Linah akiwa jukwaani wakati wa shoo ya Fiesta 2013 jijini Dar. |
Mavazi ya nusu utupu ambayo msanii Esterlina Sanga ‘Linah’ hupenda
kuyavaa hasa kwenye matamasha yamekuwa yakiwadatisha wanaume na wengine
kuomba kupiga naye picha kwa lengo la ‘kujipoza’ kama ilivyotokea kwenye
Fiesta, Dar hivi karibuni.
Linah akipozi na baadhi ya wanaume walioomba kupiga naye picha.
Ijumaa limekuwa likimfuatilia Linah na kubaini kuwa kila mara hupenda
kuvaa nguo zinazoacha wazi mapaja na kitovu chake na watu ambao amekuwa
akipiga nao picha ni wanaume ambao wengi huonekana wakiwa wamemshika
kimahaba.
Hata hivyo, licha ya mwenyewe mara kadhaa kueleza kuwa, hayo ni mvazi
ya kikazi zaidi, baadhi ya mashabiki wamemponda na kumtaka kubadilika
hasa ikifahamika kuwa ni mtoto aliyetokea kwenye familia iliyoshika dini
na kwamba kuvaa hivyo ni kujidhalilisha