STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' alizaliwa Octoba 2, 1989. Sherehe ya bethidei yake ilifanyika ukumbi wa Golden Jubilee usiku wa kuamkia leo na kuhudhuriwa na mastaa miongoni mwao ni T.I.D, Chidi Benz, Profesa Jay, B12, Elizabeth michael 'Lulu', Ommy Dimpoz na wengine
Showing posts with label wema. Show all posts
Showing posts with label wema. Show all posts
Friday, October 3, 2014
SHEREHE YA BETHIDEI YA DIAMOND PLATINUMZ GOLDEN JUBILEE, DAR
Thursday, October 2, 2014
KAJALA AAMUA KUJIBU MAPIGO MATUSI YAMPONZA MAMA WEMA SEPETU

Habari ya mjini kwa sasa ni bethidei ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutimiza miaka 26 tangu kuzaliwa, lakini ndani ya tukio hilo, mengine yameibuka!
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Kajala Masanja. Miongoni mwa yaliyoibuka kwenye sherehe hiyo iliyofanyika Jumapili iliyopita nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ni madai ya mama Wema, Mariam Sepetu kudaiwa kupewa nafasi ya kutoa ‘neno la hekima’ lakini akaitumia kumvurumishia mitusi aliyekuwa shosti wa Wema, Kajala Masanja.
Baada ya sherehe hiyo, Jumatatu na Jumanne, mitandao mingi ya kijamii ilitumbukiza video yenye sauti ikimuonesha mama Wema akimrushia matusi Kajala kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na kukorofishana kwa mwanaye na Kajala aliyewahi kumfadhili mahakamani kwa kumlipia faini ya shilingi milioni 13 asiende jela kwa kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa na zuio la kisheria.
Katika kufuatilia sakata hilo, Amani lilinyetishiwa kwamba Kajala baada ya kushindwa kuvumilia, ameamua kumshitaki mahakamani mama Wema. Chanzo chetu kinadai kuwa Kajala alifikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na familia sanjari na wafuasi wake (Timu Kajala) ambapo sasa, timu hiyo na Timu Wema wameingia vitani tena.BOFYA KUSOMA ZAIDI>>
“Kajala ameshawasiliana na wanasheria wawili na kutoa maelezo yake, wao wanaandaa faili ili mashitaka yafike mahakamani, amekasirika sana.“Amesema mama Wema ametumia nafasi ya kukutana na watu kumdhalilisha bila kumpa nafasi ya kujitetea, ameona si sawa hata kidogo,” kilisema chanzo hicho ambacho ni jirani na Kajala.
Katika sauti, mama Wema anasikika akitamka matusi (hayaandikiki gazetini) huku Wema naye anasikika akimsihi mama yake asimtaje jina Kajala kwa kuwa kufanya hivyo ni kumpaisha. Hapa inamaanisha kwamba, Wema alitaka mama yake afunguke lakini bila kutamka jina la mtu.
AGUNDUA TIMU KAJALA IMO NDANI YA BETHIDEI
Katika hatua nyingine, mama Wema alisema kauli iliyoashiria kwamba Timu Kajala ilikuwemo ndani ya bethidei ya mwanaye. “Nasema haya huku najua humu ndani kuna Timu Kajala, lakini nasema….(matusi mazito)”
KAJALA SASA
Baada ya madai hayo yote, juzi, Amani lilimsaka Kajala kwa njia ya simu ili kumuuliza ukweli wa madai hayo. Licha ya kutopokea simu ya paparazi wetu, alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno ‘SMS’ na kuulizwa kila kitu.
Hata hivyo, badala ya kujibu alikaa kimya, baada ya dakika kama kumi na tano alimrushia kwa simu mwandishi wetu video hiyo ambayo anadai kutukanwa na mama Wema bila kusema chochote hali iliyotafsiriwa kuwa kama alisema; ‘hebu oneni wenyewe jamani, nimemkosea nini mama Wema?’
Katika hatua nyingine siku hiyo, meneja wa Wema, Martin Kadinda alikuwa na kazi ya ziada kuhakikisha, mama Wema na mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ hawakai jirani au meza moja licha ya kwamba watoto wao wamependana.
