Jana October 26 2013 ndio Wanawake nchini Saudi Arabia walipanga
kuandamana kupinga wao kunyimwa kuendesha magari sehemu yoyote nchini
humo ikiwa ni nchi pekee duniani ambayo inakataza Wanawake kuendesha
magari hata kama wanaweza.
Unaambiwa kwa sasa Mamlaka za Saudi Arabia zimewaonya Wanawake hao
kutoandamana katika maandamano hayo yatakayokua ya aina yake na ya tatu
kutokea nchini humo toka mwaka 1990 ambapo Wanawake kadhaa walikamatwa
na wengine kuachishwa kazi, onyo hilo linakwenda pia kwa Mwanamke yeyote
ambae amepanga kuendesha gari
Msemaji wa Serikali amesema Mwanamke yoyote atakae endesha gari leo
atachukuliwa hatua za kisheria ambapo wakati siku hii ya kuandamana
ikisubiriwa Wanawake kadhaa wa Saud Arabia tayari walishaweka video zao
wakiendesha magari sehemu mbalimbali za Saudia lakini mpaka sasa
hawajakamatwa.
Mpaka sasa zaidi ya watu elfu 17 wamesain kura ya ndio itakayo waruhusu
Wanawake wa Saudi kuendesha magari ambapo pia idadi ya Wanaume
wanaosupport imeendelea kuongezeka kwa kasi.