Monday, December 2, 2013

LULU Awahamasisha vijana juu ya Upimaji wa Virusi vya Ukimwi..


Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael aka Lulu amesema vijana wanatakiwa wawe mstari wa mbele katika kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
 
Akizungumza na mwandishi wetu jana katika usiku wa Red Ribbon Fashion Galla iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam, Lulu alisema siku ya Ukimwi duniani inatukumbusha kuangalia tumetoka wapi na tunakwenda wapi na kuangalia wangapi wamepoteza maisha kwaajili ya gonjwa la Ukimwi.
 
Najumuika na Watanzania leo ,siku ya Ukimwi duniani ambayo hufanyika kila mwaka, kwa kuangalia wangapi wamepoteza maisha, pamoja na kuwahamasisha zaidi vijana Wakitanzania kutumia kinga ili kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi ambavyo vinapoteza nguvu ya Taifa,” alisema Lulu.
 
Pia Lulu alisema amekuwa akipima Ukimwi mara kwa mara ili kuangalia afya yake,huku akiwashauri vijana kwenda kupima ili kujua afya zao.
 
“Nimekuwa nikipima HIV kila mara katika hatua za maisha yangu,kuangalia kuhakikisha najiweka katika usalama wa afya yangu,pamoja na kupanga matarajio ya maisha.Sio kuwa ukipima ukagundulikana una HIV utashindwa kupanga malengo yako hapana! ukipata ushauri nasaha, ukajua uishi vipi kwa kuboresha afya yako, maisha yataendelea kama kawaida. Kwahiyo kinachotakiwa vijana ni kujua afya zetu mapema