Watanzania, Agnes Masogange na mwenzake Melisa Edward, wanatarajiwa kupandishwa tena kizimbani Septemba 18 mwaka huu katika mahakama moja nchini, Afrika Kusini.
Wanawake hao watasomewa mashtaka ya kukutwa na kilo 150 za kemikali za kutengenezea dawa za kulevya aina ephedrine, zenye thamani ya Sh7bilioni.
Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifika katika mahakama hiyo ya mjini Johannesburg Septemba 13 mwaka huu.
Hata hivyo wote walikana mashtaka hayo na kurudishwa rumande kwa sababu upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa haujakamilika
Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, aliliambia gazeti jana kuwa washtakiwa watapandishwa kizimbani kwa mara ya pili na kwamba wao wanasubiri maamuzi ya mahakama kwa mara nyingine.
“Kama upelelezi wa kesi yao utakamilika huenda wakaachiwa kwa dhamana kama watatimiza masharti lakini dhamana hiyo siyo kurudi hapa nchini watabaki huko huko, Afrika ya Kusini kama sheria zao zinavyoeleza,” alisema Kamanda Nzowa.
MWANANCHI: