
MAJERUHI Francis Shumira aliyejeruhiwa katika tukio la kushambuliwa kwa risasi Ilala Dar es salaam juzi amefariki dunia jana asubuhi Hospitali ya Muhimbili alikolazwa MOI kwa matibabu.
Kufariki kwa Francis kunafanya idadi ya watu watatu waliofariki katika tukio hilo hadi hivi sasa huku ikiacha majeruhi wawili ambao ni Christina Alfred Newa Mwanafunzi wa masuala ya Mawasiliano visiwa vya Syprus na mama mzazi wa Christina, Hellen Elieza Newa.
Familia imekiri kuwa Christina na Marehemu Munisi walikuwa na mahusiano lakini ni zamani na walitengana kutokana na vurugu alizowahi mfanyia siku za nyuma.

Taarifa za Polisi zinapasha kuwa, Watu walio poteza maisha katika tukio hilo ni Gabriel Munisi ambaye aliwapiga risasi wenzake na kisha kujiua mwenyewe , Alfa Alfred ambaye ni mdogo wake Christina , na Francis Khiranga Shumira ambaye amefariki jana akiwa Muhimbili