“Kadinda ana kazi ngumu sana, unajua anatakiwa kuhakikisha kwamba mama Wema na mama Diamond hawakai meza moja. Sijui anaogopa nini, kwani hawa si watu ambao watoto wao wana mpango wa kuoana?” alihoji mwalikwa mmoja.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Katika bethidei hiyo, Wema alizawadiwa magari mawili, Nissan Murano lenye thamani ya shilingi milioni 36 alilopewa na Diamond na BMW 545i lenye thamani ya shilingi milioni 56, inadaiwa alizawadiwa na Kadinda
Thursday, September 4, 2014
AUDIO:Wema Sepetu Ajibu Kuhusu Kuajiriwa Na Kajala, Na Meninah Kutoka Na Diamond.
Baada ya mitandao na gazeti moja siku chache zilizopita kutoka na
habari kuwa kajala kwasasa ana utajiri mkubwa kuliko Wema Sepetu kiasi
cha kuweza kumwajiri Wema anayedaiwa kuwa na pesa za mawazo sasa baada
ya kuchezea pesa kipindi cha nyuma. leo Wema kapatikana na kakubali
kuongelea isue hizo zote ikiwemo hiyo ya Kajala.
Kupitia You heard ya XXL ya Clouds Fm Soudy Brown alianza kwa kutaka kufahamu kama kweli Kajala anaweza kumuajiri yeye [Wema]. Wema Sepetu akamjibu "Inawezekana,kila kitu kinawezekana Soudy"
Kuhusu mshahara ambao anataka kulipwa na Kajala,Wema Sepetu amejibu "Kwa Kajala mi sihitaji mshahara hata bure nitafanya kazi kwa Kajala,shughuli yoyote nitafanya Soudy"
Soudy Brown alipomuuliza kuhusu fununu za Meninah kutoka na Diamond,Wema amejibu "Mimi sijui Soudy bwana na wala sijali"
Monday, September 1, 2014
HII NDIO SABABU YA KAJALA KUMWAJIRI WEMA KATIKA KAMPUNI YAKE
AMA kweli fedha mwanaharamu! Kama bado ulikuwa
ukiamini kwamba Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu anayependelea
kuitwa Madam ana mtonyo (fedha) kumzidi aliyekuwa shosti wake, mwigizaji
Kajala Masanja ‘Kay’, umekosea sana kwani upepo umegeuka, ungana na
Ijumaa Wikienda.
Habari za ‘ufukunyuku’ zinadai kwamba, kwa utajiri alionao kwa sasa, Kajala anaweza kudiriki kumwajiri Wema kama kisemavyo chanzo.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na wote kwa maana ya kutafuna pande zote, mwigizaji huyo ambaye enzi za ushosti wake na Wema alikuwa akionekana kama kijakazi, sasa fedha imemtembelea kiasi cha kutosha wakati mwenzake kwa bahati mbaya eti ‘anatembelea ringi’.
Chanzo kilisema kwamba Kajala kwa sasa ana maisha ya ‘kitonga’, amepanga kwenye nyumba nzuri ya ghorofa, ana kampuni yake ya filamu (KAY Entertainment), magari manne, anatembea na wapambe (walinzi) huku akaunti yake benki ikiwa imetuna.
“Kajala ameonesha jeuri ya fedha. Ametoka katika nyumba ya kawaida sasa analala angani. Kwa taarifa yenu amepanga ghorofa nzima maeneo ya Sinza-Madukani jijini Dar.
“Yupo vizuri, anamiliki ofisi kubwa ya kuzalisha sinema, magari mawili ya ofisi pamoja na magari mawili ya kutembelea (Brevis na Harrier) na anaishi katika nyumba anayolipa kodi kwa mwezi dola 2,000 (zaidi ya Sh. milioni 3.2),” kilidai chanzo hicho na kudai kwamba si mbaya Kajala akamkumbuka mwenzake hata kwa kumwajiri kwenye kampuni yake.
KAJALA AMEHONGWA?
Akizungumza na waandishi wetu, Kajala alisema anamshukuru Mungu kwani fedha hizo amezizalisha kupitia kazi zake pamoja na biashara mbalimbali alizokuwa akizifanya, hajahongwa na mtu yeyote.
“Sijahongwa na mtu yeyote, kila mtu ana akili zake katika kutafuta fedha, nafanya biashara huku nikiigiza sinema zangu na Mungu amenijalia mambo yanakwenda vizuri,” alisema Kajala.
Kuhusu kumwajiri staa mwezake huyo, Kajala hakutaka kulizungumzia hilo.
Kama hiyo haitoshi, ilidaiwa kuwa hata akaunti benki haijanona na hata wapambe wa kutembea naye wameyeyuka.
WEMA ATAFUTWA
Ili kutaka kujua anazungumziaje ‘challenge’ hiyo ya kudaiwa kuporomoka kiuchumi, wanahabari wetu walimtafuta Wema kwa siku tatu mfululizo lakini hakupatikana huku simu yake ikiita muda mrefu bila kupokelewa.
SHOSTI WAKE
Akizungumza na waandishi wetu kwa sharti la kutoanika jina gazetini, rafiki wa karibu wa Wema alikiri kuwa staa huyo mwenye nyota isiyochuja, ameshuka kiuchumi tofauti na enzi zile ambazo walikuwa wakitanua katika viunga mbalimbali na msururu wa watu huku Madam akisimamia shoo nzima ya malipo.
“Madam kwa sasa ameshuka kiuchumi kwani hatutanui mjini kama ilivyokuwa zamani, yaani naamini anaweza kuajiriwa na Kajala ambaye wakati ule alikuwa chini kwake,” alisema rafiki huyo.
KUMBUKUMBU YA JUZIKATI
Hivi karibuni, baadhi ya mashabiki wa Wema ambao wanajiita Team Wema, walimuonya staa wao huyo wakidai ananyonywa na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye pia amekuwa akimdhalilisha katika majukwaa pindi anapofanya shoo zake.
Walimtaka abadilike kwani yeye ndiye mwenye nyota ya kung’aa lakini Diamond ananufaika yeye peke yake na muziki wake.
DIAMOND ALINENA
Baada ya Diamond kushambuliwa na Team Wema, naye alitoa majibu ambayo yalionesha dhahiri kwamba ndiyo sababu inayomfanya Wema ashuke kisanaa na kiuchumi.
“Kama kweli mnampenda huyo msanii wenu (Wema) basi mngemshauri kwanza akaacha kufanya starehe kuliko kuelekeza lawama kwangu, mimi kama mume, jukumu langu ni kuhakikisha namwezesha kuanzisha biashara lakini jukumu la kuendeleza ni la kwake, mnataka hata kuigiza nikamuigizie?,” alihoji Diamond mtandaon
Habari za ‘ufukunyuku’ zinadai kwamba, kwa utajiri alionao kwa sasa, Kajala anaweza kudiriki kumwajiri Wema kama kisemavyo chanzo.
Mwigizaji wa filamu Bongo, Kajala Masanja ‘Kay’.
TUJIUNGE NA CHANZOKwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na wote kwa maana ya kutafuna pande zote, mwigizaji huyo ambaye enzi za ushosti wake na Wema alikuwa akionekana kama kijakazi, sasa fedha imemtembelea kiasi cha kutosha wakati mwenzake kwa bahati mbaya eti ‘anatembelea ringi’.
Chanzo kilisema kwamba Kajala kwa sasa ana maisha ya ‘kitonga’, amepanga kwenye nyumba nzuri ya ghorofa, ana kampuni yake ya filamu (KAY Entertainment), magari manne, anatembea na wapambe (walinzi) huku akaunti yake benki ikiwa imetuna.
“Kajala ameonesha jeuri ya fedha. Ametoka katika nyumba ya kawaida sasa analala angani. Kwa taarifa yenu amepanga ghorofa nzima maeneo ya Sinza-Madukani jijini Dar.
“Yupo vizuri, anamiliki ofisi kubwa ya kuzalisha sinema, magari mawili ya ofisi pamoja na magari mawili ya kutembelea (Brevis na Harrier) na anaishi katika nyumba anayolipa kodi kwa mwezi dola 2,000 (zaidi ya Sh. milioni 3.2),” kilidai chanzo hicho na kudai kwamba si mbaya Kajala akamkumbuka mwenzake hata kwa kumwajiri kwenye kampuni yake.
KAJALA AMEHONGWA?
Akizungumza na waandishi wetu, Kajala alisema anamshukuru Mungu kwani fedha hizo amezizalisha kupitia kazi zake pamoja na biashara mbalimbali alizokuwa akizifanya, hajahongwa na mtu yeyote.
“Sijahongwa na mtu yeyote, kila mtu ana akili zake katika kutafuta fedha, nafanya biashara huku nikiigiza sinema zangu na Mungu amenijalia mambo yanakwenda vizuri,” alisema Kajala.
Kuhusu kumwajiri staa mwezake huyo, Kajala hakutaka kulizungumzia hilo.
WEMA HALI IPOJE?
Utafiti uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba Wema aliyemlipia Kajala Sh. milioni 13 asiende jela mwaka jana, ambaye kipindi kifupi kilichopita alikuwa na kampuni ya kuzalisha sinema, wapambe, akaunti iliyonona benki, magari ya kifahari ya kutembelea na samani nyingine, nyingi zimepotea kama si kuyeyuka kabisa.
Utafiti umeonesha Wema ambaye alikuwa akimiliki magari kadhaa
likiwemo la kufanyia kazi za sinema, kwa sasa amebakiwa na gari moja tu
ambalo ni Toyota Harrier. Utafiti uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba Wema aliyemlipia Kajala Sh. milioni 13 asiende jela mwaka jana, ambaye kipindi kifupi kilichopita alikuwa na kampuni ya kuzalisha sinema, wapambe, akaunti iliyonona benki, magari ya kifahari ya kutembelea na samani nyingine, nyingi zimepotea kama si kuyeyuka kabisa.
Kama hiyo haitoshi, ilidaiwa kuwa hata akaunti benki haijanona na hata wapambe wa kutembea naye wameyeyuka.
WEMA ATAFUTWA
Ili kutaka kujua anazungumziaje ‘challenge’ hiyo ya kudaiwa kuporomoka kiuchumi, wanahabari wetu walimtafuta Wema kwa siku tatu mfululizo lakini hakupatikana huku simu yake ikiita muda mrefu bila kupokelewa.
SHOSTI WAKE
Akizungumza na waandishi wetu kwa sharti la kutoanika jina gazetini, rafiki wa karibu wa Wema alikiri kuwa staa huyo mwenye nyota isiyochuja, ameshuka kiuchumi tofauti na enzi zile ambazo walikuwa wakitanua katika viunga mbalimbali na msururu wa watu huku Madam akisimamia shoo nzima ya malipo.
“Madam kwa sasa ameshuka kiuchumi kwani hatutanui mjini kama ilivyokuwa zamani, yaani naamini anaweza kuajiriwa na Kajala ambaye wakati ule alikuwa chini kwake,” alisema rafiki huyo.
KUMBUKUMBU YA JUZIKATI
Hivi karibuni, baadhi ya mashabiki wa Wema ambao wanajiita Team Wema, walimuonya staa wao huyo wakidai ananyonywa na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye pia amekuwa akimdhalilisha katika majukwaa pindi anapofanya shoo zake.
Walimtaka abadilike kwani yeye ndiye mwenye nyota ya kung’aa lakini Diamond ananufaika yeye peke yake na muziki wake.
DIAMOND ALINENA
Baada ya Diamond kushambuliwa na Team Wema, naye alitoa majibu ambayo yalionesha dhahiri kwamba ndiyo sababu inayomfanya Wema ashuke kisanaa na kiuchumi.
“Kama kweli mnampenda huyo msanii wenu (Wema) basi mngemshauri kwanza akaacha kufanya starehe kuliko kuelekeza lawama kwangu, mimi kama mume, jukumu langu ni kuhakikisha namwezesha kuanzisha biashara lakini jukumu la kuendeleza ni la kwake, mnataka hata kuigiza nikamuigizie?,” alihoji Diamond mtandaon
Friday, August 29, 2014
SHEMEJI WA WEMA ATANGAZA NDOA NA DADA WA DIAMOND
MAPENZI bwana! Baada ya
kuogelea kwa muda mrefu katika penzi la muigizaji Kajala Masanja,
hatimaye shemeji wa aliyekuwa rafiki wa mwigizaji huyo, Wema Sepetu,
Ahmed Hashimu ‘Petit Man’ ametangaza ndoa na dada wa Mbongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Abdul.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilicho karibu na Diamond na Wema
ambao penzi lao lilipata ‘mushkeli’ kidogo hivi karibuni, Petit Man
tayari ameshakamilisha kila kitu kinachotakiwa kufanyika kabla ya ndoa
na kilichobaki ni kutamka siku husika tu.
