Friday, March 7, 2014

HAWA NDIO MASTAA WANAONGOZA KUWA NA NYOTA ZA NGONO...

Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hussein Yahya ameanika nyota za baadhi ya mastaa wa Bongo katika kipengele cha mapenzi au ngono.
Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hussein Yahya.
Akizungumza na mapaparazi wetu katikati ya wiki hii ofisini kwake Magomeni-Mwembechai jijini Dar, Maalim alitumia saa kadhaa kuangalia nyota ya mmoja baada ya mwingine na kueleza sifa zao katika sekta ya uhusiano na tendo la ndoa.
Wema Sepetu.
Baadhi ya mastaa alioweza kuwasoma nyota zao kirahisi ni pamoja na ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, waigizaji Wema Sepetu, Vincent Kigosi ‘Ray’, Aunt Ezekiel, Steven Jacob ‘JB’, Jacqueline Wolper, Blandina Chagula ‘Johari’ na wengine.
ALIANZA NA WEMA
Akimzungumzia Wema aliyezaliwa Septemba 28, Maalim alisema nyota yake ni Mizani hivyo ana tabia zifuatazo katika masuala ya mapenzi:
“Kwanza yeye (Wema) na Diamond nyota yao ni moja hivyo mambo yao mengi yanafanana.
“Wanapenda kuwa kwenye ulimwengu wa mapenzi na mahaba wakati wote. Wanathamini sana masuala ya ngono kuliko maisha mengine.”
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Wema Sepetu katika pozi la kimahaba.
NDOA NA DIAMOND
“Hawa watakuwa watu wa kuachana na kurudiana mpaka watakapofunga ndoa ya kifahari hapo baadaye.
“Kuhusu mambo mengine kinyota ni kwamba wana sifa ya uongozi, wanapenda kuwa huru na kujitegemea. Wanapenda kuheshimika kwenye jamii na ni wacheshi, wana hekima na diplomasia.”
Vincent Kigosi ‘Ray’.
KUHUSU RAY
Kwa upande wake Ray ambaye amezaliwa Mei 28, Maalim alisema nyota yake ni Mapacha.
Akimchambua kinyota kuhusu masuala ya mapenzi, alisema:
“Akimpenda mwanamke ana uwezo wa kumpa chochote, kimawazo na kila kitu, anaweza hata kuhamia nyumbani kwa mwanamke huyo.
Vincent Kigosi ‘Ray’ akiwa na mpenzi wake Chuchu Hans.
“Ila ni mtu anayechoka haraka na hawezi kudumu kwa muda mrefu kwenye penzi na mwanamke mmoja tu.
“Pia anapenda kuwa na mapenzi ya siri siku zote. Hata akioa ni lazima ataendelea kuwa na mwanamke wa nje ‘nyumba ndogo’.
“Mbali na masuala hayo, ni mtu mwenye hisia kali sana ambapo hukasirika upesi. Ni mtu mwenye uwezo wa kujieleza na kuzungumza, ana ushawishi mbele za watu.”
Aunt Ezekiel.
AUNT EZEKIEL NAYE
Akimchambua Aunt Ezekiel ambaye alizaliwa Oktoba 27, mtabiri huyo alisema nyota yake ni Nge.
“Kinyota, ni mtu mwenye ‘muwashawasha’ wa mapenzi, anapokuwa na hasira tu hupenda kuzimaliza kwa kufanya tendo la ndoa.
“Ni msiri sana. Ana wapenzi wengi lakini kwa siri. Kwake tendo la ndoa ni ishu muhimu sana katika maisha yake hasa ikizingatiwa kuwa, nyota ya Nge inatawala sehemu za siri.
“Kwa mwenye moyo mdogo, asifanye mapenzi na mtu mwenye nyota hii kwani atajuta maisha yake yote. Lakini hayumbi na hakubali kushindwa hata kwa jambo ambalo halitamharibia popote.”
Jacqueline Wolper.
JB & WOLPER
Kwa upande wa JB aliyezaliwa Desemba 4, Wolper aliyezaliwa Desemba 6, Maalim alisema wote wana nyota moja inayofanana ya Mshale. Anaichambua nyota hiyo hivi:
“Wanapenda kufanya ngono kwa muda mrefu, hivyo mwanamke au mwanaume atakayekuwa nao kimapenzi lazima awe amekula akashiba vizuri kabla ya tendo lenyewe.
Jacob Steven ‘JB’.
“Wapenzi wao wanapowaonesha dalili ya kuwapenda sana basi wao huwa wanajiondoa kwa hofu.
“Wanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu na wanakolea vilivyo. Mara nyingi wanapenda sana kuwa na wapenzi wapya, lakini hawapendi mapenzi ya kudumu kwa sababu yanawanyima uhuru.
Blandina Chagula ‘Johari’.
NYOTA YA JOHARI SASA
Akimzungumzia Johari aliyezaliwa Agosti Mosi, mtaalam huyo alisema nyota yake ni Simba. Anasema:
“Kinyota ana tatizo la kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani ni mtu anayeumia.
“Mara nyingi hujipa hisia za kupendwa na mpenzi wake kama anavyompenda yeye.
“Ni mkarimu lakini ni jeuri, anapenda sana kuonea wenzake. Anapenda kujionesha na humharibu mpenzi wake.”
GPL.