“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond.
Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.
“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.
“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.”
Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa. Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa.