STAA katika tasnia ya filamu Bongo, Jackline Wolper amefungukia kipaji
cha wanaume kuhonga na kusema kuwa, si kila mwenye pesa nyingi anafanya
hivyo bali inategemea na hulka ya mtu
Akifafanua juu ya madai kuwa wauza unga wengi Bongo wanaongoza kwa
kuwahonga mastaa, Wolper alisema siyo kweli kwani mtu unaweza kuwa na
mpenzi mfanyabiashara mwenye pesa nyingi lakini akawa mbahili.
“Si kweli kuwa wauza unga ndiyo wanahonga sana wanawake au sisi mastaa,
unaweza kuwa na bwana mfanyabiashara na mwingine kaajiriwa lakini huyo
aliyeajiriwa akawa ana kipaji cha kuhonga, akakupa hata asilimia 75 ya
mshahara wake na yule mwenye pesa nyingi akawa mbahili sana, ni kipaji
tu,” alisema