Kilidai kuwa, Petit alichukua uamuzi huo
baada ya kushauriwa na Wema kuwa umri unakwenda na vishawishi ni vingi
hivyo ni bora aoe mapema.“Unajua Petit Man anamheshimu sana Wema kwa
hiyo alipomwambia Petit kuwa umri unazidi kwenda na anahitaji kuwa na
familia yake akaukubali ushauri wake,” kilinyetisha chanzo hicho.
Baada ya kupata maelezo hayo, Ijumaa lilimtafuta Petit Man na
kumuuliza kuhusiana na ishu hiyo, bila kuumauma maneno alikiri.“Ni kweli
mama (Wema) aliniweka chini na kuniambia kuwa umri unakwenda hivyo
nahitaji niwe na familia yangu kwa hiyo siwezi kuwa na familia bila ya
kuwa na mke ndipo aliponichagulia mke ambaye ni dada yake wa damu kabisa
na Nasibu Abdul ‘Diamond’ anayeitwa Esma na kwa taarifa yako tu, tayari
nimeshakamilisha kila kitu,” alisema Petit.Alipoulizwa kuhusiana na wanawake aliowahi kuwa nao kipindi cha nyuma akiwemo Kajala, Petit alisema huko kote ilikuwa ni njia ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio ambayo ni ndoa yake na Esma.
“Acha nipumzike na madhira ya dunia maana huko kote nilipopita hakukuwa chaguo langu ila kwa Esma nimekufa nimeoza bado kuzikwa tu yaani mimi ni mfu ninayetembea mbele ya Esma.
Saturday, August 23, 2014
EXCLUSIVE:Diamond Platnumz Atangaza Kumuoa Wema Sepetu, Ndoa Kuhudhuriwa Na Mashabiki Uwanja Wa Taifa
“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond.

Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.
“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.
“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.”
Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa. Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa.
Sunday, August 17, 2014
#TEAMDIAMONDTZ YAMPA MAKAVU WEMA..SOMA HAPA UJIONEE UONDO...

Wednesday, August 13, 2014
EXCLUSIVE:ALIYEKUWA KOCHA WA SIMBA ATOKA NA WEMA KIMAPENZ PATA STORY KAMILI HAPA
MALOVEE? Mzungu
aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Zdravko Logarusic ‘Loga’
anadaiwa kuingilia penzi la mwigizaji Wema Sepetu.
Ishu hiyo imebumburuka ikiwa ni siku chache tangu Diamond atangaze kuwa hayupo tayari kuoa akidai atashuka kimuziki.
Ishu hiyo imebumburuka ikiwa ni siku chache tangu Diamond atangaze kuwa hayupo tayari kuoa akidai atashuka kimuziki.
KUMBE ALIMZIMIA KITAMBO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Mcroatia huyo alimzimia Wema mara tu baada ya kutua nchini Desemba, mwaka jana na kumuona mlimbwende huyo ‘akishaini’ kupitia vyombo vya habari, akajiwekea nadhiri kwamba lazima ampate.

CHANZO CHATIRIRIKA
“Loga alimzimia kinoma Wema baada ya kumuona kwenye vyombo vya habari na kuanza kufuatilia baadhi ya filamu zake ambazo zilikuwa zilimkonga moyo kila alipozitazama.
“Baada ya kuvutiwa naye, mtu mzima (Loga) akaanza kutafuta mbinu za kumuimbisha Wema,” kilidai chanzo.

Chanzo
hicho kilidai kwamba baada ya kocha huyo kupata wazo la kumtongoza
Wema, alianza kumsaka katika viwanja ambavyo aliamini mrembo huyo
anatembelea ili aweze kufanikisha azma yake ya kuonja penzi la Beautiful
Onyinye.
Zdravko Logarusic ‘Loga'akiwa kazini.
