Saturday, August 23, 2014

VIFAA VYA KUBAINI DALILI ZA AWALI ZA UGONJWA WA EBOLA KUPITIA JOTO LA MWILI VYAWASILI NCHINI, KUANZA KUTUMIKA VIWANJA VYA NDEGE

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Kebwe Steven Kebwe (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Afya na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Afya na Ustawi Dkt. Elias Chinamo moja ya kifaa (kamera) itakayotumika kupima dalili za ugonjwa wa Ebola kwa wasafiri wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege ili kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama kwa kuuzuia ugonjwa huo kuingia nchini.
Mkurugenzi wa Ugavi wa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD),Heri Mchunga (kushoto)  akimpima Mkurugenzi wa Afya na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Afya na Ustawi Dkt. Elias Chinamo (kulia) kuonyesha namna moja ya kifaa cha kupimia joto la mwili wa Binadamu kinavyofanya kazi kwa kubaini dalili za Ugonjwa wa Ebola eneo la uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Moja ya kifaa (kamera) nne zilizoagizwa na Serikali kupimia dalili za ugonjwa wa Ebola maeneo ya viwanja vya ndege. Kifaa  hicho kina uwezo wa kutunza picha na kumbukumbu za msafiri, muda , joto la msafiri, tarehe aliyoingia nchini pia uwezo wa kupata takwimu kutoka kwenye hali ya majimaji au jasho la Binadamu pindi kinapoelekezwa kwake

SOURCE:GPL