Taasisi
isiyo ya kiserikali ya Flaviana Matata Foundation (FMF) inafanya kazi
ya kuhamasisha, kuwezesha na kusaidia wasichana nchini kwa kuwaelimisha
na kuwapa misingi ya kuwajenga kuwa kati ya watendaji wazuri
wanaochangia katika shughuli za maendeleo ya jamii. Ili kufanikisha
hayo, Flaviana Matata Foundation (FMF) inawadhamini
wanafunzi wasichana kwa kuwalipia ada za shule, kuwanunulia sare za
shule pamoja na misaada mingine mbali mbali yenye kumwezesha mwanafunzi
kusoma vizuri kuanzia elimu ya msingi, upili na hatimaye kufikia kwenye
taasisi mbali mbali za elimu ya juu.
Malengo makuu ya Flaviana Matata Foundation ni pamoja na:
i. Kusaidia kuongeza idadi ya watoto wa kike wanaojiunga katika ngazi mbali mbali za elimu.
ii. Kuhamasisha harakati za kutokomeza umasikini Tanzania kupitia miradi mbali mbali ya elimu.
iii. Kuhamasisha wasichana kujiendeleza kufikia elimu ya juu pamoja na elimu ya ufundi.
iv. Kuwasaidia wanawake kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli za kijasiriamali.
Katika
kufikia malengo hayo, Flaviana Matata Foundation inazindua mradi wake
unaootambulika kama “FMF Stationeries Project” hapa Tanzania.
Mradi
huu unahusisha uuzaji na usambazaji wa vifaa vya shule (madaftari,
kalamu za wino, kalamu za risasi, rula, mikebe n.k.) kwa mashirika,
taasisi mbalimbali na watu binafsi.
"Tunataraji
kutumia mapato yatakayopatikana kutokana na mradi huu katika kulipia
ada, kununua sare za shule pamoja gharama nyingine zinazohusiana na
kuwapatia elimu bora watoto wote ambao wapo chini ya Flaviana Matata
Foundation pamoja na kufanya miradi mingine ya maendeleo inayohusiana na
elimu".
Kuhitimisha
uzinduzi wa mradi huu, Flaviana Matata Foundation imeamua kuitembelea
Shule ya Msingi Minazini iliyopo Mwananyamala wilaya ya Kinondoni,
jijini Dar es Salaam na kutoa msaada wa madaftari, kalamu za wino na
kalamu za risasi kwa wanafunzi wenye uhitaji ikiwa ni ishara ya mwanzo
wa utendaji wa Tasisi kuelekea kufikia malengo ya mradi.
FMF
inaamini kwamba hii ni njia mojawapo ya kuwafikia Watanzania na
kuwahamasisha kutoa misaada katika shughuli za kuendeleza elimu. Katika
uzinduzi huu, Mwasisi wa taasisi ya Flaviana Matata Foundation,Flaviana
Matata ameambatana na wanamuziki pamoja na vijana wengine mashuhuri
nchini ambao ni vioo katika jamii yetu.
Dhumuni
ni kuhamasiha vijana wengine kujitolea katika kusaidia shughuli
zinazohusiana na maendeleo ya elimu na kupiga vita na kutokomeza
umasikini.
Flaviana
Matata akimkabidhi mwalimu mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi ya
Minazini,iliyopo Mwananyamala B, Fina Kiocho msaada wa madaftari,pen na
pensel ambao utasaidia wanafunzi wasiona uwezo wanaosoma shuleni hapo.
Baadhi
ya FMF Stationaries Project zikiwemo pen, penseli pamoja na madaftari
makubwa na madogo ambayo yatakuwa yazalishwana Taasisi ya Flaviana
Matata Foundations ambapo zaidi kutoa msaada pia kuna zitakazokuwa
zinauzwa na pia Taasisi inakaribisha makampuni ambayo yanahitaji kutoa
msaada wa vifaa vya shule kuwasiliana nao na nembo yao itawekwa kwenye
vifaa hivyo
Flaviana
Matata akiongea na wanafunzi wa shule ya Mnazini akiwaambia wasome kwa
bidii kwani alimu ndio kila kitu na kuwakumbusha kwa wale watoto wakike
ambao watafaulu na wazazi hawatakuwa na uwezo FMF itasaidia kuwasomesha
baadhi yao .
wasanii pamoja na warembo mbalimbali walijitokeza kuunga mkono harakati hizo za Flaviana
Flaviana Matata akiwa sambamba na waliowahi kuvikwa taji la Miss Tanzania Nancy Sumari na Faraja Kokota na Miss Ilala Kisa Zimba
Mwanamuziki Ommy Dimpoz alipata wasaa wakusaini kitabu cha wageni cha shule ya Minazini