AMSAKA NYUMBANI KWAKE
Ilisemekana kuwa mara kadhaa alishafanya jitihada za kumfuata Wema nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar lakini kila alipotia mguu, hakufanikiwa kuonana na mrembo huyo.
Hata hivyo, ilisemekana kwamba Loga hakukata tamaa kwani alionekana kudata kadiri siku zilivyozidi kuyoyoma.

“Jamaa
alipiga sana misele pale Kijitonyama lakini bahati mbaya, misele yake
haikuzaa matunda lakini kwa kuwa alikuwa na nia, hakukata tamaa,
aliendelea kumsaka katika viunga mbalimbali ambavyo aliamini Wema yupo,”
kilidai chanzo hicho.
ZALI LA MENTALI
Kikizidi kumwaga taarifa, chanzo hicho kilibainisha kuwa jitihada za Loga kukutana na Wema zilizaa matunda Aprili 22, mwaka huu maeneo ya Mwenge ambapo bila kutegemea, wawili hao walikutana kila mmoja alipokuwa katika mizunguko yake ya kikazi.

“Ilikuwa
kama zali tu siku hiyo, Wema alikuwa katika ofisi moja hivi ambayo
alikuwa akifanya shughuli zake za kikazi lakini wakati huohuo Loga naye
alitia timu katika ofisi hiyo kwa shughuli zake za kikazi ndipo
ilipokuwa golden chance,” kilizidi kudai chanzo hicho ambacho ni mtu wa
karibu wa Wema.
Mkali wa Bongo Fleva na Mpenzi wa Wema Sepetu, Abdul Naseeb, 'Diamond'.
NDOTO ZAANZA KUTIMIA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, mara baada ya wawili hao kukutana, pointi ya kwanza muhimu kwa Loga ilikuwa ni kubadilishana namba na mrembo huyo kisha kufanya naye mazungumzo ya kawaida kwa dakika kadhaa.

Ilisemekana
kwamba, siku hiyo Loga alionekana mwenye furaha kwani licha ya
kubadilishana namba za simu, ilielezwa kuwa walipata fursa ya kupiga
picha za pamoja na kutumiana kupitia simu zao hivyo ukaribu wao kuanza
kushamiri kuanzia hapo.
AANZA KUIMBISHA
Ilidaiwa kuwa kitendo cha kocha huyo kupata namba ya Wema ilikuwa bahati kama kuokota madafu kwenye miti ya miembe, haraka alianza kutuma maombi ya penzi pasipo kufunguka moja kwa moja kisha badaaye alifunguka kabisa.

“Alianza
kwa salamu, akawa anachombezachombeza na maneno ya mitego ambayo mtu
mzima ukitumiwa meseji kama hizo unajua kabisa kuna kitu mtu anakitaka
kutoka kwako.
“Alipoona Wema haelekei mtegoni, akaamua bora kufunguka laivu, akamtumia meseji zinazoeleza hisia kali ya mapenzi,” kilidai chanzo hicho.
“Alipoona Wema haelekei mtegoni, akaamua bora kufunguka laivu, akamtumia meseji zinazoeleza hisia kali ya mapenzi,” kilidai chanzo hicho.
USHAHIDI HADHARANI
Ili kuupata ukweli wa madai hayo, paparazi wa Risasi Jumatano alianza kuchimba undani wa sakata hilo ambapo kwa kutumia njia za ‘kiintelejensia’, alifanikiwa kunasa meseji (SMS) zilizotoka kwa Loga kwenda kwa Wema ambazo zilionesha dhahiri kwamba kocha huyo amedatishwa na staa huyo wa filamu na kuomba hifadhi ya kimalovee.

Meseji
hizo zilikuwa zikisisitiza kwamba Loga anamhitaji Wema lakini mtoto wa
kike alikuwa mzito kumkubalia mzungu huyo ambaye sasa amesitishiwa ajira
yake na uongozi wa Msimbazi, mwishoni mwa wiki iliyopita kutokana na
makosa mbalimbali.
WEMA ANASEMAJE
Ili kujiridhisha zaidi, paparazi wetu alimvutia waya Wema na kumuuliza kuhusiana na uhusiano wake na kocha huyo.
Ili kujiridhisha zaidi, paparazi wetu alimvutia waya Wema na kumuuliza kuhusiana na uhusiano wake na kocha huyo.
