Thursday, August 22, 2013

WATU SABA WANUSURIKA KWA AJALI YA NDEGE ILIYOTUA ZIWA MANYARA


Ndege ndogo ya shirika la Tanzanair iliyokuwa ikitokea mjini Bukoba mkoani Kagera kwenda Dar ss Salaam imelazimika kutua kwa dharura katika ziwa Manyara baada ya injini yake moja kuzimika ghafla ikiwa angani. 


Ndege hiyo ilikuwa na abiria sita na rubani mmoja ambapo wote wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Seliani mjini Arusha kwa matibabu.

Chanzo: ITV