AL MARKHIYA SPORTS CLUB
P O BOX 21923
DOHA, QATAR
TANZANIA FOOTBALL FEDERATION
P O BOX 1574
DAR-ES-SALAAM
TANZANIA
YAH: KUOMBA MSAMAHA KWA CHAMA CHA MPIRA TANZANIA
Husika
na kichwa cha habari hapo juu mimi mchezaji MWINYI KAZIMOTO naomba
msamaha kwa kitendo nilichokifanya cha kuondoka kambini timu ya taifa na
kuiacha nchi yangu katika kipindi kigumu hali ya kuwa walikuwa na mechi
ngumu na muhimu dhidi ya Uganda.
Halikuwa
lengo langu kuidhoofisha nchi yangu bali ni tamaa yangu ya kucheza
mpira nje ya nchi ndiyo iliyonifanya niondoke katika kipindi hicho, na
nashukuru mungu nimefanikiwa kupata team nchini Qatar, naamini
watanzania wataipokea habari hii kwa vizuri.
Mwisho
kabisa napenda kuwahakikishia watanzania na chama cha mpira kwa ujumla
kwamba naahidi nitaitumikia nchi yangu muda wowote watakaponihitaji.
Natumai chama cha mpira na watanzania kwa ujumla watanielewa na watanisamehe.
Wenu mtiifu
MWINYI KAZIMOTo