Paparazi: Tumesikia Loga anakuimbisha, vipi umemkubalia au vipi?
Wema: Mh! Nani kakwambia?
Paparazi: Nijibu swali langu maana hata ushahidi wa meseji alizokutumia akionesha anakuhitaji, tumeziona na tunazo.
Wema: Mh! Nani kakwambia?
Paparazi: Nijibu swali langu maana hata ushahidi wa meseji alizokutumia akionesha anakuhitaji, tumeziona na tunazo.
Wema: Kwani kuna tatizo akinihitaji? Si mwanaume, ana haki ya kupenda kama walivyo wengine lakini ishu ni kumkubalia.
Paparazi: Kwa hiyo wewe umemkubalia?
Wema: Aaaa wapi, sipo interested na wazungu hata kidogo by the way mimi nina baby wangu Diamond.
Paparazi: Kwa hiyo wewe umemkubalia?
Wema: Aaaa wapi, sipo interested na wazungu hata kidogo by the way mimi nina baby wangu Diamond.
MADAI MENGINE
Wakati huohuo, mtu wa karibu na kocha huyo amepenyeza madai kuwa Loga alipanga kumhamisha Wema na kwenda kuishi naye nje ya nchi lakini haikujulikana mara moja kwamba ni nchi gani achilia mbali kama ilikuwa ni ‘gia’ ya kumpata mwigizaji huyo.
Alipotafutwa Loga ili kuzungumzia madai hayo, hakupatikana mara mojaWakati huohuo, mtu wa karibu na kocha huyo amepenyeza madai kuwa Loga alipanga kumhamisha Wema na kwenda kuishi naye nje ya nchi lakini haikujulikana mara moja kwamba ni nchi gani achilia mbali kama ilikuwa ni ‘gia’ ya kumpata mwigizaji huyo.
Wednesday, July 9, 2014
Martin Kadinda:Nilimtamani sana Kimapenzi Wema Sepetu
Fashion designer wa Tanzania, Martin Kadinda amesema kabla hajawa manager wa Wema, awali aliwahi kumtamani kimapenzi Wema Sepetu, lakini alighairi baada ya kugundua ni mwanamke wa kudekadeka
Kadinda alitoa kauli hiyo wakati akizungumza naGlobalpublishers kuhusu masuala mbalimbali yanayomhusu msichana huyo ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.
Kuhusu maisha wanayoishi nyota hao wawili wapenzi, Kadinda alisema kwa jinsi wanavyoishi ni kama watu wanaoigiza, akitolea mfano wa kipindi walichorudiana wakiwa nchini China, ambako wenyewe walisema wanaigiza filamu wakati ndiyo kwanza walikuwa wanarejesha penzi lao lililovunjika mara ya kwanza.
Tuesday, July 8, 2014
Alichokisema WEMA siku ya birthday ya Mama DIAMOND PLATINUMZ
Mara kadhaa mama Wema Sepetu alikaririwa akisema hamkubali Diamond kuwa katika uhusiano na mwanae. Na kwa upande mwingine habari zilidai mama Diamond hamkubali Wema bali anamkubali VJ Penny.
Sasa basi jana ilikuwa ni birthday ya mama Diamond ambapo Wema ameweka picha katika mtandao mmoja wa kijamii akiwa amekumbatiana na mama Diamond kuonyesha kuwa hakuna ugomvi tena kati yao…..
Picha hizo ziliambatana na ujumbe huu:
“Today is this amazing woman’s birthday…naanzaje kutokumpenda na kumtakia kila lenye kheri mama’ngu kipenzi …Mungu akutangulie mummy….akuweke na azidi kukufungulia milango ya baraka mzaa chema wangu…..love you mama’ke”
Sunday, January 26, 2014
PICHA:BAADA YA KIGOGO WA WEMA KUAMUA KUMUACHA WEMA NA KUMNYANG'ANYA VITU VYOTE,SASA AMNASA RAFIKI YAKE WEMA KIMAPENZI
NOMA
sana! Baada ya kupigwa cha mbavu (kuachwa) na Beautiful Onyinye, Wema
Isaac Sepetu huku akimnyang’anya vitu vyote vya ofisini, yule kigogo wa
ikulu, Clement a.k.a CK, hivi sasa anadaiwa kutoka na shosti wa staa
huyo, Naima Shaa.
