Wednesday, October 30, 2013

MPENZI WANGU ANATAKA NIMPE RAHA NA UTAMU (TUFANYE NGONO) WAKATI MIE BADO BIKIRA,NIFANYEJE



Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 23,naishi kigamboni,nimemaliza chuo mwaka jana.Nina Tatizo linanisumbua,nashukuru Mungu nimeweza kuvumilia kwa muda mrefu bila kulala na Mwanaume.Nimeweza kuhifadhi zawadi nzuri yenye thamani kubwa ambayo kwa mwanamke mwenye Heshima zake anastahili awe nayo kwa ajili ya kumpa mume wake baada ya kufunga Ndoa(namaanisha kuwa mie bado bikra).


Tatizo Linalonisumbua ni kwamba kila muda mpenzi wangu ananisumbua anataka nimpe Raha na Utamu,nikimnyima anasema kuwa simpendi,na kiukweli mi nampenda tena sana,na ninajisikia vibaya ninapomuona mpenzi wangu amenuna amekosa furaha,Kwani hakuna Njia nyingine ya kumfanya aniamini kuwa nampenda bila kumpa Raha na Utamu? Ninachotaka mimi Nimpe Raha na Utamu kwenye Usiku wa Fungate kama Zawadi Special kwa ajili yake lakini Naogopa nikiendelea kumnyima nahisi ataniacha,Naombeni Ushauri Nifanyeje?

USHAURI WA DOKTA WA MAPENZI
Hongera sana mrembo kwa kuweza kujitunza muda wote huo,maana huko mtaani siku hizi ni wasichana wachache sana wanaojua thamani ya Bikira.Nisingependa kukuchosha sana,labda nikuonyeshe Faida na Hasara za kumpa mpenzi wako Bikra,

HASARA ZA KUMPA MPENZI WAKO BIKRA KABLA YA NDOA

1.UNAWEZA UKAPATA MIMBA AMBAYO HUKUITARAJIA

Unaweza ukasema utatumia condoms lakini unadhani mpenzi wako nae atakuwa teyari kudo the same? je unadhani atakubali mzitumie mpaka mfunge Ndoa? Kama akikubali kuzitumia mwanzoni halafu baadae hapo katikati kabla hamjafunga Ndoa akabadili mawazo,mkado bila Condoms,si utakuwa unarisk Maisha yako just for Lo*ve? Maisha yako ni kitu Muhimu kuliko Mapenzi so mimi siwezi kukushauri urisk maisha yako for Lo*ve.

2.ANAWEZA AKAKUACHA MUDA WOWOTE ULE BAADA YA KUMPA BIKIRA YAKO
Inawezekana anakusumbua umpe Raha na Utamu kwa sababu anataka kuprove kama wewe ni bikra au uongo,na una uhakika gani kuwa atazidi kukupenda ukishampa Raha na Utamu? Labda nikupe Siri kidogo,Wanaume wengi wanachukulia kufanya ngono kama ni something PHYSICAL,na wakati nyie Wanawake mnachukulia ngono kama Something EMOTIONAL,ukishamaliza kumpa Raha na Utamu,wewe utazidi Kumpenda lakini Mwenzako Upendo wake Hautokuwa sawa na wako

3.ATAENDA KUTANGAZA NA KUJISIFU KWA MARAFIKI ZAKE
Kumtoa Bikra Demu sio jambo la kawaida,kama mpenzi wako akili zake bado za kitoto lazima ataenda kuwasimulia marafiki zake wote.Na kama akiwasimulia hatua kwa hatua jinsi tendo zima lilivyofanyika,itakuwa ni kama amekuvua Nguo mbele za marafiki zake,sasa hebu niambie utajisikiaje ukipita mtaani halafu kila mtu anajua jinsi ulivyotolewa bikra?

4.UTAKUJA KUJUTA SANA KAMA UKISHAMPA HALAFU AKAKUACHA
Kitendo cha yeye kuwa Mwanaume wako wa kwanza na kama haitoshi ukampa na Bikira yako,obviously lazima atastay so deep ndani ya Moyo wako,na The More U Lo*ve Someone The More it Is Goin to H*urt When You Lose them,so ask yourself this question,Je Upo Teyari Kuvumilia maumivu yote ya kihisia ambayo utayafeel ndani ya Moyo ikitokea akakuacha baada ya kumpa Raha na Utamu?

5.MUDA WOTE ULIOPOTEZA KUJITUNZA UTAKUWA HAUNA MAANA TENA
Maana,Umuhimu na Thamani ya kuitunza Bikra ni Pale unapotoa hiyo zawadi kwa mume wako baada ya Ndoa,Sasa kama ukimpa Raha na Utamu mpenzi wako akafanikiwa kuitoa hiyo bikra,ina maana miaka yote hiyo 23 uliyoteseka,ukajinyima na kuvumilia itapotea bure bila maana yeyote.

Lakini pia zipo Faida ambazo unaweza kupata wewe na hata mpenzi wako kama ukimpa Raha na Utamu,hizo Faida na Conclusion ntazitoa kwenye toleo lijalo