ombaomba,” alisema dereva huyo.
Ofisa wa Polisi kutoka 'Central Police' Posta akifafanua jambo kuhusiana na mkasa huo.
Jader Sapi, anayefanya kazi katika ofisi moja zilizo ndani ya jengo la IPS, alisema mtoto huyo aliwahi kuingia ofisini kwao na alipotoka, wafanyakazi wawili walilalamika kupotea kwa simu zao, kitu kilichowafanya wajue ni yeye.
Mama mmoja aliyeshuhudia Irene akichukuliwa na askari, alisema ameshawahi kumpa fedha mara kadhaa denti huyo, akiamini alivyomweleza kuwa hakuna na wazazi na hivyo hana nauli ya kumpeleka shuleni.
Akizungumza na gazeti hili akiwa mikononi mwa polisi kwenye Kituo Kikuu, Irene alisema ni mwanafunzi wa shule moja ya msingi (jina kapuni) iliyopo Mbezi-Shamba na siyo kama alivyokuwa akidanganya kuwa anasoma Kigamboni, Dar.
Wananchi wakishuhudia laivu tukio hilo lililotokea maeneo ya Posta mpya, Dar es Salaam.
Pia alikiri kwamba amekuwa akidanganya kuwa hana wazazi wakati ukweli ni kwamba wazazi wake wapo.“Ni shetani tu aliniingia nikawadanganya raia,’’ alisema Irene.
Baada ya kushuhudia tukio hilo, wanahabari wetu walimsaka mkuu wa shule anayosoma mtoto huyo, Yusuph Zenny ambaye alikiri kumfahamu Irene na kudai kuwa tayari taarifa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi, Dar zilimfikia.
Alitobosa siri kuwa ameshapata malalamiko mara kadhaa kuhusiana na binti huyo na kwamba amekuwa akifanya uchunguzi ili kupata ukweli.
Hata hivyo, alisema anawasiliana na wazazi ili kulifuatilia sakata hilo hivyo kuwaomba wanahabari wetu wampe muda atatoa majibu au hatua itakayochukuliwa huku Irene akiwa bado mikononi mwa polisi kwenye dawati la jinsia
CREDIT:GPL

Friday, September 5, 2014

AJALI MBAYA YA BASI YASABABISHWA FIESTA KUAHIRISHWA MKOANI MARA...PICHA ZAID HAPA

http://photos-d.ak.instagram.com/hphotos-ak-xaf1/10693452_1502229216688067_890487850_n.jpg
http://photos-b.ak.instagram.com/hphotos-ak-xfa1/10666127_892770504085025_689598648_n.jpg
HABARI ZAIDI ZITAWAJIA HAPAHAPA

Tuesday, September 2, 2014

HATARIII:MAMA MCHUNGAJI AJIFUNGUA HIRIZI!

NI maajabu ya dunia! Mke wa Mchungaji wa Kanisa la EAGT ‘Bonde la Baraka’ lililopo Kata ya Kerege Manofu, Bagamoyo mkoani Pwani, Boniface Onesmo Mahera (38) (pichani), Bentha Seth (27) baada ya kubeba mimba kwa miezi tisa  hatimaye amejifungua hirizi, gazeti la kijamii, Uwazi lina mkasa wote.
Mke wa Mchungaji wa Kanisa la EAGT ‘Bonde la Baraka’,  Bentha Seth aliyejifungua hirizi.
Akizungumza na waandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake, mchungaji huyo alisema mbali na mkewe kujifungua hirizi, pia alitoa mawe mawili, mkaa usiotumika na kitambaa chekundu chenye ukumbwa wa ‘hendkachifu’.
NI MIMBA YA TATU KUTOKA KIMAAJABU
Akisimulia mkasa huo, mchungaji huyo alisema kuwa, awali mkewe alikuwa akipata ujauzito lakini ukifikisha miezi mitatu hutoka.“Tangu mwaka 2009 zimeshatoka mimba tatu kimaajabu. Alikuwa akishika ujauzito, ukifikisha miezi mitatu  unatoka akienda kujisaidia, hali ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba tulikuwa tunafanya maombi kila mara na wakati huo wote mimi nilikuwa bado sijasimikwa kuwa mchungaji,” alisema mchungaji huyo.

Hirizi, mawe mawili, mkaa na kitambaa chekundu vinavyo daiwa kutoka tumboni mwa Bentha Seth .
UJAUZITO TAYARI
Akisimulia kilichotokea siku ya tukio, mchungaji huyo alisema mimba hiyo iliyozaa ‘mtoto hirizi’ iliingia Desemba mwaka jana na tangu ilipokuwa na mwezi mmoja walikuwa wakienda kliniki kupima.
“Ikiwa na mwezi mmoja tulikwenda kliniki kupima. Vipimo vilikuwa vikitoa majibu tofauti, mara hana mimba, mara mimba imetunga nje ya mfuko wa uzazi au kugoma kabisa kutoa majibu yoyote. Kwa kweli mke wangu amepitia majaribu mengi.

