Wednesday, December 4, 2013

MOROGORO: KONDAKTA AGONGWA NA LORI NA KUFA AKIWAVUSHA BARABARA WANAFUNZI WA CHEKECHEA.



Marehemu William Francis,28, enzi za uhai wake


Baadhi ya viongozi wa chama cha waendesha daladala wakiendelea kukusanja michango ya rambi rambi leo mchana




Baadhi ya madereva na makondakta wa daladala wakiwa na nyuso za hudhuni baada ya kupokea taarifa za tukio hilo.
NA DUSTAN SHEKIDELE, MOROGORO.
KATIKA hali ya kuhuzunisha kondakta wa Hiace inayofanya safari zake Kihonda - Mjini William Francis,28, jana mchana amegongwa na Lori na kufa papo hapo eneo la Kihonda barabra kuu ya Morogoro-Dodoma, alipokuwa akiwavusha abiria wake ambao ni wanafunzi wa chekechea uapande wa pili wa barabara hiyo isiyokuwa na vituo vya kushusha na kupakia abiria.

Akihojiwa na mwandishi wa habari hizi msemaji wa chama cha madereva na makondakta wa daladala mkoani Morogoro Bw Kigola Pazi alisema marehemu aligongwa na gari hilo alipokuwa akiwavusha abiri wake ambao ni madenti wa shule ya awali 'chekechea'

"Kwa nyinyi waandishi wa habari mtusaidia kufikisha kilio chetu kwa mamlaka husika mwenzetu amekufa akitetea roho za abiri wake kufutia barabara ya Kihonda kukosa vituo vya kushusha na kupakia abiri, Wille aligongwa na gari wakati akirudi upande wa pili wa barabra baada ya kuwavusha watoto wawili wa shule ya chekechea akisema kwa uchungu msemaji huyo wa chama hicho.

Mwandishi wa habari hizi alifika kwenye kituo kikuu cha daladala kilichopo katikatika ya mji kasoro bahari 'Morogoro' na kushuhudia baadhi ya madereva na makondakta wakiwa na nyuso za huzuni baada ya kupokea taariza hizo za kifo cha ghafla cha mwenzao.

'Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake libarikiwe Amen