Rehema Chalamila the award winning
singer ambaye aliathirika na matumizi ya dawa za kulevya na baadae
kupona. Ameendelea kuwa kioo cha jamii kwa ku-share experience yake
baada ya kupona kwenye ishu ya dawa za kulevya. Ray C ametoa ujumbe mpya
ambao ni muhimu kila mtu kuujua kwasababu kwenye mazingira yetu kuna
waathirika wengi wa dawa za kulevya.
Haya ndiyo maneno ya Ray C mwenyewe ambayo yana ujumbe mzuri ndani yake:
“Wote hawa
tuliokaa hapa(picha hapo chini) tuliathirika na dawa za kulevya na
tumepona kwa kunywa dawa moja tu inayoitwa Methadone. Inapatikana
Muhimbili na Mwananyamala pekee na ni bure kabisa.
Tunamshukuru
sana Mh Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutuletea dawa hii.Ningependa
kuwashauri walioathirika wa dawa za kulevya iwe wewe,ndugu
yako,rafiki,kaka,dada,mjomba,jirani au yoyote aliye karibu na
wewe.Usiogope amua tu kwamba unataka kupona na nenda kanywe hii dawa
utapona kabisa.”