Kaimu Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Joseph Konyo ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai akitoa taarifa. |
Matukio hayo ambayo niya kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu
kutokana na wizi huo uliofanywa na makundi ya watu mbalimbali
yanaujihusisha na utapeli, wananchi hao ambao baadhi ni watu maarufu
Jijini hapa, ‘wamelizwa’ kiasi cha shilingi Milioni 309 kwa kipindi
hicho.
Kaimu Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Joseph Konyo ambaye ni Mkuu wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoani hapa akitoa taarifa za matukio hayo
jana kwa waandishi wa habari ofisini kwake, alisema kuwa ,baadhi ya
matapeli waliokamatwa wameisha fikishwa mahakamani huku wengine
wakiendelea kusakwa.
Katika tukio la hivi karibuni mwezi uliopita, mwananchi mmoja maarufu
jijini Mwanza (hakutajwa) mkazi wa Kiseke wilayani Ilemela, alinaswa na
mtego wa matapeli hao na kujikuta akiuziwa kilo kumi za unga wa sembe
ambao ulikuwa umehifadhiwa kwenye begi ikidaiwa ni madini ya Rubi (Green
Tourmaline)
“Huyu alilazimika kuuza nyumba yake jijini Mwanza na kwenda na matapeli
hao hadi Morogoro ambapo alionyeshwa madini hayo na kutoa pesa na kisha
kufungiwa kwenye begi bila kutakiwa kulifungua hadi atakapofika Mwanza
na kukaa siku saba vinginevyo atakiuka masharti na kukuta majini.”
Alielza Konyo.
Alieleza kuwa , baada ya siku tatu kupita, mkazi huyo aliwapigia simu
wauzaji akitaka kufungua lakini walimzuia kuwa asubiri hadi
watakapomueleza, akilazimisha atakuta majini, hali iliyomfanya akimbilie
polisi ili kuomba msaada wa kulifungua na ndipo ilipobainika kulikuwa
na unga wa sembe na si madini.
“Huwezi kuamini na ukimuona huto amini kama angesitahili kuibiwa
kiurahisi (Kutapeliwa) namuna huyo ni mtu anaheshimika hata kimuonekano
wake na kibaya zaidi alimpa talaka kwanza mkewe ndiyo akuza nyumba yake
ili kupata fedha za kupata madini hayo, sasa mke kamkosa, nyumba
imeenda, fedha na madini kavikosa.” Alisema.
Tukio jingine, ni mkulima mmoja aliuza nyumba yake kwa thamani ya sh
milioni 7 na fedha hizo kuuziwa chupa ya dawa feki ya kuhifadhia mazao
ambayo alidanyanywa kuwa angeweza kuiuza kwa wakulima wenzake kwa sh
milioni 100 na kwamba dawa hiyo inatafutwa na wazungu na inapatikana
katika Chuo cha Utafiti Ukiriguru pekee hivyo kwake atweza kuvuna kiasi
hicho.
“Mwingine aliuziwa chupa tatu za chuma (Mitungi midogo) zilizojazwa
kokoto na cimenti (ndani) kwa tahamani ya shilingi milioni 26,
akidanganywa kuwa ni za asidi (mercury) ya kuoshea dhahabu na mwingine
akadanganywa asiweke fedha benki wamuuzie dhahabu, akauziwa gorori za
baiskeli kwa shilingi milioni 6 baada ya kuonyeshwa vipande vya kufuli
vilivyosagwa na kung’aa kama dhahabu.” Alisema Konyo.
Kamanda huyo alieleza kuwa, katika tukio jingine, mwananchi mmoja
aliyeuza nyumba yake shilingi milioni 200, alidanganywa kuwa wanaweza
kuzarisha fedha zake mara mbili na kuziweka kwenye boksi la mganga mmoja
ili ziwe sh milioni 400, matokeo yake alibiwa, watuhumiwa walikamatwa
kesi iko mahakamani.
Akihitimisha matukio hayo la mwisho, alisema kuwa mwanamke mmoja
mfanyabiashara alijikuta akibakwa, kulawitiwa na kuibwa pesa
(hazikutajwa) baada ya kufanya mazungumzo katika chumba cha Hoteli moja
jijini hapa na kujikuta akinyweshwa dawa za kulevya na watu hao
waliojitambulisha kwake kuwa ni wafanyabiashara kutoka Miji mikubwa
Kaimu kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mwanza, alisema
matapeli hao wakati mwingine wanatumia majina ya viongozi wa ngazi za
juu mkoa na taifa hivyo wawe makini kubaini mbinu zinazotumiwa na
ikiwezekana kutoa taarifa mapema kabla ya kutoa fedha kwani mbinu
nyingine ni za kizamani, zinahitaji akili ya utambuzi wa ukweli na
uongo.
“Ebu sasa viongozi na wafanyabiashara ambao kila kukicha matapeli
wanapanga njama za kuwadanganya kwa lengo la kuwaibia na kuwatapeli
wafanye mawasiliano kwanza emdapo matapeli hao watawafika na kutumia
majina ya viongozi wengine wakiwemo wa vyombo vya ulinzi na usalama
kabla ya kutekeleza kile walichoombwa ikiwemo kutoa taarifa kwa Jeshi la
Polisi ili kuwakamata” alisisitiza