Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), DK Joyce Ndalichako (kulia) akizungumza baada ya kupata maelezo ya namna teknolojia mpya ya kusahihisha maswali ya kujieleza inavyofanya kazi. Wengine ni maofisa wa Kampuni ya DRS iliyobuni teknolojia hiyo.
Teknolojia hiyo ilianza kutumika miaka 12 iliyopita, na kwamba inaongeza ubora wa usahihishaji wa mitihani na kutoa majibu sahihi kwa watahiniwa.
Mwaka jana Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), lilianza kutumia
teknolojia mpya ya usahihishaji wa mitihani ya kumaliza elimu ya
msingi.
Kabla ya matumizi ya teknolojia hiyo inayotumia
kompyuta (Optical Mark Reader), baraza lilisema teknolojia hiyo
ingesaidia kupunguza muda pamoja na gharama za usahihishaji.
Ilisema pia teknolojia hiyo, ingetoa fursa ya
wanafunzi kupimwa kwenye nyanja mbalimbali walizofundishwa na pia
kuongeza umakini katika kusahihisha mitihani.
Ili kuweza kutumika kwa teknolojia hiyo wanafunzi
walipaswa kutumia karatasi maalu mu za kujibia mitihani,
zilizosahihishwa na mashine ya OMR, ambayo pamoja na mambo mengine pia
huonyesha maswali yaliyojibiwa vizuri na yale yenye changamoto.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa
(Necta), Dk Joyce Ndalichako anasema kuwa matumizi ya OMR mbali na
kupunguza gharama za usahihishaji na kuharakisha shughuli hiyo,
yamesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza makosa yaliyokuwa yakifanyika
wakati wa kusahihisha mitihani hiyo kwa kutumia mikono.
“Baada ya kufanya tathmini ya mfumo huu kwa mwaka
jana, tumebaini kuwa mashine haikufanya kosa hata moja. Baadhi ya makosa
yaliyojitokeza yalisababishwa na watu na mashine iliwaumbua,” anasema
na kuongeza:
“Watu wanasema kuwa mtihani wa maswali ya kuchagua
ni rahisi, lakini siyo kweli, inatungwa na wataalamu na unalenga
kumpima mtoto katika kila nyanja. Ndiyo maana hata mtihani wa darasa la
saba mwaka jana ilibidi Serikali ishushe alama za kwenda kidato cha
kwanza zikawa 70 badala ya 100.”
Anasema kwa kidato cha nne na kuendelea, wameweka
mfumo ambao baada ya kumaliza kusahihisha, mhusika anaingiza alama zake
kwenye mfumo ambao hakuna mtu anayeweza kuubadilisha.
“Zikishaingizwa kwenye mfumo kutoka kwenye kituo
cha usahihishaji, hakuna mtu anayeweza kuzigusa na akigusa anaonekana.
Hata msahihishaji akishaziweka mara moja hawezi kuzigusa tena na
hakigusa anaonekana. Kwa hiyo kwa mfumo huu huwezi kumuongezea
mwanafunzi alama,” anabainisha.
Teknolojia ya maswali ya kujieleza
Mwaka jana baadhi ya watu walihoji kama teknolojia
ya OMR ingeweza kumudu kusahihisha maswali ya kujieleza, Dk Ndalichako
anasema wako mbioni kujiandaa kutumia teknolojia nyingine ya kompyuta
itakayokuwa na uwezo wa kusahihisha maswali ya kujieleza.
Tofauti na teknolojia ya OMR, anasema kuwa
kwenye mfumo huu wa kusahihisha mitihani ya kujieleza, zoezi la
kusahihisha litakuwa linafanywa na mtu kwa msaada wa kompyuta