Wakati Naibu Spika, Job Ndugai akisema maelezo binafsi ya Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM) kuhusu biashara ya dawa za kulevya na athari zake aliyoyatoa bungeni juzi jioni hayatajadiliwa, Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini kimeshtukia mbinu mpya zinazotumiwa na wafanyabiashara wa dawa za hizo.
Ndugai alitoa ufafanuzi huo jana baada ya Mbunge
wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola kuomba mwongozo jana, akitaka Bunge
likubali mjadala wa suala hilo kutokana na unyeti wake.
Akizungumza na Mwananchi Dar es Salaam jana,
Kamanda wa kitengo hicho, Godfrey Nzowa alisema wameshtukia mbinu mpya
zinazotumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya, ambao sasa wanatumia
barabara badala ya anga.
“Mfano mzuri, tumeshtukia usafirishaji wa epedrine
na Juni 24 mwaka huu, Saada Ally Kilongo (26) alikamatwa Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kilo 11,000 za dawa za kulevya
aina ya epedrine, ambazo ni mali ghafi za thamani zaidi ya Sh170 mil,”
alisema.
SOURCE:MWANANCHI
SOURCE:MWANANCHI