Wednesday, August 14, 2013

KAMPUNI YA BLACK BERRY YASHINDWA USHINDANI-IPO HATARINI KUUZWA...

Ushindani wa biashara ya simu za mkononi ‘smartphones’ uliopo sokoni hivi sasa umeiathiri kampuni kongwe ya Blackberry na kusababisha ifikirie uwezekano wa kujiuza.

Jumatatu ya wiki hii bodi ya kampuni hiyo imesema imeunda kamati maalum kutafuta njia mbadala za kimkakati, kwa matumaini ya kuongeza thamani ya kampuni na kuongeza nguvu ya toleo lao jipya la Blackberry 10. Kampuni hiyo imedai kuwa kati ya mbinu wanazofikiria kuzitumia ni pamoja na ubia, ushirikiano na njia zingine.

Kampuni ya BlackBerry iliyoanzishwa mwaka (1999) ilikuwa ndio kampuni kubwa ya smartphones kabla ya kuanza kupata ushindani kutoka kwa Apple waliotambulisha simu za iPhone mwaka (2007) na kuendelea kupokea ushindani kutoka katika simu zingine za Android.

Mwezi January mwaka huu Blackberry ilizindua toleo lake jipya la Blackberry 10 kwaajili ya kukabiliana na ushindani, kitu ambacho hakijasaidia kutokana na soko lake kuendelea kuporomoka ambapo kwa mauzo ya smartphone duniani inakamata nafasi ya 4.

Mchambuzi wa Canaccord Genuity Mike Walkley, amesema mambo yanazidi kuwa mabaya kwa Blackberry pamoja na kushuka kwa gharama za simu zake mpya