|
Bi. Flora Mtegoa. |
Katika hali ya kushangaza, baba wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu
Bongo, marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba amempiga marufuku mama
mzazi wa msanii huyo, Flora Mtegoa kutumia jina la Kanumba kwa namna
yoyote.
|
Mzee Charles Kanumba.
|
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni baba Kanumba alisema mama Kanumba
hana mamlaka ya kulitumia jina la Kanumba kwani hana uhusiano nalo.
“Mimi ndiye mwenye mamlaka na jina la Kanumba kwa sababu ni la kwangu
lakini namshangaa mama Kanumba kuendelea kulitumia jina hilo hata kwa
watoto wasionihusu kama mtoto wa mwanaye aliyezaliwa hivi karibuni na
kuitwa Kanumba Junior.
“Anahusiana nini na hilo jina wakati huyo siyo damu yangu, yeye ana
baba yake kwa nini asitumie jina lake, sitaki kabisa atumie jina langu
mwanangu ameshafariki na mimi ndiye mwenye mamlaka ya kutumia hilo
jina,” alisema mzee huyo.
Akilizungumzia suala hiyo, mama Kanumba alisema: Sitaki kumsikia kabisa,kama vipi aende mahakamani.