AOMBA NA KUFUNGA SIKU KUMI
“Basi, tukawa tunaendelea hivyohivyo huku tukiomba na kufunga kwa siku kumi kwa maombi maalum kwa mke wangu na wanawake wengine waliokuwa hawashiki ujauzito. Hatimaye tukamaliza na kusubiria mtoto atakayezaliwa,” alisema mtumishi huyo wa Mungu.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT ‘Bonde la Baraka’, Boniface Onesmo Mahera (38).
MAAJABU YAANZA
Baba mchungaji akaendelea kusema kuwa, mimba ilipofikisha miezi sita, mkewe akaanza kupata mauzauza, alianza kutokwa na haja ndogo kila wakati kama vile kuna mtu alikuwa akimmwagia maji.
“Kama hilo halitoshi kila ilipofika saa nane mchana alikuwa akichapwa viboko na mtu asiyemwona jambo lililowapa wakati mgumu zaidi.

AUZA NYUMBA, VIWANJA KUMTIBU MKEWE
Mchungaji huyo alisema baada ya kuyaona hayo aliamua kuuza mashamba na viwanja alivyokuwa navyo sanjari na nyumba aliyojenga Kigoma ili akamtibie mkewe kwa kuamini kuwa  alikuwa akisumbuliwa na Ugonjwa wa Fistula.

Mchungaji akiwa amezungukwa na majirani walioshudia mkasa huo.
Alisema alimpeleka Hospitali ya Comprehensive Community Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT), Msasani jijini Dar ambapo vipimo vilionesha hakuwa na ugonjwa wowote, wakarudi nyumbani na kuendelea na maombi.“Nimeishapoteza karibu shilingi milioni nane kwa ajili kumtibia mke wangu na sasa hivi sina fedha tena na matatizo bado yanaendelea kuikumba ndoa yangu kila kukicha, nina imani shetani aliyeikumba nyumba yangu ataiachia kwa uwezo wa damu ya Yesu,” alisema.
SIKU YA TUKIO, SAUTI YA CHURA KWANZA
Hatimaye siku za mama mchungaji kujifungua ziliwadia, Agosti 19, mwaka huu asubuhi, mwanamke huyo alianza kwa kusikia sauti ya chura ikitokea tumboni ndipo saa tatu usiku alishikwa na uchungu huku mumewe akiwa na shilingi 1,500 tu mfukoni pesa ambayo haikuwa ikitosha hata usafiri wa kwenda hospitali.
Cheti cha ndoa baina ya Bentha Seth na mchungaji huyo.
“Nilifanya maombi mazito na kumtayarishia mkewe wangu sehemu ambayo atajifungulia hapahapa nyumbani, cha ajabu muda wa kujifungua nikashangaa kumwona anatoa haja ndogo kama ujazo wa lita kumi. Nikiwa naendelea kufanya maombi tumbo lilijaa na kupungua, ilibidi nimfunge kitambaa na mpira wa tairi la baiskeli ili tumbo lipungue.
“Kwa hatua aliyokuwa amefikia mke wangu  nilijua anaaga dunia kwa sababu niliisha kinga ndoo nne zilizokuwa zimejaa haja ndogo na hakukuwa na hata tone moja la damu.
“Ilipotimu saa sita usiku mke wangu akaanza kulalamika huku akisema anakufa, mara nikaona kitu kimechomoza, akasema nisaidie basi, nilipochungulia nikaona uzi, nikapeleka mkono kuuvuta, ikawa kama tunavutana lakini nilifanikiwa kuvuta ndiyo nikatoa hirizi lakini sikumwambia nilichokiona na muda huohuo yeye alipoteza fahamu.

“Kwa sababu ilikuwa kitu cha ajabu sana kwangu, nilitoka kwenda kuwaita majirani zangu ili waje washuhudie kilichotokea kwa mke wangu. Walikuja na kumkuta bado amepoteza fahamu.
“Alipokuja kuzinduka alianza kunidai mtoto ikabidi nimwambie ukweli mbele ya majirani. Niliichukua ile hirizi nikaifungua nikakuta ndani kuna kitambaa chekundu, mawe, mkaa na manyoya, nikaviombea na kuvichoma moto.

“Haya yote naona ni majaribu ya shetani tu na ninasema hili ni jaribu lake la mwisho haitatokea tena na kama ikitokea basi nitamteketeza huyo shetani kwa maombi,” alisema mchungaji huyo.
MAMA MCHUNGAJI SASA
Kwa upande wake, mama mchungaji huyo alisema anamshukuru Mungu kwa majaribu yote aliyopitia na kuamini ni sehemu ya maisha lakini kubwa ni uzima alionao mpaka sasa