Naima Shaa.
Kwa
mujibu wa chanzo makini cha gazeti namba moja la burudani Bongo, Ijumaa
Wikienda, Naima anatamba na kuwapiga vijembe wasichana wa mjini kuwa
anatoka na CK mwenye mkwanja mrefu (bado fedha hazijaisha).Nakwambia hatunywi maji, mtoto kadata kabisa hadi ameamua kujichora ‘tatuu’ ya jina la Clement kwenye bega lake la kulia. Inahusu?” kilihoji chanzo chetu.
NI MTOTO WA MBUNGE
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa Naima ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shaa (CCM) hivi sasa anaonekana na mdogo wa CK huku wakiitana shemeji wa ukweli.
“Sasa hivi jamaa anajilia vyake mdogomdogo kwa mtoto Naima pale kati, naona ameamua kumalizia machungu ya Wema kwa Naima.
“Unaambiwa nyuma ya pazia stori ni kwamba anataka Wema aumie ndiyo maana ameamua kubanjuka na Naima huku akijua kabisa kuwa ni marafiki.
“Unajua kama mtu akikuumiza kimapenzi, ukitembea na rafiki yake naye anaumia vibaya mno. Kwani hukumbuki ilivyokuwa kwa Penny (Penniel Mungilwa) alipochukuliwa na Diamond (Nasibu Abdul)? Ilikuwa ni ili kumuumiza Wema na kweli walifanikiwa. Ndicho anachokifanya CK,” kilitiririka chanzo hicho.
WATU WAMEDATA
Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa Naima ambaye mara nyingi haoni soni kuonesha tatuu ya jina la Clement, amekuwa akijinadi kuwa yeye ndiye mrithi halali wa Wema na kwa sasa kigogo huyo haoni wala hasikii kwake.
Tatoo ya Clement mgongoni mwa Naima.
“Naima
naye amedata kabisa na sidhani kama anaogopa Wema kujua kama yeye ndiye
hasa anatembea na kigogo huyo kwa kipindi hiki,” kilisema chanzo hicho.UNATAKA KUMSIKIA NAIMA?
Baada ya kupata taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Naima ili kuthibitisha madai hayo ambapo alikiri kumfahamu CK lakini akadai watu wanamsingizia.
Alipoulizwa kuhusu tatuu aliyochora yenye jina la Clement, Naima alisema ameandika ‘Element’ na siyo ‘Clement’ (tazama picha, akili ya kuambiwa changanya na yako).
“Yeleuuuwi...jamani watu wananisingizia. Hii tatuu niliyochora nimandika jina Element na siyo Element (angalia maneno yanafafa! Moja alikuwa anamaanisha Clement),” alisema Naima na kukata simu.
WEMA ANAJUA CHOCHOTE?
Baada ya kuwasiliana na Wema kwa njia simu na kumuuliza kuhusiana na madai ya zilipendwa wake kulipiza kisasi kwa rafiki yake, Naima, alisema kuwa habari hizo ameshazisikia lakini anasikitika kwa kuwa kigogo huyo karuka majivu na kwenda kukanyaga moto.
Alisema kuwa ishu hiyo haimuumizi na zaidi sana anawaombea wawili hao maisha mema ya kimapenzi ilimradi moyo wake umeshatua kwa umpendaye.
“Moyo wangu ulishatulia kwa nimpendaye, nawatakia maisha mema,” alisema Wema.
NYUMA YA PAZIA
Uchunguzi wa gazeti ulibaini kuwa nyuma ya pazia la habari hii kuna mambo mengi ya namna CK na Naima walivyokutana.
“Ni Kinondoni pale Mwanamboka. Mke wa CK alikuwa na baa pale ambayo siku hizi imefungwa.
“Naima alikuwa ni mke wa mtoto wa Mwanamboka. Walikuwa wanakutana pale baa. Ndipo mambo yalikoanzia.
“Unajua hata Naima ameingia kwenye gogoro la kindoa na mumewe kwa muda mrefu. Kisa ni huyo CK. Ona sasa wote wamekosa ndoa. Sinema inaendelea,” kilimalizia chanzo chetu.