Thursday, October 31, 2013

UFOO SARO ALA KIAPO CHA SIRI BAADA YA KURUHUSIWA HOSPITALINI

Ufoo Saro akiwa hospitali baada ya kupigwa risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther Mushi.
SIKU chache baada ya Mtangazaji wa Runinga ya ITV, Ufoo Saro kuruhusiwa hospitalini alipokuwa amelazwa baada ya kudaiwa kupigwa risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther Mushi, ameibuka na kula kiapo cha siri.

Ufoo ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, katika tukio la yeye kupigwa risasi, alimpoteza mama yake mzazi aitwaye Anastazia Saro aliyedaiwa kuuawa na marehemu Mushi aliyejiua kwa risasi.
Akizungumza na gazeti hili Ufoo alisema, kamwe hawezi kusema kilichokuwa kikiwagombanisha yeye na marehemu Mushi mpaka siku ya mwisho wa uhai wake.
Ufoo Saro.
“Siwezi kuzungumzia kabisa chanzo wala ugomvi wetu mimi na marehemu Mushi. Hiyo itakuwa siri yangu,” alisema Ufoo.
Katika mahojiano na gazeti hili, mtangazaji huyo alipoulizwa kuhusu msimamo wake wa uhusiano baada ya kupona kabisa alisema, hawezi kujiingiza tena kwenye mapenzi kwa sasa.
“Sitaki kabisa kusikia juu ya mapenzi, siwezi kuliweka suala hilo akilini tena,” alijibu kwa kifupi kwa sauti ya chini lakini yenye mkazo