Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uboreshaji wa huduma za
magonjwa ya moyo katika hospitali ya taifa muhimbili, kushoto ni
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Zamaradi Kawawa.
Mkuu
wa Kitengo Cha Moyo toka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Robert
Mvungi akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) sababu za
tatizo la ugonjwa wa Moyo katika jamii.
Mkuu
wa Kitengo Cha Moyo toka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Robert
Mvungi akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mchoro
unaoonesha matundu katika Moyo.
Mkurugenzi
wa Fedha na Mipango wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Agnes Kuhenga
(kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) juu
ya gharama za matibabu katika kitengo cha magonjwa ya moyo katika
hospitali ya Taifa Muhimbili, katikati ni Mkuu wa Kitengo hicho Dkt.
Robert Mvungi na wa mwisho kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya
Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela
akiwaonesha waandishi wa habari moja ya chumba cha kupumzika wagonjwa
mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Mkuu
wa Kitengo Cha Moyo toka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Robert
Mvungi akiwaonesha waandishi wa habari mtambo wa Cath Lab unaosaidia
kuangalia mishipa ya damu inayokwenda kwenye Moyo.Picha Zote na Eliphace
Marwa (MAELEZO).