Monday, September 1, 2014

DIAMOND ADAIWA KUOKOLEWA NA POLISI WA UJERUMANI,KUFUATIA MASHABIKI WAKE KUSHIKWA NA HASIRA

 Gari ya Polili ilioibuka kumuokoa Diambond kufuatia sakata la mashabiki wake kupandwa na jazba
Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini stuttgart,ujerumani
UJERUMANI SI SHWARI KIMENUKA !!
POLISI UJERUMANI WAMUOKOA DIAMOND KUTOKA KWA WASHABIKI WENYE HASIRA ! KASHINDWA KUWIKA STUTTGART KISA ?

KAFIKA UKUMBINI SAA 10 ALFAJIRI ! WASHABIKI WANASURI SHOW TANGU SAA 4 USIKU

PROMOTA MNAIJERIA AINGIA MITINI ,DJ APATA KISAGO HETI VYOMBO VIBOVU ! HAIBU

Stuttgart,Ujerumani,
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show,washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki  Diamond na promota wake,Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muzikima-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.
Mmoja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ  Flor alipatwa shock mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo  DJ Drazee naye yupo hoi hospatal. Polisi nchini ujerumani wanamesema tukio hili la haibu alijawahi kutokea,kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwawanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara