Rapper Ney Wa Mitego ameniambia kuwa hii picha hapo juu tukio hilo
limetokea Jana wakati wana shoot video ya wimbo wake Unaofanya vizuri
kwa sasa kwenye radio stations ' Salam Zao'.
Ney Wa Mitego Amesema ' Nikweli nilituwa sero jana baada ya raia
wasio julikana kuleta fujo eneo la kazi yangu kwasababu kulikuwa na
waigizaji waliokuwa na sare za polisi. Watu hao sijuani nao na
walijitambulisha kama askari na kutaka kujua kwanini natumia sare za
polisi kwenye video yangu bila kibali. hicho ndio kitu kilichopelekea
nikapelekwa polisi.
Mitego ameendelea kusema kuwa baada ya kukaa sero kwa dakika kama 15
mkuu wa kituo alikuja na kusikiliza tatizo hilo na ndio aliachiwa huru
baada ya kutoa maelezo kuhusu tukio hilo na sare hizo kuoneknaA
uraiani.
Ney aliwekwa sero Kwenye kituo cha polisi Urafiki kilichopo Manzese
na wiki ijayo video hii itaonekana kwenye vituo vya televison Tanzania